Zitto: Ndio ninautaka urais

Zitto: Ndio ninautaka urais

Status
Not open for further replies.
Kwa wiki kama mbili hivi kumekuwa na mabandiko humu JF yanayoashiria kana kwamba huko CDM kuna Gogoro. Haya mabandiko yamekuwa yakipingwa na wengine kuja na tafiti kuyapinga. Nakumbuka alianza Tuntemeke wakafuatia akina PAA na TII kisha akaja Mwanahalis. Niliona kama watu wa CDM wa ndani kabisa wakiwa wanapingana. Mfano Dr. Mkumbuko alipingana na Rev. K ambaye alisema ana habari za ndani. Katika moja ya post zake, Tuntemeke alisema kwamba wananyimwa kuila keki ambayo wameipika! Sikumuelewa. Kisha ukaja uzi ambayo ulisema kwamba wakati Dr. Mkumbo yuko London alisema ya kwamba ndani ya CDM kuna makundi ya Urais ambayo yanangozwa na Zitto, Mbowe na Dr. Slaa. Aliyeleta uzi akashambuliwa kwa kila aina ya matusi na kejeri. Dr. Mkumbo hakukanusha hili. Amekuja Zitto anasema wazi wazi kwamba anautaka Urais na ameenda mbali zaidi na kuonyesha jinsi alivyojitolea kukijenga chama wakati huo wengine wakiwa wanapumzika na wengine wakiogopa kuingia chamani (amepika keki kwa nini asiile?). Baada ya Zitto kujitokeza na makundi ndani ya washabiki/wana CDM yamejitokeza hadharani ili kutimiza lile neno lililonenwa na mtu mmoja akisema alimsikia Dr. Mkumbo akisema kuna makundi ya Urais huko CDM.

Kwa hakika ni dhahiri shahiri sasa kwamba kuna Gogoro huko CDM na bundi ametua mtaa wa Togo. Gogoro linatakiwa lishughulikiwe. Naanza kuhisi watu/wanachama wakitolewa kafara ili kulinda himaya. Tusubiri tu tumelizane na Meru.
 
Sasa hapa ningependa wapenda ukweli wote wayapitie haya uliyoyaandika kwa makini halafu pumba na mchele vitaeleweka katika post yako hii.
Naawachia wadau wataamuwa kama kweli wewe ni mwanasiasa kweli au vipi!! Mimi binafsi hapa umeshanijibu dought zangu zote kwako umeziweka wazi mwenyewe hapa.

Hili halinitishi.....!

[Nashindwa kuelewa mtu anaposema fulani ana urafiki na Rostam sijui anamaanisha nini? Je,wanaofanya biashara na Rostam je? Kama una simu yenye laini ya VODA hufanyi biashara na Rostam?Mbona humfanyii Economic Embargo? Je ni Zitto pekee kwenye kambi ya upinzani mwenye urafiki na wana-CCM?

Hapa hatuongelea nadharia wala ununuzi wa bidhaa za RA bali tunaongelea mahusiano ya karibu au yale yasiyo ya kawaida kati ya Zito na RA. Mimi kwa kuwa ni mteja wa Vodacom, haimaanishi kuwa nina uhusiano binafsi na RA. Zito ana mahusiano binafsi ya karibu na RA. Hatushangai mahusiano ya RA na Zito eti kwa sababu RA ni mwana CCM bali kwa sababu RA ni mtu ambaye jina lake lipo katika kila kashfa kubwa ya fedha nchini. Pia huyu ni mtu ambaye licha ya kutokuwa ndani ya serikali lakini ndiye mgawaji wa vyeo ndani ya serikali (Rejea barua ya Rweyemamu. Rweyemamu alipotaka kupewa kazi ndani ya serikali ambayo aliipigia kampeni kupitia kalamu, alimwomba RA amkumbuke, hakumwomba JK, na baada ya muda akapewa nafasi hiyo aliyo nayo). Huyu RA, kwa Tanzania anaonekana kama mafia aliyeshindikana. Ufisadi wote unaopigiwa kelele na CHADEMA, katikati yake yupo RA, halafu mtu huyo huyo ni rafiki wa karibu wa Naibu katibu Mkuu (Zito) wa chama kinachomsakama.

Tuliwahi kumwuliza Zito atuambie ni nini alikuwa akijadiliana na RA pale Sea Cliff Hotel kuanzia saa 4 mpaka saa 7 usiku kwenye chumba maalum, wiki mbili tu kabla ya uchaguzi, Zito mpaka leo hajajibu. Zito ni mtata, ni vigumu sana kuelewa kilichomo moyoni na akilini mwake, yeye ndiye anajua anachokitaka LAKINI kwa tulio wengi tunamwona ni mtu hatari pengine kuliko hata hao CCM tunaowalaumu. Zito anaweza kufanya kazi, na hakuna mashaka juu ya uwezo wake lakini kuna mashaka makubwa juu ya uadilifu, uzalendo na dhamira yake. Ni mtu anayestahili kufanya kazi chini ya watu wengine ambao wakiona na kuhakikisha kuwa dhamira yake siyo safi, wanamwondoa LAKINI siyo yeye awe overall in charge wa nchi.

Mkuu,

Ndiyomaana nasema hapa tuwe fair. Hivi Zitto akikuambia alitambulishwa kwa Rosatam Aziz na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe utasemaje?mawazo yako yatakuwa haya haya au yatabadilika?
Haya hapa ni maneno ya Zitto

"Rostam Aziz alikuwa mbunge mwenzangu na nimeshasema hapa nimekuwa nikiwasialiana naye sana Kama Mbunge na Kujadiliana naye mambo mengi tu. Hajawahi kunihonga. Hajawahi Kujadiliana na mimi lolote kuhusu chama changu wala chama chake. Rostam Aziz nimetambukishwa kwake kupitia Mwenyekiti wangu wa chama ndugu Mbowe. Urafiki wangu naye imetoka kwa Mbowe maana sikumjua kabla.

Haya majungu haya yameshachacha. Kubenea kayasema wee lakini wananchi bado wana imani kubwa sana na mimi. Tafuteni majungu Mapya."

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...akutana-na-keneth-kaunda-lusaka-zambia-3.html

 
Mwenye PROFILE ya Yericko Nyerere aimwage hapa ili tujiridhishe kama ushauri wake ni wa kuzingatiwa au la. Mfano Livingstone Lusinde kwa profile yake hata aje na hoja nzuri kiasi gani mimi Ulukolokwitanga nitaipuuza tu...
Wewe umechelewa sana tena bado uko mbali sana na dunia ya leo, hivi unadhani ni nani mwenye akili timamu anathamini makaratasi? wewe kama ni mtu makini unatakiwa umvalue huyo Yericko kwa alichokiandika na hapo ndipo utakapoipata Profile yake halisi na sio zile za kukariri darasani na kujaza mavyeti feki na udaktari feki kama Nchimbi.
 
Vyama vya siasa vingi vinapoteza mvuto kwa kukosa demokrasia. Mrema alipata kura nyingi 95 alikosa urais alitakiwa akae pembeni, Lipumba nae hivyo hivyo mwaka 2000 bado akangangania, maalim Seif zenji mara 3 anashindwa kwa kura asilimiaa chache. Tujifunze kwa wamarekani ukishakosa unakaa pembeni.

Watakuambia Wade aligombea mara nne na mara ya tano ndio akaukwaa ila hawatakuambia kwamba baada ya kuutwaa akiwa mkongwe alitamani kufia Ikulu hadi aibu imemkuta jana!
 
Matola,

Nimekuambia nidhamu ni jambo muhimu sana.Tafadhali unapojenga hoja uwe na ushahidi.NAOMBA UTHIBITISHE kwamba chama changu CHADEMA kilisema kuwa mimi ni USALMA WA TAIFA.Njoo na facts hapa.
Kama unataka facts kuwa chama kilisema wewe ni usalama wa taifa hizi hapa

HATIMAYE uchaguzi wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) ulimazika jana kwa kumpata Bw. John Heche kuwa Mwenyekiti wa umoja huo.

Pamoja na kupatika kwa kiongozi huyo, uchaguzi huo uligubikwa na mizengwe mbalimbali ikiwemo rushwa na mambo ya 'kujuana' yaliyooneshwa wazi na viongozi wa chama hicho.

Kwa mujibu wa uchuguzi uliofanywa na Majira juzi usiku, uchaguzi huo ulifanyika huku kukiwa na makundi matatu, makundi hayo ni yale yanayomuunga mkono Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Zitto Kabwe na lile lisilomuunga mkono mtu yeyote katika chama hicho.

Uchunguzi huo ulibaini kuwa kundi linalomuunga mkono, Bw. Mbowe ndilo lilokuwa na nguvu zaidi na ndilo lilochukua kiti hicho kutokana na mwanzilishi wa chama hicho, Bw. Edwin Mtei kuliunga mkono kwa asilimia mia.

Chanzo cha habari kutoka ndani ya Baraza la Wazee kilidokeza kuwa, maamuzi ya kufanya uchunguzi wa wagombea yalifikiwa baada ya kugopa kivuli cha Bw. Zitto ambaye ameonekana kuungwa mkono na vijana wengi ndani ya chama hicho.

Kilisema kuwa baada ya kubaini uwezekano wa kundi hilo kushinda, baraza la wazee lilikubaliana kutafuta mambo yatakayowamaliza wagombea hao ili wasipitishwe katika kugombea kiti hicho.

"Ndugu yangu napenda kusema kuwa chama hiki sasa kinaenda pabaya walitafuta kila njia ya kuwamaliza vijana na njia waliyoipata ni kuwatutafutia tuhuma zitakazowafanya waondoke katika kuwania nafasi hiyo...lakini tulipigana na ikashindikana," alisema mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo.

Alieleza kuwa tuhuma hizo ni kundi hilo kutaka kuunganisha nguvu katika uchaguzi huo ili kumpigia kura mtu moja jambo ambalo kamati ya wazee ilipingana na suala hilo ikidai kuwa ni jambo linalowagawa vijana ndani ya chama.

Chanzo hicho kilisema kuwa katika uchaguzi wowote makundi lazima yawepo ndo maana mgombea hawezi kupata kura kwa asilimia mia moja hata akiwa pekee yake.

Alisema tuhuma nyingine zilizofanya kuenguliwa kwa wagombea hao ni kupokea wajumbe kutoka Zanzibar jambo ambalo halikuwa na ukweli wowote lakini kutokana na mizengwe iliyoandaliwa na kamati hiyo ilibidi watu hao waadhibiwe.

Alisema kuwa tuhuma nyingine ilikuwa ni kupiga kampeni kabla ya muda uliopangwa na tume hiyo hali iliyosababisha kuenguliwa dakika za mwisho katika uchaguzi huo.

"Tuhuma nyingine iliyoelezwa ni wagombea hao kutaka kupindua chama hicho kwa kuhamisha agenda za chama hicho na
wengine walihofiwa kuwa ni usalama wa taifa," kilisema chanzo chetu.

Hata hivyo Mjumbe huyo wa baraza la wazee alisema kwa upande wa Bw. Heche nako kulikuwa na tuhuma za kupokea wajumbe ambao kamati haikutaja kuwa wanatoka katika mkoa upi lakini alijitetea kuwa ni ndugu zake.

"CHADEMA tumekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa kigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anapokosea tunataka awajibishwe, sisi leo mtu anakosea wakati wa mchakato wa uchaguzi lakini tunasema tunafanya uchunguzi je akipata madaraka tunamchukulia hatua gani kwani atakuwa tayari amepata madaraka," kilisema chanzo.

Chanzo hicho kiliendelea kuhoji ni kwa nini mgombea huyo aachwe na kuchukua madaraka huku akiwa na tuhuma hivyo akataka haki itendeke kwa wote.

Naye Tumaini Makene anaripoti kuwa;

Kamati ndogo maalum, kwa ajili ya uchunguzi wa uchaguzi huo iliyoundwa na kamati kuu ya chama hicho ilibaini kuwepo kwa vitendo vichafu ikiwemo baadhi ya wagombea kutaka kuundwa makundi ili kudanganya wapiga kura kwa nia ya kutaka ashinde mtu wanayemtaka kwa hila zao.

Akizungumza na majira jana akiwa katika uchovu, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Wilbroad Slaa, pamoja na kutotaka kuzungumzia tuhuma hizo za rushwa kwa undani akisema "mengine yanahitaji maamuzi ya juu", alisema kuwa wagombea hao watatu walioenguliwa baada ya kuthibitisha kuwa wamekwenda kinyume na katiba na kanuni za chama, kifungu cha 10, wamekiri pia kuwa wao walijihusisha kutengeneza agenda ya BAVICHA.

"Sasa hilo ni suala kubwa agenda ya BAVICHA ni suala la mkutano na haliwezi kuwa la wao watatu lakini walibainika kujihusisha na kundi la Bw. Habib Machange ambapo ilibidi chama kiingie gharama ikiwemo wajumbe wa kamati hizo kufanya kazi tangu saa saba usiku wa juzi mpaka asubuhi jana na baadhi ya wajumbe walishindwa kurejea kwao," alisema Dkt. Slaa.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa Majira ilibainika kuwa mmoja wa wabunge wa chama hicho alijihusisha na kusimamia vikao vya usiku wa manane vilivyokuwa vikitumika kuwalubuni wajumbe kugawa fedha, kuwanunulia pombe usiku wa kuamkia uchaguzi akitaka kuweka mtandao unaodaiwa kuwa na lengo la kusambaratisha chama hicho.

Mbunge huyo machachari kutoka Kanda ya ziwa ametajwa pia kutoa udhamini wa mmoja wa mgombea aliyeenguliwa kwa lengo hilo ambapo imeelezwa kuwa suala lake pamoja na vituko vingine vitafikishwa mbele ya Kamati Kuu kwa maamuzi zaidi.

Alipoulizwa juu ya tuhuma kwa mbunge huyo (jina tunalo), Dkt. Slaa hakuwa tayari kulizungumzia na kusema kuwa liko ngazi ya juu ya kamati kuu.

Wakati hayo yakiendelea Bw. Heche alisema yuko tayari kufanya kazi katika nafasi hiyo akishirikiana na wenzake ili BAVICHA iwe sauti ya kupigania maslahi ya wananchi wanyonge.

Akizungumza na majira jana, Bw. Heche alisema kuwa BAVICHA itasimama kwa maslahi ya nchi na chama hicho kwa jitihada za kuchukua dola kwa ridhaa ya wananchi.

Bw. Heche alipata kura 147 sawa na asimilia 56 ya kura zote zilizopigwa 267 ambapo kura tatu ziliharibika.

Walioenguliwa katika uchaguzi huo ni Greyson Nyakarungu, Mwampamba na Bernard Saanane.



Source: GAZETI MAJIRA. 30 May 2011
 
Zitto sio kwamba bado umri mdogo tu bali hafai kuwa Rais hata ikifikisha miaka mingapi?Ikulu sio mahala pa kukimbilia kuna biashara gani pale?angesubiri kuombwa na watanzania kama Slaa japo mie sio shabiki wa Dk. Anasumbuliwa na uroho wa madaraka na ubinafsi. Kataka Uenyekiti kakosa,kataka ukuu wa kambi ya upinzani kakosa,uraisi ndio asahau kabisa.ubunge nafikiri unamtosha na hv hajawahi fanya kazi ingine zaidi ya ubunge na namshauri atafute kwanza mke aoe amekua sasa itamsaidia kuacha kukurupuka. Mie ni kijana namkumbali Zitto na uwezo wake wa kujenga hoja lakini Sio kuwa Rais kwa sasa.Kazi kwenu vijana wa Tz ambao ni wavivu wa kufikiri endeleeni kumjaza upepo kichwa mwenzenu
 
Kwanza ni zamu ya Wakristo. So long as Zitto ni mjahidina asubiri mpaka 2025

Naitamani hii iingizwe kwenye katiba mpya ili iwekwe wazi kabisa kwamba post ya urais ni ya kubadilishana kati ya waislam na wakristo at the same time kwa mawaziri wakuu.
that means
rais akiwa muislam na waziri mkuu awe mkristo kama ilivyo sasa, pia raisi akiwa mkristo waziri mkuu awe muislam. hapo itakuwa mswano. ama kwa katiba ya sasa hilo haliko ivo ivo Zitto ana haki ya kuonesha dream zake wala hupaswi kupoteza muda katika hili
 
Watakuambia Wade aligombea mara nne na mara ya tano ndio akaukwaa ila hawatakuambia kwamba baada ya kuutwaa akiwa mkongwe alitamani kufia Ikulu hadi aibu imemkuta jana!
Kabila amepewa Urais akiwa bado kijana mdogo, sasa anatakiwa atoke ikulu akiwa bado umri wake ni kama kijana lakini sasa anang'ang'ania madaraka!! labda utueleze what is your point on this? i mis something.....
 
Mwono wako unaonyesha wazi ni chuki au wivu........sijui umempima huyu Zito kwa kutumia vipimo gani?.....kama kuungombania urais basi ni haki yake ya Kikatiba.......mbona Nyerere alipochukua nchi alikuwa na umri mdogo na alikuwa hajakomaa kisiasa na aliwza kuongoza nchi hii kwa muda mrefu tu.

nani kakwambia mwalimu hakuwa amekomaa kisiasa? Au unamshushia mwalimu heshima ili kumtetea zito kabwe?
Hivi watu wa aina yako mbona mnazidi kuwa wengi ndani ya CHADEMA.. Kunani hapa?
 
Zitto bado mapema, tulia kwanza ukomae baadae utakuja kuwa Rais. komaa kwanza katika kukijenga chama, una umuhimu mkubwa katika kukijenga chama kwanza, tumia uzoefu wako katika kukiimarisha chama kwani bado Chadema kinahitaji kukuwa na bado watanzania wengi wanahitaji kupata ukombozi wa kifikra bado mapema. naamini kabisa kwa kazi utakayoendelea nayo ya kukiimarisha chama utazidi kujifunza mengi kutoka kwa watu mbalimbali na baadae utakuja kuwa rais. kwani kazi uliyoifanya kwenye chama tumeiona lakini usikubali watu kukujaza upepo, na kukuvimbisha kichwa urais bado.

vilevile ningependa kukushauri sio kila swali unapaswa kujibu, na kila jibu lina wakati wake na mahali pake kumbuka mko kwenye uchaguzi Arumeru, Usingependa kuona Watanzania wanaanza kukufikiria vibaya yaani badala ya kuangalia kujenga chama unaanza kufikiria urais. Fikiria kidogo.
 
Tatizo la watanzania wengi hasa wa JF huwa wanasau upesi kwa sababu ya siasa za kishabiki.Mimi kwa kumbukumbu zangu Zitto wakati wa uchaguzi 2010 aliwaambia wapiga kura wake kuwa akirudi tena atarudi kama mgombe Urais.Bora Zitto anaeonyesha nia yake kwa uwazi kabisa kuliko Mbowe anaye tumia watu wake kumsemea.Mwacheni aonyeshe nia kama hamumtaki si mumuonyeshe kwenye sanduku la kura kwenye uchaguzi wa ndani.Hivi katiba yenu CHADEMA inakataza mtu kuonyesha nia ya kugombea urais?

Mkuu nimewakumbusha hii habari huko nyuma lakini watu hawataki kabisaa kusikia. Mwaka 2010 kulikuwa na mgombea urais (dr. Slaa) ambaye kama angeshinda tulitegemea chama chake kimpe kipindi cha pili lakini Zitto akasema 2015 ataenda kuomba Urais. Baada ya Zitto kujitokeza na kurudia kusema kwamba anautaka Urais tunaambiwa timing mbaya! Hivi kati ya tangazo la sasa na tangazo la mwaka 2010 wakati tupo katikati ya kampeni ni hatuoni kwamba hapo ndipo kulikuwa na timing mbaya. Lakini sikusikia kelele!
 
Kama unataka facts kuwa chama kilisema wewe ni usalama wa taifa hizi hapa
Narudia tena Ben Saanane hawezi kupita kwenye vetting yoyote makini ili awe Itelligence securty officer, sana sana tu anaweza akawa ni sehemu vya mainformer wadogo wadogo tu kupitia Zitto Kabwe through Jack Nzoka.
 
Kabila amepewa Urais akiwa bado kijana mdogo, sasa anatakiwa atoke ikulu akiwa bado umri wake ni kama kijana lakini sasa anang'ang'ania madaraka!! labda utueleze what is your point on this? i mis something.....

Nasubiri nione kama atang'ang'ania baada ya kipindi chake cha pili kikatiba kuisha. Sijaona ameng'ang'ania bado kwa kuwa yuko ndani ya vipindi vya katiba. Kwa hiyo Mkuu unataka wapewe wazee wakitoka wakutane na umauti?
 
Mkuu nimewakumbusha hii habari huko nyuma lakini watu hawataki kabisaa kusikia. Mwaka 2010 kulikuwa na mgombea urais (dr. Slaa) ambaye kama angeshinda tulitegemea chama chake kimpe kipindi cha pili lakini Zitto akasema 2015 ataenda kuomba Urais. Baada ya Zitto kujitokeza na kurudia kusema kwamba anautaka Urais tunaambiwa timing mbaya! Hivi kati ya tangazo la sasa na tangazo la mwaka 2010 wakati tupo katikati ya kampeni ni hatuoni kwamba hapo ndipo kulikuwa na timing mbaya. Lakini sikusikia kelele!
Dr Slaa he was seek for one term Presidencial......Je una lingine?
 
Nasubiri nione kama atang'ang'ania baada ya kipindi chake cha pili kikatiba kuisha. Sijaona ameng'ang'ania bado kwa kuwa yuko ndani ya vipindi vya katiba. Kwa hiyo Mkuu unataka wapewe wazee wakitoka wakutane na umauti?
Mtu aliyeshindwa uchaguzi na akabaki madarakani kwa nguvu bado unasema swala la katiba hapo? kuna katiba inayoruhusu kung'ang'ania madaraka?
Swala la urais sio la mzee wala kijana ni mtu mwenye uwezo tu na si vinginevyo ikulu hakuna mashindano ya kutafuta marijali ndio mtueleze habari za ujana.
 
I would like to give advise to any new aspiring president to come out now, condemn what is happening offer a reconsilaiton and healing process. Offer hope to the children of Tanzania, stand up and give a speech worth of a standing ovation.

If you are a young inspiring true leader who can lead our country to the next level please lets start hearing from you now. However this should be done under a new constitution. Well done Zitto.
 
Kama unataka facts kuwa chama kilisema wewe ni usalama wa taifa hizi hapa
Mkuu this is not a fact as you called it..............................

Labda mimi ninacho kiona hapa ninyi akina Quinine na wenzako ni aina ya watu ambao hamtambui makundi yanapaswa kuisha punde tu uchaguzi unapokwisha, maana katika kila uchaguzi makundi ni lazima yatakuwepo.

Ni kwanini basi mnaziba watu midomo kwa kigezo cha makundi wakati wa uchaguzi wa ndani. kila mara mara inapotokea hoja inayo muhusu zitto au kwa namna yoyote Ben akichangia tu mnaanza mashambulizi binafsi na kurukia makundi wakati wa uchaguzi? mbona mimi sioni wapi hawa akina Ben wakilalamikia haya mambo ya makundi ya uchaguzi kwa sasa zaidi ya nyinyi kuyakomalia?.

Mimi si mwana CDM lakini sioni hoja yenu iko wapi zaidi ya kuishia the same old story "uroho wa madaraka"
 
Sema unayotaka kusema lakini ujue kwamba ukweli ndio huu. Zitto acha kulewa misifa utapotea!!
Uraisi unatakiwa uonwe sio ujione kuwa unafaa kuwa Rais.

kwa yoyoye anayetakia mema chadema atakubaliana na mimi. au abishe
 
Zitto bado kwa sasa kuwa Rais. Nakubali Tz tunahitaji Rais kijana wa kuweza kuweka sawa mambo kulingana na wakati lakini rafiki yangu Zitto bado. Sasa hivi hoja kubwa tuliyonayo ni kuikomboa nchi (Kuiondoka mikononi mwa CCM). Tuombe Mungu atusaidie tufanikiwa katika harakati za ukombozi mwaka 2015. Then Zitto apewe wizara nyeti (Nishati na Madini). Hii wizara inaweza kuleta mabadiliko makubwa katika maendeleo ya nchi. Mwaka 2020 Zitto anaweza kupewa uwaziri mkuu kulingana na utendaji wake katika wizara ya nyeti. Then 2025 Zitto utakabidhiwa nchi kwa kuangalia ulivyotenda katika miaka 10.

Ni nadhani kwa sasa umetumwa na CCM kuvuruga chama chetu ili tuwe kama wao.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom