- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
PICHA A
PICHA B
- Tunachokijua
- Picha za Akili Mnemba (Artificial Intelligence) ni picha zinazoundwa au kuboreshwa na teknolojia ya akili bandia. Hizi picha zinaweza kuwa zimeundwa kutoka mwanzo kabisa na AI, kwa kutumia michoro, maandishi, au maelezo yaliyotolewa na mtumiaji. AI hutumia algorithimu na mitandao ya neural ili kuunda picha ambazo zinaweza kuonekana kama zimechorwa na binadamu, lakini zimeundwa na kompyuta. Pia, AI inaweza kutumika kuboresha picha zilizopo, kama vile kuongeza ubora, kurekebisha rangi, au kuondoa dosari.
Picha halisi ni picha ambazo zimechukuliwa moja kwa moja kutoka kwa mazingira halisi, kwa kutumia kamera au kifaa kingine cha kurekodi picha. Hizi picha zinakamata muonekano wa vitu, watu, au mazingira jinsi vilivyo, bila uhariri au uundaji wa kidigitali.
Novemba 15, 2023 James Martin Mpiga Picha wa CNET aliandaa na kuzichanganya picha halisi na nyingine zilizotengenezwa kwa Akili Mnemba (AI) ili kupima uwezo wa watu kuzitambua (Andiko limehifadhiwa hapa). Miongoni mwa picha katika andiko hilo, mbili zilizozotumika hapo juu zilizochukuliwa na JamiiCheck.com ili kushiriiana na Wadau wae kuzitambua.
Wadau wengi wa JamiiCheck wametoa maoni yao huu asilimia 99 wakisema picha inayoonesha milima yenye rangi ya Jangwa imetengenezwa kwa Akili Mnemba wakati nyingine nyingine ikiwa halisi.
UKWELI NI UPI?
James Martin katika andiko aliloliandaa ametoa majibu katika kila picha na kubainisha zilizo halisi na ambazo zimetengenezwa kwa AI. Mpigapicha huyo anaeleza kuwa picha ya safu za Milima yenye ukungu wa baharini iliyo chini katika bonde iliundwa na Akili Mnemba (AI).
Aidha, JamiiCheck pia imeichunguza picha hiyo kwa kutumia Freepik.com imeleta majibu yenye picha yaidi ya 50 zilizotengenezwa kwa Akili Mnemba zenye kuwiana na picha hiyo (Majibu hayo yamehifadhiwa hapa).
Picha iliyotengenezwa kwa Akili Mnemba (AI)
Pia, sifa inayoweza kuonekana kwa macho kuwa picha hiyo imetengenezwa ni mimea iliyo sehemu ya mbele ya picha inaonekana kama miti lakini ukiizingatia haina maumbo yanayoeleweka.
Kwa upande wa picha ya pili yenye muonekano wa mazingira ya Jangwa James Martin anaeleza kuwa, ingawa kwa muonekano inaonekana kama ni picha ya kuchorwa, picha hiyo yenye mandhari ya jangwa ni picha halisi iliyopigwa katika maeneo ya Zabriskie Point, kwenye Hifadhi ya Kitaifa ya Bonde la Kifo lililopo Jimbo la California nchini Marekani.
Picha halisi iliyopigwa Zabriskie Point kwenye Hifadhi ya Kitaifa ya Bonde la Kifo California
JamiiCheck imehakiki picha hii kwa kutumia Google Reverse Search na kupata majibu (haya) yanayowiana na yale yaliyotolewa na James Martin katika andiko lake. Picha hii ni mazingira halisi ya Zabriskie Point, kwenye Hifadhi ya Kitaifa ya Bonde la Kifo lililopo Jimbo la California nchini Marekani.