Zitto: Tunapata maduhuli na si "gawio"

Zitto: Tunapata maduhuli na si "gawio"

Zitto ungekaa kimya pia ingependeza sanaa. Si kila jambo ulitolee tamko ni hekima na busara siku zote unapokuwa umenyamaza kuliko unapokuwa unazungumza.

Nawaombeni enyi mnaojiita wanasiasa kujitafakari wakati mwengine kwa michango yenu kama inaumuhimu wowote kwa maendeleo ya taifa au la.

Hivi mtu akiita gawiwo au mchango au pato au duhuli na akalitoa kwa mwenye hisa unapungukiwa na nini ukinyamaza kimya bila ya wewe usiye na kiasi hicho kuchangia kwa jamii?

Tuwe wastaarabu wakati mwengine badala ya kuwa washenzi na wenye kukosa adabu kwa matamko yasiyokuwa na tija kwa taifa letu.

Nimuulize zito na mnaomuunga mkono maelezo yake hapo juu yamesaidia nini kwa taifa ukilinganisha na shughuli iliyofanyika leo? Je tule maneno au fedha zilizochangiwa leo?
Hivi wewe unawafahamu wale Maprofesa wa usanii: wanao uwezo wa kugeuza karatasi ukaziona ni fedha haswa. Usipokuwa mwangalifu umeliwa.
Zito anayafahamu haya kwa sheria, maana alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma. Wewe unataka akae kimya ili usanii wenu ukolee au!!!?
 
Mayonene!! Kwaio jiwe alipanga Kabisa aje atulishe matango pori watu wote milioni 45 hv maprofesa WA UDSM ,MZUMBE wanafanya nini? Bila Zitto kushtuka tulikua tunaingizwa chaka kumbe,, Kenyatta alikua sahihi kumwambia Nyerere kua ana bahati anaongoza watanzania ambao ni Maiti wanaotembea
 
Kwani TCRA nao wametoa?,
Sio kwamba waliotoa ni mashirika kama crdb,nmb,Tamwa,reli,tanesco etc
Wametoa, tena na among top three waliopewa vyeti kwa kutoa huge sums wengine ni NCAA na TANAPA.
 
Ni sawa na mtu akasema umelipa adhabu ya sh laki 5, mwingine akasema umetoa mchango wa laki 5, tofauti ni nini? Zote si hela?
Fedha za adhabu /fine zina running costs ambazo mwishowe lazima uzitoe out of hiyo laki tano..... Mchango hauna costs maana umeshaziondoa na kilichobaki utakoa laki tano ukapeleka
 
Mashirika yapo zaidi ya 100
Lakini yaliyotoa gawio ni mashirika 47 tu .

Swali kwa Zito hiyo 15 % huwa yanakatwa hayo 47 tu na yanayobaki hayakatwi ?

Kama hoja ya Zito ina kweli basi tungeyaona mashirika yote zaidi ya 100 yakitoa gawio leo
Sasa shirika Kama ATCL kamati ya bunge imesema shirika hilo limepata hasara kwa miaka miwili mfululizo gawio watapata wapi?
 
Safi sana zitto.

Nakushauri uitishe mkutano wa waandishi wa habari ufafanue jambo hili kwa umma.
Ushauri wako ni mzuri lakini mwandishi wa habari gani atasogeza pua yake hapo? Umesahau ya 1.5 T zilizokosa maelezo. Zt alipoitisha kikao kuna mwandishi alitia kucha zake zaidi ya TV za mitandaoni? Waandishi wameufyata kama vijibwa vya uswazi vikikutana na mtu mkia unashuka!
 
Magufuli kufanya siasa bila mipaka hata kwenye mambo ya msingi kama haya huwa namdharau sana. Lissu hakukosea kusema tuna Rais wa ajabu mno haijawahi kutokea

Na taarifa zitakazokuwa zinatolewa kwenye vyombo vya habari zitakuwa "Jinsi Magufuli alivyoweza kuyafanya mashirika yetu ya Umma kuanza kuwa yanapata faida na kulipa baadhi ya faida hiyo serikalini." Sifa gedegede zimwendee yeye kwa uongozi uliowezesha faida hizo. Kumbe ni danganya toto tu!
Tatizo ni kwamba Rais yuko kwenye "permanent political campaign mode." Moves zake zote ni 'self-promotion'. Watu watapata taabu sana.
 
Zitto nahisi hakusikiliza vizuri kakimbilia kuandika na kupotosha watu. Imesemwa wazi, kuna walio toa gawio hasa wenye muundo wa kampuni na shareholding structure mf. Kadco. Baada ya hapo ikatangazwa yanakuja mashirika yanayotoa maduhuri mf. Tcra, ewura na wengine. Tofauti imesemwa wazi kwa waliosikiliza na ikatajwa kuwa ni 15% ya mapato kulingana na sheria. Zitto hoja huna tena.
Hata mimi nilisikia vivyo hivyo mkuu wangu; bado nikajiuliza, je haya mashirika yasiyo ya kibiashara yanapata wapi pesa hizo. Ndipo nikafafanuliwa na mtu mwingine kuwa mashirika hayo yasiyokuwa ya kibiashara hutoza wadau wake ushuru wa aina mbalimbali kwa mfano kutoa hati, leseni na kadhalika. Wanaruhusiwa kutumia sehemu ya mapato yatokanayo na ushuru huo kujiendesha na sehemu nyingine ndiyo hiyo inayopelekwa serikalini. Kwa mfano vituo vyote vya redio, TV, na makampuni ya simu hulipia leseni zao huko TCRA. Sehemu ya mapato yatokanayo na leseni hizo ndiyo hayo yanayopelekwa serikalini na TCRA.

Madai ya kuwa haya mambo yalikuwapo siku zote, kwa nini leo ndipo yatangazwe ni lawama za abunuwasi tu. Ni kweli kuwa hata leo kuna mashirika ambayo yalikuwa yameshakabidhi michango yao, na yalitambuliwa, ila yale yote ambayo yalikuwa hayajawasilisha ndiyo yaliyofanya hivyo leo. Kuna sababu nyingi ingawa mimi sijui ni sababu gani iliopelekea waamua kutangaza leo. Hata hivyo kuamusha awareness ni sababu mojawapo kubwa sana ninayoona mimi, kusudi yale mashirika yasiyopata faida yajionee aibu na kujiandaa kufanya vizuri baadaye; vile vile ni kuyatia moyo yale yaliyofanya vizuri kwa kuyapa hati za recognition hadharani. Ni mbinu mojawapo katika management.

SIasa za siku hizi za upinzani zimekuwa na upotoshaji sana; huenda ni kwa vile labde yale ya kukososa yamepungua au hayapo kabisa.
 
Ha ha ha ha mkuu umejibu kisiasa sana na siyo kitaaluma kabisa, anyways mimi nimekuelewa lakini swali linabaki pale pale, kati ya Rais na Zitto nani mkweli katika hili swala la gawio na maduhuli? Ukiniambia kuwa eti Rais hawezi kusema uongo nakataa kabisa.

Wanachotaka kujua Watanzania ni UKWELI tu basi.
The boss is always right, hivyo mkweli ni rais.
Watanzania wanataka maendeleo.
P.
 
Mwenyekiti Mstaafu wa PAC,Bwana Zitto,anaelezea juhudi zake za kuishauri Bunge la 9 kufanya marekebisho ya Sheria ya Mashirika ya Umma ili kiwango Fulani cha Mapato ghafi (turnover) kipelekwe Serikalini,Leo Mwenyekiti huyo anapinga Mapato hayo kuitwa faida lakini kama mapato hayo yangekosekana angekuwa wa kwanza kuyaita hasara na kuutangazia Umma kuwa Serikali inapata hasara.

Moja ya vigezo ambavyo wawekezaji hasa kwenye hisa wanashauriwa sana kuangalia ni utoaji wa gawio. Unaponunua hisa kwenye kampuni inayotoa gawio, unanufaika zaidi na uwekezaji wako.

Makampuni yanatofautiana kwa namna yanavyotoa faida yake kwa wawekezaji wake.

Zipo kampuni ambazo zinatoa gawio moja kwa moja, hapo zinatoa sehemu ya faida kwa wanahisa. Kiasi cha gawio hupatikana kwa kugawa faida inayotolewa kwa wanahisa kwa idadi ya hisa. Na hapo kinapatikana kiasi cha fedha kitakacholipwa kwa kila hisa moja.

Zipo kampuni ambazo faida inayopatikana inarudishwa kuwekezwa kwenye kampuni, ili kuikuza zaidi na kuongeza thamani ya hisa zake. Hapa wanahisa wananufaika kwa ongezeko la thamani kwenye uwekezaji wao.

Pia zipo kampuni ambazo zinaweza kutumia faida yake kununua hisa zake yenyewe, kutoka kwa wanahisa. Kama itanunua kwa bei nzuri wanahisa wananufaika.

Utoaji wa gawio ni lazima uridhiwe na wanahisa kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa kampuni. Na ikisharidhiwa basi kila mwanahisa, kulingana na daraja la hisa zake anapata kile anachostahili, kwa idadi ya hisa anazomiliki.

Gawio ni faida ya moja kwa moja ambayo mwekezaji anaweza kuipata kutokana na uwekezaji wako. Hivyo unapochagua kampuni za kuwekeza kwa kununua hisa zake, kigezo cha utoaji wa gawio ni muhimu.

- Maana Ya Gawio Katika Uwekezaji na Utolewaji Wake.

Kampuni au taasisi ambayo inauza hisa zake kwenye soko la hisa, inapaswa kutoa hesabu zake za mwaka kila mwaka. Katika hesabu hizi kampuni itaonesha mapato, matumizi, faida na hata hasara.

Iwapo kampuni imepata faida mwisho wa mwaka wa fedha, faida ile inapaswa kurudi kwa wanahisa wa kampuni hiyo.

Ile sehemu ya faida ya kampuni inayolipwa kwa wanahisa ndiyo inaitwa gawio. Hichi ni kipato ambacho mwekezaji anapata kutokana na uwekezaji ambao amefanya.

Kupata gawio, hakupunguzi chochote kwenye hisa za mwekezaji, badala yake anakuwa amepata faida, huku hisa zake zikiendelea kuwa kama zilivyokuwa. Hivyo hata kama atapokea gawio kila mwaka kwa miaka mitano, akija kuamua kuuza hisa zake atapata thamani ya zile hisa.

Nimalizie kwa kusema 15% ya mapato ghafi ya Taasisi za Umma kuwa mapato Serikali ni faida ambayo inaingia hazina.Zitto kwa kusema mashirika ya Umma hayana faida ni namna ya kushiriki pamoja na Mafisadi waliosababisha hasara Mara zote ambazo Serikali imekosa gawio lake kutoka katika mapato hayo.Ni kusihi Bwana Zitto kuwa na muono chanya katika kila jambo na si kusema hatuwezi au hatuna faida.
 
Nina hakika umemuelewa Zitto ila ukaaandika maelezo mengi yasiyokuwa na maana. Kwenye maelezo yako yote hujajibu swali la msingi, je serikali ilipokea gawio tu au maduhuri?

Na kama ilipokea gawio Taasisi na wakala wa serikali zisizofanya biashara zimewakilisha gawio gani? Tupe mfano TANROADS wametoa gawio kutoka wapi wakati hawana biashara wanayofanya, ilihali wao wenyewe hupewa allocations kuendesha shughuli zao?
 
Tena mie siiti Maduhuli, walichotoa mashirika ni Levy (tozo) na ndio maana ipo fixed kama percentage of their total collection. Ni aibu sana kwa mkuu kuita gawio, anaona raha sana kutaja hilo neno bila hata kujua maana yake
Hayo ni mambo ya lugha tuu, kwa sisi wa Kanda ya Ziwa, ukigawiwa fedha yoyote, jina la fedha hiyo ni gawiwo!.
P.
 
Hivi wewe unawafahamu wale Maprofesa wa usanii: wanao uwezo wa kugeuza karatasi ukaziona ni fedha haswa. Usipokuwa mwangalifu umeliwa.
Zito anayafahamu haya kwa sheria, maana alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma. Wewe unataka akae kimya ili usanii wenu ukolee au!!!?
Hakuna usanii wowote, zile ni fedha kweli serikali imegaiwa. Fedha yoyote inayogaiwa ni gawio.
P
 
Yaani maelezo mareeefu, halafu hujajibu hoja yoyote. Halafu kwanini nyie watu wa jiwe mnapenda kulazimisha nyekundu iwe nyeupe?
 
Back
Top Bottom