Zitto: Sitagombea uongozi CHADEMA

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Zuberi Kabwe, amesema kuwa hana nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama chake katika Uchaguzi wa ndani wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.

Zitto aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na NIPASHE jijini Mbeya, alikokuwa amekwenda kuongeza nguvu katika kampeni za uchaguzi wa udiwani katika kata ya Kiwira wilayani Rungwe.

Alisema kuwa hana nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama hicho kwa sababu anaona timu ya sasa ya uongozi wa chama hicho inatosha na inafaa kuendelea kukiongoza kwa miaka mingine mitano ijayo.

"Sina interest (nia) na sifikirii kama nitagombea uongozi ndani ya chama katika uchaguzi wa ndani wa Chadema mwaka huu, naona timu iliyopo inatosha na inafaa kuendelea kukiongoza chama," alisema Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini.

Alisema ingawa katika uchaguzi uliopita alijitosa kuwania nafasi ya mwenyekiti wa chama hicho, lakini safari hii nafsi yake haimtumi kufanya hivyo kwa kuwa ana imani kuwa uongozi wa sasa unastahili kuendelea kuwa madarakani kwa manufaa na maslahi ya chama na Watanzania kwa ujumla.

Chanzo: Gazeti la Nipashe

UPDATE:
Kairudia kauli hii Juni 16, 2012 akiwa Iringa (M4C)
 
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Zuberi Kabwe, amesema kuwa hana nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama chake katika Uchaguzi wa ndani wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.

Gazeti la Nipashe.

Mmmh! Haya mahesabu mbona makali! Naweza kuyalinganisha na kauli mbiu ya uhuru wa miaka 50: Tumetubutu, tumeweza, na tunazidi kusonga mbele!
Tafakari yangu:
Kugombea uongozi ndani ya chama ni kujitengenezea mazingira ya kujichafua na hivyo kushindwa kutimiza azma ya kugombea urais ifikapo 2015.
Please correct me!
 
hili kundi ni hatari sana.chadema naona mnashindwa kulidhibiti
 
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Zuberi Kabwe, amesema kuwa hana nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama chake katika Uchaguzi wa ndani wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.

Zitto aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na NIPASHE jijini Mbeya, alikokuwa amekwenda kuongeza nguvu katika kampeni za uchaguzi wa udiwani katika kata ya Kiwira wilayani Rungwe.

Alisema kuwa hana nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama hicho kwa sababu anaona timu ya sasa ya uongozi wa chama hicho inatosha na inafaa kuendelea kukiongoza kwa miaka mingine mitano ijayo.

"Sina interest (nia) na sifikirii kama nitagombea uongozi ndani ya chama katika uchaguzi wa ndani wa Chadema mwaka huu, naona timu iliyopo inatosha na inafaa kuendelea kukiongoza chama," alisema Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini.

Alisema ingawa katika uchaguzi uliopita alijitosa kuwania nafasi ya mwenyekiti wa chama hicho, lakini safari hii nafsi yake haimtumi kufanya hivyo kwa kuwa ana imani kuwa uongozi wa sasa unastahili kuendelea kuwa madarakani kwa manufaa na maslahi ya chama na Watanzania kwa ujumla.
 
Lala salama Arumeru Mashariki, habari za uongozi ndani ya chama Zitto ni baadae.
 
Yeye tayari kashasema anautaka urais. Hivi vyeo vya chini tena vya kichama ni kujishusha hadhi.
I see!......kwahiyo unamshauri Jakaya Kikwete asigombee uenyekiti wa CCM mwaka huu maana ni kujishusha!!.....no wonder ndio maana ukaripoti kwamba ile meli iliyozama Nungwi imeonekana inaelea, kwa akili hizi hakuna la kushangaza.
 
na wewe unamuunga mkono?acha ujinga wewe

Kumuunga mkono kutokugombea uongozi Chadema au kuutaka Urais?

I see!......kwahiyo unamshauri Jakaya Kikwete asigombee uenyekiti wa CCM mwaka huu maana ni kujishusha!!.....no wonder ndio maana ukaripoti kwamba ile meli iliyozama Nungwi imeonekana inaelea, kwa akili hizi hakuna la kushangaza.

Kumbe Chadema sawa na CCM tuu eh?
 
hili kundi ni hatari sana.chadema naona mnashindwa kulidhibiti
Chadema haidhibiti watu kwa nguvu inadhibiti kisaikolojia hata kitendo cha Zitto kutogombea jua ameshadhibitiwa kisaikolojia. Kwa maana hiyo yeye na kundi lake lote wameshakubali uongozi wa Chadema hadi baada ya uchaguzi mkuu 2015.
 
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Zuberi Kabwe, amesema kuwa hana nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama chake katika Uchaguzi wa ndani wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.

Gazeti la Nipashe.

Uvivu wa kusoma na kuelewa. Umesoma hadi mwisho na kuelewa? Acha kukurupuka.
 
Zitto anajua kuwa Mbowe ni kichwa zas y alijaribu kupima urefu wa bahari kwa miguu but akagundua kwamba Mbowe ashikiki ni mtu mwenye msimamo na hana njaa, sasa anajaribu kupima moto wa slaa ngoja tumwache then atatupa jibu.
 
kwani kugombea urais mpaka uwe kiongozi wa chama?kugombea urais ni mbaya kuliko huo uongozi ndani ya cdm na kupunguza kura 2015.
 
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Zuberi Kabwe, amesema kuwa hana nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama chake katika Uchaguzi wa ndani wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.

Gazeti la Nipashe.
Ok, aghasante kwa taarifa, tutarudi kujadiri ishu zake baadaye ngoja tumalizane kwanza na Arumeru
 
Chadema haidhibiti watu kwa nguvu inadhibiti kisaikolojia hata kitendo cha Zitto kutogombea jua ameshadhibitiwa kisaikolojia. Kwa maana hiyo yeye na kundi lake lote wameshakubali uongozi wa Chadema hadi baada ya uchaguzi mkuu 2015.

mkuu hilo kundi haliaminiki.hapo kuna hesabu kali sana mwana.chadema watimueni tu hao
 
Uvivu wa kusoma na kuelewa. Umesoma hadi mwisho na kuelewa? Acha kukurupuka.
Hivi wewe una akili kwani hayo ni maneno yangu hata husomi source ya habari? mpuuzi kweli kweli.
 
Back
Top Bottom