Zitto mbabe wa Bungeni, hakususia hotuba ya Rais

Zitto mbabe wa Bungeni, hakususia hotuba ya Rais

attachment.php
Zitto bado hajafa kisiasa tu ??
 
Nakumbuka wakati zzk anaingia bungeni mara ya kwanza aliibua kashfa ya mgodi sikumbuki kashfa gani, na bwana 6 kipindi hicho ni spika akamtoa nje na kumfumgia asiingie bungeni kwa kipindi flani, wakati zito anatoka hao hao ccm walikuwa wakimzomea, leo hao hao ccm wanamsifia, kweli kuishi tz ni kuona mengi nakataa ule msemo unaosema kuishi kwingi ni kuona mengi, kuishi tz ni kuona mengi

kuishi TZ ni kuona ya Lowasa & co. with Ukawa. hapo unasemaje?
 
Niliwahi ambiwa Ukiona wazungu wanasifia sana Raisi hasa kutoka Africa basi jua kwamba huyo Raisi mambo mengi sana anayo yafanya niyakuwafurahisha wao, the same na hapa, Kamwe CCM hawawezi sifia Zitto bila kuwa kwamba Zitto kuna mambo mengi anafanya ya kuwafurahisha wao CCM na huu ndo ukweli.

Mimi ni mgeni jf nimeingia humu wkt wa kampeni, lakini wewe unaonesha kuwa hujaqualify kuwa great thinker, so learn from gthnker!! Wazungu wanasema practice make perfect, then nobody is perfect! Who makes practice if not bodies???don't quote from whites you will not be a great thinker!!!! Answer to whites about being perfect, perfection does not exist to human beings but to almighty GOD!!! STO NONSENSIOUS!!!!
 
Ni manyumbu tu wanaunga mkono ukawa na mafisadi wao...

Mtabaki kuwa vilaza hivi mafisadi wa escrow,meremeta,meno ya tembo,madawa ya kulevya,twiga kupanda ndege,mikataba mibovu ya gas na mafuta,Iptl,mabehewa fake na mengine mengi wapo ukawa!??
 
Hivi mnamsema Zitto Zuberi Kabwe au Zitto CCM? Huyo aliyebaki ndani ya bunge wakati wapinzani wenzake walitoka ni Zitto CCM. Yule mwingine alikuwa mpinzani kwa hoja na msimamo. Lakini huyu sasa ni mtu wa maslahi yaani pesa mbele kwa mbele
 
Jamii ya kina Shibuda, Cheyo na Mrema lazima wawepo. Kwenye msafara wa Mamba hata Kenge wamo. So tusimshangae Mzito wakabwela, kama jimbo lake tu aliliuza unategemea nini amemponza Manchali wawatu huyo ndio YUDA bwana
 
Ni kama vile anasema:

Kikwete- Dr Huyu kijana ana siasa makini za hoja zinazoweza kuharibu kabisa serikali yako......Buzwagi, escrow alizisimamia kweli kiasi cha kuniletea madhara.

Magufuli- Nataka nimteue Mghwira ubunge, shida utakua na nguvu sana na kutishia uhai wa ccm

Hahaa ..sio kuwa anasema asinge kuwa zito na mm zile pesa za stanbic bank ninge tajwa.....
 
Sipendi siasa za kishabiki ingawa naweza sanif hapa na pale ninipoamini panaongelewa cheap politics, lkn ninapoamini ukweli unapindishwa makusudi nitaeleza kile ninachoamini kipo sahihi.
Zitto ZUBERI KABWE ni mwanasiasa wa kipekee hapa Tanzania. Inawezekana jamii ikashindwa kumwelewa hapa na pale kutokana na aina ya siasa za kishabiki. Lakini ktk tafakuri zilizotulia huwezi kumbeza Zitto kirahisi hivyo, ni mtu asiyependa cheap politics za kutafuta umaarufu na kuvuta attention hata km ni kwa vitu vya msingi lkn ni kwa njia gani ndio swala.

Nnachojua mm Zitto ni mbunge wa kitaifa, Watanzania wengi walitaka arudi bungeni, huyu ni muhimu ktk combination zinazofanya bunge letu liwe hai kabisa, km alivyo Tundu Lissu.

Kwa mtizamo wangu, tayari bungeni tuna combination muhimu ambayo inatufanya sisi watazamaji tuelewe kinachoendelea bungeni.

Siasa za bungeni mara nyingi zinahusisha pande mbili zinazovutana, pia inaweza kuwa vigumu kwa ss wasikilizaji kujua nani yupo katika ukweli, anapokuwepo mtu wa tatu itasaidia kujua ukweli uko wapi na unafiki ujitenge hasa kwa maswala ambayo ni tata zaidi ukiacha kurahisisha ufumbuzi wa maswala ambayo huliunganisha bunge kutoka ktk pande zote ( ie. swala la ESCROW ).

So far Zitto anaiva kila siku na kubadilika kuzidi kuwa mtu wa kutegemewa na kuaminiwa na kuheshimiwa kitaifa kutoka vyama vyote, ni hazina muhimu ya taifa hili, aina ya watu unaowezs kusema watalipeleka taifa hili mahala linapostahili kuwa, ajipange vizuri kabisa, ajenge imani kwa vitendo ili 2025 panapo majaaliwa akabidhiwe nchi kama ilivyo ndoto yake
 
Last edited by a moderator:
Mtabaki kuwa vilaza hivi mafisadi wa escrow,meremeta,meno ya tembo,madawa ya kulevya,twiga kupanda ndege,mikataba mibovu ya gas na mafuta,Iptl,mabehewa fake na mengine mengi wapo ukawa!??

