Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Mbowe maandamano.png

Nimeona video ikizunguka kwenye mitandao ya Kijamii ikonesha kuwa jioni ya leo, mwenyekiti wa CHADEMA amesitisha maandamano yaliyokuwa yafanyike Septemba 23


 
Tunachokijua
Freeman Mbowe ni ni mwanasiasa maarufu nchini Tanzania. Yeye ni kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambacho ni chama kikuu cha upinzani nchini.

Baada ya taarifa ya kifo cha aliyekuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu Ally Mohamed Kibao kilichotokea Septemba 8, 2024, chama cha CHADEMA kiliweka azma ya kufanya maandamano Septemba 23, 2024 kupinga utekaji na mauaji yanayoendelea nchini (Soma Hapa). Baada ya azma hiyo tukio siku ya September 13, 2024 Jeshi la Polisi lilifanya Mkutano na Waandishi wa Habari kukikataza chama hicho kufanya maandamano hayo (Soma hapa).

Kama alivyodokeza mdau mleta mada hii leo kupitia mtandao wa X (Twitter) katika akaunti hii na hii kumechapishwa taarifa iliyoambatana na video ikimuoonesha Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akitangaza uamuzi wa chama hicho kusitisha mpango wa Maandamano ili kutoa nafasi ya Viongozi wa dini kutafuta suluhu. Katika video hiyo yenye sekunde 33 Freeman Mbowe anaonekana akisema:

Tunaomba na kuwatangazia Viongozi wa ngazi zote za CHADEMA pamoja na Wanachama, Wabunge wakiwemo, Madiwani, Wafuasi na Mashabiki wetu Watanzania wote popote pale walipo, kwamba tunaahirisha mikutano na maandamano ya amani yaliyopanga kufanyika nchi nzima ili kutoa nafasi kwa viongozi wetu wa kiroho kutafuta suluhu ya jambo hili kwa kukutana na rais na serikali yake
Upi ukweli wa Video hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao wa JamiiCheck kupitia mtandao wa YouTube kwa kutumia maneno CHADEMA yasitisha Maandamano tumepata majibu kuwa video hii si ya mwaka huu wala haihusiani na mpango wa Maandamano ya CHADEMA ya mwaka huu. Video hii ilichapishwa kwenye mtandao huo mara ya kwanza Agosti 31, mwaka 2016 (tazama hapa na hapa) huku ikieleza uamuzi wa CHADEMA kusitisha kwa mwezi mmoja maandamano ya UKUTA waliyoyapanga kuyafanya Septemba 1, 2016.
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom