- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Kuna taarifa mitandaoni zimekuwa zikisambaa na kutanabaisha kuwa mazoezi ya "kegels" yanaweza kuongeza au kutibu shida ya nguvu za kiume kwa ufanisi, Je ni kweli?
- Tunachokijua
- Nguvu za kiume ni hali inayomuwezesha mwanaume kushiriki tendo la ndoa kwa ufanisi, ambapo ukosefu au upungufu wa nguvu hizo hupelekea kushindwa kwa mwanaume kushiriki kikamilifu katika tendo la ndoa kwani husababisha uume kulegea, kushindwa kusimama kabisa au kuwahi kumaliza tendo.
Sababu zinazoweza kusababisha hali hiyo ni pamoja na tabia ya kujichua, ulevi wa pombe, magonjwa kama vile kisukari, shinikizo la damu, magonjwa ya moyo.
Kegels ni mazoezi ya viungo yanayofanyika kwa ajili ya kuimarisha misuli ya nyonga na mifupa miwili ya miguu ambayo inashikilia viungo vya uzazi kwa wanawake na wanaume. Mazoezi ya kegels yaliasisiwa na Dkt. Arnold Kegel kutokea nchini Marekani kwa ajili ya kuwasaidia wakina mama waliokuwa wakipata shida ya kushindwa kubana mkojo mara baada ya kujifungua.
Mazoezi ya kegel si muhimu kwa wanawake tu lakini ni muhimu kwa wanaume pia, kwa mujibu wa andiko lilochapishwa katika tovuti ya Harvard health publishing, linaeleza kwamba Udhaifu wa misuli ya sakafu ya nyonga (Pelvic floor muscles) una athari ya moja kwa moja katika afya ya uzazi baina ya mwanaume pamoja na mwanamke kutokana na kuwa na uhusiano wa moja kwa moja na misuli muhimu inayowezesha ushiriki kamilifu katika tendo la ndoa.
Kwa mujibu wa Chapisho kutoka tovuti ya maktaba ya tiba ya taifa ya Marekani inaonyesha kuwa mazoezi ya kegel yanatajwa kuwa na matokeo chanya kwa wanaume wenye changamoto ya kuwahi kumaliza tendo la ndoa mapema zaidi ama wenye changamoto ya uume kulegea (dhaifu).
Aidha Tathmini iliyofanywa mwaka 2021 na kuchapishwa katika tovuti ya maktaba ya tiba ya taifa ya marekani, ambayo ilihusisha tafiti 37 kuhusu Upungufu wa nguvu za kiume, Tafiti nyingi zilirekodi kuwa kwa, kuimarisha misuli ya sakafu ya nyonga (Pelvic Floor Muscles) kupitia mazoezi ya mara kwa mara ya kegels, inaweza kuboresha uimara kwa mwanaume katika kushiriki tendo la ndoa kikamilifu na kuwa na uume imara ikiwa matibabu ya tiba za mikono (manual physical therapy) yataunganishwa na mazoezi ya misuli ya nyonga (Pelvic flow muscles exercise) ama kegels.
Tafiti nyingine inayothibitisha suala hilo ipo hapa.