Stoudemire
JF-Expert Member
- Mar 24, 2012
- 839
- 208
Kila mleta mada zitto , zitto hadi tumechoka sasa kama mnamfukuza kwenye chama chenu mfukuzeni tujue moja, si mna katiba ya chama?
- Nothing but majungu na empty theories nimeshindwa hata kuichambua neno kwa neno kwa sababu hamna hoja ila chuki tupu, naomba kusema hivi kama haya maneno ndio yanatakiwa kuwa a standard ya kua Rais wa Tanzania then ninawaomba wale wote mnaounga mkono mtoa mada hii mtuambie kwamba Zitto hawezi kuwa Rais bora kulinganisha na Mwinyi, Mkapa na Rais wa sasa kwa sababu wao wote wanatimiza ubora wa huu waraka ndio maana Tanzania tumeendela sana Zitto akiingia ataharibu maendeleo yetu tuliyoyapata na ma-Rais waliopita!
- I mean hizi chuki Wa-Tanzania tumejifunzia wapi we are very good na machuki yasiyo na hoja wala msingi, I mean li-article lirefu lakini ndani yake hewa tupu! Muandishi anajikanyaga kanyaga tu, pelekeni hizi chuki huko kwenye vyama venu msituletee kwenye Taifa, kuna a big progress ya Vijana na uongozi wa taifa letu, sasa msiharibu the pattern kwa sababu ya chuki zenu za binafsi huko kwenye vyama vyenu, Zitto ni just a symbol people sasa tuwe waangalifu na hii mijadala kwa sababu itaishia kuweka mandate kwa taifa kwamba vijana wote ni kama Zitto na wakati hana kosa lolote zaidi tu ya machuki machuki ya binafsi, I mean binadam anawezaje kuwa positive na maisha yake ya binafsi na machuki yote haya ya hii article in him? no wonder hili taifa tumekwama tumebakia chuki tupu1
Es!
kaka jibu basi una undugu na Nyerere baba wa taifa?Hehehee haya bwana!
YAANI MWAKA WA TAABU,halafu mke wake namtorosha pale hotelini ili achanganyikiwe zaidi.Padre alijua amesha MONOPOLIZE u candidate; lazima achanganyikiwe.. CHURCH keshaharibu, huku CDM vijana wamekuja juu. NICE MOVE ZK
Najua Mh.Zitto Kabwe hauna nia wala dhati ya kuwa raisi Tanzania..! hiyo ni moja ya mkakati wako na CCM kuimaliza CHADEMA huku ukishirikana na swahiba wako January Makamba..,siujui wemekupa shs.ngapi mheshimiwa au wamekuahidi cheo gani serikalini (mkuu wa wilaya,katibu CCM)..!
Lakini Jua Nguvu ya Umma Haichezewi..,wako wapi madiwani wa Arusha (watano) waliosaliti chama..,yuko wapi Walid Kabourou,yuko wapi Tambwe Hiza..yuko wapi Agustino Lyatonga Mrema, ingawa anapata pensheni ya ubunge lakini heshima hana kama zamani..!
Zitto Kabwe Watu wamekufa,kuteseka na kufungwa kuitetea CDM..,leo hii wewe unataka kukiuza CDM kwa bei chee...kumbuka ulipotoka Zitto..,hivi ungegombea ubunge CCM mwaka 2005 ungelipata hilo jimbo la kigoma Kaskazini..,wengeshakutosa zamani kwenye kura za Maoni..,CHADEMA wakakupokea leo unakiuza chama "KWELI SHUKRANI YA PUNDA NI MATEKE'' najua ni haki yako kikatiba kugombea uraisi lakini inaonyesha nia yako ni kuimaliza CHADEMA..!
Ni mapema sana jamani kumshutumu ZITTO, tusubiri, tusikie na kauli za SLAA na MBOWE ndipo tumshambulie. Tukumbuke kuwa anayo haki ya kugombea yeye kama mtanzania. Sidhani kama akifuata taratibu na chama kikamteua tutakuwa na cha kusema.
Lakini kusema kwa Kabwe kuhusu hamu yake ya kuwa rais ina ubaya gani? Kila mtu anayo ndoto yake, wengine hukaa kimya na ndoto zao na wengine huropoka hadharani. Hata aliyeko madarakani alikuwa na ndoto ya urais, ndio maana baba wa taifa alimnyamazisha baada ya kuona anasemasema kuutaka urais wakati huo baba wa taifa alishaona muda bado na kumbe ni kweli, si mnaona anachofanya sasa? Ni rafiki yake sana Kabwe, kwa hiyo akiukwaaa urais sitaona tofauti na aliyepo sasa, watabaki kulindana na kuhamasishana utundu wa kuchanga karata za kuiona siku inapita hata kama kwa mazingaombwe.
Kama alivyotumia haki yake kuongea Kabwe, huyo Yeriko naye katumia haki yake kutoa uchambuzi juu ya mambo yaliyoanikwa na Kabwe ili yachambuliwe kwa faida ya walaji ambao ni umma. Wabaya sio wanaoomba bali wabaya ni wale wawapao waombaji ambao wanaonekana wazi kwamba hawahitajiki kupewa sasa. Urais sio kuwa msomi ingawa inasaidia, lakini wapo wasomi wengi wanavurunda kila kukicha. Tusipendelee kusikia yale tunayoyataka tu, siasa ni pamoja na kuvumiliana kwa kusikia yanayotuumiza. Cha msingi ni kujenga hoja na kuhakikisha hoja yako yenye mshiko inapita.
Hayo maneno hapo juu kwenye Red ni nani kayasema?Nimekwambia ulete uthibitisho kwamba chama changu kiliniita usalama.Ni wapi ambako chama kiliniita usalama wa Taifa ?
Matola,
Kuwa mstaarabu na kwa muungwana ukikosea unaomba msamaha.
Halafu mimi sina uwezo wa kupelekesha mtu na ndiyo maana hata mimi napinga kupelekeshwa.Napenda demokrasia,uhuru wa mawazo sipendi utumwa wa fikra.Siabudu,sisujudii fikra mfu.Ningekuwa napenda hayo ningekuwa naongea lugha nyingine tofauti na hii ambayo najua nudhi watu wengi,siyo hapa JF tu.Ila sijenge hoja kwa matamanio au katika kufurahisha watu.Naangalia uhalisia na logic.Kwa hiyo kupelekesha watu huwa nina-discourage hiyo tabia.Naheshimu kila mwanadamu,naamini katika utu
Ati hunifahamu na wala sikufahamu? Kwani hili lina uhusiano gani na huu mjadala?Nimekuuliza maswali,ukashindwa kujadiliana kistaarabu na kuaanza kuita watu majina,je ningekujibu kwa stahili hiyo ingekuwaje? Tuwaache watu waamue ni nani ameenda personal au too low.....
Tuendelee na mjadala au utoe majibu ya maswali niliyokuuliza.Kuhusu ninaofanya nao kazi/siasa ni issue nyingine wanajua wao.Sihitaji unijue au nikufurahishe ndiyo niwe mwanasiasa/kiongozi au mtu mzuri kwenye jamii.
Kuhusu Zitto kumpigia kampeni mgombea wa NCCR-Mageuzi hilo ni tatizo? Kwani ni yeye tu aliyefanya hivyo?Hebu kuweni fair,tena NCCR-Mageuzi ni kambi ya Upinzani.Nikuulize swali lingine,Katika harakati za kambi ya upinzani Kijana David Kafulila aliungana na chadema kuibana CCM hadi wakatolewa nje ya ukumbi wa bunge.Je,kule Kyela ni nani aliyempigia kampeni Dr.Mwakyembe (CCM) ? Kama Zitto kufanya vile kwa NCCR-Mageuzi na ikageuka kosa je kwa aliyempigia/waliompigia kampeni Dr.Mwakyembe 9in regardless of conditionalities) hawakufanya kosa?
Je,kwenye issue yoyote/harakati za upinzani bungeni Dr.Mwakyembe ni lini aliwahi kuungana na CHADEMA kwenye movement yoyote ndani ya Bunge?
You talk too much kama kasuku, be short and precise unafikiri kuongea sana ndio utafuta uchafu wako.Nikikuuliza ni wapi wazee walisema Ben Saanane huna maadili utanijibu?Do credibility a favour na uje uthibitishe hilo.Tuache upotoshaji.
Matola,
Just as everyone is entitled to their opinion then everyone should be entitled to their own actions(good or bad).
Unajua ukitaka kuheshimika ni lazima pia uwe na nidhamu.Heshima na nidhamu ni two way traffic.
Kuhusu Mnyika,sina utamaduni wa kujadili watu kama unataka kujadili watu jadili mwenyewe.Mnyika ni kiongozi wangu,ni rafiki yangu tunaheshimiana.Kuhusu suala la vyeo mimi sipo hapa kujadili hilo kuna mamlaka ya uteuzi kawaulize maswala hayo
Kuhusua Alliance ndani ya chama,ni alliance ipi niliyoitetea? Nakiri uchaguzi wa BAVICHA nilifanya Alliance.Je hilo ni tatizo? kuna political theory yoyote inayokataza aliance?chama kinakataza makundi,ofcourse makundi si healthy kwa mustakabali wa chama..Na hilo naunga mkono.hakuna uchaguzi unaofanyika bila kuwa na makundi ila cha msingi ni jinsi ambavyo kila mmoaja anakuwa tayari kuvunja makundi baada ya uchaguzi
Nilipomaliza uchaguzi wa BAVICHA nilisema nitaendelea kutetea zoezi la demokrasia ndani ya chama changu.Kama ilivyo kwa mimi kutokuwa tayari kuona Dr.Slaa anazushiwa tuhuma za uongo au Kamanda mbowe ndivyo hivyo nitakavyopambana na upotoshaji unaofanywa dhidi ya kamanda Zitto na wanachadema wengine wa CHADEMA kwa ujumla.
Comrade Kimbunga,
I had thought that with more education and analytical thinking, our people would get past these narrow highly subjective conclusions about our reality. Unadhani baadhi ya watu hawajaelewa hili suala?wengine ndiyo hivyo hawewezi kuelewa lolote,na wengine wameelewa ila ni husda zao tu.Wengine wapo kazini.lol
Matola,
Kuhusu suala la kuwa Interested na zitto kuja hapa akueleze sijui nini siwezi kulijadili,atalijadili yeye mwenyewe.
Kwa hiyo suala la katiba kujadiliwa watu wanazuiwa kusema wanachoamini? Kweli hata katiba mpya itaandikwa hakuna mabadiliko yoyote kama tunafikia hatua kuchagulia watu marafiki na kitu cha kusema.
Tuna safari ndefu huko mbele.Guys,let us be matured,tatizo la hii hoja ni nini?mara wengine wanasema kuna uchaguzi Arumeru kwa hiyo timing ni mbaya.Nguvu zinazotumika ku-condemn hili kwa nini zisitumike kuelewesha watu kama unadhani hili lina athari kwenye hizi chaguzi?
Mwakalinga,
Well, Apologies if i don't paint out my wishes concisely.
Nikikuuliza ulete uthibitisho wa kukigawa chama,unaweza kuleta? Wanaonituhumu ?
You are basing all your accusation on a hearsay plus you jumped into conclusion. We'll damage ourselves before we can able to fix ourselves.
Bora umenipa benefit of doubt.Mara nganpi tumekosoana na kubishana sana hapa JF tangu niwe member 5 years ago na sijawahi kumkosea heshima yeyote anayenipinga kistaarabu? Akina Mugongo Mugongo,ACID,MTM,Field Marshal,Waberoya,Kimbunga,Kasheshe,Mwanakijiji,Mkandara na wengineo wengi watakushangaa sana kwa kauli hii ya kwamba ninaweza kuwa sikubali kukosolewa.
Nitasema kile ninachoamini na nitasimamia kile ninachoamini.Upotoshaji wowote utakaofanywa kwa maslahi ya wachache siwezi kuvumilia,siogopi kuchafuliwa na siogopi matusi wala vitisho.Ninachojali ni maslahi ya watanzania kupitia dira sahihi,najali maslahi ya vijana na nitapigania kwa gharama yoyote ile.Mkuu waangu pengine haupo ground kujua kinachoendelea,vijana wanatumika kama daraja la watu kisiasa.busara za viongozi wetu waliokuwa above 40 ndizo zilizozalisha hili bomu ambalo wanafiki wanajaribu kujifanya kwamba linawaumiza.Leo hii wanapita wanasiasa waliosababisha lindi la umaskini na wengine walioshindwa kuishinikiza serikali ilifanyie kazi tataizo la ajira kwa vijana leo hii wanalia machozi ya mamba.siwezi kucheka naoa
Umeongelea kuhusu kuheshimu mawazo ya wengine,huwa ninaheshimu mawazo ya wengine sana hasa wale ambao wanaonipinga.Wnaonipinga huwa ninawasikiliza zaidi,hata katika maisha yangu ya Uongozi vyuo vikuu na Eneo langu la kazi wanajua hivyo.Anayenipinga namsikiliza zaidi
Mkuu,kwa hiyo hata majukumu yake ya kamati ya hesabu za serikali na mashirika ya umma anayafanya kwa msukumo?suala la Posho anafanya kwa msukumo?
Field Marsha ES,
Bravo mkuu,Unajua tangu upotee na akina Mugongo mugongo jukwaa hili limepwaya sana .Wamebaki akina Mkandara,Mwanakijiji,na wakuu wengine wachache kutetea heshima ya JF kwa hoja.
Nashindwa kuelewa mtu anaposema fulani ana urafiki na Rostam sijui anamaanisha nini? Je,wanaofanya biashara na Rostam je? Kama una simu yenye laini ya VODA hufanyi biashara na Rostam?Mbona humfanyii Economic Embargo? Je ni Zitto pekee kwenye kambi ya upinzani mwenye urafiki na wana-CCM?
Nuclear1,
Naomba ulete uthibitisho wa hayo uliyoandika.Ongeza list kabisa Willy malecela,Baraka Kange,Makongoro Nyerere,Ole Millya,Julius Mtatiro,David kafulila na wengineo! Tujadili mada iliyoko mezani achana na personal vendatta na kuchafua majina ya watu.Kwa bahati mbaya sijengi hoja au kusimamia hoja katika kufurahisha watu.Usidhani kila mtu yuko kama wewe mkuu
Remove the hatred induced politics of Tanzania and misguided priorities.Throw away your "no victor, no vanquished" mantra. It does not exist in practise. Surely, it does not exist in the minds of CHADEMA elites
The problem with most guys including you is that they are selectively hypermetropic. They see only what they want to see and blank-out others from their view. You are assertions are just inflammatory. Well you have the right to your opinion but not to your facts.
In reality you think you are doing good and giving Opposition what they want but in reality you are just hurting the Opposition camp legacy and most importantly the CHADEMA name with you silly fact fixing games.
Never.......now i know him enough, nilidhani mlikuwa mnamuonea kumbe this is virus inside CHADEMA.You talk too much kama kasuku, be short and precise unafikiri kuongea sana ndio utafuta uchafu wako.
Wana jf hii nimeinasa kwenye blog iitwayo yerickonyerere.wordpress.com
Nimeshangaa kuona kumbe wengi wanamuogopa zito kiasi cha kusema sana.
25 Mar 2012
Tanzania ni nchi iliyo mithiri ya karia hivi leo na ni nchi yenye lasilimali adhimu duniani,
Jambo la kujiuliza ni je watanzania ni watu wa aina gani? wanaendana na Tanzania ilivyo?
Ukweli ni kuwa watanzania ni wanafiki wakutisha zaidi ya baraza la Sanhedrin, unafiki wetu unatisha kwakuwa umechanganyika na ujinga, Hatuendani kabisa na wasifu wa taifa, Jambo hili ni hatari kwa mstakabali wa taifa kwakuwa kati yetu wajinga na wanafiki kumeibuka kundi la wahuni
Wahuni hawa ambao mbegu yake ni ujinga na unafiki wamekuwa hatari kuliko kawaida, haimithiriki hata kuwatazama kwa jicho la makengeza tu.
Watu hawa wahuni, wanafiki na walanguzi wa fikra wamefanikiwa kuvunja mlango wa siasa za Tanzania na kujikita humo wakiliyumbisha taifa watakavyo, Wanatumia mwito wa utandawazi msonge kujidukiza kisiasa.
Ninavyoamini taifa halijengwi na mwanasiasa bali mwanasiasa ana nafasi kubwa ya kulivunja taifa! Sasa tukiacha siasa hizi za kinafiki zitamalaki ndani ya ardhi ya Tanzania, vitukuu wetu watakuja kuyachapa viboko makaburi yetu. Watanzania kila mmoja kwa imani yake turudi uwalii.
Nashangaa namna siasa za majitaka zilivyoshamiri, magazeti na wanaoitwa waandishi tegemezi nao hawana tofauti, magazeti yamejaa taarifa ambazo hazina msaada wowote kwa watanzania, hatusikii juu ya Mafuta yetu, juu ya dhahabu yetu, juu ya ardhi yetu, juu ya kilimo chetu, juu ya afya zetu, juu ya utamaduni wetu, juu ya tunu za taifa, juu ya mustakabali wa taifa na utaifa wetu.
Heshima yetu imepotea mbele ya walimwengu, utu na nafasi yetu imedharaulika, wengine wanatuamulia mambo yetu, Kenya imetutawala, imetuzuia kujenga barabara serengeti, tumefyata mkia, wazalendo mkowapi? wapiganaji mkowapi? Wenye nchi mkowapi? Arumeru ni kitu kidogo sana ndani nchi, mama zetu, baba zetu, dada zetu, kaka zetu, wadogo zetu vijijin wanalia hawana afya, magonjwa, njaa umasikini vimewazonga, tunafanya nini mijini? Ni hili la Pamela Lowassa, Siyoi Sumari, na Nassari?
Nashindwa kuelewa, nchi imebaki na Wasira tu? Nape? Ndio policymakers wetu? Mwigulu? Slaa? Zitto? Kweli jamani? Usalama wa Taifa mnabeba dhamana kubwa sana ndani na nje ya ya Tanzania, fanyeni kazi kwaajili ya taifa la leo na lakesho si kwa kikundi fulani wala chama furalani, rasilimali zetu zinatoroshwa na magenge mumiani laki taasisi hii ipo na inatajwa kuwa kila palipo na watu watano basi mmoja wao ni Usalama wa taifa, lakini kwanini hali iwe hivi?
Tutumie fikra machipuko kwa upinde wa kijana, japo kuwa vijana wengi wanaakili za kuku, lakini kwa sauti ya mangamuzi ya hekima watafunguliwa na kuacha utegemezi wa fikra,
Mimi ni muamini wa mtandao wa Twitter nikihudumu kwa njia ya @YerickoNyerere Niseme wazi, nimefadhaishwa na baadhi ya wanaoitwa wanasiasa vijana, hasa kijana mwenzangu mbunge wa Kigoma Kaskazini ndugu Zitto Zuberi Kabwe
Nimemtaja Zitto Kabwe kwakuwa anatumia ujinga na unafiki wa watanzania hasa vijana kujidukiza kisiasa kwa hoja dhaifu ya umri wa uraisi, na amefanikiwa kuteka mioyo ya wakware wa fikra kinyume na haki ya fikra huru.
Ukifuatitia vijana wengi wanaojadili na kuunga mkono juu ya hoja hiyo ya Umri wa Urais utabaini kuwa ni waumini wa upepo wa Zitto, Hawasemi faida ya hoja yao, wala hasara ya umri utumiwao kwa sasa, bali kwa jicho la tatu wamekuwa ni mashabiki wamuangaliao Zitto tu bila kujua mstakabali wa taifa lao.
Zitto ninamwamini sana kiutendaji ndani ya chama chake na nje ya chama, kupingwa kwa hoja yake hakutafsiriwi kuwa si kijana mtendakazi bora laa hasha, bali ni ashirio la kengele imwamshayo toka usingizini, tena usingizi wa ulevi mtawalia wa sifa za kisiasa.
Urais ni taasisi nyeti sana, tena hii ni nchi yoyote duniani huheshimu sana taasisi hii, Nimestushwa sana kuona kijana wetu Zitto aliyeonyesha dalili nzuri za kujengeka kisiasa na kiuongozi, akiwahi kuopoa nyama hata kabla ya kunawa mikono, anasema ndio ninautaka urais Hii ni kauli rahisi sana kisiasa lakini inabeba ujumbe wa aina mbili kwa mwanasiasa na raia wa kawaida.
Anawaarifu wanachama wake na wapambe wake kuwa uchaguzi ujao atagombea urais
Anawaonya viongozi wenzeke ndani ya chama kuwa yeye sasa ndiye lulu pekee ya urais.
Zitto bado hajafikia kuwa kiongozi wa juu zaidi kitaifa ndani ya chama chake achilia mbali kuwa rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Urais unahitaji hekima, Zitto hana kwa sasa, Urais unahitaji busara, Zitto hana kwa sasa, Urais ujasiri wa kweli Zitto hana kwa sasa,Urais unahitaji mtu wa kutafakuri, Zitto hana kwa sasa, Urais hauhitaji mtu mnafiki, Zitto kwa sasa ni mnafiki, Kwa ujumla Urais unahitaji mtu aliyepevuka, na Zitto bado hajapevuka.
Zitto anarubuniwa na kundi la wenye mtindio wa ubongo hasa vijana, wanaomuaminisha kuwa kapevuka na aweza kuongoza kizazi hiki cha nyoka ilihali bado safari yake ni ndefu.
Nimsihi kijana mwenzangu Zitto Kabwe, kuwa ni kweli anautaka urais lakini avute subira na kauli yake imeweka kovu ktk safari yake kisiasa, ambapo atumie muda uliopo kuliziba kovu hili. Ajitahidi kuwa na kifua kigumu chenye kuhifadhi magumu ya kisiasa, Si kila hoja imuhusuyo ni lazima aijibu na akiamua kujibu awatumie washauri wa masuala ya kisiasa.
Turekebishane ili kujenga taifa lenye uchumi imara, demokrasia imara, na siasa safi!
Mungu ibariki Tanzania mungu ibariki afrika!
Zitto ni mwanasiasa mzuri lakini not katika level ya uraisi,hawezi na hata kura hawezi kupata,nani wa kumpa kura.Pia ni mroho wa madaraka na kale katabia ka kimkoa anako sana,ni mnafiki mzuri tu na opportunist lakini hautambua vizuri uwezo wake.Pia kwa tunao mjua afya yake ni questionable
Najua Mh.Zitto Kabwe hauna nia wala dhati ya kuwa raisi Tanzania..! hiyo ni moja ya mkakati wako na CCM kuimaliza CHADEMA huku ukishirikana na swahiba wako January Makamba..,siujui wemekupa shs.ngapi mheshimiwa au wamekuahidi cheo gani serikalini (mkuu wa wilaya,katibu CCM)..!
Lakini Jua Nguvu ya Umma Haichezewi..,wako wapi madiwani wa Arusha (watano) waliosaliti chama..,yuko wapi Walid Kabourou,yuko wapi Tambwe Hiza..yuko wapi Agustino Lyatonga Mrema, ingawa anapata pensheni ya ubunge lakini heshima hana kama zamani..!
Zitto Kabwe Watu wamekufa,kuteseka na kufungwa kuitetea CDM..,leo hii wewe unataka kukiuza CDM kwa bei chee...kumbuka ulipotoka Zitto..,hivi ungegombea ubunge CCM mwaka 2005 ungelipata hilo jimbo la kigoma Kaskazini..,wengeshakutosa zamani kwenye kura za Maoni..,CHADEMA wakakupokea leo unakiuza chama "KWELI SHUKRANI YA PUNDA NI MATEKE'' najua ni haki yako kikatiba kugombea uraisi lakini inaonyesha nia yako ni kuimaliza CHADEMA..!
Zitto Kabwe, muda wa kutangaza nia sio huu!
Tofautisha upayukaji na utoaji wewe, sana sana mnataka kusema hii ndo style na level ya CHADEMA kusimamia mamboyakeHivi wewe ni mtu wa aina gani?hivi kusema anautaka uraisi tu imekuwa nongwa? basi hiki Chama ni noumer!!kwa hiyo si ruhusa kutoa maoni ndani ya chama midomo yote inafungwa ila midomo miwili au mitatu ndiyo inaruhusiwa kusema? kama ni hivyo kazi ipo na sijui kama kuna dhamira ya kweli.Wacheni kukandamiza demokrasia.