Zitto: Tunapata maduhuli na si "gawio"

Zitto: Tunapata maduhuli na si "gawio"

Zitto nahisi hakusikiliza vizuri kakimbilia kuandika na kupotosha watu. Imesemwa wazi, kuna walio toa gawio hasa wenye muundo wa kampuni na shareholding structure mf. Kadco. Baada ya hapo ikatangazwa yanakuja mashirika yanayotoa maduhuri mf. Tcra, ewura na wengine. Tofauti imesemwa wazi kwa waliosikiliza na ikatajwa kuwa ni 15% ya mapato kulingana na sheria. Zitto hoja huna tena.
sasa hilo la kutoa maduhuli lilihitaji kuweka live coverage?Tuna viongozi malimbukeni wapenda kiki kama bongo movie..Mbona Nyerere hakufanya hivyo
 
Na Zitto Kabwe

Kwamba Mashirika ya umma nchini yanamkabidhi Rais cheki za magawio (dividends) ya faida zao ni ama Ofisi ya Rais inafanya Siasa au hawajui maana ya gawio.

Tukiwa Bunge la 9, Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC na baadaye PAC) ililishauri Bunge kufanya marekebisho ya Sheria ya baadhi ya mashirika ya umma Ili kiwango fulani cha Mapato ghafi (turnover) kitolewe Serikalini kama maduhuli ya Serikali.

Serikali ya wakati huo ilikubali na Sheria zikabadilishwa na kutenga 15% ya Mapato ghafi ya Taasisi za Umma kuwa Mapato ya Serikali kuingia Mfuko Mkuu wa Hazina. SIO FAIDA maana mashirika haya mengi hayana faida. Faida ya TCRA ni nini? Ama EWURA? Ama TANROADS?

Kusema Rais anakabidhiwa gawio la faida ya mashirika ya umma ni ulaghai ambao hauna maana yeyote, kwani Taarifa za Ukaguzi za Mashirika hayo zitaonyesha kuwa hakuna faida (na hivyo hakuna gawio), na hivyo kuumbuka kwa Serikali yenyewe.

Kinachotolewa ni nini? Haya ni maduhuli tu, ama ni kodi maalumu ambayo imewekwa kwa mashirika kwa kiwango cha 15% ya Mapato ghafi. Maduhuli au kodi hii imekuwa ikilipwa miaka yote ya nyuma. Sielewi ni kwanini sasa Rais amewaleta mbele wakuu wa mashirika Eti kutoa gawio! Gharama za kuwaleta hao wakuu wa hizi taasisi hazikupaswa kuingiwa kabisa, kwani kodi hizo hukatwa moja kwa moja kuingia Mfuko Mkuu wa Serikali. Sielewi hizi hadaa ni za Nini?

Ni muhimu pia kueleza kuwa kuna hoja ya Ukaguzi ya CAG kuhusu makato haya kwa baadhi ya taasisi. Kwamba makato haya yanapaswa kuwa ‘Tax deductibles’ - yaani wakati wa kukokotoa kodi ya Mapato ya baadhi ya Mashirika malipo haya yanapaswa kuondolewa kwanza.

Hata hivyo TRA wamekuwa hawafanyi hivi na hivyo kukuta mashirika kama TANAPA, NCAA, TPA nk yanalipa Fedha zaidi ya yanavyopaswa kulipa na kusababisha shughuli zao za msingi kushindwa kutekelezwa.

Watanzania msihadaiwe leo, hatupokei gawio, bali tunapokea maduhuli tu.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Julai 23, 2018.

Mheshimiwa Zito, leo kwenye hotuba yake Raisi kasema kwa mashirika yasiyotoa dividents serikalini na viongozi wake wanahudhuria mikutano ya bodi na wanalipwa posho za wakurugenzi " directors fees" ni afadhali hata wangechukua hizo posho wapeleke serikalini kama dividends
 
Zitto ungekaa kimya pia ingependeza sanaa. Si kila jambo ulitolee tamko ni hekima na busara siku zote unapokuwa umenyamaza kuliko unapokuwa unazungumza.

