Zitto: Ndio ninautaka urais

Zitto: Ndio ninautaka urais

Status
Not open for further replies.
Mwakalinga na Matola, nafikiri sasa mmeanza kuelewa kitu ambacho wengine tulikiona tangu zamani. Kadri muda unavyokwenda ndivyo mambo yanavyozidi kuwa wazi zaidi.
Mkuu Feedback naoma tafiti kwanini CUF leo ipo hapo ilipo.................
Hakuna kitu kibaya kwenye uongozi wa siasa kama KUABUDU watu fulani fulani, yaani inafikia hatua kuwa na mawazo mbadala na hawa waabudiwa unaonekana msaliti........Nakuhakikishia Feedback hao mnao waabudu mnatengeneza akina Maalim Seif na Akina Lipumba.

CCm yenye ipo hapo ilipo kwasababu hizi hizi mnazozipigania hapa, kwamba waabudiwa watakalo amua ndio hilo, no challenge to them
Mmeulizwa hebu toeni hoja za maana kosa la zito ni nini kusema anaweza kugombea kama katiba na chama kitampa fursa?
Mnaanza mara usalama wa Taifa, mara hajakomaa, yaani hamna kitu mnaongea zaidi ya chuki binafsi, hii ndio demokrasia jamani

Dr.SLAA kachanganyikiwa coz anaomba dua baya kwa ZITTO atimuliwe haraka sana...subiri wapoteze Arumeru ili wamjeruhi ZITTO kama walivyofanya CUF na NCCR.

wabongo bana ndo mana hatuendele tunapenda kuhisi vitu, au kuamini vitu vya kufikirika visivyo vyakweli kabisa, ona sasa nae huyu mawazo yake yalivyo.....

duu kazi kweli kweli...........
 
Wenzengu tuache ushabiki huu wa ajabu. Hii mada sio nzuri wakati huu. Lakini pia ninawaomba tujaribu kutofautisha kati ya kiongozi na mtendaji. Hawa wawili ambao leo kwa makusudi mmeamua kuwafanya MADA, hawafanani hata kidogo. Zifa zao ziko tofauti kabisa. Mmoja anafaa kuwa waziri mkuu na mwingine kuwa rais. Slaa na Kabwe hawafananishwi kwa lolote iwe kwa utendaji kazi wao au uzalendo wao. Kwa mjadara huu ninapata kuelewa nini watanzania wanakichokihitaji kwa mujibu wa umri wao, makundi yao ya kijamii na hata uwezo wao wa kuelewa siasa na maendeleo.

Zito ameonyesha nia yake ya kuutaka urais wa Tanzania, hii ni haki ya kila mtu kuutaka urais. Nani asiyeutaka? Kwenye maelezo yake amesema, kama chama kitaona anafaa na iwe hivyo kama chama kitaona hafai na iwe hivyo. Kwa wale mliousoma ujumbe wake hakuna popote alipokusudia kuanzisha haja ya kumlinganisha yeye na Slaa.

Leo hii sisi kwa sababu zetu tunataka kuabadirisha maneno ya Zito.

Naamini Zito anajua taratibu zote za kuwania nafasi hiyo ua urais, anajua uzito na umuhimu wa kuwa mfano mzuri. Sitegemei mtu mwenye uelewa kama yeye aanzishe na kueneza upuuzi huu ili kujinufaisha binafsi.

Nanawasihi watanzania msio wavivu wa kusoma na kuelewa, tutofautishe kati ya MTAWALA, KIONGOZI NA MTENDAJI.

Nchi yetu imefika hapa kwa sababu ya KUTAWALIWA na wale tuliowaamini na kuwapa nafasi za UONGOZI. Tuko hapa tulipo kwa sababu hatuna WATENDAJI wazuri.

Kwa mtazamo wangu Zito ni moja kati ya mifano ya WATENDAJI wazuri tulionao leo hapa Tanzania. Anafaa sana KULIONGOZA baraza la Mawaziri.
 
Wakati CDM wakiwa ktk mapambano makari ya kushinda ubunge ktk jimbo la Arumeru mashariki, kushinda udiwani mwanza na kule songea, Mh.Zitto Kabwe anatumia muda huu wa uchaguzi kutanganza kwamba anataka kugombea urais kupitia chadema 2015.Tunajua Zitto kama mwanachama yeyote wa CDM ana haki ya kugombea nafasi yeyote ndani chama na kitaifa.Lakini utata siyo zito kutaka kugombea urais ila ni kutangaza anataka kugombea urais wakati chama kipo kwenye mapambano ya kushinda chaguzi zake ndogo.Je huu ni muda muafaka kwa Zitto kutangaza anataka kugombea urais?isn't this controversial?
 
Binafsi sipingi hoja ya Zitto kutaka umri wa kugombea urais ujadiliwe na hoja yake ya kutangaza nia ya kuutaka urais, wasiwasi wangu ni timming ya hoja zake. Sidhani kama kuna busara imetumika au washauri wake wamemshauri ndivyo sivyo. Nachelea kusema hata kama Zitto anautaka urais mguu alioingia nao ndio utaifanya ndoto yake isitimie, maana mjadala huu unaoendelea ndani na nje ya chama chake utamwonyesha mengi na ataona wapi alipojikwaa. Namshauri tu kama kweli ana busara azingatie mawazo ya pande zote asiangalie ya wale wanaomshangilia kwa kumwambia mfalme umevaa nguo asikilize na wanaomwambia mfalme uko uchi.

Hoja ya umri, ni kweli lakini kama suala ni vijana kwa nini iwe 35 na si 18 au 25, kwani kukomaa kwa ujana kunaanzia miaka mingapi, Na kuna utafiti wowote wa kisayansi kuwa kuanzia 35 ndio anaweza kuwa rais mzuri na si 40 ya sasa. Sipingi miaka 35 lakini lazima tujiulize what is the motive behind 35 yrs.

Hoja ya yeye kuutaka urais, nayo si mbaya lakini je huu ni muda mwafaka? kwa taifa? kwa chama chake? Generally tujiulize mtu anayetangaza kutaka kitu huwa ni wa aina gani, jasiri, ana tamaa, au? Kuna wengi tu wanadhani Lowassa anautaka urais ila mbali ya kuulizwa hajatamka wazi, je yeye si jasiri kama Zitto au yeye hana tamaa kama ya Zitto? Kwa kweli kuna maswali mengi ya kujiuliza na kumuuliza Zitto achilia mbali kuwa chama chake cha Chadema kwa sasa kiko kwenye kinyang'anyiro cha ubunge.
 
Zitto alikuwa anajibu nakala fulani. Nafahamu Zito anatambua CDM ni chama makini sana,na hawakurupuki kuteua wagombea wa nafasi mbali mbali. Ikiwapendeza CDM na wananchi wote atateuliwa yeye au Dk Slaa au Mbowe au mwingine awaye yote. Chapeni kazi wa-TZ acheni bla bla,
 
Zitto mlinganishe na mdee, mnyika, wenje, nape,
Mi tu hanifikii, itakuwa Dr. Slaa? Dr. Salim, prof. Mwandosha,? Unyaji wa swala na tembo? Nimeshasema tumsamehe, ni mpayukaji? Kumbe aliletwa udsm na mkumbo?
 
Mwakalinga na Matola, nafikiri sasa mmeanza kuelewa kitu ambacho wengine tulikiona tangu zamani. Kadri muda unavyokwenda ndivyo mambo yanavyozidi kuwa wazi zaidi.

Endeleeni kudanganyana.....!

Hata kama nilikuwa sijui kusoma sasa nimeletewa picha ili nione.......Kuna mahala nimewaomba wenye notebook na wandike maneno haya, halitokuwa jambo la kushangaza ukisikia Zitto Kabwe ameangushwa Ubunge na mgombea wa CCM uchaguzi wa 2015, inashangaza sana mtu ambaye hata Ubunge wa jimboni kwake ameshinda kwa mbinde kwa simple majority anakuja na ndoto za Urais in wrong timing!! interesting.
Jibu maswali niliyokuuliza.enga hoja,hayo majina unayoniita ungeweza kuyaepuka kama kweli unataka kutendewa haki na kama kweli wewe ni mwanasaikolojia kama unavyotaka kutuaminisha hapa.Usidhani kwamba hatuna uwezo wa kufanya siasa za mipasho.Naweza hizo siasa but i wont go too low.....

Kuhusu kupata kura kidogo jinsi mlivyo out of touch na siasa za Tanzania hamuelewi hata juu ya kugawanywa kwa jimbo na amabyo ilikuwa ni ngome yake kuu?hamuongelei juu ya ghiliba za baadhi ya wanasiasa waliohujumu jimbo wakiwa tayari kuona hawi mbunge ili kumpoteza kwenye ramani ya siasa kwa maslahi na tamaa zao binafsi?Najua huku tuendako mengi yatasikika,yatasemwa....kama watu walikuwa tayari kuttumia fedha zao kuhujumu wenzao kwa matamanio binafsi kwenye ubunge ni lipi litakaloshindikana?kutuma vijana kwenye mtandao kuja kutukana itashindikana?

Haya matamanio ya kuangushwa ubunge hayawezi kuzuilika.Vipi kama hataenda kwenye ubunge?na hata kama hatakuwa Mbunge bado wimbi hili la vijana na mtizamo kama wake wataibuka kwa wingi.Utaendeleza matamanio yako?

Ati Kwamba wewe ni kijana kama mimi,haimaanishi tunafanana.Naomba urudi kwenye mada au ujibu hayo niliyokuuliza.Pia kama wewe ni mstaarabu leta uthibitisho kwamba chama changu kiliniita Usalama wa Taifa.

Mkuu Feedback naoma tafiti kwanini CUF leo ipo hapo ilipo.................
Hakuna kitu kibaya kwenye uongozi wa siasa kama KUABUDU watu fulani fulani, yaani inafikia hatua kuwa na mawazo mbadala na hawa waabudiwa unaonekana msaliti........Nakuhakikishia Feedback hao mnao waabudu mnatengeneza akina Maalim Seif na Akina Lipumba.

CCm yenye ipo hapo ilipo kwasababu hizi hizi mnazozipigania hapa, kwamba waabudiwa watakalo amua ndio hilo, no challenge to them
Mmeulizwa hebu toeni hoja za maana kosa la zito ni nini kusema anaweza kugombea kama katiba na chama kitampa fursa?
Mnaanza mara usalama wa Taifa, mara hajakomaa, yaani hamna kitu mnaongea zaidi ya chuki binafsi, hii ndio demokrasia jamani

Najua Mh.Zitto Kabwe hauna nia wala dhati ya kuwa raisi Tanzania..! hiyo ni moja ya mkakati wako na CCM kuimaliza CHADEMA huku ukishirikana na swahiba wako January Makamba..,siujui wemekupa shs.ngapi mheshimiwa au wamekuahidi cheo gani serikalini (mkuu wa wilaya,katibu CCM)..!
Lakini Jua Nguvu ya Umma Haichezewi..,wako wapi madiwani wa Arusha (watano) waliosaliti chama..,yuko wapi Walid Kabourou,yuko wapi Tambwe Hiza..yuko wapi Agustino Lyatonga Mrema, ingawa anapata pensheni ya ubunge lakini heshima hana kama zamani..!
Zitto Kabwe Watu wamekufa,kuteseka na kufungwa kuitetea CDM..,leo hii wewe unataka kukiuza CDM kwa bei chee...kumbuka ulipotoka Zitto..,hivi ungegombea ubunge CCM mwaka 2005 ungelipata hilo jimbo la kigoma Kaskazini..,wengeshakutosa zamani kwenye kura za Maoni..,CHADEMA wakakupokea leo unakiuza chama "KWELI SHUKRANI YA PUNDA NI MATEKE'' najua ni haki yako kikatiba kugombea uraisi lakini inaonyesha nia yako ni kuimaliza CHADEMA..!
 
Binafsi sipingi hoja ya Zitto kutaka umri wa kugombea urais ujadiliwe na hoja yake ya kutangaza nia ya kuutaka urais, wasiwasi wangu ni timming ya hoja zake. Sidhani kama kuna busara imetumika au washauri wake wamemshauri ndivyo sivyo. Nachelea kusema hata kama Zitto anautaka urais mguu alioingia nao ndio utaifanya ndoto yake isitimie, maana mjadala huu unaoendelea ndani na nje ya chama chake utamwonyesha mengi na ataona wapi alipojikwaa. Namshauri tu kama kweli ana busara azingatie mawazo ya pande zote asiangalie ya wale wanaomshangilia kwa kumwambia mfalme umevaa nguo asikilize na wanaomwambia mfalme uko uchi.

Hoja ya umri, ni kweli lakini kama suala ni vijana kwa nini iwe 35 na si 18 au 25, kwani kukomaa kwa ujana kunaanzia miaka mingapi, Na kuna utafiti wowote wa kisayansi kuwa kuanzia 35 ndio anaweza kuwa rais mzuri na si 40 ya sasa. Sipingi miaka 35 lakini lazima tujiulize what is the motive behind 35 yrs.

Hoja ya yeye kuutaka urais, nayo si mbaya lakini je huu ni muda mwafaka? kwa taifa? kwa chama chake? Generally tujiulize mtu anayetangaza kutaka kitu huwa ni wa aina gani, jasiri, ana tamaa, au? Kuna wengi tu wanadhani Lowassa anautaka urais ila mbali ya kuulizwa hajatamka wazi, je yeye si jasiri kama Zitto au yeye hana tamaa kama ya Zitto? Kwa kweli kuna maswali mengi ya kujiuliza na kumuuliza Zitto achilia mbali kuwa chama chake cha Chadema kwa sasa kiko kwenye kinyang'anyiro cha ubunge.
Anachokisema winnet forever hapa chini ndio na mimi ninachokijua,
Zitto hajatangaza rasmi hapa JF kama wengi wanavyojenga picha ionekane hivyo, Zitto alikuwa anajibu hoja na si kwamba alifanya timing eti kipindi hiki ndio atangaze

Zitto alikuwa anajibu nakala fulani. Nafahamu Zito anatambua CDM ni chama makini sana,na hawakurupuki kuteua wagombea wa nafasi mbali mbali. Ikiwapendeza CDM na wananchi wote atateuliwa yeye au Dk Slaa au Mbowe au mwingine awaye yote. Chapeni kazi wa-TZ acheni bla bla,
 
Dr.SLAA kachanganyikiwa coz anaomba dua baya kwa ZITTO atimuliwe haraka sana...subiri wapoteze Arumeru ili wamjeruhi ZITTO kama walivyofanya CUF na NCCR.
stupid_warning_labels_640_22.jpg
 
mwambie huyo zito na ayapate yanayosemwa sio vizur kujitangaza ninauwezo wa kufanya kumbe watu wanakucheka lakin mwamuzi wa yote ni halmashaur kuu ya chadema kuamua nani anafaa na mwanzo wa makundi ni hapo zito atakaposhindwa katika mchakato wa awali wa chama ndio atakapoanza kuhaha!
 
Mod mpo wapi, unganishe sasa hizi sredi kuhusu zitto, zimezidi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom