Zitto Nani Akuuwe?

Wakubwa,

Jana kwenye taarifa ya habari TBC1 nikamsikia Kanumba akitamka kuhusu habari kwamba Zitto kutishiwa kuuawa, mimi sikubaliani kabisa kwamba hivi nani amuue zitto? kwa lipi hasa?

Binafsi naona watu wanataka kuzidi kumpandisha chati kwa sababu zao binafsi, Tanzania hatuna utamaduni wa kuuwana, walikuwapo viongozi waadilifu sana na hayakuwapata haya iweje leo wewe zitto watu wakutoe roho kwa lipi hasa?

Sababu imetangazwa si jambo la kubeza tena, tujadili tuone kweli hivi kuna njama za kumtoa roho au propadanda za kisiasa tu?

Sisi watanzania tuna matatizo yetu na wala hili za Zitto naona halina umuhimu kwa sasa haya magazeti yanalikuza tu bila sababu ya msingi,hebu tumalize hili la umeme na katiba yetu tafadhali.

Kwani Kanumba ni mtangazaji wa TBC? au inawezekana alikuwa anahojiwa juu ya filamu yake yenye character anayeitwa Zito?
 
Wanataka kum-frame mtu ukiona hivo, mie sioni Zitto kama ana umuhimu wowote kwa taifa hili.
 
Nilisha onya mara kadhaa hapa jamvini kuwa biashara anayofanya Zitto ya kuwa double agent itamgharimu maisha yake. Kama kuna mpango wa kumuua basi ni TISS na CCM kisha wailengeshe ishu kwa Chadema kama walivyofanya kwa Chacha Wangwe.
 
Nilisha onya mara kadhaa hapa jamvini kuwa biashara anayofanya Zitto ya kuwa double agent itamgharimu maisha yake. Kama kuna mpango wa kumuua basi ni TISS na CCM kisha wailengeshe ishu kwa Chadema kama walivyofamya kwa Chacha Wangwe.
Analikoroga mwenyewe na atalinywa.
 
Nani amuuwe, alishindwa uawa enzi akili yake inafanya kazi vizuri iwe leo kwenye diminishing return yake!
 
Elnino usitake kujifanya kama umeahamia Tanzania wakati umezaliwa, viongioz wangapi waliuliwa, wapi Kigoma Malima, wapi Edward sokoine, wapi yule proff wa ud, nini kilimkuta Kubenea? fuatilia mambo kiundani.
 
I always presume that the death of Mr. Chacha Wangwe was planned and organized along such a plot-KILLING AND LETTING SOMEONE ELSE TO BARE BLAMEs. Zitto may need to be careful not because of the happenings in CHADEMA but b'se He may be a good target for CCM to finish CHADEMA.

We also need to have some reflections: was Mr. Mwakembe's accident some years back normal or a failed plot? What about the death of the late Hon. Salome Mbatia? a normal accident cause or a missed catch of somebody's else, Zitto?!. A recent failed target of the son's of traditional CCM member and business philanthropy, Mr. Mengi.
 
kwani zito ni nani katika nchi hii hadi auawe,acheni kupandisha chati huyo zitto wenu kwa hoja zisizo na msingi wala maslahi yoyote kwa taifa letu
 
kwani zito ni nani katika nchi hii hadi auawe,acheni kupandisha chati huyo zitto wenu kwa hoja zisizo na msingi wala maslahi yoyote kwa taifa letu

Tatizo wabongo tunakuwa kigeu geu, utasikia mara leo mtu anashabikia hili, kesha analiponda.
Suala la Zitto kutishiwa lichunguzwe ili ukweli upatikane kama kweli kulikuwa na Mission ya kumpoteza.
Japo kwa tabia yake ya kigeugeu mara yupo CHADEMA mara anamfagilia Mkwere, kwangu mimi hata akichakachuliwa poa tu, ili iwe mfano kwa ndumila kuwili kama yeye.
 
wa kumuua zitto ni zitto mwenyewe na madudu aliyojiingiza kwayo

huwezi ukawa mchawi halafu ukaja kupiga kelele ati wanataka kuniroga

Zitto, you have two options; either to come out clean or run away as fast as you can from your current personality and behaviour...

Unfortunately sikuonei huruma mdogo wangu zitto kwani huwezi uza utumbo usinuke
 
kwenye red, yeye alisema kile alichoambiwa na daktari, sasa wewe kama unapingana na vipimo basi unamatatizo.
zito nikiongozi chadema mbona muda mrefu hatuone aandamane na viongozi wengine wa chadema? Kaka chacha wangwe alikuwa na migogoro na freeman akaishia kaburini kwa nini hili la zito tulidharau? lisimwalo lipo au li njiani linakuja. haya si mambo ya kupuuzwa hata kidogo. Lakini tunasubiria tu litokee halafu watajua shughuli yake kwani itakuwa pevu. Lets we wait and see.

---------
I will not be surprised for Zitto getting killed, ccm ni mafia na ni mtandao hatari sana, hiyo shauri yake Zitto kwa kuwa na uroho wa pesa. Ccm imeua innocent people wengi tu akiwemo muasisi wa chama chao, kolimba, kombe, sokoine etc.

Zitto amefikia angle mbaya maana hawezi kurudi nyuma kwani akifanya hivyo ccm watammaliza ili siri isivuje na hawezi kuendelea mbele maana cdm wana evidence zake kwa hiyo watamchafua kisiasa pia. He is really in a complicated shit ya kujitakia.
 
Tafadhali sana ELNIN0,

Edward Sokoine,
Imran Kombe,
Horace Kolimba,
Kigoma Malima,
Judge Mwaikusa,
Chacha Wangwe,

e.t.c

Zitto hajafikia status ya hawa makamanda plse!