Mkuu wa wa mafisadi yupo ukawa....na jinsi ukawa mlivyokuwa vipanga, hata kutamka neno fisadi hamuwezi tena kwa kuhofia kumuudhi anayewaweka mjini
....hahaha...Mtasubiri sana.
 
Leo hii zitto anapongezwa na wanaccm kwa kitendo kimoja tu cha kubaki bungeni jana..........zitto huyu huyu anayeitwa mpinzani wa kweli sikuwahi kusikia akipongezwa wala kusifiwa na mwana ccm wakati wa swala la buzwagi,richmond, kagoda wala escrow.Cha ajabu sifa zake hazina mwendelezo unaotoka nyuma kukumbushia alichokifanya bungeni ila unaanzia jana na kuendelea.......ni zitto huyu huyu aliyehofia mpaka chakula cha hotelini wakati wa uwasilishwaji wa ripoti ya PAC mpaka kulazimika kumwita ndugu yake aje kumpikia chakula dodoma......leo ni shujaa wa ccm.......Jamani tusiwafanye watanzania wajinga kiasi hiki,..........Hizi siyo sifa ni kejeli kwa ndugu yangu zitto.


.
Hizo sifa zilikua kwa Lyatonga kabla hajafa rasmi kisiasa. sasa zimehamia kwa zitto. ziliwahi kupelekwa kwa Lamwai, Kabouru, Ngawaiya na Cheyo na wengine wa namna hiyo.
.
 
Lakini kama Zitto angeamua kutoka nje angekaa wapi? Maana mi namini UKAWA walipotoka nje kuna mahali walienda kukusanyika na kuongea mambo yao. Je, Zitto angekaa wapi na angeongea na nani na nini? Nampongeza sana kwa hilo.

Lakini ssem wakae wakijua kuwa Zitto kubaki ndani sio kwamba aliwaunga wao mkono. Jengo la bunge na bunge lenyewe sio mali ya ssem. Zitto alibaki ndani kama mbunge na sio mwanachama wa ssem. Alibaki ndani kutimiza wajibu wake kisheria, pia alibaki ili ajifunze na kuona kasoro ziko wapi ili apate mahali pa kuanzia katika kutekeleza mipango yake ya upinzani kisiasa. Asante Zitto kwa kujitambua na naamini hutakuwa kama mzee Cheyo au Lyatonga. Pia najua hutakuwa tayari kucheza ngoma usiyoijua
 
Mkuu wa wa mafisadi yupo ukawa....na jinsi ukawa mlivyokuwa vipanga, hata kutamka neno fisadi hamuwezi tena kwa kuhofia kumuudhi anayewaweka mjini
....hahaha...Mtasubiri sana.

Kwanini hamjamfunga kama akili zenu zipo timamu? nitaendelea kuwaita vilaza hadi mtakapochukua action.
 
2010 CHADEMA iliposusia hotuba ya Jk CUF hawakutoka bungeni kwa kuwa hawakuwa na makubaliano na Chadema sasa leo Ukawa haikuwahi walau kumjulisha Zitto kuhusu jambo hilo rasmi kwa hiyo walitaka akiona Ukawa wananyanyuka na kutoka nae aunge tela bila ya kujua hata mwelekeo au what next? Ukifika nje ya gheti wanaitisha kikao cha Wabunge wa Ukawa nawe kwa kuwa si sehemu ya ukawa unabaki unazunguka zunguka kama tiara!! Angetoka nae ningemuona kama tumbili anaekimbia bila kujua anakimbia kitu gani au anakimbilia wapi!!
 
Zito ni Act, chadema cuf nk ni ukawa. Angeenda kukaa kiti gani ukawa wakati kabla hakikuwepo kwa ajili yake? Lkn pia kile walichokipinga ukawa na zito alikipinga, au shida ni kwa sababu zito hakutoka nje na ukawa?
 
Watanzania now wameshikwa na upepo wa Magufuli
hawazungumzi why UKAWA walitoka nje
wanazungumza Magufuli alisema nini na nini kimetokea after..

UKAWA wanaweza jikuta wako sidelined na 'hot issues'...na upepo wa siasa...

Mkuu umenena! sijui wamepeleka wapi kile kitufe cha like?
 
Alipewa Rushwa na ccm ili abaki mjengoni.

Kwa akili yako angetoka nje angeenda wapi? Huoni kama angechekesha sana kujiingiza kwenye mambo ambayo hakuhusishwa?
Fikiria vizuri kabla hujaropoka.
 
Zito sio ukawa so kukataa kutoka ni haki yake
Na alipoulizwa why hakutoka alisema sikutoka sababu mimi sio Ukawa . sasa wana cccm mnampongeza kwa lipi hasa? Au mwatafuta huruma tu. Huyo mrema mkomavu si kapata kura 6000 tu kati ya malaki. Na huyu Membe ambaye wizara yake imeongoza kutafuna hela zetu kwa maziara kibao anaongea kama nani? Au ndio anabembelezea uwaziri kwa kuteuliwa
 
CCM wanampenda sana Zitto kwa sababu zifutazo
1.Zitto si tishio kwa CCM kukaa kuendelea kukaa madarakani.
2.ACT imesaidia kwa majimbo mengi ya Kigoma kurudi CCM.
3.Sera za ACT zinashabiana na za CCM kuhusu kupinga uwepo wa UKAWA.

Ulichosahau ni kwamba huyu ndiyo kwa asilimia kubwa amechangia sana kuibua madudu mengi sana bungeni dhidi ya CCM hiyo hiyo,anyway kama kuwa tishio la CCM ni kupiga sana kelele Bungeni au kupambana sana na Polisi,hapo sawa
 
Back
Top Bottom