SI KWELI Picha ya Joseph Mbilinyi (Sugu) akiwa amelazwa hospitali ilikuwa na chupa ya Konyagi kwa pembeni

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Salaam Wakuu,

Nimekutana na chapisho hili kutoka Twitter, ina ukweli?

1726325862022.png
 
Tunachokijua
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa picha hiyo ni halisi lakini imehaririwa kwa kuongezwa chupa ya pombe sehemu kabati upande wa kushoto karibu na kichwa cha sugu.

Kupitia Google Image Search umepata matokeo yanayoonesha picha hiyo ya ilichapishwa mtandaoni kwa mara ya kwanza kwenye Mtando wa X (Twitter)Agosti 14, 2024 kwenye akaunti rasmi ya Joseph Mbilinyi Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa (hii) na haikuwa na chupa ya pombe kama picha (hii) iliyochapishwa na Mzalendo Daily.

1726331059896-png.3095827

Picha iliyochapishwa na Joseph Mbilinyi Agost 14, 2024
Hiyo page ya mzalendo daily ndio kazi yake kuchukua picha za viongozi wa Chadema na kuongeza pombe,
 
Wekezeni zaidi kwa ma graphic designer. Yani hii ni uozo wa photoshop. Hata kipofu anaona magumashi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom