- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Wakuu salaam,
Kuna mdudu anaitwa Mjusi kafiri, kumekuwa na hoja mbalimbali kwamba mdudu huyo ni hatari na ana sumu kali ikiwa atadondokea kwenye chakula na ukakila.
Je kuna ukweli kuhusu hoja hii?
Kuna mdudu anaitwa Mjusi kafiri, kumekuwa na hoja mbalimbali kwamba mdudu huyo ni hatari na ana sumu kali ikiwa atadondokea kwenye chakula na ukakila.
Je kuna ukweli kuhusu hoja hii?
- Tunachokijua
- Mjusi kafiri ni aina ya mjusi mdogo anayejulikana pia kama house gecko kwa Kiingereza. Hawa mijusi hupatikana sana kwenye maeneo ya makazi ya binadamu, kama vile majumbani na kwenye majengo. Wanapenda kukaa kwenye kuta, dari, au maeneo yenye mwanga, kwani huvutia wadudu ambao wanawinda kama chakula, kama vile mbu na nzi.
Mjusi Kafiri/ house gecko
Kumekuwa na hoja mbalimbali za kijamii zikidai kuwa Mjusi Kafiri ni hatari ndani ya nyumba ikiwa atadondokea kwenye chakula na asipoonwa basi huacha sumu kali ambayo huweza kuua mtu. Hoja hizo zimetolewa na kuwekwa mitandaoni na watu mbalimbali tazama hapa, hapa, hapa, hapa na hapa (kwa kuwamulika wachache)
Zaidi ya hoja hizo Kuna baadhi ya taarifa zimewahi kuripoti watu kufariki baada ya kula chakula kilichoangukiwa na Mjusi, taarifa hiyo imehifadhiwa hapa
Je upi uhalisia kuhusu madai hayo?
Taarifa iliyoripoti vifo vya watu waliokula chakula kinachidaiwa kuwa na sumu
Katika kutafuta uhalisia wa madai kwamba Mjusi Kafiri ana sumu kali, JamiiCheck imepitia tafiti kutoka National Library of Medicine (Umehifadhiwa hapa) April, 2011 na Fact Crescendo wa Srilanka uliofanywa Julai 10, 2024 (umehifadhiwa hapa). Tafiti zote zinaonyesha kuwa Mijusi Kafiri (house geckos) hawana sumu inayoweza kumuua au kumdhuru binadamu. Hakuna ushahidi wa kisayansi unaoonyesha kuwa mijusi hawa wana sumu kali.
Mathalani, Fact Crescendo wa Srilanka katika andiko la utafiti wao wanaeleza kwa kina tabia na sifa za Mjusi Kafiri na ukweli kuhusu mdudu huyu kuwa na sumu. Sehemu ya andio lao inafafanua:
Geckos wanapopata mawindo, hutumia ulimi wao kuwanasa. Ulimi huo unafanana kidogo na ule wa chura, ni mrefu, unaobadilika na umefunikwa na mate yenye utelezi. Ulimi huu hauna sumu yoyote ya kupooza mawindo. Mijusi hutumia ulimi wao kushika mawindo kwa nguvu ili yasitoroke. Geckos huingiza mawindo waliyonasa kwa nguvu ndani ya midomo yao bila kuwaua, kisha huwatafuna kwa meno yao kwa kuwatafuna kwa nguvu.Mara nyingi, geckos hulamba macho yao kwa ulimi kwa sababu yanakauka. Kwa kulamba macho, wanaweza kuyafanya yabaki na unyevu kwa safu ya mate kutoka kwenye ulimi. Kwa hiyo, mate ya gecko, ulimi au meno yao hayana sumu yoyote maalum.Geckos wa majumbani wanajulikana kubeba aina mbalimbali za vijidudu mwilini mwao vinavyosababisha sumu ya chakula baada ya kula vyakula vilivyochafuliwa. Kwa kuwa geckos hawa si wenye sumu, sumu ya chakula inayosababishwa na uwepo wao kwenye chakula haiwezekani.Nayo taasisi ya Geeksforgeeks (GFG) inayojihusisha na kutoa Elimu mtandaoni, imeandaa makala maalumu kumfafanua Mjusi Kafiri kwa kina. Aidha, kuhusu kiumbe huyu kuwa na sumu GFG wameeleza kuwa kiumbe asiye na sumu kwa binadamu na hata Wanyama.
Aidha, GFG wanatoa tahadhari kuwa licha kuwa viumbe hawa hawana sumu bado wanapaswa kuangaliwa kwa makini sababu huweza kubeba bakteria na kinyesi chake huwa na uchafu ambao unaweza kuleta shida kwa binadamu, (makala hiyo imehifadhiwa hapa).