SI KWELI Ujumbe huu ni wa onyo la kufungia akaunti kutokea Kampuni ya Meta

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Nimetumiwa hii text kwenye whatsapp kwamba ibatoka meta na account itafungwa ndani ya masaa 24 yajayo kwamba nakiuka sheria za mata.

1000130015.jpg
 
Tunachokijua
Meta ni jina jipya la kampuni iliyokuwa inajulikana kama Facebook, Inc. Kampuni hiyo ilibadilisha jina lake kuwa Meta Platforms, Inc. mnamo Oktoba 2021 ili kuonyesha mwelekeo mpya wa kampuni hiyo kuelekea kwenye "metaverse" — mfumo wa kidijitali unaowezesha watu kuingiliana kwa njia ya mtandao wa 3D na teknolojia ya ukweli pepe (VR) na ukweli ulioboreshwa (AR).

Meta bado inamiliki na kuendesha huduma kama Facebook, Instagram, WhatsApp, na Messenger, lakini inajikita pia kwenye kujenga teknolojia za metaverse.

Kampuni hiyo kupitia bidhaa zake kama FaceBook, Instagram na WhatsApp wanaweza kutoa onyo na kufungia watumiaji wake ikiwa watakiuka se sera zake za matumizi. Baadhi ya sababu zinazoweza kusababisha akaunti ya mtumiji wa WhatsApp kufungiwa ni:
  1. Kutuma ujumbe mwingi kwa watu wasiohifadhi namba yako – Kutuma ujumbe wa kikundi au matangazo kwa watu wengi ambao hawajakuhifadhi kwenye mawasiliano yao kunaweza kusababisha akaunti yako kudhibitiwa au kufungiwa.
  2. Matumizi ya WhatsApp isiyo rasmi – Kutumia programu za WhatsApp ambazo si rasmi (kama WhatsApp GB au WhatsApp Plus) kunaweza kusababisha akaunti kufungiwa kwa sababu hazikubaliki na WhatsApp.
  3. Kutuma maudhui yasiyofaa au hatari – Kusambaza taarifa za uongo, vurugu, unyanyasaji, au maudhui ya chuki kunaweza kusababisha akaunti kufungiwa.
  4. Kufanya spam au kueneza virusi – Kutuma ujumbe wa mara kwa mara bila ridhaa ya mpokeaji au kueneza programu za hatari kunaweza kusababisha akaunti kufungiwa.
  5. Matumizi mabaya ya vikundi – Kuongeza watu kwenye vikundi bila ridhaa yao au kutumia vibaya majukwaa ya vikundi pia kunaweza kuathiri akaunti yako.
  6. Kukiuka sera za faragha – Kukusanya au kutumia taarifa za watumiaji wa WhatsApp kwa njia zisizoruhusiwa, kama vile kutumia programu za kukusanya namba za simu.
Kuna ukweli kwenye onyo alilipewa Mdau wa andiko hili?
JamiiCheck imefuatilia onyo hili na kubaini mambo kadhaa ambayo hayaendani na Kampuni ya Meta. Baadhi ya mambo hayo ni:

1. Namba iliyotumika kutoa onyo:
Namba iliyotumika kutoa onyo hilo sio ya Kampuni ya Meta, namba hiyo ni ya mtu binafsi yenye msimbo (Code) ya nchi ya Vietnam.

2. Makosa ya kiuandishi
Onyo hilo linalodaiwa ni la kampani ya Meta lina makosa ya kiuandishi kwenye kichwa na hitimisho lake. Andiko limetumia neno 'Arifa' badala ya neno 'taarifa'. Makosa haya yanaongeza nguvu ya kuwa na uwezekano Mkubwa andiko hili limeandaliwa na mtu na sio Kampuni.

3. Kiunganishi (link) kimetengenezwa
Andiko hilo linaonekana kutoa onyo na kumsisitiza mtumiaji awasikiane nao kwa link. Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini link hiyo si ya Meta bali imetengenezwa na Akili Mnemba (Unicody AI)
Matapeli hao, hiyo Ni google translate kabisa from English to Swahili. Bwana Mark Hana Muda huo mchafu
 
Hata mimi wamenitumia huo ujumbe, nikashangaa sana wakati ni muda kidogo sijatumia FB wala Insta.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom