- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Habari wapendwa, kuna taarifa inatembea mitandaoni kuwa Dkt. Slaa amepata taarifa ya Deusdedit Soka ya kwamba atauawa leo na kutupwa msituni, je, Taarifa hiyo ni kweli imetoka kwa slaa? Na ina ukweli?
- Tunachokijua
- Deusdedith Soka ni Mwenyekiti wa Vijana Temeke kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA).
Mnamo tareheAgosti 8, 2024 alitoweka na mpaka leo tarehe 22,08,2024 haijafahamika alipo licha ya jitihada za watu mbalimbali na chama chake kuendelea kumtafuta alipo.
Taarifa ya CHADEMA kuelezea tukio hili imehifadhiwa hapa.
Mnamo tarehe 21, Agosti 2024, zilianza kusambaa taarifa zilizodai kuwa ni taarifa kutoka kwa Dtk. Wilbroad Slaa ambaye alidai amepata taarifa kuwa Soka atauawa usiku wa tarehe 21, 08, 2024 kabla ya saa 8 usiku na kutupwa kwenye msitu na kwamba hiyo ni amri imetolewa. Tazama
Jamiicheck, Imemtafuta na kuzungumza na Dkt Slaa ili kupata uhalisia wa taarifa hiyo ambaye amekiri kuwa ni kweli ujumbe huo ni yeye ameutoa na taarifa hizo ana uhakika nazo.
"Jana majira ya saa 10 jioni nilipokea taarifa kutoka kwenye vyanzo vyangu vya kawaida, kuhusu kijana wetu ambaye ni Soka, Soka ni kijana ambaye namfahamu nimewahi kufanya naye kazi mara kadhaa namfahamu namna anavyofanya kazi zake na mara kadhaa mekuwepo kwenye press coference zangu, namfahamu kwa undani, nafahamu nia yake kwa Tanzania, namfahamu namna ambavyo anavyolipenda taifa lake ambalo ni Tanzania.
Ni dhahiri ukipata taarifa kama hiyo ya mtu unayemfahamu kuwa leo usiku maisha yake yatafika mwisho leo usiku, nilistuka sana, kwa hiyo nikawashirikisha viongozi wa sauti ya mtanzania. Na tukafanya mkutano na kuweka maazimio juu ya jambo hilo.
Hili sio jambo ambalo tungeweza kukaa nalo, hivyo tukaweka maazimio juu ya namna ya kuwajulisha watanzania kupitia sauti ya Mtanzania.
Watu waliopewa kazi ya Kufikisha mwisho maisha ya Soka ndio haohao walioshughulika na Sativa, na wanajulikana majina yao, Hivyo nilipopata taarifa hiyo nikaona ni vyema kuwajulisha watanzania. Hao ndio waliohusika na mchakato wa kumkamata ikiwamo yule msichana ambaye anatembea na bodaboda, ni msichana, mwanamke mweupe umri wa makadirio ni miaka 20 kwenda 30 ambaye huwa anatembea na bodaboda, ni mwanamke hatari kwa kuwa yeye ndiye ambaye huwa anaweka mitego ya kuwakamatisha ambao hao wote ambao huwa wanakamatwa.
Katika hatua hiyo, picha tuliyoambiwa usiku huo ni kwamba walikuwa wanaondokea pale kwenye kituo cha polisi pale cha Mikocheni, cha Osterbay kwa hiyo watawapeleka kwenye uelekeo ambao wamepangiwa , uelekeo hasa ni upi kati ya Tanga na Arusha hatukua tunajua ila ilibidi tupate taarifa kwa wakati huo, na baada ya hapo watu wetu watajadili kama ambavyo wamekuwa wakijadili mambo yetu.
Kwa sasa watanzania tumefikishwa mwisho wa uvumilivu, kama wanaweza kutunzwa ndani ya vituo leo anaweza kuwa Soka kesho ni mwingine.
Labda nikukumbushe namna ambavyo Soka alikamatwa safari hii, Soka alikamatwa kwa kuitwa kwenda kituo cha polisi kutambua pikipiki yake ambayo mwaka jana polisi Waliikamata na haikurudishwa mpaka leo wala kupigiwa simu. Kwa hiyo alipoitwa hakuwa wala na wasiwasiila kwa tahadhari ya kawaida alichukuzana na rafiki yake wa kawaida walikwenda pamoja na mbele ya rafiki yake alichukuliwa tu akawekwa ndani na rafiki yake akaachiwa.
Na ndio sababu ya watu kuwa na wasiwasi kama ambavyo sasa hivi kuna vituo vinavyoitwa vya gereji, Kama mmewahi kusoma kitabu cha Mdude Nyagali ambacho aliandika baada ya kushinda kesi ya kukutwa na madawa ya kulevya na mahakama kuthbisha kuwa Polisi ndio walimuwekea Mdude madawa ya kulevya hivyo huo ni uthibitisho wa yanayotokea vituoni, Tulidhani Sativa atakuwa mtu wa mwisho kupotea, ila sasa Aliyechora picha ya Rais na kuichoma naye haonekani na sasa Soka sasa ndio maana hii taarifa tuliona kuna umuhimu wa kulishughulikia na tumepeleka taarifa kila sehemu ikiwemo mabara mbalimbali. Dkt Wildroad Slaa Akizungumza na Jamiicheck