Nahitaji kufahamu taarifa inayosambaa kwamba dawa za ARV zinatumika kunenepesha mifugo.
- Tunachokijua
- Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo duniani ARVs ni dawa ambazo hutumiwa na watu walioathirika na Virusi vya UKIMWI, ARV ni ufupisho wa neno Antiretrovirals ambapo ni dawa ambazo hufanya kazi ya kuzuia Virusi Vya Ukimwi kuzaliana huku zikiongeza nguvu kwenye kinga ya mwili (CD4). ARV hazitibu Virusi Vya UKIMWI lakini husaidia kuzuia Virusi hivyo kutokuleta madhara kwa mwili wa Binadamu.
Kumekuwepo na taarifa juu ya matumizi yasiyo sahihi ya ARV, ikielezwa kuwa baadhi ya wafugaji hutumia dawa hizo kwa ajili ya kunenepeshea na kukuza haraka mifugo yao mfano nguruwe, ng’ombe, kuku na wanyama weningine.
Uhalisia wa jambo hili umekaaje na madhara yake ni yapi kwa binadamu?
Utafiti uliofanyika nchini Uganda na kuchapishwa katika tovuti ya International Journal of One Health ukihusisha wilaya kumi na nchi hiyo, ulipima matumizi ya dawa za ARV’s kwa sampuli ya kuku, nguruwe na ulishaji wa wanyama ambapo pia ulilenga kubaini uwepo wa dawa za ARV kwenye nyama pamoja na kufahamu uelewa na mitazamo ya wafugaji juu ya matumizi ya dawa hizo.
Matokeo ya utafiti huo yalionyesha washiriki wote kutoka wilaya zote kumi, kutoka makundi yote yaani wafugaji wa nguruwe, kuku wa nyama na mayai walibainika kutumia dawa za ARV ili kunenepesha mifugo yao.
Ripoti ya mamlaka ya dawa nchini Uganda ya mwaka 2014 pia ilithibitisha uwepo wa baadhi ya wafugaji hasa wa nguruwe kutumia ARV kunenepesha na kukuza haraka mifugo yao.
Wataalamu wanaonya juu ya matumizi ya dawa za ARV kwa mifugo mfano kuku ili kunenepesha mifugo hiyo kwani husababisha usugu wa vimelea katika kuitikia kutibika na dawa yaani Anti-Microbial Resistance AMR na kuayoathiri afya ya binadamu, mimea na wanyama.