Zitto: Ndio ninautaka urais

Zitto: Ndio ninautaka urais

Status
Not open for further replies.
Topical,

..mimi nadhani busara tu ilipaswa kumuelekeza Zitto kwamba huu si wakati wa kutangaza nia ya kugombea Uraisi.

..wakati mwingine haya mambo yanakuja na UMRI, na pia EXPOSURE.

Hujasoma article alikuwa akimjibu mwandishi na jamaa wakaichukua out of context

Besides kwa taratibu za chadema sidhani kama amekiuka katiba na haki yake

Kama ni mwiko kufanya hivyo ni wakati muafaka kwa chadema kufanya maamuzi magumu

Wampe adhabu stahili mhusika, naamini hakuna aliye juu ya chama
 
Mahaba yako kwa Zitto Kabwe ndiyo yanayokutia upofu, mpaka dakika hii ninavyotype comment hii, Zitto hana sifa za kuwa mgombea Urais wa nchi hii, achilia mbali Urais wenyewe.......
Ningekushauri wewe ndio ukalale ujipange upya, labda nikupe home work ya kurudi nayo hapa, ni sababu zipi zinazowafanya CCM na vibaraka wake wampende Zitto na siyo Dr Slaa!!??.......

Umejuaje vibaraka wa ccm?

Umejuaje kwamba ccm wanamuogopa Slaa?

Any evidence, given that alipigwa chini 2010; unafikri 2015 na majeraha yote ana lolote huyo padre? sidhani
 
Mahaba yako kwa Zitto Kabwe ndiyo yanayokutia upofu, mpaka dakika hii ninavyotype comment hii, Zitto hana sifa za kuwa mgombea Urais wa nchi hii, achilia mbali Urais wenyewe.......
Ningekushauri wewe ndio ukalale ujipange upya, labda nikupe home work ya kurudi nayo hapa, ni sababu zipi zinazowafanya CCM na vibaraka wake wampende Zitto na siyo Dr Slaa!!??.......

Mkuu mimi huwa sina mahaba na mtu; mimi huwa nina mahaba na hoja zinazopalilia demokrasia kuanzia kwenye vyama vya siasa ili kustawisha demokrasia ndani ya nchi.

Kama CCM na vibaraka wake wanampenda mimi sijui labda unisaidie hizo sababu labda ndizo zinakufanya useme hana sifa.

Ninachokipinga ni kwamba Zitto hana sifa. Mimi najua kwamba ana sifa za kikatiba (ukiachilia hiyo ya umri) ambayo yeye mwenyewe ameisema vizuri tu kwamba kama Katiba itakuwa imeruhusu. Sasa Mkuu wewe unasema hana sifa ila husemi hana sifa kwa vipi? Hapo ndipo nashindwa kukuelewa.
 
Tanzania siyo nchi ya kifalme..kwa hiyo kila mtu anaweza kuwa rais, kupitia sanduku la kura!

Kama hutaki unaonyesha hasira yako kweny ballot box.

Au mnamzuia asigombee kwenye chama chenu ambacho huwaga ina watu special wanaotakiwa kuwa marais..

Naomba nikuulize hao watu ambao wanafaa kuwa marais (special species) wanatokea wapi? tutafute ubini wao..

Huwa najiuliza mara nyingi ni kwa nini kiwango cha ufaulu kinashuka kila matokeo yakitangazwa kumbe jibu lake ni rahisi sana.
Ni nani aliyekwambia Tanzania ni ya kifalme? na nakuthibitishia si kila Mtanzania mwenye haki ya kuwa Rais, bali ni Watanzania wale wenye sifa tu ndio wanaweza kupata fursa hii ya kugombea au kuupata huo Urais na kwa bahati mbaya Zitto Kabwe hana sifa za kuwa Rais kwa sasa.

Na ningeshauri Watanzania wawe makini na hawa wansiasa uchwara wanaopenda katiba mpya iandikwe kwa maslahi yao maana wakipata madaraka watu wa Namna hii watakuwa ni kazi yao kubadilisha katiba ili wabaki madarakani.
 
Mkuu mimi huwa sina mahaba na mtu; mimi huwa nina mahaba na hoja zinazopalilia demokrasia kuanzia kwenye vyama vya siasa ili kustawisha demokrasia ndani ya nchi.

Kama CCM na vibaraka wake wanampenda mimi sijui labda unisaidie hizo sababu labda ndizo zinakufanya useme hana sifa.

Ninachokipinga ni kwamba Zitto hana sifa. Mimi najua kwamba ana sifa za kikatiba (ukiachilia hiyo ya umri) ambayo yeye mwenyewe ameisema vizuri tu kwamba kama Katiba itakuwa imeruhusu. Sasa Mkuu wewe unasema hana sifa ila husemi hana sifa kwa vipi? Hapo ndipo nashindwa kukuelewa.

Shule mnazosoma sina hakika kama huwa zinawasaidia, hivi kijana wa miaka 15 akija kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura inatakiwa umjibu lipi kati ya haya?
a. Unazo sifa za kuandikishwa
b. Huna sifa za kuandishwa
 
Kuwa wazi basi mkuu. Nataka niamini kwamba una maana kwamba hana sifa kwa sasa kwa sababu ya umri au? Kama hivyo sawa
 
Huwa najiuliza mara nyingi ni kwa nini kiwango cha ufaulu kinashuka kila matokeo yakitangazwa kumbe jibu lake ni rahisi sana.
Ni nani aliyekwambia Tanzania ni ya kifalme? na nakuthibitishia si kila Mtanzania mwenye haki ya kuwa Rais, bali ni Watanzania wale wenye sifa tu ndio wanaweza kupata fursa hii ya kugombea au kuupata huo Urais na kwa bahati mbaya Zitto Kabwe hana sifa za kuwa Rais kwa sasa.

Na ningeshauri Watanzania wawe makini na hawa wansiasa uchwara wanaopenda katiba mpya iandikwe kwa maslahi yao maana wakipata madaraka watu wa Namna hii watakuwa ni kazi yao kubadilisha katiba ili wabaki madarakani.

Sawa mwalimu ambaye una akili sana..mshukuru mungu wako..

Haya tuambie hao wenye sifa ya kuwa rais ni kina nani?

Na sifa zenyewe ni zipi?
 
Shule mnazosoma sina hakika kama huwa zinawasaidia, hivi kijana wa miaka 15 akija kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura inatakiwa umjibu lipi kati ya haya?
a. Unazo sifa za kuandikishwa
b. Huna sifa za kuandishwa

Mkuu mimi huwa sina mahaba na mtu; mimi huwa nina mahaba na hoja zinazopalilia demokrasia kuanzia kwenye vyama vya siasa ili kustawisha demokrasia ndani ya nchi.

Kama CCM na vibaraka wake wanampenda mimi sijui labda unisaidie hizo sababu labda ndizo zinakufanya useme hana sifa.

Ninachokipinga ni kwamba Zitto hana sifa. Mimi najua kwamba ana sifa za kikatiba (ukiachilia hiyo ya umri) ambayo yeye mwenyewe ameisema vizuri tu kwamba kama Katiba itakuwa imeruhusu. Sasa Mkuu wewe unasema hana sifa ila husemi hana sifa kwa vipi? Hapo ndipo nashindwa kukuelewa.

Mkuu Zitto mwenyewe ameongea kuhusu umri na kusema kama katiba itaruhusu. Kwa hiyo hilo si suala la kujadili tunajadili sifa zingine ukiachilia mbali hiyo ambayo ni subject to change of the Constitution reagrding minimum age of presidential aspirants. Sasa ugomvi uko wapi?
 
Ndipo hoja ya umri hapa inapopata nguvu zaidi, yaani tupo kwenye mchakato wa Katiba ya Wananchi na ni sisi Wananchi ndio tutakaosema tunataka katiba gani halafu anatakoa mtu mwenye uchu na ulevi wa madaraka na kuanzisha mijadala ambayo haina tija!...nadhani kwa mtu mzima mwenye busara za kutosha hawezi kufanya hivyo na hapa hoja ya umri inazidi kupata nguvu kwamba miaka 35 BIG NO.

Niko interested sana Zitto aje hapa kutoa maelezo ni nini kinaendelea kati yake na Deputy Director wa Idara ya Usalama wa Taifa. hapa ninajuwa ninachokisimamia na ninachoamini, na tukienda mbali zaidi nasikitika kuwajulisha mashabiki wake msishangae Zitto akikataliwa Ubunge jimboni kwake mwaka 2015 katika masanduku ya kura.
Zitto Kabwe ndiye mbunge pekee ambaye alitaka kugombea Ubunge kwenye majimbo matano tofauti kwenye uchaguzi wa 2010, na alipogombea kwao Kigoma Ushindi wake ulipungua kura alizopata kufananisha na zile za mwaka 2000.
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Zitto: Nitagombea urais 2015[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD]
zitto-kabwe-top-safi.jpg
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema),Zitto Kabwe​
Sitta awashangaa CCM wanamhofia kwa nafasi hiyo
Fidelis Butahe
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Zitto Kabwe ameibuka na kusema kuwa anataka kuwa rais wa Tanzania mwaka 2015.Wakati Zitto akitoa kauli hiyo nzito, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta naye amesema anashangazwa na watu wanaoweweseka wanaposikia kuwa mwanasiasa huyo anayeongoza vita dhidi ya ufisadi ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki, anataka kuwania urais.

Kauli hiyo ya Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini na Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni huenda ikaibua mjadala mzito ndani ya chama chake, ukiacha zile mbio za vigogo wa CCM wanaotajwa kuutaka urais 2015.

Katika taarifa yake aliyoituma jana kwa gazeti la Mwananchi Jumapili, Zitto alisema; “ Kwanza niseme wazi kabisa kuwa Urais ninautaka, nchi inahitaji kiongozi wa juu atakayekabili changamoto hizi. Ninaamini ninaweza kuwaongoza Watanzania wenzangu kukabili changamoto hizi.” Alitamba anao uwezo kwa kuwa ni mzalendo, mwenye utashi wa kuleta mabadiliko stahiki kulingana na nchi inavyoongozwa. Katika taarifa hiyo ameeleza kuwa kwa sasa nchi imesahau maendeleo ya watu badala yake imejikita katika maendeleo ya vitu.

“Ninajua kuwa hivi sasa viongozi wetu wengi wanaangalia zaidi mitindo badala ya mambo ya msingi,” Zitto amesema taarifa na kuongeza: “Ninajua kuwa maendeleo vijijini yamesahaulika, ninajua nchi yetu inahitaji uongozi wa kufanya mabadiliko makubwa badala ya mabadiliko ya juujuu.” Alieleza kuwa mabadiliko makubwa yanahitaji maamuzi magumu yatakayoudhi wengi hasa vigogo wa nchi za Magharibi huku akitoa mfano kuwa ni pamoja na kuzuia nchi kuuza malighafi pekee. Alisisitiza kuwa rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma ndio kikwazo kikubwa cha maendeleo ya nchi na kwamba lazima hatua madhubuti zichukuliwe kuzuia na kutokomeza ufisadi.

“Rasilimali kama madini, mafuta, gesi asilia, ardhi na nyinginezo ni lazima zifaidishe wananchi wa nchi yetu,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo. Sababu za kutaka Urais Katika taarifa hiyo Zitto alieleza kuwa kwa sasa nchi inahitaji kiongozi wa juu atakayekabili changamoto muhimu na kwamba yeye anaweza kuwaongoza Watanzania kukabiliana na changamoto hizo. “Sio kazi rahisi, lakini ni kazi ambayo lazima Mtanzania mmoja aifanye, mimi nataka kuifanya, nina uwezo wa kuifanya,” alitamba katika taarifa hiyo.

Alieleza kuwa hata kama anaitaka kazi hiyo, ni lazima Watanzania walio wengi waamue, pia ni lazima Chadema kiseme wazi kuwa yeye ndio anastahili kuifanya kazi hiyo na kwamba kuitaka tu nafasi hiyo hakutoshi bila ridhaa hizo. “Kama wananchi watasema huyu Zitto anapaswa kubeba jukumu hili mwaka 2015 tuache iwe. Kama watasema hapana wewe bado mpaka mwaka 2020 au 2025 tuache iwe hivyo. Pia Kama hawataki kabisa tuache iwe hivyo,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Umri wa kugombea urais Katika taarifa hiyo, Zitto alieleza kuwa mjadala wa umri wa kugombea urais umekuwa mkali na kwamba baadhi ya watu kwa sababu zao binafsi, wameamua kuuita ni mjadala wake na Mbunge wa Bumbuli January Makamba ambao unaowabagua wazee.
Alisema kuwa mjadala huo aliouita wa ‘kupandikiza chuki na sumu za kibaguzi’ ni wa kitabaka, unaonyesha kuwa Zitto na January sio tabaka stahili la vijana walio wengi. Huku akionyesha kujibu makala katika moja ya magazeti(sio ya Mwananchi Communications Limited) ambayo haikupinga umri bali hoja ya wanaoujadili urais na vyama wanavyotoka kutowapika vilivyo vijana kuwa viongozi, Zitto alieleza kuwa hali hiyo inaonyesha ubaguzi wa wazi.

“Ingawa sisi sio waanzilishi wa hoja hii lakini ni hoja ya kibaguzi. Nawashangaa wasomi wa siku hizi kwa kujadili watu badala ya hoja,” ilieleza taarifa hiyo. Chadema kukuza vijana Alieleza kuwa Chadema kinalea na kukuza vijana kuwa viongozi na kwamba yeye alijiunga na chama hicho akiwa na umri wa miaka 16 huku akipewa majukumu mbalimbali.
Alisema kuwa wakati akisoma Chuo Kikuu Dar es Salaam(UDSM), Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wakati huo akiwa Mbunge wa Jimbo la Hai, alimuomba kushiriki kikamilifu kukijenga chama hicho kutokana na kukimbiwa na wanachama isipokuwa wale waliokuwa wakitokea Kigoma, Kilimanjaro, Shinyanga, Karatu na Ukerewe.

“Mwaka 2001 muongo mmoja uliopita ni mimi na Mbowe ndio tuliofanya mabadiliko yote yanayoonekana Chadema. Tumeingiza watu wapya na tumeandika Katiba upya, tulichambua mambo mengi na Mbowe kuijenga Chadema,” alieleza katika taarifa hiyo.

Alieleza kuwa mwaka 2005 Mbowe aligombea urais na kwamba walijua kuwa watashindwa ila walitaka kukijenga chama hicho na walipata wabunge na kuongeza kuwa mwaka 2010, Chadema kilishiriki uchaguzi mkuu kama chama imara kinachokwenda kuchukua dola. Huo ndio ukawa mwanzo wa kuibuka kwa wabunge John Mnyika (Ubungo), Halima Mdee (Kawe), wabunge ambao alieleza kuwa awali walionyesha wasiwasi mkubwa kujiingiza katika siasa.
“Baadhi ya watu wazima waliingia Chadema kwa sababu ya vijana, nani anasema hatulei vijana kuwa viongozi wazuri, nani haoni hazina ya viongozi vijana hivi sasa ndani ya Bunge kutoka vyama vyote. Kuna namna bora ya kulea viongozi zaidi ya kuwapa majukumu?” Alihoji katika taarifa hiyo.

Hoja ijadiliwe Katika taarifa hiyo Zitto alifafanua kuwa hoja ya umri wa kugombea urais iwe na mahali pakuanzia na inapaswa kujadiliwa bila kuangalia majina ya wanaotetea hoja hiyo. Suala hilo lijadiliwe kwa faida na hasara zake na kufafanua kuwa hakuna anayejua kuwa yeye atakuwa hai mwaka 2015 na kwamba isiandikwe katiba yenye kupanua wigo wa kutoa haki ya kugombea urais kwa sababu yake.
Samuel Sitta

Akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali katika Tamasha Vyombo vya Habari lililofanyika jana kwenye Ukumbi Msasanki Beach, Dar es Salaam, Sitta alieleza kuwa anashangazwa na watu wanaoweweseka wakisikia anataka kuwania urais mwaka 2015.

"Nashangaa watu wanapata kiwewe kusikia nataka kuwania urais, kuwania urais ni haki ya kila Mtanzania na Watanzania ndiyo watakaoamua nani ni mzuri na atawafaa," alisema Sitta na kushangiliwa na waliohudhuria tamasha hilo.

"2015 tunataka kuwa na mwelekeo mzuri, nikiwa na maana mambo ya hongo, ubadhirifu hatutaki yawe na nafasi, alisema Sitta na kuongeza:

"Kuna hadithi moja, siku moja trafiki mmoja alikamata gari pale Mwenge (Dar es Salaam) akaomba, leseni, akaangalia kadi ya gari sasa yule mama alikuwa na mtoto wake ana miaka kama minane, akamwambia mama yake, mpe kitu kidogo...hivi imefikia hatua hata mtoto wa miaka minane anajua rushwa."

Alisema rushwa imesababisha nchi kuingia mikataba ya uongo, kuna mikataba mingi ya uongo na ndio maana leo hii nchi imefika hapa ilipo.

"Hii imesababisha matatizo hadi ya umeme, tungeweza kuuza umeme wetu nje, lakini leo haiwezekani, nasema haya kama mzee wenu na kiongozi wenu.

"Sasa, nawaasa waandishi, msikubali kuwa mawakala wa viongozi waongo, msikubali uongo na kama tungeendelea kule uongo, nchi ingeharibika...hatuwezi kusonga mbele kwa uongo na vyombo vyenu visitumike kusambaza mambo ya uongo," Sitta alishauri.
Alisema watu wanatumia fedha nyingi kusaka urais na hata wengine kutumia ndumba kwa kwenda Mlingotini, Bagamoyo, kwa nia ya kutaka uongozi na matokeo yake kama watu hao watashinda lengo la kwanza linakuwa kurudisha fedha walizotumia.

Alivipongeza vyombo vya habari kwa kazi nzuri ya kufichua maovu ndani ya jamii na kuwataka viongozi wawe wastahimilivu wanapoandikwa maovu yao.Aliwaasa viongozi wenzake kutanguliza uzalendo kwa nchi na kuwataka wachape kazi kwa maslahi ya taifa vinginevyo watarudisha nyuma maendeleo ya nchi[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Zitto: Nitagombea urais 2015

Last edited by a moderator:
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Zitto: Nitagombea urais 2015[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD]
zitto-kabwe-top-safi.jpg
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema),Zitto Kabwe​
Sitta awashangaa CCM wanamhofia kwa nafasi hiyo
Fidelis Butahe
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Zitto Kabwe ameibuka na kusema kuwa anataka kuwa rais wa Tanzania mwaka 2015.Wakati Zitto akitoa kauli hiyo nzito, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta naye amesema anashangazwa na watu wanaoweweseka wanaposikia kuwa mwanasiasa huyo anayeongoza vita dhidi ya ufisadi ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki, anataka kuwania urais.

Kauli hiyo ya Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini na Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni huenda ikaibua mjadala mzito ndani ya chama chake, ukiacha zile mbio za vigogo wa CCM wanaotajwa kuutaka urais 2015.

Katika taarifa yake aliyoituma jana kwa gazeti la Mwananchi Jumapili, Zitto alisema; " Kwanza niseme wazi kabisa kuwa Urais ninautaka, nchi inahitaji kiongozi wa juu atakayekabili changamoto hizi. Ninaamini ninaweza kuwaongoza Watanzania wenzangu kukabili changamoto hizi." Alitamba anao uwezo kwa kuwa ni mzalendo, mwenye utashi wa kuleta mabadiliko stahiki kulingana na nchi inavyoongozwa. Katika taarifa hiyo ameeleza kuwa kwa sasa nchi imesahau maendeleo ya watu badala yake imejikita katika maendeleo ya vitu.

"Ninajua kuwa hivi sasa viongozi wetu wengi wanaangalia zaidi mitindo badala ya mambo ya msingi," Zitto amesema taarifa na kuongeza: "Ninajua kuwa maendeleo vijijini yamesahaulika, ninajua nchi yetu inahitaji uongozi wa kufanya mabadiliko makubwa badala ya mabadiliko ya juujuu." Alieleza kuwa mabadiliko makubwa yanahitaji maamuzi magumu yatakayoudhi wengi hasa vigogo wa nchi za Magharibi huku akitoa mfano kuwa ni pamoja na kuzuia nchi kuuza malighafi pekee. Alisisitiza kuwa rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma ndio kikwazo kikubwa cha maendeleo ya nchi na kwamba lazima hatua madhubuti zichukuliwe kuzuia na kutokomeza ufisadi.

"Rasilimali kama madini, mafuta, gesi asilia, ardhi na nyinginezo ni lazima zifaidishe wananchi wa nchi yetu," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo. Sababu za kutaka Urais Katika taarifa hiyo Zitto alieleza kuwa kwa sasa nchi inahitaji kiongozi wa juu atakayekabili changamoto muhimu na kwamba yeye anaweza kuwaongoza Watanzania kukabiliana na changamoto hizo. "Sio kazi rahisi, lakini ni kazi ambayo lazima Mtanzania mmoja aifanye, mimi nataka kuifanya, nina uwezo wa kuifanya," alitamba katika taarifa hiyo.

Alieleza kuwa hata kama anaitaka kazi hiyo, ni lazima Watanzania walio wengi waamue, pia ni lazima Chadema kiseme wazi kuwa yeye ndio anastahili kuifanya kazi hiyo na kwamba kuitaka tu nafasi hiyo hakutoshi bila ridhaa hizo. "Kama wananchi watasema huyu Zitto anapaswa kubeba jukumu hili mwaka 2015 tuache iwe. Kama watasema hapana wewe bado mpaka mwaka 2020 au 2025 tuache iwe hivyo. Pia Kama hawataki kabisa tuache iwe hivyo," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Umri wa kugombea urais Katika taarifa hiyo, Zitto alieleza kuwa mjadala wa umri wa kugombea urais umekuwa mkali na kwamba baadhi ya watu kwa sababu zao binafsi, wameamua kuuita ni mjadala wake na Mbunge wa Bumbuli January Makamba ambao unaowabagua wazee.
Alisema kuwa mjadala huo aliouita wa ‘kupandikiza chuki na sumu za kibaguzi' ni wa kitabaka, unaonyesha kuwa Zitto na January sio tabaka stahili la vijana walio wengi. Huku akionyesha kujibu makala katika moja ya magazeti(sio ya Mwananchi Communications Limited) ambayo haikupinga umri bali hoja ya wanaoujadili urais na vyama wanavyotoka kutowapika vilivyo vijana kuwa viongozi, Zitto alieleza kuwa hali hiyo inaonyesha ubaguzi wa wazi.

"Ingawa sisi sio waanzilishi wa hoja hii lakini ni hoja ya kibaguzi. Nawashangaa wasomi wa siku hizi kwa kujadili watu badala ya hoja," ilieleza taarifa hiyo. Chadema kukuza vijana Alieleza kuwa Chadema kinalea na kukuza vijana kuwa viongozi na kwamba yeye alijiunga na chama hicho akiwa na umri wa miaka 16 huku akipewa majukumu mbalimbali.
Alisema kuwa wakati akisoma Chuo Kikuu Dar es Salaam(UDSM), Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wakati huo akiwa Mbunge wa Jimbo la Hai, alimuomba kushiriki kikamilifu kukijenga chama hicho kutokana na kukimbiwa na wanachama isipokuwa wale waliokuwa wakitokea Kigoma, Kilimanjaro, Shinyanga, Karatu na Ukerewe.

"Mwaka 2001 muongo mmoja uliopita ni mimi na Mbowe ndio tuliofanya mabadiliko yote yanayoonekana Chadema. Tumeingiza watu wapya na tumeandika Katiba upya, tulichambua mambo mengi na Mbowe kuijenga Chadema," alieleza katika taarifa hiyo.

Alieleza kuwa mwaka 2005 Mbowe aligombea urais na kwamba walijua kuwa watashindwa ila walitaka kukijenga chama hicho na walipata wabunge na kuongeza kuwa mwaka 2010, Chadema kilishiriki uchaguzi mkuu kama chama imara kinachokwenda kuchukua dola. Huo ndio ukawa mwanzo wa kuibuka kwa wabunge John Mnyika (Ubungo), Halima Mdee (Kawe), wabunge ambao alieleza kuwa awali walionyesha wasiwasi mkubwa kujiingiza katika siasa.
"Baadhi ya watu wazima waliingia Chadema kwa sababu ya vijana, nani anasema hatulei vijana kuwa viongozi wazuri, nani haoni hazina ya viongozi vijana hivi sasa ndani ya Bunge kutoka vyama vyote. Kuna namna bora ya kulea viongozi zaidi ya kuwapa majukumu?" Alihoji katika taarifa hiyo.

Hoja ijadiliwe Katika taarifa hiyo Zitto alifafanua kuwa hoja ya umri wa kugombea urais iwe na mahali pakuanzia na inapaswa kujadiliwa bila kuangalia majina ya wanaotetea hoja hiyo. Suala hilo lijadiliwe kwa faida na hasara zake na kufafanua kuwa hakuna anayejua kuwa yeye atakuwa hai mwaka 2015 na kwamba isiandikwe katiba yenye kupanua wigo wa kutoa haki ya kugombea urais kwa sababu yake.
Samuel Sitta

Akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali katika Tamasha Vyombo vya Habari lililofanyika jana kwenye Ukumbi Msasanki Beach, Dar es Salaam, Sitta alieleza kuwa anashangazwa na watu wanaoweweseka wakisikia anataka kuwania urais mwaka 2015.

"Nashangaa watu wanapata kiwewe kusikia nataka kuwania urais, kuwania urais ni haki ya kila Mtanzania na Watanzania ndiyo watakaoamua nani ni mzuri na atawafaa," alisema Sitta na kushangiliwa na waliohudhuria tamasha hilo.

"2015 tunataka kuwa na mwelekeo mzuri, nikiwa na maana mambo ya hongo, ubadhirifu hatutaki yawe na nafasi, alisema Sitta na kuongeza:

"Kuna hadithi moja, siku moja trafiki mmoja alikamata gari pale Mwenge (Dar es Salaam) akaomba, leseni, akaangalia kadi ya gari sasa yule mama alikuwa na mtoto wake ana miaka kama minane, akamwambia mama yake, mpe kitu kidogo...hivi imefikia hatua hata mtoto wa miaka minane anajua rushwa."

Alisema rushwa imesababisha nchi kuingia mikataba ya uongo, kuna mikataba mingi ya uongo na ndio maana leo hii nchi imefika hapa ilipo.

"Hii imesababisha matatizo hadi ya umeme, tungeweza kuuza umeme wetu nje, lakini leo haiwezekani, nasema haya kama mzee wenu na kiongozi wenu.

"Sasa, nawaasa waandishi, msikubali kuwa mawakala wa viongozi waongo, msikubali uongo na kama tungeendelea kule uongo, nchi ingeharibika...hatuwezi kusonga mbele kwa uongo na vyombo vyenu visitumike kusambaza mambo ya uongo," Sitta alishauri.
Alisema watu wanatumia fedha nyingi kusaka urais na hata wengine kutumia ndumba kwa kwenda Mlingotini, Bagamoyo, kwa nia ya kutaka uongozi na matokeo yake kama watu hao watashinda lengo la kwanza linakuwa kurudisha fedha walizotumia.

Alivipongeza vyombo vya habari kwa kazi nzuri ya kufichua maovu ndani ya jamii na kuwataka viongozi wawe wastahimilivu wanapoandikwa maovu yao.Aliwaasa viongozi wenzake kutanguliza uzalendo kwa nchi na kuwataka wachape kazi kwa maslahi ya taifa vinginevyo watarudisha nyuma maendeleo ya nchi
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Zitto: Nitagombea urais 2015

[h=2]
icon1.png
Breaking news: Rais Wade akubali kushindwa[/h]
Rais wa Senegal Abdulaye Wade amekubali matokeo katika mzunguko wa pili wa uchaguzi wa urais. Wade ambaye ana miaka zaidi ya 80 alibadili katiba ili aweze kugombea mara ya tatu.​
 
Last edited by a moderator:
Ndipo hoja ya umri hapa inapopata nguvu zaidi, yaani tupo kwenye mchakato wa Katiba ya Wananchi na ni sisi Wananchi ndio tutakaosema tunataka katiba gani halafu anatakoa mtu mwenye uchu na ulevi wa madaraka na kuanzisha mijadala ambayo haina tija!...nadhani kwa mtu mzima mwenye busara za kutosha hawezi kufanya hivyo na hapa hoja ya umri inazidi kupata nguvu kwamba miaka 35 BIG NO.

Niko interested sana Zitto aje hapa kutoa maelezo ni nini kinaendelea kati yake na Deputy Director wa Idara ya Usalama wa Taifa. hapa ninajuwa ninachokisimamia na ninachoamini, na tukienda mbali zaidi nasikitika kuwajulisha mashabiki wake msishangae Zitto akikataliwa Ubunge jimboni kwake mwaka 2015 katika masanduku ya kura.
Zitto Kabwe ndiye mbunge pekee ambaye alitaka kugombea Ubunge kwenye majimbo matano tofauti kwenye uchaguzi wa 2010, na alipogombea kwao Kigoma Ushindi wake ulipungua kura alizopata kufananisha na zile za mwaka 2000.

Kwani Zitto amekosa sifa ya kuwa mwananchi asitoe mawazo yake kwamba rais anatakiwa awe na 35 yrs?

Swala ni kushinda na kura kupungua hiyo ni hoja dhaifu yenye mchanganyiko wa wivu..

Duh kumbe na wewe ni mwana usalama hadi unafahamu mawasiliano na Deputy ...
 
Ukiongea maneno hayo ambayo nimekuwekea RED mbele ya Jakaya Kikwete anaweza hata kukunasa kibao!........
Muulize vizuri JK ndio atakupa jibu zuri ni nini maana ya kura kupunguwa.
 
Ukiongea maneno hayo ambayo nimekuwekea RED mbele ya Jakaya Kikwete anaweza hata kukunasa kibao!........
Muulize vizuri JK ndio atakupa jibu zuri ni nini maana ya kura kupunguwa.

Mimi siyo mwana usalama kama wewe nitapata wapi nafasi ya kuongea na rais?
 
Mtu yeyote anayesema nataka kuwa rais lakini kwanza chama changu kinipe ridhaa, katika siasa za Tanzania, namuona si makini.

Hii si kauli ya kutoa nusunusu, ama ushapata ridhaa unatangaza kugombea urais, ama hujapata ridhaa unatafuta ridhaa kabla ya kusema nia yako.

Sasa hivi Zitto kashawaweka wazee na viongozi wa CHADEMA katika nafasi mbaya kwa kutangaza hili kabla -seemingly- mambo hayajafanyiwa uamuzi kichama
 
Wana jf hii nimeinasa kwenye blog iitwayo yerickonyerere.wordpress.com

Nimeshangaa kuona kumbe wengi wanamuogopa zito kiasi cha kusema sana.

25 Mar 2012

Tanzania ni nchi iliyo mithiri ya karia hivi leo na ni nchi yenye lasilimali adhimu duniani,

Jambo la kujiuliza ni je watanzania ni watu wa aina gani? wanaendana na Tanzania ilivyo?

Ukweli ni kuwa watanzania ni wanafiki wakutisha zaidi ya baraza la Sanhedrin, unafiki wetu unatisha kwakuwa umechanganyika na ujinga, Hatuendani kabisa na wasifu wa taifa, Jambo hili ni hatari kwa mstakabali wa taifa kwakuwa kati yetu wajinga na wanafiki kumeibuka kundi la wahuni

Wahuni hawa ambao mbegu yake ni ujinga na unafiki wamekuwa hatari kuliko kawaida, haimithiriki hata kuwatazama kwa jicho la makengeza tu.

Watu hawa wahuni, wanafiki na walanguzi wa fikra wamefanikiwa kuvunja mlango wa siasa za Tanzania na kujikita humo wakiliyumbisha taifa watakavyo, Wanatumia mwito wa utandawazi msonge kujidukiza kisiasa.

Ninavyoamini taifa halijengwi na mwanasiasa bali mwanasiasa ana nafasi kubwa ya kulivunja taifa! Sasa tukiacha siasa hizi za kinafiki zitamalaki ndani ya ardhi ya Tanzania, vitukuu wetu watakuja kuyachapa viboko makaburi yetu. Watanzania kila mmoja kwa imani yake turudi uwalii.

Nashangaa namna siasa za majitaka zilivyoshamiri, magazeti na wanaoitwa waandishi tegemezi nao hawana tofauti, magazeti yamejaa taarifa ambazo hazina msaada wowote kwa watanzania, hatusikii juu ya Mafuta yetu, juu ya dhahabu yetu, juu ya ardhi yetu, juu ya kilimo chetu, juu ya afya zetu, juu ya utamaduni wetu, juu ya tunu za taifa, juu ya mustakabali wa taifa na utaifa wetu.

Heshima yetu imepotea mbele ya walimwengu, utu na nafasi yetu imedharaulika, wengine wanatuamulia mambo yetu, Kenya imetutawala, imetuzuia kujenga barabara serengeti, tumefyata mkia, wazalendo mkowapi? wapiganaji mkowapi? Wenye nchi mkowapi? Arumeru ni kitu kidogo sana ndani nchi, mama zetu, baba zetu, dada zetu, kaka zetu, wadogo zetu vijijin wanalia hawana afya, magonjwa, njaa umasikini vimewazonga, tunafanya nini mijini? Ni hili la Pamela Lowassa, Siyoi Sumari, na Nassari?

Nashindwa kuelewa, nchi imebaki na Wasira tu? Nape? Ndio policymakers wetu? Mwigulu? Slaa? Zitto? Kweli jamani? Usalama wa Taifa mnabeba dhamana kubwa sana ndani na nje ya ya Tanzania, fanyeni kazi kwaajili ya taifa la leo na lakesho si kwa kikundi fulani wala chama furalani, rasilimali zetu zinatoroshwa na magenge mumiani laki taasisi hii ipo na inatajwa kuwa kila palipo na watu watano basi mmoja wao ni Usalama wa taifa, lakini kwanini hali iwe hivi?

Tutumie fikra machipuko kwa upinde wa kijana, japo kuwa vijana wengi wanaakili za kuku, lakini kwa sauti ya mang’amuzi ya hekima watafunguliwa na kuacha utegemezi wa fikra,

Mimi ni muamini wa mtandao wa Twitter nikihudumu kwa njia ya @YerickoNyerere Niseme wazi, nimefadhaishwa na baadhi ya wanaoitwa wanasiasa vijana, hasa kijana mwenzangu mbunge wa Kigoma Kaskazini ndugu Zitto Zuberi Kabwe

Nimemtaja Zitto Kabwe kwakuwa anatumia ujinga na unafiki wa watanzania hasa vijana kujidukiza kisiasa kwa hoja dhaifu ya umri wa uraisi, na amefanikiwa kuteka mioyo ya wakware wa fikra kinyume na haki ya fikra huru.

Ukifuatitia vijana wengi wanaojadili na kuunga mkono juu ya hoja hiyo ya Umri wa Urais utabaini kuwa ni waumini wa upepo wa Zitto, Hawasemi faida ya hoja yao, wala hasara ya umri utumiwao kwa sasa, bali kwa jicho la tatu wamekuwa ni mashabiki wamuangaliao Zitto tu bila kujua mstakabali wa taifa lao.

Zitto ninamwamini sana kiutendaji ndani ya chama chake na nje ya chama, kupingwa kwa hoja yake hakutafsiriwi kuwa si kijana mtendakazi bora laa hasha, bali ni ashirio la kengele imwamshayo toka usingizini, tena usingizi wa ulevi mtawalia wa sifa za kisiasa.

Urais ni taasisi nyeti sana, tena hii ni nchi yoyote duniani huheshimu sana taasisi hii, Nimestushwa sana kuona kijana wetu Zitto aliyeonyesha dalili nzuri za kujengeka kisiasa na kiuongozi, akiwahi kuopoa nyama hata kabla ya kunawa mikono, anasema “ndio ninautaka urais” Hii ni kauli rahisi sana kisiasa lakini inabeba ujumbe wa aina mbili kwa mwanasiasa na raia wa kawaida.

Anawaarifu wanachama wake na wapambe wake kuwa uchaguzi ujao atagombea urais

Anawaonya viongozi wenzeke ndani ya chama kuwa yeye sasa ndiye lulu pekee ya urais.

Zitto bado hajafikia kuwa kiongozi wa juu zaidi kitaifa ndani ya chama chake achilia mbali kuwa rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Urais unahitaji hekima, Zitto hana kwa sasa, Urais unahitaji busara, Zitto hana kwa sasa, Urais ujasiri wa kweli Zitto hana kwa sasa,Urais unahitaji mtu wa kutafakuri, Zitto hana kwa sasa, Urais hauhitaji mtu mnafiki, Zitto kwa sasa ni mnafiki, Kwa ujumla Urais unahitaji mtu aliyepevuka, na Zitto bado hajapevuka.

Zitto anarubuniwa na kundi la wenye mtindio wa ubongo hasa vijana, wanaomuaminisha kuwa kapevuka na aweza kuongoza kizazi hiki cha nyoka ilihali bado safari yake ni ndefu.

Nimsihi kijana mwenzangu Zitto Kabwe, kuwa ni kweli anautaka urais lakini avute subira na kauli yake imeweka kovu ktk safari yake kisiasa, ambapo atumie muda uliopo kuliziba kovu hili. Ajitahidi kuwa na kifua kigumu chenye kuhifadhi magumu ya kisiasa, Si kila hoja imuhusuyo ni lazima aijibu na akiamua kujibu awatumie washauri wa masuala ya kisiasa.
Turekebishane ili kujenga taifa lenye uchumi imara, demokrasia imara, na siasa safi!

Mungu ibariki Tanzania mungu ibariki afrika!
 
Zito ni mnafiki sana na anataka kukiharibu chama..kwanza nchi imeyumba sana maisha ni magumu sana mafisadi wanaitafuna nchi ,,huyu kibaraka zitto yeye anakuja na stori ili watu waache kujadili mambo ya maana .nchi imeharibika sana jk keshaishindwa na 100% zitto sio mkombozi wetu huyu katumwa ama anataka kuiharibu nchi.zitto ana uroho wa madaraka na hatutaki watu kama hawa an huyu kijana inabidi avuliwe madaraka kwenye chama.ni mnafiki hana lolote ..watu wanataabika sana nchi inatafunwa yeyemiudenda inamtoka eti anautaka urais.
huyu ni mtu hatari sana kuweni makini na nina uhakika 100% huyu akiingia madarakani lazima aibadili katika ili akae hadi azeeke madarakani.
sio hivyo tu chadema mkimpitisha zito mjue chama ndio kimekufa hivyo kwani huyu jamaa ametumwa na mafisadi.
mimi binafsi SITAMPA KURA YANGU
kwa sababu kule twitter aliuliza swali na kijana mmoja yeye akajibu kuwa eti kura moja hana haja nayo..kumbe hajui kuwa sio kura moja tu ya yule kijana ni kura za wengi kwa sababu wengi tulikuwa tunasubiri ajibu lile swali,,sasa mntaka kuniambia ni rais gani huyu mwenye nyodo?
huyu hafai na huu ulikuwa sio muda wa kuja kujitangaza uroho wake wa madaraka hapa hata kama katiba inaruhusu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom