Zitto: Ndio ninautaka urais

Zitto: Ndio ninautaka urais

Status
Not open for further replies.
Unajuwa kuna unafki mwingine mimi huwa sielewi unatokea wapi au mmejifunzia chuo gani kuwa wanafki, naomba hapa mnijibu kuanzia wewe na huyo @New York, ni lini nafasi ya uenyekiti wa CCM ngazi ya Taifa fomu za kugombea zilichukuliwa na zaidi ya mgombea mmoja? je hivi wakati Mohamed Gharib Bilal anataka kugombea Urais wa Zanziba dhidi ya Karume ni demokrasia gani waliyoitumia CCM?

Je mnakumbuka Shibuda alipotaka kugombea Urais na Kikwete ni kitu gani kilichomtokea? sasa nadhani ni muda muafaka wa Edward Lowasa kuwa Mwenyekiti wa CCM na Jakaya Kikwete abaki na Urais wake ili tukomaze demokrasia kwa vyama vyote.
Hadithi ni zile zile. kwanini umeiba kuku,......... jibu, mbona fulani kaiba ng'ombe,.............
CCM wanautaratibu wao tuliouchoka na uliotufiksha hapa tulipo, sasa je CDM nao wanafuata utaratibu huo huo
Ndio maana naamini Tz hakuna mkombozi wote wasanii tu
 
Hadithi ni zile zile. kwanini umeiba kuku,......... jibu, mbona fulani kaiba ng'ombe,.............
CCM wanautaratibu wao tuliouchoka na uliotufiksha hapa tulipo, sasa je CDM nao wanafuata utaratibu huo huo
Ndio maana naamini Tz hakuna mkombozi wote wasanii tu
Asante kwaheri....... heri mimi sijasema kwamba akina Zitto Kabwe ni wasanii tu!!
 
Hii ni mind game. Iko kitu ingine hapa na wala sii urais. Wa TZ kaeni chonjo!.
 
Kwanza ni zamu ya Wakristo. So long as Zitto ni mjahidina asubiri mpaka 2025

Nelsweeter,
Acha uvivu wa kufikiri,usikurupuke kujibu mambo ambayo hujui msingi wake. Unaposema ni zamu ya Wakristo,una-refer katiba ya nchi gani au chama gani,CCM,CDM,CUF..??Kwamba kama zamu hii katawala Muislam basi next time atawale mkristo?..BTW,unajua maana ya Mujahidina au unaropoka tu! Jibu hoja na sio kum-attack Zitto!
 
If wishes were horses even beggars would ride horses. Yericho endelea kuwaumbua
 
Ni Obvious Dr Slaa now yuko kwenye take off stage,Zitto anafaa lakini sio kwa sasa,Asubiri.Hata Zitto hajafanya kosa jamani.Amesema endapo chama chake kitamwona anafaa,na kama atapendekezwa mwanachama mwingine atamuunga mkono.Zitto yuko sahihi.Hata hivyo hatuwezi kumlinganisha na dakratr slaa kwa sababu daktari hajawahi kuthubutu kusema atagombea.

Kasoro ya zitto ni kuwa mbinafsi,anadhani kwamba he can fight the war alone.Kosa kubwa alilofanya la kuhamisha attention ya Chama kule Arumeru na kumjia yeye ,hajafanya timing ya kutoa makala yake,namfananisha na TUNTEMEKE.Always huwa hashirikiani na harakati za chama chake,Hakuna maandamano Zitto ameshiriki.ANASIFIWA NA WATU WA CCM,Kweli kweli jamani hata kama ni wewe adui yako anakusifia ,huoni kasoro hapo? Dr Slaa anashsmbuliwa kutwa kuchwa,huyu ni mpinzani sahihi.
 
Nashangaa namna siasa za majitaka zilivyoshamiri, magazeti na wanaoitwa waandishi tegemezi nao hawana tofauti, magazeti yamejaa taarifa ambazo hazina msaada wowote kwa watanzania, hatusikii juu ya Mafuta yetu, juu ya dhahabu yetu, juu ya ardhi yetu, juu ya kilimo chetu, juu ya afya zetu, juu ya utamaduni wetu, juu ya tunu za taifa, juu ya mustakabali wa taifa na utaifa wetu.

Mwandishi katika habari uliyoileta nimeikubali hii paragraph, huko kwingine :hand::hand:

Holy c.r.a.p!!!!

He was saying his dreams!!! He even said if his party will ALLOW HIM!!! if not he will support any one endorsed by his party!! WHATS WRONG WITH THAT???

Mkuu Wabs! nakubaliana na wewe, watanzania tumekuwa na uvivu wa kufikirisha akili zetu...

 
Hadithi ni zile zile. kwanini umeiba kuku,......... jibu, mbona fulani kaiba ng'ombe,.............
CCM wanautaratibu wao tuliouchoka na uliotufiksha hapa tulipo, sasa je CDM nao wanafuata utaratibu huo huo
Ndio maana naamini Tz hakuna mkombozi wote wasanii tu

Mkuu mimi siku zote huwa nashangaa na najiuliza maswali mengi tu mojawapo likiwa hili: CDM wanasema ni chama mbadala wa CCM lakini kila kitu wanataka kujilinganisha na CCM; huo ubadala utatoka wapi sasa? Bilal alikataliwa kugombea basi na Zitto akataliwe! Shibuda alikataliwa basi hakuna mtu wa kuchukua form dhidi ya Dr. Slaa; heee jamani tunataka chama mbadala chenye mitazamo tofauti kabisa na CCM na siyo chama ninachojilinganisha na ku copy ubaya wa CCM. Afadhali kingekuwa kina copy mazuri ya CCm lakini chenyewe kinacopy mabaya tuuuuu! Nashindwa kuona tofauti hapo.
 
Hatimaye sasa nimejiridhisha pasipo na shaka ni kwa nini zitto Kabwe ni swahiba mkubwa wa Deputy Director wa Usalama wa Taifa ndugu Jacky Nzoka, Zitto aje hapa kuuelezea umma wa JF ni sababu zipi za msingi zilizokuwa zinamfanya awe na mawasiliano ya mara kwa mara wakati chama chake kiko katika uchaguzi mkuu na Idara ya usalama wa Taifa ndiyo ilikuwa inaihujumu CHADEMA? hapa sitalajii jibu rahisi kwa swali gumu.

Pili Ben Saanane nimekuwa nikifuatilia mabandiko yako kwa makini sana na kuna kipindi nilidhani huwa unaonewa, kumbe nilikuwa najidanganya, humu jamvini umejipambanuwa kwamba wewe ndio unayejuwa siasa na yeyote ambaye atakuwa kinyume na mtazamo wako basi wewe utambatiza kila aina ya jina mara mnafki mara hivi mara vile, kumbe sasa nimejiridhisha ni kweli chama chako kiliposema huna maadili hakuna walipokuwa wamekosea, kwa nini unatetea Alliance ndani ya chama? narudia kukwambia tena jifunze kwa John Mnyika, yule kijana anaaminika machoni pa watu kwa sababu he is humbled,......jiulize ni kwa nini kijana mmoja Mnyika alundikiwe vyeo na nyinyi wasomi mpo? endelea na Alliance. zako.

Nikikuuliza ni wapi wazee walisema Ben Saanane huna maadili utanijibu?Do credibility a favour na uje uthibitishe hilo.Tuache upotoshaji.

Matola,
Just as everyone is entitled to their opinion then everyone should be entitled to their own actions(good or bad).
Unajua ukitaka kuheshimika ni lazima pia uwe na nidhamu.Heshima na nidhamu ni two way traffic.
Kuhusu Mnyika,sina utamaduni wa kujadili watu kama unataka kujadili watu jadili mwenyewe.Mnyika ni kiongozi wangu,ni rafiki yangu tunaheshimiana.Kuhusu suala la vyeo mimi sipo hapa kujadili hilo kuna mamlaka ya uteuzi kawaulize maswala hayo

Kuhusua Alliance ndani ya chama,ni alliance ipi niliyoitetea? Nakiri uchaguzi wa BAVICHA nilifanya Alliance.Je hilo ni tatizo? kuna political theory yoyote inayokataza aliance?chama kinakataza makundi,ofcourse makundi si healthy kwa mustakabali wa chama..Na hilo naunga mkono.hakuna uchaguzi unaofanyika bila kuwa na makundi ila cha msingi ni jinsi ambavyo kila mmoaja anakuwa tayari kuvunja makundi baada ya uchaguzi

Nilipomaliza uchaguzi wa BAVICHA nilisema nitaendelea kutetea zoezi la demokrasia ndani ya chama changu.Kama ilivyo kwa mimi kutokuwa tayari kuona Dr.Slaa anazushiwa tuhuma za uongo au Kamanda mbowe ndivyo hivyo nitakavyopambana na upotoshaji unaofanywa dhidi ya kamanda Zitto na wanachadema wengine wa CHADEMA kwa ujumla.


Mkuu mimi huwa sina mahaba na mtu; mimi huwa nina mahaba na hoja zinazopalilia demokrasia kuanzia kwenye vyama vya siasa ili kustawisha demokrasia ndani ya nchi.

Kama CCM na vibaraka wake wanampenda mimi sijui labda unisaidie hizo sababu labda ndizo zinakufanya useme hana sifa.

Ninachokipinga ni kwamba Zitto hana sifa. Mimi najua kwamba ana sifa za kikatiba (ukiachilia hiyo ya umri) ambayo yeye mwenyewe ameisema vizuri tu kwamba kama Katiba itakuwa imeruhusu. Sasa Mkuu wewe unasema hana sifa ila husemi hana sifa kwa vipi? Hapo ndipo nashindwa kukuelewa.

Comrade Kimbunga,

I had thought that with more education and analytical thinking, our people would get past these narrow highly subjective conclusions about our reality. Unadhani baadhi ya watu hawajaelewa hili suala?wengine ndiyo hivyo hawewezi kuelewa lolote,na wengine wameelewa ila ni husda zao tu.Wengine wapo kazini.lol

Ndipo hoja ya umri hapa inapopata nguvu zaidi, yaani tupo kwenye mchakato wa Katiba ya Wananchi na ni sisi Wananchi ndio tutakaosema tunataka katiba gani halafu anatakoa mtu mwenye uchu na ulevi wa madaraka na kuanzisha mijadala ambayo haina tija!...nadhani kwa mtu mzima mwenye busara za kutosha hawezi kufanya hivyo na hapa hoja ya umri inazidi kupata nguvu kwamba miaka 35 BIG NO.

Niko interested sana Zitto aje hapa kutoa maelezo ni nini kinaendelea kati yake na Deputy Director wa Idara ya Usalama wa Taifa. hapa ninajuwa ninachokisimamia na ninachoamini, na tukienda mbali zaidi nasikitika kuwajulisha mashabiki wake msishangae Zitto akikataliwa Ubunge jimboni kwake mwaka 2015 katika masanduku ya kura.
Zitto Kabwe ndiye mbunge pekee ambaye alitaka kugombea Ubunge kwenye majimbo matano tofauti kwenye uchaguzi wa 2010, na alipogombea kwao Kigoma Ushindi wake ulipungua kura alizopata kufananisha na zile za mwaka 2000.

Matola,
Kuhusu suala la kuwa Interested na zitto kuja hapa akueleze sijui nini siwezi kulijadili,atalijadili yeye mwenyewe.

Kwa hiyo suala la katiba kujadiliwa watu wanazuiwa kusema wanachoamini? Kweli hata katiba mpya itaandikwa hakuna mabadiliko yoyote kama tunafikia hatua kuchagulia watu marafiki na kitu cha kusema.

Tuna safari ndefu huko mbele.Guys,let us be matured,tatizo la hii hoja ni nini?mara wengine wanasema kuna uchaguzi Arumeru kwa hiyo timing ni mbaya.Nguvu zinazotumika ku-condemn hili kwa nini zisitumike kuelewesha watu kama unadhani hili lina athari kwenye hizi chaguzi?

Kwa ushauri wa bure epuka sana hizi siasa zenye mlengo wa kugawa watu.Nadhani kwa nilivyofuatilia mjadala huu na hao wanaokutuhumu kuwa wewe unashirikiana na Zitto katika hiyo mipango yenu mnaoijua wenyewe soon itafumuka na mtaabika vibaya sana.Hawa wanaojadili humu na kutokumuunga mkono Zitto sio kwamba hawamkubali ama sio wafuasi/wanachama/wapenzi wa chadema,la hasha! hawa ni watu wanajadili kwa kina athari za maamuzi ya kamanda wao kimtazamo zaidi.

Napata shaka kuwa na wewe ni mmoja wa wanasiasa ambao hawataki kukosolewa.Napenda kukushauri upitie hoja za watu wote walioonyesha kumpinga Zitto kwa hili alilotamka kisha uyachambue ,kwa kuwa ni rafiki yako wa karibu sana umpe machache kama changamoto.Wanadamu tunatofautiana na kila mmoja anamapungufu yake ,suala la msingi ni kuheshimu mawazo na mitazamo ya watu kuhusu mapungufu yako.Hii inasaidia mtu kujijenga na kuimarika kimtazamo,hata katika kuchangia na kutetea hoja.

Mimi ni mmoja kati ya watu wanapinga kauli hii ya Zitto ya sasa ,lakini si kwamba napingana na mitazamo/hoja zake zenye malengo ya kutuondoa katika dimbwi la umasikini -kwa kutuonyesha njia na mwelekeo thabiti wa kimapinduzi.

Mwakalinga,

Well, Apologies if i don't paint out my wishes concisely.

Nikikuuliza ulete uthibitisho wa kukigawa chama,unaweza kuleta? Wanaonituhumu ?

You are basing all your accusation on a hearsay plus you jumped into conclusion. We'll damage ourselves before we can able to fix ourselves.

Bora umenipa benefit of doubt.Mara nganpi tumekosoana na kubishana sana hapa JF tangu niwe member 5 years ago na sijawahi kumkosea heshima yeyote anayenipinga kistaarabu? Akina Mugongo Mugongo,ACID,MTM,Field Marshal,Waberoya,Kimbunga,Kasheshe,Mwanakijiji,Mkandara na wengineo wengi watakushangaa sana kwa kauli hii ya kwamba ninaweza kuwa sikubali kukosolewa.

Nitasema kile ninachoamini na nitasimamia kile ninachoamini.Upotoshaji wowote utakaofanywa kwa maslahi ya wachache siwezi kuvumilia,siogopi kuchafuliwa na siogopi matusi wala vitisho.Ninachojali ni maslahi ya watanzania kupitia dira sahihi,najali maslahi ya vijana na nitapigania kwa gharama yoyote ile.Mkuu waangu pengine haupo ground kujua kinachoendelea,vijana wanatumika kama daraja la watu kisiasa.busara za viongozi wetu waliokuwa above 40 ndizo zilizozalisha hili bomu ambalo wanafiki wanajaribu kujifanya kwamba linawaumiza.Leo hii wanapita wanasiasa waliosababisha lindi la umaskini na wengine walioshindwa kuishinikiza serikali ilifanyie kazi tataizo la ajira kwa vijana leo hii wanalia machozi ya mamba.siwezi kucheka naoa

Umeongelea kuhusu kuheshimu mawazo ya wengine,huwa ninaheshimu mawazo ya wengine sana hasa wale ambao wanaonipinga.Wnaonipinga huwa ninawasikiliza zaidi,hata katika maisha yangu ya Uongozi vyuo vikuu na Eneo langu la kazi wanajua hivyo.Anayenipinga namsikiliza zaidi

Kwa dhamira ya moyo wangu kabisa, SIAMINI KAMA ZITO ANAWEZA KUWA HATA WAZIRI MKUU ACHILIA MBALI KUWA RAIS. Namwona ni mtu anayependa sana madaraka, Umwenyekiti wa CHADEMA anataka yeye, uongozi wa kambi ya upinzani bungeni anataka yeye, kila nafasi kubwa ya kiuongozi anataka yeye. Watu wa namna hiyo ni wa kuwaogopa sana, watu wa namna hiyo wakiupata uongozi huwa ni ving'ang'anizi sana maana wakati wote hawapendi kuishi au kufanya kazi chini ya mtu mwingine. Zito anafanya mambo mengi mazuri lakini yenye msukumo wa hila wa nia ya kujijenga ili aweze kuyapata madaraka makubwa. Ninafahamu kuwa viongozi wa CHADEMA wanalijua hilo lakini ni wenye busara na wanamwacha mpaka siku ile ambapo Watanzania wengi watamjua Zito ni nani na ni mtu wa namna gani. Zito anasumbuliwa sana na fikra kuwa yeye ni mtu maarufu sana na anafahamu sana. Haiwezi kuingia akilini, mtu mwenye fikra zilizotulia anafikia kutaka kuacha jimbo lake eti akagombee ubunge jimbo la Geita au Kahama, kwa sababu gani? Na wananchi wa Kigoma walimtendea wema sana kumpa hizo kura kwa kitendo alichowafanyia, na ninaamini aliupata ushindi wa ubunge kwa vile JK alitaka ashinde, na ndiyo maana JK alienda majimbo yote ya Kigoma kupiga kampeni lakini hakwenda jimboni kwa Zito.
ZITO FOR PRESIDENCY, A BIG NO. Ana haki ya kugombea kama mtanzania mwingine yeyote lakini kupewa dhamana hiyo, siungi mkono. Ninaamini leo kama kukitokea chama chochote cha siasa, iwe CCM, CUF, TLP, PPT Maendeleo, n.k. ambacho kingeweza kumhakikishia Zito kuupata Urais, ni lazima angeenda huko. Kwake kilicho muhimu ni Urais wala siyo itikadi ya chama. Ni nia hii ya Zito ndiyo inayomfanya asitulie sana, mara yupo karibu na naibu mkurugenzi wa usalama wa Taifa, mara anafanya mikutano na akina RA, hii yote ni kwa sababu hajui ni nani na ni chama gani kitakachomhakikishia kuupata urais. WATU WA NAMNA HIYO NI WA KUWAOGOPA SANA KATIKA NAFASI KUBWA KAMA YA URAIS. Sina chuki wala ugomvi na Zito, nafurahia uwezo wake wa kujenga hoja na kufuatilia lakini sina imani na dhamira yake, na hii wakati fulani huwa ni hulka

Mkuu,kwa hiyo hata majukumu yake ya kamati ya hesabu za serikali na mashirika ya umma anayafanya kwa msukumo?suala la Posho anafanya kwa msukumo?


- Ninaamini ni haki ya Zitto kikatiba kugombea anything, msiomataka Zitto mnapwaya sana kwenye hoja wengi wenu mnajikita kwenye kujali chama kuliko Taifa, that is very sad kama hatuwezi kutenganisha Taifa na Vyama vya siasa, then hili taifa tutakwama daima. Simfahamu vizuri Zitto ila siamini kwamba hawezi kuaminika na Taifa, miswaada yake yote bungeni ni masilahi ya Taifa tu na hasa wananchi, I mean wananchi wa jimbo lake wanaiamini naye sana which is the most important ishu of all.

- Zitto, kuwa rafiki na Viongozi wa CCM siamini kwamba ni ishu ya kumfanya asiwe Rais mzuri, unless kuna something else hakisemwi hapa, kwamba ana tamaa ya madaraka labda mtuambie kiongozi gani Duniani asiye na tamaa ya madaraka zaidi ya aliyonayo, mtajeni mmoja tu!

- Kwamba ni Raifiki wa Rostam, unless kama hutumiii cell phone za bongo, wewe sio rafiki wa Rostam, ila kama unatumia any of them basi wewe automatically unashirikana na Rostam vile vile, ni hoja haina mshiko kwamba anaigawa CDM then huko CDM mtakuwa wanafiki wa Dunia, jinsi mnavyoweza kuweka smilling face to the public huku mnamchukia kama mnavyojisema hapa kwenye hii thread.

- Ninasema hivi, simjui sana Zitto on a personal level, lakini wale mnao-claim kumjua so far mnashindwa kuweka hoja nzito za kutushawishi tusimjua kwa karibu kwamba hafai kuwa Rais, mnajaribu sana kuonyesha hana royalty kwa chama, hapo ndipo mnajiharibia sana maana mnathibitisha kwamba CDM kuna unafiki Zitto is good kupiga kampeni za chama chenu Arumeru, lakini hafai kugombea urais kwa chama chenu, shame on all of you mnaomchukia bila sababu za msingi!

-Again, mimi simjui sana Zitto kwa karibu, ila nawaomba wale wote mnao-claim kumjua na kwamba hafai kuwa Rais kwa tiketi ya CDM, tupeni hoja nzito za kumchukia kwenu maana so far mnapwaya sana kwenye hoja za ku-back up chuki zenu, tunaojali Taifa kwanza tunafurihishwa na uamuzi wa Zitto kwa sababu unafungua njia kwa Vijana wote wanaotaka kugombea nafasi kubwa za taifa, otherwise tusiwe part of the problem kwa kulilia mambo ya zamani tu!

Es!
Field Marsha ES,
Bravo mkuu,Unajua tangu upotee na akina Mugongo mugongo jukwaa hili limepwaya sana .Wamebaki akina Mkandara,Mwanakijiji,na wakuu wengine wachache kutetea heshima ya JF kwa hoja.

Nashindwa kuelewa mtu anaposema fulani ana urafiki na Rostam sijui anamaanisha nini? Je,wanaofanya biashara na Rostam je? Kama una simu yenye laini ya VODA hufanyi biashara na Rostam?Mbona humfanyii Economic Embargo? Je ni Zitto pekee kwenye kambi ya upinzani mwenye urafiki na wana-CCM?

Huyo jamaa ni mbishi aliyepitiliza. Ma-radicals kama huyu hawatakiwi kupewa mamlaka makubwa sana.unaongelea maadili?huyu kama alijibizana na balozi kwenye kikao kama vile anajibizana na kimada wake mbele ya jumuiya ya watanzania atashindwa kufanya nini?kama aliweza kupotosha mdahalo chuoni na kugawa darasa profesa akagomea darasa hadi likafikia kwenye seneti ya chuo na ubalozi wa tanzania unategemea nini?kama aliweza kutembea na profesa wake unategemea awe na maadili gani aidi? kama aliweza kusababisha vurugu alipokuwa angombea chuo kikafungwa badala ya kujutia yeye akawa anawahi mahakamani kupinga amri ya chuo kumzuia kugombea unategemea nini?damu ya watu ilimwagika lakini alijifaragua tu kwenye kampeni zake kusimama dakika moja kabla ya kampeni ili kuvuta kura.Hii ndiyo aina ya akina Ghaddafi,kagame au huyu wa syria?

nilishamwambia tanzania haiko tayari kuongozwa na mujahidini au ma-ayattolaah.kama wanataka wahamie Iran kwa maradicals wenzao.waroho wakubwa wa madaraka hawa.Huu mtandao wao sasa ni mkubwa kuliko mnavyofikiria wakuu.Hili ni kundi ambalo litaleta vita kali dhidi ya wazee naona hadi vijana wa CCM akina Nape,Makamba na akina Bashe wako kundi hili.aliposimama Bashe na kuwaambia wazee ni tatizo haikuwa kwa bahati mbaya.huyu dogo Ben Saanane ana kisirani kibaya sana. ila ninachoona ni kwamba kama Zitto huko baadae atakuwa mwenyekiti wa chama chao au Rais na kwa jinsi ninavyoona anaungwa mkono na hawa vijana itakuja kutokea kama ya Zuma na Malema.

Maskini Freeman Mbowe watetezi wake wanazidiwa nguvu.kiboko ya hawa ni kutafuta wasomi nguli kuliko wao wanaojua kujenga hoja kwa umahiri ili kukabiliana nao.Nimesoma andiko la zitto nimegundua anaweza kujenga hoja na kuhamisha hata mawazo ya watu.hawa ni mabingwa wa propaganda. Saanane,ana uwezo mkubwa ni msomi aliyebobea na anajiamini isipokuwa akitumia taaluma yake vizuri na kujiamini kwake anaweza kukisaidia chama.Hizi raslimali anazoelekeza kwa kundi la Zitto zitaleta athari kwa vijana.Angesaidiana na John Heche kuisuka Bavicha naamini hali ya jumuiya hiyo ingekuwa imebadilika.Huyu dogo huwezi kumshauri hilo sana sana atakujibu kwa kukudhalilisha na watu watamuamini. Bavicha imegawanyika,makamu mwenyekiti girlfriend wa saanane yupo kundi la akina zitto.je kwa staili hii huko mbele si kuna mpasuko mkubwa?wiki mbili tu nilitabiri kama zitto atagombea uenyekiti wa chama au urais tutarajie mpasuko huko chadema kwa kuwa najua vijana alio nao kundi moja mbowe hataweza kuhimili vishindo vyao.hili ndilo linalotokea sasa


hawa wako tayari kuua ili wapate wanachotaka

Nuclear1,

Naomba ulete uthibitisho wa hayo uliyoandika.Ongeza list kabisa Willy malecela,Baraka Kange,Makongoro Nyerere,Ole Millya,Julius Mtatiro,David kafulila na wengineo! Tujadili mada iliyoko mezani achana na personal vendatta na kuchafua majina ya watu.Kwa bahati mbaya sijengi hoja au kusimamia hoja katika kufurahisha watu.Usidhani kila mtu yuko kama wewe mkuu

Remove the hatred induced politics of Tanzania and misguided priorities.Throw away your "no victor, no vanquished" mantra. It does not exist in practise. Surely, it does not exist in the minds of CHADEMA elites

The problem with most guys including you is that they are selectively hypermetropic. They see only what they want to see and blank-out others from their view. You are assertions are just inflammatory. Well you have the right to your opinion but not to your facts.

In reality you think you are doing good and giving Opposition what they want but in reality you are just hurting the Opposition camp legacy and most importantly the CHADEMA name with you silly fact fixing games.
 
Ni kweli kwamba Zito ana ajenda ya siri..? Na ni kwa manufaa ya nani..? Jee haya magari ya kifahari anayoyamiliki ameyapata kwa njia gani..? Ni kweli Zito na JK wako so close..? Kwa nini amekuwa na kauli ambazo ni very controversial..? Na mwisho ya yote anataka ku-achieve nini..? ni kweli anataka uraisi au anatumika kujaribu kukisambaratisha chama..? Kwa nini atangaze nia kipindi hiki ambako nguvu zote ziko Arumeru..? Na jee hii kauli yake ina uhusiano wowote na post moja ambayo iliwekwa hapa JF ilio (supposedly) mnukuu Dr Kitilah kuhusu mpasuko wa uongozi CDM..? Duh.. Kamanda Zito mbona wanipasua kichwa..? ntapata wapi majibu haya mie..?
 
MBONA hamsemi ukweli tu kwamba ZITTO ni immaterial kwenye urais?
=upapeti mwingiii!
=watanzania wengi mtamjua tu kabla ya 2015
=ana kaugonjwa kanakoitwa mega-mania
=kuhusu ugomvi wake na MBOWE si urais bali wale watu wa viti maalum mle cdm.kila mmoja wao anataka awe juu ya mwingine we subiri mpaka watauana labda hizo nafas ziondolewe.
 
Nashindwa kuelewa mtu anaposema fulani ana urafiki na Rostam sijui anamaanisha nini? Je,wanaofanya biashara na Rostam je? Kama una simu yenye laini ya VODA hufanyi biashara na Rostam?Mbona humfanyii Economic Embargo? Je ni Zitto pekee kwenye kambi ya upinzani mwenye urafiki na wana-CCM?
Urafiki wa Zitto Kabwe na Jack Nzoka Deputy Director wa Idara ya Usalama wa Taifa wewe unataka kutuaminisha ni wa kawaida? hivi si wewe chama chako ndio kilisema Usalama wa Taifa ndio waliokuwa wanachakachuwa kura za CHADEMA? je inaingia akilini wakati chama kiko vitani kwenye uchaguzi mkuu halafu Zitto Kabwe anakuwa na mawasiliano ya karibu sana na one of your party enemy? (TISS)

Zitto Kabwe ni rafiki yako na kama alitoa makala hii ili kumjibu huyo mwandishi sasa mfikishie na ujumbe huu, aje hapa atupe ufafanuzi wa yeye kuwa karibu na Usalama wa Taifa. nitamuhesabu Zitto Kabwe kama ni Double Agent until he proves otherwise without resonable dought.
 
Hivi yule kiongozi wa Korea Kaskazini ana umri gani vile...??

Yule kiongozi wa Korea Kaskazini ana miaka 28 ila uongozi wa nchi yao ni tofauti na sisi yeye hajachaguliwa ki-domocrasia karithi urais.Mimi binafsi nakubaliana na wale wanaosema kwamba Zitto Kabwe bado hajapevuka kisiasa.The right time for him to run for presidency is 2020 or 2025.
 
Urafiki wa Zitto Kabwe na Jack Nzoka Deputy Director wa Idara ya Usalama wa Taifa wewe unataka kutuaminisha ni wa kawaida? hivi si wewe chama chako ndio kilisema Usalama wa Taifa ndio waliokuwa wanachakachuwa kura za CHADEMA? je inaingia akilini wakati chama kiko vitani kwenye uchaguzi mkuu halafu Zitto Kabwe anakuwa na mawasiliano ya karibu sana na one of your party enemy? (TISS)

Zitto Kabwe ni rafiki yako na kama alitoa makala hii ili kumjibu huyo mwandishi sasa mfikishie na ujumbe huu, aje hapa atupe ufafanuzi wa yeye kuwa karibu na Usalama wa Taifa. nitamuhesabu Zitto Kabwe kama ni Double Agent until he proves otherwise without resonable dought.

Mkuu hivi ukiambiwa kwamba hao TISS, achilia mbali Zitto, wamejikita ndani ya CDM na wana madaraka utajisikiaje? Hivi mkuu mtu kuwa na urafiki na watu inakuwa ni jambo la kumhukumu? Kwa hiyo unataka Zitto awe na marafiki ambao ni wana CDM tu?

Nakumbuka Dr. Slaa alikuwa akiishi na Diwani wa CCM. Hapo unasemaje?
 
Mkuu hivi ukiambiwa kwamba hao TISS, achilia mbali Zitto, wamejikita ndani ya CDM na wana madaraka utajisikiaje? Hivi mkuu mtu kuwa na urafiki na watu inakuwa ni jambo la kumhukumu? Kwa hiyo unataka Zitto awe na marafiki ambao ni wana CDM tu?

Nakumbuka Dr. Slaa alikuwa akiishi na Diwani wa CCM. Hapo unasemaje?
Umetumwa? wewe ndio Zitto Kabwe, unadhani sifahamu ninachokiuliza au unadhani wote humu viherehere vya wanasiasa? Mabere Marando alishajibu siku nyingi Mahusiano yake na TISS, hapa yanahitajika maelezo ya Zitto Kabwe na siyo maelezo ya wapambe wa Zitto Kabwe. tena ningekushauri kama unampenda kaa mbali na hili.
 
=BARRICK walikuwa wanamlipa $25000 kila mwez for 6 months in2009.
=Kwa kuitetea DOWANS alilipwa 80mil (TSH)
=Kuhusu post ya Mkumbo alikuwa sahihi kwa sababu hata yeye KITILA pale cdm yuko kwa ZITTO na anamfahamu vizuri ZITTO kwani ni KITILA aliyemleta Zito UDSM akitokea ZANZBAR UNIVERSITY wakati ule KITILA alikuwa RAIS wa DARUSO
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom