Zitto: Ndio ninautaka urais

Zitto: Ndio ninautaka urais

Status
Not open for further replies.
Hivi yule kiongozi wa Korea Kaskazini ana umri gani vile...??
yulke alichaguliwa au alirithishwa tu, umeshaona jokes wanazompiga huko kwao??? wanaonyesha yuko bize na playstation

tafuta mifano mizuri next time
 
Ni wiki moja sasa baada ya Zitto kabwe kutangaza kwamba atangombea urais uchaguzi ujao endapo atapitishwa na chama chake kumekuwa na hoja kwamba Zitto anafaa kugombea wengine wakipinga vikali na kudai Dr slaa bado anastahiri kugombea urais kwa mwaka 2015, sasa basi we unaonaje?
Kwa upande wangu napendekeza Dr slaa angombee ndiye agombee uchanguzi ujao ili tu aweze kubadilisha mfumo mzima wa nchi kwa miaka mitano tu na baada ya hapo ndipo Zitto aombe ridhaa kwa chama. Kwani watu wengi bado wanaimani sana na Dr Slaa kuliko hata Zitto.
Nawasilisha
 
Wana jf hii nimeinasa kwenye blog iitwayo yerickonyerere.wordpress.com

Nimeshangaa kuona kumbe wengi wanamuogopa zito kiasi cha kusema sana.

25 Mar 2012

Tanzania ni nchi iliyo mithiri ya karia hivi leo na ni nchi yenye lasilimali adhimu duniani,

Jambo la kujiuliza ni je watanzania ni watu wa aina gani? wanaendana na Tanzania ilivyo?

Ukweli ni kuwa watanzania ni wanafiki wakutisha zaidi ya baraza la Sanhedrin, unafiki wetu unatisha kwakuwa umechanganyika na ujinga, Hatuendani kabisa na wasifu wa taifa, Jambo hili ni hatari kwa mstakabali wa taifa kwakuwa kati yetu wajinga na wanafiki kumeibuka kundi la wahuni

Wahuni hawa ambao mbegu yake ni ujinga na unafiki wamekuwa hatari kuliko kawaida, haimithiriki hata kuwatazama kwa jicho la makengeza tu.

Watu hawa wahuni, wanafiki na walanguzi wa fikra wamefanikiwa kuvunja mlango wa siasa za Tanzania na kujikita humo wakiliyumbisha taifa watakavyo, Wanatumia mwito wa utandawazi msonge kujidukiza kisiasa.

Ninavyoamini taifa halijengwi na mwanasiasa bali mwanasiasa ana nafasi kubwa ya kulivunja taifa! Sasa tukiacha siasa hizi za kinafiki zitamalaki ndani ya ardhi ya Tanzania, vitukuu wetu watakuja kuyachapa viboko makaburi yetu. Watanzania kila mmoja kwa imani yake turudi uwalii.

Nashangaa namna siasa za majitaka zilivyoshamiri, magazeti na wanaoitwa waandishi tegemezi nao hawana tofauti, magazeti yamejaa taarifa ambazo hazina msaada wowote kwa watanzania, hatusikii juu ya Mafuta yetu, juu ya dhahabu yetu, juu ya ardhi yetu, juu ya kilimo chetu, juu ya afya zetu, juu ya utamaduni wetu, juu ya tunu za taifa, juu ya mustakabali wa taifa na utaifa wetu.

Heshima yetu imepotea mbele ya walimwengu, utu na nafasi yetu imedharaulika, wengine wanatuamulia mambo yetu, Kenya imetutawala, imetuzuia kujenga barabara serengeti, tumefyata mkia, wazalendo mkowapi? wapiganaji mkowapi? Wenye nchi mkowapi? Arumeru ni kitu kidogo sana ndani nchi, mama zetu, baba zetu, dada zetu, kaka zetu, wadogo zetu vijijin wanalia hawana afya, magonjwa, njaa umasikini vimewazonga, tunafanya nini mijini? Ni hili la Pamela Lowassa, Siyoi Sumari, na Nassari?

Nashindwa kuelewa, nchi imebaki na Wasira tu? Nape? Ndio policymakers wetu? Mwigulu? Slaa? Zitto? Kweli jamani? Usalama wa Taifa mnabeba dhamana kubwa sana ndani na nje ya ya Tanzania, fanyeni kazi kwaajili ya taifa la leo na lakesho si kwa kikundi fulani wala chama furalani, rasilimali zetu zinatoroshwa na magenge mumiani laki taasisi hii ipo na inatajwa kuwa kila palipo na watu watano basi mmoja wao ni Usalama wa taifa, lakini kwanini hali iwe hivi?

Tutumie fikra machipuko kwa upinde wa kijana, japo kuwa vijana wengi wanaakili za kuku, lakini kwa sauti ya mang’amuzi ya hekima watafunguliwa na kuacha utegemezi wa fikra,

Mimi ni muamini wa mtandao wa Twitter nikihudumu kwa njia ya @YerickoNyerere Niseme wazi, nimefadhaishwa na baadhi ya wanaoitwa wanasiasa vijana, hasa kijana mwenzangu mbunge wa Kigoma Kaskazini ndugu Zitto Zuberi Kabwe

Nimemtaja Zitto Kabwe kwakuwa anatumia ujinga na unafiki wa watanzania hasa vijana kujidukiza kisiasa kwa hoja dhaifu ya umri wa uraisi, na amefanikiwa kuteka mioyo ya wakware wa fikra kinyume na haki ya fikra huru.

Ukifuatitia vijana wengi wanaojadili na kuunga mkono juu ya hoja hiyo ya Umri wa Urais utabaini kuwa ni waumini wa upepo wa Zitto, Hawasemi faida ya hoja yao, wala hasara ya umri utumiwao kwa sasa, bali kwa jicho la tatu wamekuwa ni mashabiki wamuangaliao Zitto tu bila kujua mstakabali wa taifa lao.

Zitto ninamwamini sana kiutendaji ndani ya chama chake na nje ya chama, kupingwa kwa hoja yake hakutafsiriwi kuwa si kijana mtendakazi bora laa hasha, bali ni ashirio la kengele imwamshayo toka usingizini, tena usingizi wa ulevi mtawalia wa sifa za kisiasa.

Urais ni taasisi nyeti sana, tena hii ni nchi yoyote duniani huheshimu sana taasisi hii, Nimestushwa sana kuona kijana wetu Zitto aliyeonyesha dalili nzuri za kujengeka kisiasa na kiuongozi, akiwahi kuopoa nyama hata kabla ya kunawa mikono, anasema “ndio ninautaka urais” Hii ni kauli rahisi sana kisiasa lakini inabeba ujumbe wa aina mbili kwa mwanasiasa na raia wa kawaida.

Anawaarifu wanachama wake na wapambe wake kuwa uchaguzi ujao atagombea urais

Anawaonya viongozi wenzeke ndani ya chama kuwa yeye sasa ndiye lulu pekee ya urais.

Zitto bado hajafikia kuwa kiongozi wa juu zaidi kitaifa ndani ya chama chake achilia mbali kuwa rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Urais unahitaji hekima, Zitto hana kwa sasa, Urais unahitaji busara, Zitto hana kwa sasa, Urais ujasiri wa kweli Zitto hana kwa sasa,Urais unahitaji mtu wa kutafakuri, Zitto hana kwa sasa, Urais hauhitaji mtu mnafiki, Zitto kwa sasa ni mnafiki, Kwa ujumla Urais unahitaji mtu aliyepevuka, na Zitto bado hajapevuka.

Zitto anarubuniwa na kundi la wenye mtindio wa ubongo hasa vijana, wanaomuaminisha kuwa kapevuka na aweza kuongoza kizazi hiki cha nyoka ilihali bado safari yake ni ndefu.

Nimsihi kijana mwenzangu Zitto Kabwe, kuwa ni kweli anautaka urais lakini avute subira na kauli yake imeweka kovu ktk safari yake kisiasa, ambapo atumie muda uliopo kuliziba kovu hili. Ajitahidi kuwa na kifua kigumu chenye kuhifadhi magumu ya kisiasa, Si kila hoja imuhusuyo ni lazima aijibu na akiamua kujibu awatumie washauri wa masuala ya kisiasa.
Turekebishane ili kujenga taifa lenye uchumi imara, demokrasia imara, na siasa safi!

Mungu ibariki Tanzania mungu ibariki afrika!

- Nothing but majungu na empty theories nimeshindwa hata kuichambua neno kwa neno kwa sababu hamna hoja ila chuki tupu, naomba kusema hivi kama haya maneno ndio yanatakiwa kuwa a standard ya kua Rais wa Tanzania then ninawaomba wale wote mnaounga mkono mtoa mada hii mtuambie kwamba Zitto hawezi kuwa Rais bora kulinganisha na Mwinyi, Mkapa na Rais wa sasa kwa sababu wao wote wanatimiza ubora wa huu waraka ndio maana Tanzania tumeendela sana Zitto akiingia ataharibu maendeleo yetu tuliyoyapata na ma-Rais waliopita!

- I mean hizi chuki Wa-Tanzania tumejifunzia wapi we are very good na machuki yasiyo na hoja wala msingi, I mean li-article lirefu lakini ndani yake hewa tupu! Muandishi anajikanyaga kanyaga tu, pelekeni hizi chuki huko kwenye vyama venu msituletee kwenye Taifa, kuna a big progress ya Vijana na uongozi wa taifa letu, sasa msiharibu the pattern kwa sababu ya chuki zenu za binafsi huko kwenye vyama vyenu, Zitto ni just a symbol people sasa tuwe waangalifu na hii mijadala kwa sababu itaishia kuweka mandate kwa taifa kwamba vijana wote ni kama Zitto na wakati hana kosa lolote zaidi tu ya machuki machuki ya binafsi, I mean binadam anawezaje kuwa positive na maisha yake ya binafsi na machuki yote haya ya hii article in him? no wonder hili taifa tumekwama tumebakia chuki tupu1

Es!
 
Chanel zote zipo Arumeru Mashariki, haya mengine tutayazungumzia wakati ukifika
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Zitto siyo kuwa hajakoma, ana haki na kakomaa, hebu fikilieni wanajamvi hivi mnakumbuka marais wa nchi hii, mbona wengine Zitto keshawashinda vigezo? Labda umri lakini mambo mengine yuko juu yao, Kwa hekima hebu pima kati ya Zitto na Mkapa!!
 
Lete hoja zenye kwenda na wakati. Tuna mambo mengi ya kufanya sasa kabla ya kuuuliza rais 2015 ni nani. Tuchangie katiba mpya wakati ukifika. Tutoe nafasi kwa wagombea binafsi tupanue wigo. Mjadala huu umeminywa na katiba ya sasa ya mgombea lazima atoke kwenye chama. Wapo wengi wanaoweza kugombea urais na wakawa wazuri bila chama
 
hoja hazina msingi, wakati ukifika chama kitaamua mbinu gani kitumie kumpata mgombea, chadema sio ccm jamani!
 
Huyo jamaa ni mbishi aliyepitiliza. Ma-radicals kama huyu hawatakiwi kupewa mamlaka makubwa sana.unaongelea maadili?huyu kama alijibizana na balozi kwenye kikao kama vile anajibizana na kimada wake mbele ya jumuiya ya watanzania atashindwa kufanya nini?kama aliweza kupotosha mdahalo chuoni na kugawa darasa profesa akagomea darasa hadi likafikia kwenye seneti ya chuo na ubalozi wa tanzania unategemea nini?kama aliweza kutembea na profesa wake unategemea awe na maadili gani aidi? kama aliweza kusababisha vurugu alipokuwa angombea chuo kikafungwa badala ya kujutia yeye akawa anawahi mahakamani kupinga amri ya chuo kumzuia kugombea unategemea nini?damu ya watu ilimwagika lakini alijifaragua tu kwenye kampeni zake kusimama dakika moja kabla ya kampeni ili kuvuta kura.Hii ndiyo aina ya akina Ghaddafi,kagame au huyu wa syria?

nilishamwambia tanzania haiko tayari kuongozwa na mujahidini au ma-ayattolaah.kama wanataka wahamie Iran kwa maradicals wenzao.waroho wakubwa wa madaraka hawa.Huu mtandao wao sasa ni mkubwa kuliko mnavyofikiria wakuu.Hili ni kundi ambalo litaleta vita kali dhidi ya wazee naona hadi vijana wa CCM akina Nape,Makamba na akina Bashe wako kundi hili.aliposimama Bashe na kuwaambia wazee ni tatizo haikuwa kwa bahati mbaya.huyu dogo Ben Saanane ana kisirani kibaya sana. ila ninachoona ni kwamba kama Zitto huko baadae atakuwa mwenyekiti wa chama chao au Rais na kwa jinsi ninavyoona anaungwa mkono na hawa vijana itakuja kutokea kama ya Zuma na Malema.

Maskini Freeman Mbowe watetezi wake wanazidiwa nguvu.kiboko ya hawa ni kutafuta wasomi nguli kuliko wao wanaojua kujenga hoja kwa umahiri ili kukabiliana nao.Nimesoma andiko la zitto nimegundua anaweza kujenga hoja na kuhamisha hata mawazo ya watu.hawa ni mabingwa wa propaganda. Saanane,ana uwezo mkubwa ni msomi aliyebobea na anajiamini isipokuwa akitumia taaluma yake vizuri na kujiamini kwake anaweza kukisaidia chama.Hizi raslimali anazoelekeza kwa kundi la Zitto zitaleta athari kwa vijana.Angesaidiana na John Heche kuisuka Bavicha naamini hali ya jumuiya hiyo ingekuwa imebadilika.Huyu dogo huwezi kumshauri hilo sana sana atakujibu kwa kukudhalilisha na watu watamuamini. Bavicha imegawanyika,makamu mwenyekiti girlfriend wa saanane yupo kundi la akina zitto.je kwa staili hii huko mbele si kuna mpasuko mkubwa?wiki mbili tu nilitabiri kama zitto atagombea uenyekiti wa chama au urais tutarajie mpasuko huko chadema kwa kuwa najua vijana alio nao kundi moja mbowe hataweza kuhimili vishindo vyao.hili ndilo linalotokea sasa


hawa wako tayari kuua ili wapate wanachotaka

Mwenye uwezo wa kujenga hoja na anayekubalika ushindi wa simple majority below 50% unaleta picha gani kwa mwanasiasa makini?

[TABLE="class: arc90_altrows-Blue"]
[TR]
[TD="bgcolor: #B3D5E6, colspan: 4"]KIGOMA
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: #B3D5E6, colspan: 4"]WILAYA YA KIGOMA[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: #B3D5E6, colspan: 4"]KIGOMA KASKAZINI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 30%, bgcolor: #B3D5E6"]Candidate[/TD]
[TD="width: 20%, bgcolor: #B3D5E6, align: center"]
Political Party
[/TD]
[TD="width: 20%, bgcolor: #B3D5E6, align: center"]
Number of Votes
[/TD]
[TD="width: 15%, bgcolor: #B3D5E6, align: center"]
Percentage Votes
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 30%"] ZITTO KABWE ZUBERI [/TD]
[TD="width: 20%"]
CHADEMA
[/TD]
[TD="width: 20%"]23,366[/TD]
[TD="width: 15%"] 48.57[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 30%"] LEMBO ROBINSON FULGENCE [/TD]
[TD="width: 20%"]
CCM
[/TD]
[TD="width: 20%"]18,352[/TD]
[TD="width: 15%"] 38.15[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 30%"] OMARY MUSSA NKWARULO [/TD]
[TD="width: 20%"]
CUF
[/TD]
[TD="width: 20%"]4,839[/TD]
[TD="width: 15%"] 10.06[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 30%"] CHONGERA HARUNA CHONGERA [/TD]
[TD="width: 20%"]
CHAUSTA
[/TD]
[TD="width: 20%"]264[/TD]
[TD="width: 15%"] 0.55[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 30%"] MFAUME HAMISI MFAUME [/TD]
[TD="width: 20%"]
APPT - MAENDELEO
[/TD]
[TD="width: 20%"]108[/TD]
[TD="width: 15%"] 0.22[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 30%"] AUGUSTINO PETER MBOLEGWA [/TD]
[TD="width: 20%"]
SAU
[/TD]
[TD="width: 20%"]88[/TD]
[TD="width: 15%"] 0.18[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 30%"] GERMANI MAULIDI MLETE [/TD]
[TD="width: 20%"]
DP
[/TD]
[TD="width: 20%"]87[/TD]
[TD="width: 15%"] 0.18[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 30%"] HAMISI FADHILI KISWAGA [/TD]
[TD="width: 20%"]
NRA
[/TD]
[TD="width: 20%"]47[/TD]
[TD="width: 15%"] 0.1[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 30%"] MAUWA SHAURI KAMANA [/TD]
[TD="width: 20%"]
JAHAZI ASILIA
[/TD]
[TD="width: 20%"]19[/TD]
[TD="width: 15%"] 0.04[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 30%"] TATU SAIDI HUSSEIN [/TD]
[TD="width: 20%"]
UMD
[/TD]
[TD="width: 20%"]8[/TD]
[TD="width: 15%"] 0.02[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 30%"] [/TD]
[TD="width: 20%"] [/TD]
[TD="width: 5%"] [/TD]
[TD="width: 15%"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 10%"]SPOILT VOTES[/TD]
[TD="width: 20%"] [/TD]
[TD="width: 20%"]927[/TD]
[TD="width: 15%"] 1.93 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 10%"]TOTALS[/TD]
[TD="width: 20%"] [/TD]
[TD="width: 20%"] 48,105[/TD]
[TD="width: 15%"] 100 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 30%"] [/TD]
[TD="width: 20%"] [/TD]
[TD="width: 5%"] [/TD]
[TD="width: 15%"] [/TD]
[/TR]
[/TABLE]

 
Kikwete na Lowasa nani anafaa kuwa mwenyekiti wa CCM? nadhani hapa ndipo tunapopaswa kuanzia maana CCM ndio ina uchaguzi wa ndani mwaka huu.
 
Haya ndio zitto alikuwa akiyataka kwa kuhamisha macho na mawazo ye2 toka Arumeru kuzungumzia urais wa 2015.
 
Wote wanafaa kama ilvyo pia kwa Tundu Lissu na Mnyika. Ikifika 2015 ndo itajulikana nani anafaaa zaidi kwa wakati huo. Kwa sasa hata ukiambiwa haitakusaidia kitu.
 
Mwenye uwezo wa kujenga hoja na anayekubalika ushindi wa simple majority below 50% unaleta picha gani kwa mwanasiasa makini?

Hivi matokeo ya ushindi wa simple majority below 50% yana uhusiano wowote na uwezo wa kujenga hoja na kukubalika?
 
Hivi matokeo yana uhusiano wowote na uwezo wa kujenga haoja na kukubalika?
Hapa unajaribu kuuliza nini!?......hueleweki hivi mwanasiasa kama hukubaliki na huna hoja ulizojenga ni kwa nini uchaguliwe wewe unategemea utapigiwaje kura? labda members wengine watakuelewa mimi nimeshindwa kukuelewa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom