Zitto: Sitagombea uongozi CHADEMA

Kila mwanachama wa chadema ana haki ya kugombea nafasi ya uongozi ndani ya chama, lakini halazimishwi, kama Zitto kasema hana nia ya kugombea uongozi atakuwa na sababu ya msingi yenye maslahi kwa chama, na hiyo sababu iheshimiwe.
 
napenda mtazamo wa Ipande na mtoa mada. chama cha siasa si mali ya mtu. Tulisikia mala nyingi ccm wakisema chama hicho kinawenyewe na matokeo yake leo tunayaona. nivyema viongozi wetu na wananchi wakaliona ili. kwamba uongozi wakupokezana na kujengeana uwezo ktk hilo ni muhimu. reference nzuri ni Nyerere na Mandela kwa upande watu afrika. Lakini pia ushauri wangu kwa chadema: viongozi wote wa chama wapimwe kwa uwezo wao na mapenzi ya kulitumikia taifa lao.

Leo hii najiuliza sana kuhusu uwezo(kiakili)na na jinsi (style) viongozi wetu wakubwa serikalini. mmoja wetu hapa jf husema 'hakili ndogo kuongoza hakili kubwa' . hili halikubaliki. Bilashaka katiba ya chama chama chadema na katiba inayokuja ya Tanzania vitakuwa na dira sahihi ya upatikanaji viongozi ktk taifa letu.

Mimi ni muumini wa Democrasia,kwahiyo sipingani na mawazo yako, pia naamini Mbowe ni moja ya viongozi mahiri sana hapa nchini, ambaye amekiongoza chama kwa mafanikio makubwa sana, na mimi naamini kwa kipindi hiki chama ambapo kinaelekea kujijenga kwa mtazamo wa kuchukua dola si vyema kubadili safu ya uongozi, itayumbisha chama na kukipitezea dira, maana kiongozi anayekuja anaweza kuja na maono tofauti na style tofauti ya uongozi chama kikapoteza momentam na kasi kilichokuwa nayo. Mbowe anajenga misingi ya chama ni nyema msingi ukawa imara hata wakija wengine wakaendeleza ujenzi kwa urahisi. Nyerere alitumia muda mwingi sana kuimarisha CCM, ndio maana viongozi waliofuta wameendelea kuogelea kwenye mafanikio ya Nyerere kwa muda, mpaka walipoharibu misingi wenyewe.
 
hana jipya.Madaia yake anautaka urais.Ila hii habari ya long time inamuelezea vizuri huyu jamaa.
Siri za Zitto nje

picture-4.jpg

Na Saed Kubenea - Imechapwa 09 December 2009

Mawasiliano yake yanaswaAponzwa na mwandishi wa habari


zitto_2.jpg



SIRI kubwa kuhusu mwenendo wa Zitto Kabwe (Mb) ndani ya chama chake zimeanikwa mitaani na zinaweza kumzamisha kisiasa, MwanaHALISI sasa linaweza kuripoti.
Siku nne baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Willibrod Slaa kusema wamenasa taarifa za mawasiliano ya Zitto, baadhi ya taarifa zimepatikana jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Zitto ananukuliwa akiapa kusaidia wagombea uongozi katika vyama vingine; na katika moja ya taarifa ananukuliwa akisema atasaidia David Kafulila kupata ubunge "hata kabla ya akina John Mnyika…"
Mnyika ni Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CHADEMA na Kafulila alikuwa Afisa Habari ambaye baada ya kuondolewa wadhifa huo amekimbilia NCCR-Mageuzi. Mnyika anatarajia kugombea ubunge jimbo la Ubungo.
Naye Zitto amenukuliwa na gazeti la Mwananchi la Jumatatu akilalamika kuwa ameingiliwa katika mawasiliano yake ya baruapepe (e-mail); jambo ambalo Mkurugenzi wa Upelelezi, Robert Manumba, amedakia haraka na kusema Zitto akiwapelekea malalamiko watashughulikia.
Kwa mujibu wa mpangilio wa taarifa husika, lazima aliyezitoa amepata ufunguo wa baruapepe (password) wa ama Zitto au mwandishi wa habari wa Mwananchi, Denis Msacky.
Karibu mawasiliano yote ni kati ya Zitto na Msacky juu ya "ushujaa" wa Zitto na jinsi anavyopendwa nje ya chama huku "akichukiwa" na viongozi wake wakuu.
Katika moja ya mawasiliano, inaonyeshwa kuwa Msacky alimwandikia Zitto akieleza, "Leo hii Mrema (Augustine Lyatonga) anasema anakuheshimu wewe, lakini si Mbowe; hivyo hivyo, Lipumba (Profesa Ibrahim) na James Mbatia wanasema wewe una visheni."
Katika mawasiliano hayo ya Jumanne, 1 Desemba 2009, saa 6.45 adhuhuri, Msacky anaonyeshwa kumwambia Zitto pia kuwa, "CCM nao…wanakusifu kwamba pamoja na kwamba unawaliza sana, lakini ni kiongozi shupavu."
"Leo hii siasa za CHADEMA zingekuwa zinatisha kama ungekuwa mwenyekiti wa CHADEMA, vijana nchi nzima wangejiunga na chama, uko nao karibu, unaongea nao, una elimu nzuri, unajua mambo, unasoma sana," imeeleza sehemu ya mawasiliano kutoka kwa Msacky kwenda kwa Zitto.
Kinacholeta wasiwasi ndani ya CHADEMA kinaweza kuwa lugha inayotumiwa katika mawasiliano hayo. Kwa mfano, katika waraka huohuo, Msacky ananukuliwa akiandika:
"Wanataka kukumaliza, nami sitakubali mtu ammalize rafiki yangu nikiangalia…wanasema Mbowe hata Mbatia akikaa vema anaweza kumpita kama siasa za kufukuza zitaendelea. Muhimu, usisikilize watu, tulia, urudi tupange tufanye nini? Lakini ukweli ni kwamba sasa wanakuogopa…Mwenyekiti Mtarajiwa…"
Mawasiliano yanaonyesha kuwa Zitto hakufurahishwa sana na taarifa za Mwananchi kuwa amemsaidia Kafulila magari matatu kwenda Kigoma kufanya kampeni chini ya NCCR-Mageuzi, lakini Msacky anaonyesha kumfariji.
"Kaka, mimi nimeiona story, haina matatizo zaidi ya kuwafanya akina Mbowe kusitisha mpango mbaya dhidi yako maana wanaanza kuogopa. Hata Mrema Lyatonga amesema kwamba Zitto huwa unamsaidia akiwa na shida. This shows that ur a leader katika opposition, wewe ni mtu wa maridhiano, unakuza upinzani Kigoma," anaeleza.
Anasema, "Leo nasikia akina Mnyika wanahaha sana, waambie familia yako wasiingie katika mtego wa kuanza kuhojiwa na akina Kubenea (Saed wa MwanaHALISI), watawachanganya. Wewe usiongee kitu chochote, wabaki wanahaha, lakini for sure you are safe, na hizo kampeni za Mnyika kukuchafua huku akitaja majina ya Kafulila, ataziacha."
Akionyesha juhudi za kushawishi, kuliwaza au kufarakanisha, Msacky anaandika, "Katika hili Zitto, mimi niko na wewe, huna kosa ambalo umefanya, na wala usihofu maana wewe utakuwa nguzo ya upinzani Tanzania…Wanakupa majina ya ajabu, wanakuita Mr Dowans, wanatumia akina Halima Mdee kukuchafua katika magazeti…"
Awali Zitto alikuwa amemwandikia Msacky akisema, "Stori niliyoiona kwenye mwananchi itaniletea matatizo sana." Hiyo ilikuwa Jumatatu 30 Novemba 2009, saa 5.21 asubuhi. Baruapepe hiyo ilikuwa na kichwa kisemacho: "Muhimu na haraka."
Aidha, katika mawasiliano mengine, Zitto anaendelea kuonyesha kutofurahishwa na taarifa juu ya magari matatu kwa safari ya Kafulila.
Naye anaandika kwa Msacky, "tatizo la stori ni wingi wa magari, itaonekana mimi nina magari mengi na ni fisadi unajua? Hilo ndio tatizo."
Saini ya Zitto inatofautiana katika baadhi ya baruapepe. Pengine anaandika "zitto" na kwingine anaandika "Zi."
Moja ya mawasiliano ambayo yanazua mashaka yanaonyesha Zitto akikiri kuwa na mawasiliano na waasi nchini Kongo akiandika, "take it from me (niamini), nina contacts nyingi sana Congo na hao rebels (waasi) huwa wananiomba sana ushauri na kutaka kuwaunganisha."
Katika moja ya mawasiliano, Msacky anamwonya Zitto kutotumia baruapepe ya "CHADEMA kwa mawasiliano ya siri" na kutaka amwambie mama yake Shida Salum akatae kuongea na waandishi wa habari. "…nasikia Mbowe anataka mama awe akiongea na waandishi, usikubali," alieleza.
Zitto alipoulizwa kuhusu taarifa ya Mwananchi kuwa anatembea na barua mfukoni ya kujiuzulu uanachama CHADEMA, alisema "Sina la kusema."
Alipong'ang'anizwa kwamba imekuwaje hawezi kuzungumzia suala hilo ambalo ni muhimu kwa mustakabali wake wa kisiasa kwa chama chake, Zitto alisema, "Ni kwa sababu sitaki kuingia katika malumbano na katibu mkuu wangu (Dk. Willibrod Slaa) kwani malumbano hayo hayataijenga CHADEMA."
Alipotakiwa kueleza juu ya baruapepe ambazo zinadaiwa kuwa mawasiliano kati yake na Msacky, haraka alijibu, "Sina la kusema."
Alipoelezwa umuhimu wa yeye kueleza msimamo wake juu ya baruapepe hizo, Zitto alijibu, "Chochote nitakachosema sasa hivi, kitawachanganya Watanzania.
"Sitaki malumbano. Hakuna sababu ya kuwachanganya Watanzania. Hiyo haina maana yoyote," alisema Zitto kwa sauti ya ukali. Zitto alikuwa akiongea kutoka Ujerumani kwa simu Na. +4915222493231.
MwanaHALISI ilimtafuta Msacky. Baada ya kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa, hatimaye aliandika ujumbe "Kaka, niko katika kikao. Tuma ujumbe."
Msacky aliulizwa, "Kaka, tumesikia kwamba umetajwa katika sakata la Zitto na chama chake na kwamba wewe ndiye mtibuaji. Je, ni kweli?" Hakujibu ujumbe na alipopigiwa simu ilikuwa inaita hadi kukatika.
Gazeti lilipowasiliana na Mnyika na kumueleza kwamba amekuwa akitajwa katika ujumbe wa Zitto na Msacky, alikiri kupokea ujumbe huo wa baruapepe uliotoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa ni "Mtanzania mwema."
Alisema alipoona ujumbe mmoja unahusu Zitto kushauri Msacky kutochapisha habari za mkutano wake na waandishi wa habari, ndipo aliamua kupeleka ujumbe huo kwa Zitto.
"Nilimuuliza kuna hiki kitu nimetumiwa. Je, haya ni maandishi yako au kuna mtu ameingilia emaili yako na kujiandikia haya? Hadi leo hii, bado sijapata jibu," alisema Mnyika kwa sauti ya masikitiko. Alisema yeye hana cha kusema na kuongeza, "labda umuulize Zitto."
Alipoulizwa anachukuliaje suala hilo, Mnyika alisema, "Ukiniuliza mimi kwa upande wangu, nilitegemea mambo hayo yangemalizwa katika vikao vya chama na si kwa vyombo vya habari. Lakini kwa hatua ya hivi sasa, nadhani Zitto bado anayo fursa ya kulieleza hili.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe alipoulizwa juu ya madai ya kuwapo njama za kuhujumu chama chake zinazofanywa na Msacky kwa kumtumia Zitto, haraka alijibu, "tuna utaratibu wetu wa kushungulikia mambo ndani ya CHADEMA."
Alisema, "Sina la kusema. CHADEMA ina utaratibu wake wa kushughulikia mambo yake."
Kwa kadri mawasiliano ya Zitto na Msacky yanavyoonyesha na iwapo yatathibitishwa kuwa kweli, jambo ambalo linaanza kuthibitishwa na Zitto kwa kulalamika kuingiliwa kwenye faragha, basi uhusiano wake katika chama utakuwa umepata nyufa.
Wachunguzi wa siasa za upinzani nchini wanasema kwa hali hii, uwezekano wa Zitto kubaki ndani ya chama chake ni mdogo. "Ama atajiondoa mwenyewe au hatimaye atafukuzwa," ameeleza mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Hata hivyo, Zitto amenukuliwa na Mwananchi akisema, "Sitaki kugombana na mtu mimi. Wala msiniweke kwenye kifungo cha siasa. Ni bora niishi huru kuliko katika mateso ya siasa za kipumbavu kabisa. Nitafanya maamuzi ambayo hayajawahi kufikiriwa."
Wiki iliyopita Kafulila aliwaambia waandishi wa habari kwamba Zitto atafanya maamuzi makubwa ambayo hawakutegemea.
SIMPLY THE RADICAL
 
hakuna kipya kwa zitto,zaidi ya yaliyoandikwa na mwanahalisi.Kijana yupo naive,katongozwa katongozeka,akili imewehuka kabisa.
 
hakuna kipya kwa zitto,zaidi ya yaliyoandikwa na mwanahalisi.Kijana yupo naive,katongozwa katongozeka,akili imewehuka kabisa.
Mwandishi wa Mwanhalisi ni Dr.slaa muulize Kwanini Mwanahalisi huwa ahaliandiki majumba anayomiliki mbowe dubai aliyonunua Desemba 20122 baad ya kupata fedha kwa kukiuzia chama magari mtumba
 
hana jipya.Madaia yake anautaka urais.Ila hii habari ya long time inamuelezea vizuri huyu jamaa.
Siri za Zitto nje

picture-4.jpg

Na Saed Kubenea - Imechapwa 09 December 2009

Mawasiliano yake yanaswaAponzwa na mwandishi wa habari


zitto_2.jpg



SIRI kubwa kuhusu mwenendo wa Zitto Kabwe (Mb) ndani ya chama chake zimeanikwa mitaani na zinaweza kumzamisha kisiasa, MwanaHALISI sasa linaweza kuripoti.
Siku nne baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Willibrod Slaa kusema wamenasa taarifa za mawasiliano ya Zitto, baadhi ya taarifa zimepatikana jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Zitto ananukuliwa akiapa kusaidia wagombea uongozi katika vyama vingine; na katika moja ya taarifa ananukuliwa akisema atasaidia David Kafulila kupata ubunge “hata kabla ya akina John Mnyika…”
Mnyika ni Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CHADEMA na Kafulila alikuwa Afisa Habari ambaye baada ya kuondolewa wadhifa huo amekimbilia NCCR-Mageuzi. Mnyika anatarajia kugombea ubunge jimbo la Ubungo.
Naye Zitto amenukuliwa na gazeti la Mwananchi la Jumatatu akilalamika kuwa ameingiliwa katika mawasiliano yake ya baruapepe (e-mail); jambo ambalo Mkurugenzi wa Upelelezi, Robert Manumba, amedakia haraka na kusema Zitto akiwapelekea malalamiko watashughulikia.
Kwa mujibu wa mpangilio wa taarifa husika, lazima aliyezitoa amepata ufunguo wa baruapepe (password) wa ama Zitto au mwandishi wa habari wa Mwananchi, Denis Msacky.
Karibu mawasiliano yote ni kati ya Zitto na Msacky juu ya “ushujaa” wa Zitto na jinsi anavyopendwa nje ya chama huku “akichukiwa” na viongozi wake wakuu.
Katika moja ya mawasiliano, inaonyeshwa kuwa Msacky alimwandikia Zitto akieleza, “Leo hii Mrema (Augustine Lyatonga) anasema anakuheshimu wewe, lakini si Mbowe; hivyo hivyo, Lipumba (Profesa Ibrahim) na James Mbatia wanasema wewe una visheni.”
Katika mawasiliano hayo ya Jumanne, 1 Desemba 2009, saa 6.45 adhuhuri, Msacky anaonyeshwa kumwambia Zitto pia kuwa, “CCM nao…wanakusifu kwamba pamoja na kwamba unawaliza sana, lakini ni kiongozi shupavu.”
“Leo hii siasa za CHADEMA zingekuwa zinatisha kama ungekuwa mwenyekiti wa CHADEMA, vijana nchi nzima wangejiunga na chama, uko nao karibu, unaongea nao, una elimu nzuri, unajua mambo, unasoma sana,” imeeleza sehemu ya mawasiliano kutoka kwa Msacky kwenda kwa Zitto.
Kinacholeta wasiwasi ndani ya CHADEMA kinaweza kuwa lugha inayotumiwa katika mawasiliano hayo. Kwa mfano, katika waraka huohuo, Msacky ananukuliwa akiandika:
“Wanataka kukumaliza, nami sitakubali mtu ammalize rafiki yangu nikiangalia…wanasema Mbowe hata Mbatia akikaa vema anaweza kumpita kama siasa za kufukuza zitaendelea. Muhimu, usisikilize watu, tulia, urudi tupange tufanye nini? Lakini ukweli ni kwamba sasa wanakuogopa…Mwenyekiti Mtarajiwa…”
Mawasiliano yanaonyesha kuwa Zitto hakufurahishwa sana na taarifa za Mwananchi kuwa amemsaidia Kafulila magari matatu kwenda Kigoma kufanya kampeni chini ya NCCR-Mageuzi, lakini Msacky anaonyesha kumfariji.
“Kaka, mimi nimeiona story, haina matatizo zaidi ya kuwafanya akina Mbowe kusitisha mpango mbaya dhidi yako maana wanaanza kuogopa. Hata Mrema Lyatonga amesema kwamba Zitto huwa unamsaidia akiwa na shida. This shows that ur a leader katika opposition, wewe ni mtu wa maridhiano, unakuza upinzani Kigoma,” anaeleza.
Anasema, “Leo nasikia akina Mnyika wanahaha sana, waambie familia yako wasiingie katika mtego wa kuanza kuhojiwa na akina Kubenea (Saed wa MwanaHALISI), watawachanganya. Wewe usiongee kitu chochote, wabaki wanahaha, lakini for sure you are safe, na hizo kampeni za Mnyika kukuchafua huku akitaja majina ya Kafulila, ataziacha.”
Akionyesha juhudi za kushawishi, kuliwaza au kufarakanisha, Msacky anaandika, “Katika hili Zitto, mimi niko na wewe, huna kosa ambalo umefanya, na wala usihofu maana wewe utakuwa nguzo ya upinzani Tanzania…Wanakupa majina ya ajabu, wanakuita Mr Dowans, wanatumia akina Halima Mdee kukuchafua katika magazeti…”
Awali Zitto alikuwa amemwandikia Msacky akisema, “Stori niliyoiona kwenye mwananchi itaniletea matatizo sana.” Hiyo ilikuwa Jumatatu 30 Novemba 2009, saa 5.21 asubuhi. Baruapepe hiyo ilikuwa na kichwa kisemacho: “Muhimu na haraka.”
Aidha, katika mawasiliano mengine, Zitto anaendelea kuonyesha kutofurahishwa na taarifa juu ya magari matatu kwa safari ya Kafulila.
Naye anaandika kwa Msacky, “tatizo la stori ni wingi wa magari, itaonekana mimi nina magari mengi na ni fisadi unajua? Hilo ndio tatizo.”
Saini ya Zitto inatofautiana katika baadhi ya baruapepe. Pengine anaandika “zitto” na kwingine anaandika “Zi.”
Moja ya mawasiliano ambayo yanazua mashaka yanaonyesha Zitto akikiri kuwa na mawasiliano na waasi nchini Kongo akiandika, “take it from me (niamini), nina contacts nyingi sana Congo na hao rebels (waasi) huwa wananiomba sana ushauri na kutaka kuwaunganisha.”
Katika moja ya mawasiliano, Msacky anamwonya Zitto kutotumia baruapepe ya “CHADEMA kwa mawasiliano ya siri” na kutaka amwambie mama yake Shida Salum akatae kuongea na waandishi wa habari. “…nasikia Mbowe anataka mama awe akiongea na waandishi, usikubali,” alieleza.
Zitto alipoulizwa kuhusu taarifa ya Mwananchi kuwa anatembea na barua mfukoni ya kujiuzulu uanachama CHADEMA, alisema “Sina la kusema.”
Alipong’ang’anizwa kwamba imekuwaje hawezi kuzungumzia suala hilo ambalo ni muhimu kwa mustakabali wake wa kisiasa kwa chama chake, Zitto alisema, “Ni kwa sababu sitaki kuingia katika malumbano na katibu mkuu wangu (Dk. Willibrod Slaa) kwani malumbano hayo hayataijenga CHADEMA.”
Alipotakiwa kueleza juu ya baruapepe ambazo zinadaiwa kuwa mawasiliano kati yake na Msacky, haraka alijibu, “Sina la kusema.”
Alipoelezwa umuhimu wa yeye kueleza msimamo wake juu ya baruapepe hizo, Zitto alijibu, “Chochote nitakachosema sasa hivi, kitawachanganya Watanzania.
“Sitaki malumbano. Hakuna sababu ya kuwachanganya Watanzania. Hiyo haina maana yoyote,” alisema Zitto kwa sauti ya ukali. Zitto alikuwa akiongea kutoka Ujerumani kwa simu Na. +4915222493231.
MwanaHALISI ilimtafuta Msacky. Baada ya kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa, hatimaye aliandika ujumbe “Kaka, niko katika kikao. Tuma ujumbe.”
Msacky aliulizwa, “Kaka, tumesikia kwamba umetajwa katika sakata la Zitto na chama chake na kwamba wewe ndiye mtibuaji. Je, ni kweli?” Hakujibu ujumbe na alipopigiwa simu ilikuwa inaita hadi kukatika.
Gazeti lilipowasiliana na Mnyika na kumueleza kwamba amekuwa akitajwa katika ujumbe wa Zitto na Msacky, alikiri kupokea ujumbe huo wa baruapepe uliotoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa ni “Mtanzania mwema.”
Alisema alipoona ujumbe mmoja unahusu Zitto kushauri Msacky kutochapisha habari za mkutano wake na waandishi wa habari, ndipo aliamua kupeleka ujumbe huo kwa Zitto.
“Nilimuuliza kuna hiki kitu nimetumiwa. Je, haya ni maandishi yako au kuna mtu ameingilia emaili yako na kujiandikia haya? Hadi leo hii, bado sijapata jibu,” alisema Mnyika kwa sauti ya masikitiko. Alisema yeye hana cha kusema na kuongeza, “labda umuulize Zitto.”
Alipoulizwa anachukuliaje suala hilo, Mnyika alisema, “Ukiniuliza mimi kwa upande wangu, nilitegemea mambo hayo yangemalizwa katika vikao vya chama na si kwa vyombo vya habari. Lakini kwa hatua ya hivi sasa, nadhani Zitto bado anayo fursa ya kulieleza hili.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe alipoulizwa juu ya madai ya kuwapo njama za kuhujumu chama chake zinazofanywa na Msacky kwa kumtumia Zitto, haraka alijibu, “tuna utaratibu wetu wa kushungulikia mambo ndani ya CHADEMA.”
Alisema, “Sina la kusema. CHADEMA ina utaratibu wake wa kushughulikia mambo yake.”
Kwa kadri mawasiliano ya Zitto na Msacky yanavyoonyesha na iwapo yatathibitishwa kuwa kweli, jambo ambalo linaanza kuthibitishwa na Zitto kwa kulalamika kuingiliwa kwenye faragha, basi uhusiano wake katika chama utakuwa umepata nyufa.
Wachunguzi wa siasa za upinzani nchini wanasema kwa hali hii, uwezekano wa Zitto kubaki ndani ya chama chake ni mdogo. “Ama atajiondoa mwenyewe au hatimaye atafukuzwa,” ameeleza mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Hata hivyo, Zitto amenukuliwa na Mwananchi akisema, “Sitaki kugombana na mtu mimi. Wala msiniweke kwenye kifungo cha siasa. Ni bora niishi huru kuliko katika mateso ya siasa za kipumbavu kabisa. Nitafanya maamuzi ambayo hayajawahi kufikiriwa.”
Wiki iliyopita Kafulila aliwaambia waandishi wa habari kwamba Zitto atafanya maamuzi makubwa ambayo hawakutegemea.
SIMPLY THE RADICAL

Hili gazeti na mwandishi wake wanaogopa sana Kasi ya Zitto,Ndio maana huwezi kuona Likiandika kuhusu vikao vya FREEMAN NA OTHUMAN NA NGONGOSEKE PALE ADA ESTATE,PIA HUWEZI KUONA LIKIANDIKA VIKAO VYA MAFICHONI VYA MBOWE NA JK .
LITAMWANDIKA ZITTO ILILIUZE,WAPATE MTAJI WA KUJENGEA NYUMBA YA DR.SLAA BUNJU
 
Kuna mawili either ataibuka kama mgombea binafsi ili kugawa kura za CDM au kubaki kama mbunge ili kusafisha Nyota for 2020
Ingawa wanasiasa hawaaminiki come 2015 anaweza badili msimamo na kusema wananchi wameniomba kugombea
 
Amesoma alama za nyakati hata angetaka uongozi hawezi pata!

Hahahaha hawezi kupita kwa sababu ile ni kampuni ya familia ya mzee Mtei,lakini subiria mbowe atakavyokiona cha moto uchaguzi wa chama mwakani.
Ndipo utakapo tambua Zitto ni mtu wa aina gani,Kijana huyu ni threat kwa CHADEMA KAMPUNI..anajua siasa,anajua kujitambua..Ndio maana kila siku mbowe anawaza namna ya kumaliza
 
kwa maoni yangu nafasi zibaki vile vile isipokuwa nafac ya zitto apewe henche

kwikwiwkiwkwiwkwiwi Nafasi ya tembo achukue digidigi,..Heche mtumishi na mfanyakazi wa mbowe analipwa mshahara amuandalie urais mwaka 2015.
heche na mdogo wake house boys wa mbowe...Mdogo wake(Mura) ndiye anayetumika kukusanya taarifa za umbea toka pande zote za dunia
 
hayo mawazo yako mazuri ila yawe baada ya 2015,mbowe abaki kuwa m/kiti,slaa abaki palepale,zito sijui tumweke wapi,labda nafasi ya zito tumpe heche

hiki ni chama cha mkwe,mtoto,na binamu wa mtei...kampuni iliyojizolea umaarufu tanzania.mwaka 2013 itamilikiwa na nguvuya umma i mean watanzania wote watakuwa na power ya kumiliki chama.

Chama kitatoka mikononi mwa wakoloni kwenda kwa watanzania wenye nacho
 
mbowe aendelee tu kuwa mwenyekiti mpaka chadema itakapoingia madarakani ila dr.slaa awe mgombea urais,mnyika awe katibu,zitto waziri wa mambo ya nje,lema waziri wa mambo ya ndani
unataka kugeuza chama al shabab?
Yaani lema achukue uongozi ndani ya chadema????ni dhahili chama kitakuwa kimefilsika ..mwizi wa pesa za m4c leo aongoze chama?
Mbowe agombee urais iliiweje?yaani unataka uturudishe 2005????

Ni bora chama hicho kisiwe na uongozi kuliko hao madikteta(wahujumu uchumi wa chama) wakapewa chama kwa mara nyingine
 
zitto anajua kuwa mbowe ni kichwa zas y alijaribu kupima urefu wa bahari kwa miguu but akagundua kwamba mbowe ashikiki ni mtu mwenye msimamo na hana njaa, sasa anajaribu kupima moto wa slaa ngoja tumwache then atatupa jibu.

mbowe ni kichwa sana,hata mm namuogopa si unajua aliacha kusoma uingereza akarudi kusitisha uhai wa chacha maige wangwe?
Mbowe ni mtoto wa mjini..si unajua amekiuzia chama maroli ya mitumba?
Mbowe ni zaidi ya mjanja si unaona navyomtumia dr.slaa na heche..sasa subiri umafia atakao wafanyia
 
Hili gazeti na mwandishi wake wanaogopa sana Kasi ya Zitto,Ndio maana huwezi kuona Likiandika kuhusu vikao vya FREEMAN NA OTHUMAN NA NGONGOSEKE PALE ADA ESTATE,PIA HUWEZI KUONA LIKIANDIKA VIKAO VYA MAFICHONI VYA MBOWE NA JK .
LITAMWANDIKA ZITTO ILILIUZE,WAPATE MTAJI WA KUJENGEA NYUMBA YA DR.SLAA BUNJU

Mbowe ni Kiongozi wa chama na anayo haki ya kuwa na background discussions na chama tawala ili kama kuna shemu wataona panaweza rekebishwa na wakafikia muafaka ndipo walete katika public.Otherwise anaweza vitumia vikao kumlegeza na kumfix dhaifu.Hata US wana hizo back ground discussions na China,Russia, Israel, Iran etc.Hii ni njia nyingine ya kuwafix wapinzani

Zitto anasema nini?Kwania chochote anachoweza ongea lazima kiwe na baraka za wakubwa zake.Ni utoto tuu na kutoelewa mambo huku kusoboka kwingi.

Mwanahalisi aamjengee Dr. Slaa Nyumba ya nini na asiwe kubenea?Zitto is doomed,anachokifanya ndicho hiki kimeandikwa long time.

Nimeweka thread mods wakaifuta within seconds.Nilitaka watu wa discuss hii mambo na anachofanya Zitto sasa.He is damn predictable.
 
chadema haidhibiti watu kwa nguvu inadhibiti kisaikolojia hata kitendo cha zitto kutogombea jua ameshadhibitiwa kisaikolojia. Kwa maana hiyo yeye na kundi lake lote wameshakubali uongozi wa chadema hadi baada ya uchaguzi mkuu 2015.
hii vita niya karne hadi hapo chadema huru itakapo patikana,ww na kundi lako endelea kujipa matumaini kwamba zitto kadhibitiwa wakaati ndio kwanza napakia risasi kichwani mwake,huku nyuma vijana wa kazi ndio wameshakunywa damu ya kufa kupota kupigania chadema huru..
Tunawasitikia akina dr.slaa na heche watumishi wa mwenyekiit..lini watajitambua????au njaa ndio kikwazo
 
Mbowe ni Kiongozi wa chama na anayo haki ya kuwa na background discussions na chama tawala ili kama kuna shemu wataona panaweza rekebishwa na wakafikia muafaka ndipo walete katika public.Otherwise anaweza vitumia vikao kumlegeza na kumfix dhaifu.Hata US wana hizo back ground discussions na China,Russia, Israel, Iran etc.Hii ni njia nyingine ya kuwafix wapinzani

Zitto anasema nini?Kwania chochote anachoweza ongea lazima kiwe na baraka za wakubwa zake.Ni utoto tuu na kutoelewa mambo huku kusoboka kwingi.

Mwanahalisi aamjengee Dr. Slaa Nyumba ya nini na asiwe kubenea?Zitto is doomed,anachokifanya ndicho hiki kimeandikwa long time.

Nimeweka thread mods wakaifuta within seconds.Nilitaka watu wa discuss hii mambo na anachofanya Zitto sasa.He is damn predictable.

mpigie mbowe muulize OTHUMAN Na NGONGOSEKE NI akina nani?ndipo uje na jibu hapa sio haya mapovu..w
 
mpigie mbowe muulize OTHUMAN Na NGONGOSEKE NI akina nani?ndipo uje na jibu hapa sio haya mapovu..w

Wa nini sasa?Mbona hujauliza na JK ni nani?Hata kama wangekuwa nyumba ndogo wake bado kama kiongozi wa chama ana mamlaka ya kuwakuta na kufikisha au kupokea ujumbe. Kwanini unamhofia Mbowe na usimhofie JK kuwa ni kibaraka wa CDM?Kakubalia mngapi ya CDM wakati magamba wote wakipiga kelele no?Bado hujamtetea ZZK ambaye hawezi kwenda sehemu bila kupata baraka za wakuu wake kichama.MBowe anaweza waarifu wengine na kwenda na akirudi andio unasikia taarifa kama za hujuma zilizopangwa na mengine.Kama 6 alitumiwa pamoja na office yake kufanya kazi ya CDM kwanini Jk ambaye mnyika alimwita dhaifu ashindikane?

hembufungua akili hiyo na kuongea vitu halisi.Zitto kaleta ninikwa chama katika safari na JK?
 
Makamanda wa Chadema wamekamilika na wako tayari kwa 2015.Tanzania yenye uchumi wa kati hiyoooooooooooo!!!
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom