Zitto ndani ya 835KJ

Zitto ndani ya 835KJ

hilo linafahamika wazi, na lengo letu kurudisha jkt, ni kujenga moyo wa vijana kupenda chama tawala, kulinda na kutetea chama na nchi yao kwa moyo wa kizalendo zaidi. hilo ndilo lengo kuu, yaliyo baki ni malengo ya ziada. so i mean what i wrote.
Sasa nimekusoma, japo imeni cost posts tatu,
 
835kj kweli ni mgambo, nilikuwa pale kwa mwaka mmoja 92/93 , alikuweko mkuu wa kikosi akiitwa afande chale na msaidizi akiwa kipangula, those days zimeniachia a very good memory ya adventures

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Ni kambi ya jeshi ambayo kwa wakati huo wa 92/93 alikuwepo pia joseph kabila ambaye kwa sasa ni raisi wa congo DRC

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Mkuu umenikumbusha siku ya kwanza naenda kuripoti kikosini nilifika Kabuku kama saa 11 jioni. Basi wenyeji wakaniambia subiri utapata lifti ya mkuu wa kikosi kaenda Korogwe. Nikajikuta niko na dada mmoja alikuwa na ulemavu wa mguu mmoja naye anaenda kuripoti.Baada ya kama saa moja akaja mkuu wakikosi ndani ya Landrover akitokea Korogwe. Huyo ndio Kanali Mtono,sijapata ona askari kama yule tena kwa maana ya mafunzo ya kujenga ujasiri.
Alichofanya ni kumchukua yule dada mwenye ulemavu na yeye kushuka kwenye gari na kunionyesha milima ya Gendagenda na kusema,“mzalendo,kabla ya kufika milima ilee,kambi iko hapo,tembea utafika”
Sasa wakati huo ndio na giza limeanza,huo ni msitu kwa wakati huo,njia siijui na hakukuwa na sababu kwa nini hakunipa lift. Hapo ndio nilianza kuona adha ya Jeshi.
Nilikomaa mpaka nikamaliza na mengine ni historia,but nilitoka nikiwa mtu tofauti kabisa. Zitto,naambiwa mnaenda wiki kadhaa,sidhani kama mtaiva kama wale ambao walihenya mwaka na ambao walivumilia machungu yooote lakini siku ya kutoka walikuwa na kicheko wao na wakufunzi wao.
Kila la kheri.

Mkuu Chakaza, Hongera sana kwa kukutana na Kanali Mtono. Mimi nlikuwa nae mpaka akaondoka na akaja Meja Charles. Enzi zile ule msitu wa Gendagenda ulikuwa na nyati wa kufa mtu

Miaka ile machungwa, mahindi na mihogo yalikuwa ni mazao kwa maelfu ya tani na viliharibika buree kutokana na barabara mbovu kukosa usafiri wa uhakika wa kuvisafirisha kwenda sokoni ama hata kwa wenye mahitaji husika

Mgambo JKT ni kambi kubwa sana inayokubali kila aina ya zao.

Kwa mafunzo ya wiki 3 ni Upuuzi mtupu ! Mwaka mmoja ndio mafunzo hasa maana hata uchaka mtakwenda na hakuna kulala mpaka muimbe disko
 
Wiki 3 wanataka , itakuwa jeshi la voda fasta , kama walimu wa upe waache chezea jeshi .
 
Wabunge wanafki tumeweza kuwajua hata kwa hili dogo tu, kwani wameingia mitini, Zitto anasimamia maneno yake, anafaa kuwa kiongozi!
 
Osokoni nadhani tulikuwa wakati mmoja mgambo? Mi nilikuwa pia b-coy , tulikuwa na afande mchele, na afande moyo,uko wapi mkuu?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Hongera kamanda Zitto,nakutakia kila la heri....mbunge wangu Silinde sijui ameripoti huko bila kumsahau Sugu. Isije kuwa ndio wale wenye majukumu mengi majimboni, na majimboni hawako.!
 
Ok, mbio za magogoni zina mateso! Kwa nn hakufanya hvy kabla?
 
Osokoni nadhani tulikuwa wakati mmoja mgambo? Mi nilikuwa pia b-coy , tulikuwa na afande mchele, na afande moyo,uko wapi mkuu?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Unamkumbuka Afande Makambajeki ? Afande mrefu kuliko woote na mashabiki kindakindaki wa Simba sports club ?

Nime miss kuwaona mabinti kwenye kaptura fupi za jeshi na mapaja yao makubwa yaliomiminikaa wakienda gendagenda kulima miraba yao ya mahindi.
 
Ngoja warudi hapa waanze kuanguka mmoja mmoja,siyo kila kitu ni cha kushobokea mbele ya huu utawala wa kimafia wa magamba
 
Wakuu nisaidieni! Eti huyu nasikia ni Kapteni wa jeshi! ni jina au ni kweli jamaa ni kapteni wa jeshi?

Kapt+Komba+1.JPG
 
Mkipigwa sumu huko msije mkaanza kulialia na kutafuta huruma humu JF, Heri yako Nassary umefata ushaur na kutoakuamua kuto kwenda huko machinjoni, Zitto uwe makin huko JKT kwani binadamu hatuna utu kabisa kwan haya maCCM yanaweza yakakupiga hata risasi ya kifua kwny mafunzo na kusingizia bahati mbaya.
 
Last edited by a moderator:
Wabunge wanafki tumeweza kuwajua hata kwa hili dogo tu, kwani wameingia mitini, Zitto anasimamia maneno yake, anafaa kuwa kiongozi!

Mkuu kwani kuruka viunzi na kupiga gwaride mguu pande ndio sifa za kuwa kiongozi bora?
 
Wakuu nisaidieni! Eti huyu nasikia ni Kapteni wa jeshi! ni jina au ni kweli jamaa ni kapteni wa jeshi?

Kapt+Komba+1.JPG
Huyu alikwenda JKT baada ya kumaliza mafunzo ya ualimu kwa shule za msingi. Ni huko JKT kipaji chake cha kuimba kilipogundulika akachukuliwa kwende Monduli kwenye chuo cha maofisa wa jeshi.
 
Kila la kheri

Jamaa kashawaua Wafanyakazi wa Migodini wanaotegemea kujipanga kimaisha kwa kutegenea fao la kujitoa kwa kuishauri Serikali IZUIE KABISA FAO LA KUJITOA kavuta chake halafu sasa kwa raha mstarehe kaenda kujificha JKT eti anakwenda kutafuta uzalendo.

Mwenyezi Mungu wa Mbinguni amlipe malipo yake sawa na unafiki wake.
 
Huu ni usanii mwingine wa wanasiasa haiwezekani mafunzo yachukue miezi 6 na wao wachukue wiki 3 wanajidanganya wenywe
 
Back
Top Bottom