Zitto ndani ya 835KJ

Zitto ndani ya 835KJ

Hii kozi maalum kwa wabunge ni wiki 3 kama sikosei

Kwa jinsi nchi inavyoendeshwa kisiasa hata ile dhana ya kuacha cheo chako getini na kuwa mtu wa kawaida itakuwa haipo badala yake watakuwa wanapelekwa kiuheshimiwa zaidi kwa kuambiwa WAHESHIMIWA, MGUU PANDE.....................
 
835KJ ni Mgambo JKT . Kilometa kama 15 kutoka Kabuku njia kuu ya Tanga, Arusha na Dar na zaidi ya maili 9 hivi

Wakulima wazuri wa mahindi na Machungwa wenye zaidi ya hekta 300 kila zao
Mkuu umenikumbusha siku ya kwanza naenda kuripoti kikosini nilifika Kabuku kama saa 11 jioni. Basi wenyeji wakaniambia subiri utapata lifti ya mkuu wa kikosi kaenda Korogwe. Nikajikuta niko na dada mmoja alikuwa na ulemavu wa mguu mmoja naye anaenda kuripoti.Baada ya kama saa moja akaja mkuu wakikosi ndani ya Landrover akitokea Korogwe. Huyo ndio Kanali Mtono,sijapata ona askari kama yule tena kwa maana ya mafunzo ya kujenga ujasiri.
Alichofanya ni kumchukua yule dada mwenye ulemavu na yeye kushuka kwenye gari na kunionyesha milima ya Gendagenda na kusema,“mzalendo,kabla ya kufika milima ilee,kambi iko hapo,tembea utafika”
Sasa wakati huo ndio na giza limeanza,huo ni msitu kwa wakati huo,njia siijui na hakukuwa na sababu kwa nini hakunipa lift. Hapo ndio nilianza kuona adha ya Jeshi.
Nilikomaa mpaka nikamaliza na mengine ni historia,but nilitoka nikiwa mtu tofauti kabisa. Zitto,naambiwa mnaenda wiki kadhaa,sidhani kama mtaiva kama wale ambao walihenya mwaka na ambao walivumilia machungu yooote lakini siku ya kutoka walikuwa na kicheko wao na wakufunzi wao.
Kila la kheri.
 
Hii kambi ya Mgambo huko nyuma miaka ya 80 mpaka mwanzoni mwa 90 ilikuwa noma ile mbaya.

Mkuu Zitto mafunzo mema huko.


835KJ ni Mgambo JKT . Kilometa kama 15 kutoka Kabuku njia kuu ya Tanga, Arusha na Dar na zaidi ya maili 9 hivi

Wakulima wazuri wa mahindi na Machungwa wenye zaidi ya hekta 300 kila zao
 
good news

nimesikitika sana kusikia nasari amekimbia camp

the boy needed to stick to his words

Ipo siku utaelewa kwa nini nassari hajaingia kwenye hiyo kozi ya wiki 3.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Anayezungumziwa sio mwana CCM, tafadhali bwana.

hilo linafahamika wazi, na lengo letu kurudisha jkt, ni kujenga moyo wa vijana kupenda chama tawala, kulinda na kutetea chama na nchi yao kwa moyo wa kizalendo zaidi. hilo ndilo lengo kuu, yaliyo baki ni malengo ya ziada. so i mean what i wrote.
 
hilo linafahamika wazi, na lengo letu kurudisha jkt, ni kujenga moyo wa vijana kupenda chama tawala, kulinda na kutetea chama na nchi yao kwa moyo wa kizalendo zaidi. hilo ndilo lengo kuu, yaliyo baki ni malengo ya ziada. so i mean what i wrote.
product ya zamani mbona ni has?
 
Kila la heri. Ingawa muda ni mfupi, bilashhaka utasaidia kujenga na kuimarisha ujasiri na uzalendo. Viongozi maselule wameizamisha pabaya nchi yetu.

ujasiri na uzalendo unajengwa kwa kupitia jeshi?
 
Kambi yangu hii nilipigia mafunzo hapa operation vyama vingi B-coy or Bravo...,machungwa kwa wingi sana, bila kusahau kilimo cha mahindi gendagenda na kulinda wanyama waharibifu pia!
 
Zito angalia huko kuna Majoka makubwa aina ya Sawaka ni hatari ukijongo(neno la zamani) hapo kikosini likimaanisha kutorokea Porini.
 
Hivi hakuna twisheni ya JKT?
Nataka askari wa JKT wawe wanakuja kuwafundisha JKT wanangu hapa hapa nyumbani.....kama taratibu zimepindwa to three weeks I believe that hata litawezekana.
 
Vijana wa CDM should watch out, huu ni mkakati ambao kama huwezi kuona mbali ni vigumu kuugundua! mlambaza ebilo kabilalabao.......!
 
wamepima afya kujua kama zinaruhusu?wasije wakasababisha kuomboleza misiba ya kitaifa nk nk!
 
Hii kozi maalum kwa wabunge ni wiki 3 kama sikosei

Tuna shida sana nchi hii. Kila kitu ni kuchakachua tu. Hebu fikiria muda wa JKT ulikuwa wiki 52 sasa wanafanya wiki 3!! Kwa wale waliopitia JKT mtakubaliana na mimi kuwa muda huo ni kichekesho. Je watafanya kazi za shamba lini? Je mafunzo ya kwata yatapewa muda gani? Je watalima miraba lini? Je ujenzi watafanya lini?

Heri wakarudisha JKT kama lilivyokuwa awali au wakaendelea kulifuta kabisa.
 
eti wakajenge uzalendo...kwanza mafisadi yote ya nchii yamepitia jkt na huko jkt hata ule mradi wa matrekta ni ufisadi mtupu
 
Back
Top Bottom