Zitto: Tunapata maduhuli na si "gawio"

Zitto: Tunapata maduhuli na si "gawio"

Mkuu Bobby, hizo ni stereo type tuu kuwa sio kila gawio lazima liwe dividends, neno gawio limetokana na neno gawa, serikali imegaiwa mgao wake wa fedha, hivyo fedha yoyote inayogaiwa ni gawio!, hata wewe ukiwagawiya watoto wako fedha za matumizi kwa viwango ulivyo wapangia, then fedha hizo ndilo gawio lao, wanao wanakuwa wamepata gawio lao la fedha za shule kutoka kwa baba yao.

P.
We jamaa aisee😀😀 kukumbusha neno gawio sio kwa fedha tuu, hata ukiwagawia watoto wako maandazi mawili na kitumbua kimoja, hili pia ni gawio.
 
Zitto nahisi hakusikiliza vizuri kakimbilia kuandika na kupotosha watu. Imesemwa wazi, kuna walio toa gawio hasa wenye muundo wa kampuni na shareholding structure mf. Kadco. Baada ya hapo ikatangazwa yanakuja mashirika yanayotoa maduhuri mf. Tcra, ewura na wengine. Tofauti imesemwa wazi kwa waliosikiliza na ikatajwa kuwa ni 15% ya mapato kulingana na sheria. Zitto hoja huna tena.
Tuna weza kuipata recording ya hiyo shughuli Mkuu? Maana wengine tuanaamini JF ni ya ma-GT, tuweke sawa tafadhali
 
Hii nchi ilipofikia kama wananchi hatuwezi kusimama kidete kupinga huu upuuzi wa Magufuli tutakuja kuletewa vitu vya ajabu
 
Asante Sana kwa ufafanuz alafu mwambieni huyu @Pascala Mayalla aache uchochez Wa kizembe sisi humu ni wasomi Kama kashndwa kuchambua kihoja akae kimya na Kama amelpwa azile tu hawez kuja na uzi Wa kizushi Kama ule "eti zitto ashtakiwe sjui watanzania wngne tuksoma Elimu waga inaenda wapi!!
 
Back
Top Bottom