Chama ni watu na Zitto ni miongoni mwa wanaokijenga Chama Cha Demokrasia na Maendeleo- Kusema anautaka urais hakibomoi chama. Mwentekiti na Katibu na Baraaza la Wazee watakuwepo kukikuza chama Zitto ataongoza Nchi kupitia CHADEMa tatizo liko wapi? Au kuna mtu mmesha muandaa kugombea urais 2015? The early the better tukuze emokrasia ndani ya chama. wajitokeze wanaotaka watangaze nia, tuwachuje mapema kama walikuwa na madhambi wapiga kura tujue. Mnaogopa chama kitasambaratika, hamjakomaa kupambana na misukosuko ya kisiasa? Lazima tutofautiane mawazo, fikra, mitazamo na hisia mwisho wa siku tukubaliane kukubaliana. MAMBO YA ZIDUMU FIKRA SAHIHI ZA MWENYEKITI HATUZITAKI.
Mkuu kama ulikuwa hujui fahamu sasa kwamba CDM inaye mgombea 2015.Ni shujaa na mpigania haki za wanyonge Dr Wilbrod Slaa.