Nawaombeni enyi mnaojiita wanasiasa kujitafakari wakati mwengine kwa michango yenu kama inaumuhimu wowote kwa maendeleo ya taifa au la.

Hivi mtu akiita gawiwo au mchango au pato au duhuli na akalitoa kwa mwenye hisa unapungukiwa na nini ukinyamaza kimya bila ya wewe usiye na kiasi hicho kuchangia kwa jamii?

Tuwe wastaarabu wakati mwengine badala ya kuwa washenzi na wenye kukosa adabu kwa matamko yasiyokuwa na tija kwa taifa letu.

Nimuulize zito na mnaomuunga mkono maelezo yake hapo juu yamesaidia nini kwa taifa ukilinganisha na shughuli iliyofanyika leo? Je tule maneno au fedha zilizochangiwa leo?
Kuleni fedha zetu, lakini acheni mbwembwe za uongo.
 
Kama ningekuwa rais zitto ningempa nafasi fulani asaidie kuyafanya mawazo yako mengi mazuri ktk utendaji. Zitto why are you always appear to be right? Simaanishi ktk hili tu. Mara nyingi huwa ni kama mtoa mawazo mbadala.
Je hutumiki vizuri ktk bunge na serikali? Hizi gvt organs huwa hawakutani na interest groups kupata insights zao au huwa unasubiri wakosee au unajua lazima watakosea mahali then uwakosoe?
Japo mi sio Zito labda yeye anaweza kua na majibu sahihi ya maswali yako.
Lakini na wewe kama ungekua unafuatilia vizr masuala ya nchi usingeuliza haya maswali na uhakika ungekua na majibu,
Mfano Lisu alikua anashauri kuhusu makinikia je aliishia wapi?
Na je hayo makinikia yameishia wapi ? Je wametulipa ? Na kama tumelipwa ziko wapi ?
Watu wenyew hawapokei ushauri unaanza vp kuwashauri.
Mi nilichokiona ni kujaribu kutoa awareness kwa wananchi, kama Mimi imenisaidia kuelewa hali halisi ya haya mashirika yetu
 
Zitto ungekaa kimya pia ingependeza sanaa. Si kila jambo ulitolee tamko ni hekima na busara siku zote unapokuwa umenyamaza kuliko unapokuwa unazungumza.

Nawaombeni enyi mnaojiita wanasiasa kujitafakari wakati mwengine kwa michango yenu kama inaumuhimu wowote kwa maendeleo ya taifa au la.

Hivi mtu akiita gawiwo au mchango au pato au duhuli na akalitoa kwa mwenye hisa unapungukiwa na nini ukinyamaza kimya bila ya wewe usiye na kiasi hicho kuchangia kwa jamii?

Tuwe wastaarabu wakati mwengine badala ya kuwa washenzi na wenye kukosa adabu kwa matamko yasiyokuwa na tija kwa taifa letu.

Nimuulize zito na mnaomuunga mkono maelezo yake hapo juu yamesaidia nini kwa taifa ukilinganisha na shughuli iliyofanyika leo? Je tule maneno au fedha zilizochangiwa leo?
Pole sana. Naona wewe umezoea nyekundu unasema nyeupe
 
You are SMART enough.

Siku akitoka madarakani ukweli utaziirika.
Na Zitto Kabwe

Kwamba Mashirika ya umma nchini yanamkabidhi Rais cheki za magawio (dividends) ya faida zao ni ama Ofisi ya Rais inafanya Siasa au hawajui maana ya gawio.

Tukiwa Bunge la 9, Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC na baadaye PAC) ililishauri Bunge kufanya marekebisho ya Sheria ya baadhi ya mashirika ya umma Ili kiwango fulani cha Mapato ghafi (turnover) kitolewe Serikalini kama maduhuli ya Serikali.

Serikali ya wakati huo ilikubali na Sheria zikabadilishwa na kutenga 15% ya Mapato ghafi ya Taasisi za Umma kuwa Mapato ya Serikali kuingia Mfuko Mkuu wa Hazina. SIO FAIDA maana mashirika haya mengi hayana faida. Faida ya TCRA ni nini? Ama EWURA? Ama TANROADS?

Kusema Rais anakabidhiwa gawio la faida ya mashirika ya umma ni ulaghai ambao hauna maana yeyote, kwani Taarifa za Ukaguzi za Mashirika hayo zitaonyesha kuwa hakuna faida (na hivyo hakuna gawio), na hivyo kuumbuka kwa Serikali yenyewe.

Kinachotolewa ni nini? Haya ni maduhuli tu, ama ni kodi maalumu ambayo imewekwa kwa mashirika kwa kiwango cha 15% ya Mapato ghafi. Maduhuli au kodi hii imekuwa ikilipwa miaka yote ya nyuma. Sielewi ni kwanini sasa Rais amewaleta mbele wakuu wa mashirika Eti kutoa gawio! Gharama za kuwaleta hao wakuu wa hizi taasisi hazikupaswa kuingiwa kabisa, kwani kodi hizo hukatwa moja kwa moja kuingia Mfuko Mkuu wa Serikali. Sielewi hizi hadaa ni za Nini?

Ni muhimu pia kueleza kuwa kuna hoja ya Ukaguzi ya CAG kuhusu makato haya kwa baadhi ya taasisi. Kwamba makato haya yanapaswa kuwa ‘Tax deductibles’ - yaani wakati wa kukokotoa kodi ya Mapato ya baadhi ya Mashirika malipo haya yanapaswa kuondolewa kwanza.

Hata hivyo TRA wamekuwa hawafanyi hivi na hivyo kukuta mashirika kama TANAPA, NCAA, TPA nk yanalipa Fedha zaidi ya yanavyopaswa kulipa na kusababisha shughuli zao za msingi kushindwa kutekelezwa.

Watanzania msihadaiwe leo, hatupokei gawio, bali tunapokea maduhuli tu.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Julai 23, 2018.
 
Zitto nahisi hakusikiliza vizuri kakimbilia kuandika na kupotosha watu. Imesemwa wazi, kuna walio toa gawio hasa wenye muundo wa kampuni na shareholding structure mf. Kadco. Baada ya hapo ikatangazwa yanakuja mashirika yanayotoa maduhuri mf. Tcra, ewura na wengine. Tofauti imesemwa wazi kwa waliosikiliza na ikatajwa kuwa ni 15% ya mapato kulingana na sheria. Zitto hoja huna tena.
Kama Moderator wako fair hii post wanatakiwa kuiweka pale juu.
 
Na Zitto Kabwe

Kwamba Mashirika ya umma nchini yanamkabidhi Rais cheki za magawio (dividends) ya faida zao ni ama Ofisi ya Rais inafanya Siasa au hawajui maana ya gawio.

Tukiwa Bunge la 9, Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC na baadaye PAC) ililishauri Bunge kufanya marekebisho ya Sheria ya baadhi ya mashirika ya umma Ili kiwango fulani cha Mapato ghafi (turnover) kitolewe Serikalini kama maduhuli ya Serikali.

Serikali ya wakati huo ilikubali na Sheria zikabadilishwa na kutenga 15% ya Mapato ghafi ya Taasisi za Umma kuwa Mapato ya Serikali kuingia Mfuko Mkuu wa Hazina. SIO FAIDA maana mashirika haya mengi hayana faida. Faida ya TCRA ni nini? Ama EWURA? Ama TANROADS?

Kusema Rais anakabidhiwa gawio la faida ya mashirika ya umma ni ulaghai ambao hauna maana yeyote, kwani Taarifa za Ukaguzi za Mashirika hayo zitaonyesha kuwa hakuna faida (na hivyo hakuna gawio), na hivyo kuumbuka kwa Serikali yenyewe.

Kinachotolewa ni nini? Haya ni maduhuli tu, ama ni kodi maalumu ambayo imewekwa kwa mashirika kwa kiwango cha 15% ya Mapato ghafi. Maduhuli au kodi hii imekuwa ikilipwa miaka yote ya nyuma. Sielewi ni kwanini sasa Rais amewaleta mbele wakuu wa mashirika Eti kutoa gawio! Gharama za kuwaleta hao wakuu wa hizi taasisi hazikupaswa kuingiwa kabisa, kwani kodi hizo hukatwa moja kwa moja kuingia Mfuko Mkuu wa Serikali. Sielewi hizi hadaa ni za Nini?

Ni muhimu pia kueleza kuwa kuna hoja ya Ukaguzi ya CAG kuhusu makato haya kwa baadhi ya taasisi. Kwamba makato haya yanapaswa kuwa ‘Tax deductibles’ - yaani wakati wa kukokotoa kodi ya Mapato ya baadhi ya Mashirika malipo haya yanapaswa kuondolewa kwanza.

Hata hivyo TRA wamekuwa hawafanyi hivi na hivyo kukuta mashirika kama TANAPA, NCAA, TPA nk yanalipa Fedha zaidi ya yanavyopaswa kulipa na kusababisha shughuli zao za msingi kushindwa kutekelezwa.

Watanzania msihadaiwe leo, hatupokei gawio, bali tunapokea maduhuli tu.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Julai 23, 2018.

Mheshimiwa kama Bunge mnarekebishaje hii hali ili madhuhuli haya yakusanywe na TRA ili wakubali kama sehemu ya matumizi halali ya shirika kama ilivyo kodi ya stadi za kazi (SDL)?
 
Asante Zitto kwa ufafanuzi mzuri. Jambo jema ni kuwa licha ya mambo yetu kupelekwa kilaghai, angalao tuna watu wachache wazalendo wa kweli kama akina Zitto, Lisu, Bashe, and the like, ambao daima husimama katika ukweli.
Mkuu Zitto kiukweli nilikuwa nakusanya taarifa za jambo hili , kiukweli ni kama umeniwahi , hongera sana .

Swali la kujiuliza ni kwanini serikali inataka kuendesha nchi kwa uongo ?
maduhuli/gawio kuna tofauti gani...zote si pesa?
 
Nashauri Zitto akamatwe na kushitakiwa kwa uchochezi wa kumdhalilisha rais wa JMT.

Rais wa nchi ni kama baba kwenye familia, sio mtu, huyu ni an institution, na kwa mujibu wa katiba yetu, rais wetu hawezi kukosea ndio maana jashitakiwi. Hata kama Zitto ni mkweli na hayo ni maduhuli na sio gawio, kama rais kasema ni gawio, then ni gawio!.

Haiwezekani rais wetu aseme kitu hiki halafu atokee mtu mwingine, ambishie rais!.

P.
Sarcasm: the use of irony to mock or to convey contempt.
 
Inaonekana Zitto yuko sahihi. Lakini hata kama ingekuwa ni gawio, kweli tunahitaji kufanya hafla za aina hii? Haitoshi hizo fedha kupelekwa kwenye akaunti za hazina kimya kimya, mbona administrations nne zilizotangulia hazikuwa zinafanya hivi. Yaani ni vituko, dramas na theatrics za kilimbukeni kabisa..kutafuta misifa ya kijinga!
 
Bora umetutoa tongo tongo maana wengine hatuelewi hata maana ya maduhuli au makufuli ni nini. Ah jamani mjinga ni wakati wa kwenda wakati wa kurudi...
 
Zitto anazidi kushuka, from bad to worse sasa sijui kafikia wapi. Sikiliza maelezo kwa makini.
Zitto umepoteza umakini siku hizi hata wa kusikiliza wa kuchambua sidhani kama upo kabisa.
 
Ha ha haaa huyu jamaa watamtafuta tu mana si kwa uwazi huu.
Wakurupukaji hapo wamesha amini kua bila jiwe haiwezekani kumbe ni mipango iliyo pangwa kabla
 
Back
Top Bottom