Nawaambia CCM hawana muda wa kumuua zitto ili watu wahisi kuwa kauawa cha viongozi wa CDM. kama wana nia ya kuimaliza CDM mbona kuna njia nyingi tu tena zipo wazi wazi.

Mbona hamsemi ya hii ya rupia walizopenyeza kwenye uchaguzi wa vijana chadema? zikasababisha kina kafulila na wengineo kuondoka?

Cha msingi namshauri zitto amalize tofauti zake na wabunge wenzake, viongozi wenzake na aombe radhi kwa wanachama na wananchi kwa ujumla hasa washabiki wake kwa kitendo chake cha kwenda kinyume na maamuzi halali ya chama chake.
 
Waberoya na wengine,

Nafikiri USALAMA wa Zitto kwa sasa utategemea sana uhusiano wake na CHADEMA, kama hayo yasemwa ni ya kweli.

Uhusiano wake Mbaya na CDM itakuwa ni sababu tosha kwa TISS na CCM kumuuwa na kuibebesha lawama CDM. Ukiangalia hata Wangwe kama asingelikuwa na uhusiano mbaya na CDM au walau ugomvi wake asiutangaze waziwazi, nina imani leo hii angelikuwa hai.

Kama CHADEMA leo hii kingelikuwa chama cha Kijasusi, wangeliweza kabisa kumuuwa Sitta na watu wote wangeliamini kuwa CCM walikuwa na hasira naye. Wangeliweza kumuuwa Lema huko Arusha na kusingizia kuwa Lowassa na CCM wamemuuwa. Kuna nchi nyingi haya mambo yamefanyika, yanafanyika na yataendelea kufanyika.

Waberoya, kama una mawasiliano na Zitto basi mwambie haya maneno "Usalama wake uko ndani ya Chedema." Akitoka tu nje, kuna Tai huko wanaitwa TISS na CCM watamdaka na kummaliza na mwisho waseme "CHADEMA wamemuuwa."

Kibaya zaidi kuna watu wataamini kama jamaa yetu MkamaP anavyoamini kuwa CHADEMA ndiyo walimuuwa jamaa yake Wangwe. Soma kila makala yake kuhusu CDM utakuta anaandika hivyo. Kuna wengi sana wataamini kuwa FULANI kauwawa na CHADEMA.
 
wa kumuua zitto ni zitto mwenyewe na madudu aliyojiingiza kwayo

huwezi ukawa mchawi halafu ukaja kupiga kelele ati wanataka kuniroga

Zitto, you have two options; either to come out clean or run away as fast as you can from your current personality and behaviour...

Unfortunately sikuonei huruma mdogo wangu zitto kwani huwezi uza utumbo usinuke

Acid
Leo umemaliza kwa hili, you have nailed it wanasema!!!
Nakupa senksi nyingine!!
 
Heshima kwenu wanajamvi.

Wakuu mashirika ya kijasusi katika nchi nyingi za kiafrika yapo kwaajili ya kuwadhuru wanasiasa wa upinzani.Tanzania ni miongoni mwa nchi za kiafrika ambazo shirika lake la kijasusi [TISS] limetumiwa kuwatoa uhai wanachi wake ili kuinufaisha serekali iliyoko madarakani kisiasa.

CHADEMA kamwe haiwezi kutoa uhai wa Zitto bila dola kujua labda kama tunaizungumzia Tanzania nyingine si hii ninayoijua.Zitto anaweza kuuwa na dola kupitia TISS kwa lengo la kuinufaisha CCM kisiasa hasa mwaka 2015.Kinachofanyika sasa ni kuandaa mazingira mazuri ili ikitokea Zitto kafa lawama na hasira zielekezwe CHADEMA na sivinginevyo.Nina amini Zitto ana nafasi ya kujiondoa kwenye mtengo wa kutumia na hatmae kuwanufaisha wengine kwa gharama ya maisha yake.
 
kwenye red, yeye alisema kile alichoambiwa na daktari, sasa wewe kama unapingana na vipimo basi unamatatizo.
zito nikiongozi chadema mbona muda mrefu hatuone aandamane na viongozi wengine wa chadema? Kaka chacha wangwe alikuwa na migogoro na freeman akaishia kaburini kwa nini hili la zito tulidharau? lisimwalo lipo au li njiani linakuja. haya si mambo ya kupuuzwa hata kidogo. Lakini tunasubiria tu litokee halafu watajua shughuli yake kwani itakuwa pevu. Lets we wait and see.

Lakini pia wana CHADEMA WENGI WANATAMANI WAMUUE ZITO NA LAU WANGLIWEZA WANGEFANYA HIVYO. KAULI ZAO NDANI YA JF ZINADHIHIRISHA HAYO. hivyo tusitafute visingizio nje ya Chama kwani hata ndani ya Chama WAPO WAUAJI.
 
Tatizo wabongo tunakuwa kigeu geu, utasikia mara leo mtu anashabikia hili, kesha analiponda.
Suala la Zitto kutishiwa lichunguzwe ili ukweli upatikane kama kweli kulikuwa na Mission ya kumpoteza.
Japo kwa tabia yake ya kigeugeu mara yupo CHADEMA mara anamfagilia Mkwere, kwangu mimi hata akichakachuliwa poa tu, ili iwe mfano kwa ndumila kuwili kama yeye.

Haya NDIO MAWAZO YA WANA-CHADEMA. NA WAKO WENGI. HASA UKIZINGATIA WENGI WANATOKA KARIBU NA WATANI ZETU.

NAOMBA NIWAJILISHE TU KUWA ZITO ANATOKEA KULE SHOKA LILIKOUNGUA MPINI UKABAKI. UKIWEZA JARIBU!

ATAKUFA KWA AHADI YA MUNGU TUU!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom