Lekanjobe Kubinika
JF-Expert Member
- Dec 6, 2006
- 3,019
- 580
Lakini kusema kwa Kabwe kuhusu hamu yake ya kuwa rais ina ubaya gani? Kila mtu anayo ndoto yake, wengine hukaa kimya na ndoto zao na wengine huropoka hadharani. Hata aliyeko madarakani alikuwa na ndoto ya urais, ndio maana baba wa taifa alimnyamazisha baada ya kuona anasemasema kuutaka urais wakati huo baba wa taifa alishaona muda bado na kumbe ni kweli, si mnaona anachofanya sasa? Ni rafiki yake sana Kabwe, kwa hiyo akiukwaaa urais sitaona tofauti na aliyepo sasa, watabaki kulindana na kuhamasishana utundu wa kuchanga karata za kuiona siku inapita hata kama kwa mazingaombwe.
Kama alivyotumia haki yake kuongea Kabwe, huyo Yeriko naye katumia haki yake kutoa uchambuzi juu ya mambo yaliyoanikwa na Kabwe ili yachambuliwe kwa faida ya walaji ambao ni umma. Wabaya sio wanaoomba bali wabaya ni wale wawapao waombaji ambao wanaonekana wazi kwamba hawahitajiki kupewa sasa. Urais sio kuwa msomi ingawa inasaidia, lakini wapo wasomi wengi wanavurunda kila kukicha. Tusipendelee kusikia yale tunayoyataka tu, siasa ni pamoja na kuvumiliana kwa kusikia yanayotuumiza. Cha msingi ni kujenga hoja na kuhakikisha hoja yako yenye mshiko inapita.