Zitto: Tunapata maduhuli na si "gawio"

Zitto: Tunapata maduhuli na si "gawio"

Methinks Zitto anajua anachozungumzia. Lakini ama kwa kutojua au kwa makusudi, kuna watu wameamua kupotosha umma kuwa mashirika yote hayo yametoa gawaio. Kama tcra, ewura, na executive agencies kama hizo nao wametoa 'gawio' basi ni ishara kwamba kuna upotoshwaji kiasi fulani hapa. Inawezekana kweli kuna mashirika yamefanya biashara kweli na kupata faida kiasi cha kutoa gawio lakini yaliyo mengi yasingeweza kutoa gawio kwa kwa maana ya gawio kweli. Ila kama ni tozo ya turnover yao basi hilo linaleta sense.
Point!
 
Pesa ina majina mengi, maduhuli, gawio, kodi...
 
Zitto ungekaa kimya pia ingependeza sanaa. Si kila jambo ulitolee tamko ni hekima na busara siku zote unapokuwa umenyamaza kuliko unapokuwa unazungumza.

Nawaombeni enyi mnaojiita wanasiasa kujitafakari wakati mwengine kwa michango yenu kama inaumuhimu wowote kwa maendeleo ya taifa au la.

Hivi mtu akiita gawiwo au mchango au pato au duhuli na akalitoa kwa mwenye hisa unapungukiwa na nini ukinyamaza kimya bila ya wewe usiye na kiasi hicho kuchangia kwa jamii?

Tuwe wastaarabu wakati mwengine badala ya kuwa washenzi na wenye kukosa adabu kwa matamko yasiyokuwa na tija kwa taifa letu.

Nimuulize zito na mnaomuunga mkono maelezo yake hapo juu yamesaidia nini kwa taifa ukilinganisha na shughuli iliyofanyika leo? Je tule maneno au fedha zilizochangiwa leo?

Ndugu,

Kuna tofauti kubwa kati ya maduhuli na gawio. Maduhuli hukatwa kwenye mapato ghafi kabla ya kutoa gharama yoyote ile. Gawio hutolewa baada ya kupata faida, baada ya kutoa matumizi na gharama za uendeshaji.

Shirika linapotoa sehemu ya mapato yake kabla ya kutoa gharama za uendeshaji (mishahara, kodi n.k.) na uwekezaji kuna hatari ya haya mashirika kushindwa kujiendesha na zaidi ya yote kutegemea ruzuku na mikopo zaidi. Kwa sasa hatari hii inaweza isionekane. Huko mbeleni yanaweza kufa na kubinafsishwa.

Pia, pesa zote za haya mashirika kwa sasa zipo Hazina na si benki binafsi. Mwanasiasa akizitaka ili kutimiza malengo yake ya kisiasa ni rahisi kuzichukua kwa kisingizio chochote kile (hili "gawio" ni mojawapo). Kuna mkurugenzi au mjumbe wa bodi wa kubisha? Wameambiwa watafukuzwa wasipoleta "gawio".

Tunafanya siasa kwa faida ya muda mfupi, mbeleni ni giza. Shirika linaishi kwa ruzuku leo linatoa "gawio". Vitu vingine ni aibu.

Bams JokaKuu Salary Slip
 
Ndugu,

Kuna tofauti kubwa kati ya madhuhuli na gawio. Madhuhuli hukatwa kwenye mapato ghafi kabla ya kutoa gharama yoyote ile. Gawio hutolewa baada ya kupata faida, baada ya kutoa matumizi na gharama za uendeshaji.

Shirika linapotoa sehemu ya mapato yake kabla ya kutoa gharama za uendeshaji (mishahara, kodi n.k.) na uwekezaji kuna hatari ya haya mashirika kushindwa kujiendesha na zaidi ya yote kutegemea ruzuku na mikopo zaidi. Kwa sasa hatari hii inaweza isionekane. Huko mbeleni yanaweza kufa na kubinafsishwa.

Pia, pesa zote za haya mashirika kwa sasa zipo Hazina na si benki binafsi. Mwanasiasa akizitaka ili kutimiza malengo yake ya kisiasa ni rahisi kuzichukua kwa kisingizio chochote kile (hili "gawio" ni mojawapo). Kuna mkurugenzi au mjumbe wa bodi wa kubisha? Wameambiwa watafukuzwa wasipoleta "gawio".

Tunafanya siasa kwa faida ya muda mfupi, mbeleni ni giza. Shirika linaishi kwa ruzuku leo linatoa "gawio". Vitu vingine ni aibu.

Bams JokaKuu Salary Slip
Huyu mtu hafai kuwa kiongozi hata kidogo.
 
Zitto ungekaa kimya pia ingependeza sanaa. Si kila jambo ulitolee tamko ni hekima na busara siku zote unapokuwa umenyamaza kuliko unapokuwa unazungumza.

Nawaombeni enyi mnaojiita wanasiasa kujitafakari wakati mwengine kwa michango yenu kama inaumuhimu wowote kwa maendeleo ya taifa au la.

Hivi mtu akiita gawiwo au mchango au pato au duhuli na akalitoa kwa mwenye hisa unapungukiwa na nini ukinyamaza kimya bila ya wewe usiye na kiasi hicho kuchangia kwa jamii?

Tuwe wastaarabu wakati mwengine badala ya kuwa washenzi na wenye kukosa adabu kwa matamko yasiyokuwa na tija kwa taifa letu.

Nimuulize zito na mnaomuunga mkono maelezo yake hapo juu yamesaidia nini kwa taifa ukilinganisha na shughuli iliyofanyika leo? Je tule maneno au fedha zilizochangiwa leo?[/QUOTE
Watu hawataki political milage anayofanya huyu mhutu, kuita gawio badala ya duhuli sasa aliebadilisha duhuli kia gawio lengo lake ni nini?
 
Na Zitto Kabwe
  1. Kwamba Mashirika ya umma nchini yanamkabidhi Rais cheki za magawio (dividends) ya faida zao
  2. ni ama Ofisi ya Rais inafanya Siasa au hawajui maana ya gawio.
  3. SIO FAIDA maana mashirika haya mengi hayana faida.
  4. Kusema Rais anakabidhiwa gawio la faida ya mashirika ya umma ni ulaghai ambao hauna maana yeyote.
  5. Taarifa za Ukaguzi za Mashirika hayo zitaonyesha kuwa hakuna faida (na hivyo hakuna gawio), na hivyo kuumbuka kwa Serikali yenyewe.
  6. Kinachotolewa ni nini? Haya ni maduhuli tu, ama ni kodi maalumu ambayo imewekwa kwa mashirika kwa kiwango cha 15% ya Mapato ghafi.
  7. Maduhuli au kodi hii imekuwa ikilipwa miaka yote ya nyuma. Sielewi ni kwanini sasa Rais amewaleta mbele wakuu wa mashirika Eti kutoa gawio!.
  8. Watanzania msihadaiwe leo, hatupokei gawio, bali tunapokea maduhuli tu.
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Julai 23, 2018.
Mkuu ZZK, nimezisoma hoja zako na kushauri
Zitto Zuberi Kabwe Ni Mchochezi, Akamatwe, Ashitakiwe Kwa Uchochezi, Adai Rais Magufuli ni...
  1. Kwa sisi ambao sio wachumi, any income ni profits, hivyo chochote ambacho serikali imepata mgao wake kutokana na income ya taasisi zake hivyo ni sahihi kabisa kuita gawio la mapato yao!.
  2. Maana ya gawio ni mgao na sio lazima dividends.
  3. Faida ni fedha yoyote unayoipata extra, hivyo kwa mgao huo, serikali imepata faida.
  4. Sii ulaghai, bali huo ndio ukweli wenyewe, gawio hilo ni faida kwa serikali.
  5. Hata kama hakuna faida, then gawio hilo ni mgao halali wa 15% ya serikali.
  6. Maadamu yameishawekwa kisheria, neno gawio hapa linamaanisha kile unachogawa, iwe ni mchango, mgawo, gawio, call it what you may, serikali imegaiwa, hivyo kilichopokelewa ni gawio la mgao wa serikali.
  7. Amewaleta ili Watanzania tuone, jinsi serikali yetu inavyofanya kazi, na amini usiamini, kuanzia mwaka huu wa fedha, kutakuwa na tukio la TRA kwa walipa kodi wakubwa nao pia watatangazwa na vyeti vya recognition wapewe!.
  8. Zitto usipotoshe, Watanzania hatuja danganywa, zile hundi ni za ukweli, ni gawio halali kwa serikali yetu na fedha hizo zote zimeingia mfuko mkuu hazina na nchi imepata pesa!.
P.
 
Zito utakula risasi sasa hivi....Mwenzio hataki hiivyo....anataka akisema gawio wote tuseme gawio....Kwa Lisu ilikuwa hivihivi, jamaa anataka aonekane anapiga kazi na kukusanya faida...ukimwambia ukweli tu risasi zinakuhusu....

Cha msingi we achana nae, akusanye gawio akusanye maduluhu atajua mwenyewe sisi hayatuhusu, Maana hata hela zenyewe ndo kwanza anatumia kujengea mahekalu huko chato na kununua mijidege ambayo haina faida.
Tutakuwa nchi ya ajabu na watu wa ajabu iwapo tutamwona mfalme akiwa uchi halafu wote tupige makofi kama mazuzu, na wala asitokee hata mmoja wetu wa kumweleza ukweli kuwa yu uchi. 'God forbid!!!'
 
Zitto umefafanua vyema.

Au kama wanasema ni gawio ebu tujue:

1. Serikali iliwekeza sh.ngap kama mtaji wa hayo mashirika na kwenye biashara gani?

2. Kwa gawio hilo je serikali imepata Return O n Inveatment (ROI) ya asilimia ngapi?

Achaneni na mpuuzi huyu apumbazane na wapuuzi wenzie!
 
Maduhuli ni "Revenue", Gawio ni "Dividend". Zote ni pesa lakini vianzo vyake ni tofauti. Mheshimiwa Zitto amefafanua kwenye bandiko lake!
Tena mie siiti Maduhuli, walichotoa mashirika ni Levy (tozo) na ndio maana ipo fixed kama percentage of their total collection. Ni aibu sana kwa mkuu kuita gawio, anaona raha sana kutaja hilo neno bila hata kujua maana yake
 
Back
Top Bottom