Zitto mbabe wa Bungeni, hakususia hotuba ya Rais

Zitto mbabe wa Bungeni, hakususia hotuba ya Rais

Leo hii zitto anapongezwa na wanaccm kwa kitendo kimoja tu cha kubaki bungeni jana..........zitto huyu huyu anayeitwa mpinzani wa kweli sikuwahi kusikia akipongezwa wala kusifiwa na mwana ccm wakati wa swala la buzwagi,richmond, kagoda wala escrow.Cha ajabu sifa zake hazina mwendelezo unaotoka nyuma kukumbushia alichokifanya bungeni ila unaanzia jana na kuendelea.......ni zitto huyu huyu aliyehofia mpaka chakula cha hotelini wakati wa uwasilishwaji wa ripoti ya PAC mpaka kulazimika kumwita ndugu yake aje kumpikia chakula dodoma......leo ni shujaa wa ccm.......Jamani tusiwafanye watanzania wajinga kiasi hiki,..........Hizi siyo sifa ni kejeli kwa ndugu yangu zitto.

el huyu aliyetukanwa na kuchafuliwa kwa miaka, LEO hii ni msafi tena mkombozi wengine wanathubutu kumwita mjumbe wa Mungu!!!!!!!
 
Zito ni ndumila kuwili pia kigeugeu hata chama cha kinaitwa ACT wanafiki si wazalendo tena. Njaa amewafanya wajitoe fahamu mfano prefeselii kitila sasa kawa prefeselii wa mitandao kazi kuwafurahisha ccm.
Mbona una hasira sana na Zitto?
Usaliti wake ni upi hapo?
Kwani aliwaambia atatoka nje halafu hakutoka?
Wamuache, Roho inawauma sana kwa ajili ya Zitto mmoja tu?
Mmemfukuza achaneni nae.
 
Lazima pia tukumbuke kuwa ukawa wana agenda zao na Act wanazao na huenda wanatifautiana namna ya ufikishaji agenda sasa ukawa kutoka nje huenda ilipangwa kabla na zito hajui iweje aungane na msafara asiojuwa uelekeo na hatima yake?
 
Chadema inamchukia Zitto kuliko Shetani!! Hawa ndio wanaingia Misikitini na Makanisani na kujifanya watu wema!! Kila siku wanatamani sana jambo baya zaidi limtokee Zitto lakini Mwenyezimungu ni wa wote! Punguzeni Chuki kwa kuwa hamjui anayoyapanga Mungu juu yenu. Nani aliamini kuwa Dr.Slaa angepotea kwny Ulingo wa Siasa kabla ya Zitto aliemfitini kwa nguvu zote? Bunge limeanza wekeni akiba ya maneno msishangae Ukawa ikawa ni wafuasi wa Zitto kama ilivyotokea kwny escrow na Petition ya kupiga kura ya kutokuwa na Imani na pinda!!
 
Leo hii zitto anapongezwa na wanaccm kwa kitendo kimoja tu cha kubaki bungeni jana..........zitto huyu huyu anayeitwa mpinzani wa kweli sikuwahi kusikia akipongezwa wala kusifiwa na mwana ccm wakati wa swala la buzwagi,richmond, kagoda wala escrow.Cha ajabu sifa zake hazina mwendelezo unaotoka nyuma kukumbushia alichokifanya bungeni ila unaanzia jana na kuendelea.......ni zitto huyu huyu aliyehofia mpaka chakula cha hotelini wakati wa uwasilishwaji wa ripoti ya PAC mpaka kulazimika kumwita ndugu yake aje kumpikia chakula dodoma......leo ni shujaa wa ccm.......Jamani tusiwafanye watanzania wajinga kiasi hiki,..........Hizi siyo sifa ni kejeli kwa ndugu yangu zitto.

Sioni tofauti ya Zitto kama mpinzani na wenzake kama Mrema wa tlp,Cheyo wa udp nk nk mwisho wao uwa ni mfupi sana kisiasa!
 
Kuna muda watu walisema Zitto kapoteza umaarufu maana alikuwa hazungumziwi humu,ila sasa naona amerudi kwenye nafasi yake kila siku lazima azungumziwe.
 
Magufuli jana kacheza na Akili za Watanzania anawajua ni wapenda Ahadi ndiyo maana jana aliamua kubadili Hotuba yake na kuamua kujikita kwenye sera alizotumia wakati wa kampeni pia akawa anamsema JK live juu ya Safari za nje aliivua nguo Serikali iliyopita ambayo ndiyo wamemweka hapo ikulu, sasa ajiandae kuhujumiwa maana jana wametoka pale wakiwa na kunyonga mioyoni.


Hayo ni mawazo yako wewe na wewe ni moja ya watanzania wasiojielewa wanataka kiongozi wa aina gani au wanataka nini, kwa sisi wenye akili timamu tumemuelewa rais kwamba Ametueleza watanzania wooote kwa ujumla kila ambacho ameambiwa na watanzania wakati anazunguka kwenye kampeni yani amezianika shida zoooote za wananchi mbele ya wananchi wenyewe, mbele ya wabunge wetu na serikali kwa aujumla, na amesema wazi kuwa anataka kila atakaeondoka pale ajue ni shida zipi zinatakiwa kutatuliwa....Wewe ulitaka hotuba yake akae aanze kujisifu ushindi???? wakati wananchi wana matatizo?? sisi wananchi tunataka kusikia shida zetu zitatatuliwa vipi hatuna haja kusikia chochote kile, kile alichoongea ndo kile tulotaka kusikia na ndioa mana tuna furaha na amani kwa sabab tunamuamini na tunaamini atafanya hata kama si yote hayo machache kwetu ni bora zaidi pia kuliko kuyakosa kabsaa, Na alishasema hatakai kuwa mnafiki na msema kweli ni mpenzi wa Mungu ndo maana alielezea kwanini amevunja zile safari amewekwa takwimu tuone umuhimu wa safari zile kuvunjwa, nyinyi endelezeni siasa , CCM wameshaanza jenga nchi au niseme wameanza tekeleza ilani yao au wameshaanza kusikiliza kero za wananchi, safari hii hamna hata moja la kuikosoa serikali ya ccm, kwahiyo mtabaki hivyo hivyo kujitekenya na kujichekesha.
 
Jiandaeni kisaikolojia 2020 mana wafuasi wengi wa UKAWA Kimbilio lao litakuwa ACT mana kwa sasa ndo chama pekee cha Upinzani kilicho makini na chenye viongozi wenye busara na vichwa vilivyotulia ambao wako kwa ajili ya maslah ya wananchi na sio yao binafsi kama UKAWA,
 
Jiandaeni kisaikolojia 2020 mana wafuasi wengi wa UKAWA Kimbilio lao litakuwa ACT mana kwa sasa ndo chama pekee cha Upinzani kilicho makini na chenye viongozi wenye busara na vichwa vilivyotulia ambao wako kwa ajili ya maslah ya wananchi na sio yao binafsi kama UKAWA,

Eeeeh

Jifunze kuweka akiba ya maneno
 
Watanzania now wameshikwa na upepo wa Magufuli
hawazungumzi why UKAWA walitoka nje
wanazungumza Magufuli alisema nini na nini kimetokea after..

UKAWA wanaweza jikuta wako sidelined na 'hot issues'...na upepo wa siasa...

"Huo Ni upepo tuu utapita"-Dr Jakaya Kikwete
 
kuishi TZ ni kuona ya Lowasa & co. with Ukawa. hapo unasemaje?

Nenda na mada usitoke nje ya mada hapa anazungumzwa zito na ccm, lowasa katokea wapi,msitie watu ujinga kwani lowasa alikuwa wapi si huko huko, mmemtukana weeee mpaka kampeni zimeisha na kura mkamuibia, bado mnamsakama, yeye hasemi lolote mwishowe mtajiona.mazuzu, mshasema fisadi basi mahakama za akina tulia si zipo mpelekeni, si anajua vifungu vya sheria na hajawahi shindwa kesi, mpelekeni na mmfunge, tuone kama nchi haijazizima na siku atakayoongea madhambi yeni mtagwaya nyote, ipo siku tu
 
2010 CHADEMA iliposusia hotuba ya Jk CUF hawakutoka bungeni kwa kuwa hawakuwa na makubaliano na Chadema sasa leo Ukawa haikuwahi walau kumjulisha Zitto kuhusu jambo hilo rasmi kwa hiyo walitaka akiona Ukawa wananyanyuka na kutoka nae aunge tela bila ya kujua hata mwelekeo au what next? Ukifika nje ya gheti wanaitisha kikao cha Wabunge wa Ukawa nawe kwa kuwa si sehemu ya ukawa unabaki unazunguka zunguka kama tiara!! Angetoka nae ningemuona kama tumbili anaekimbia bila kujua anakimbia kitu gani au anakimbilia wapi!!

Walishaazimia kumchallenge iwe mvua iwe jua
 
Kuna watu hawajui wanataka nini .....wamejaa chuki tu ...msipofushwe na hizi siasa zetu ....angalieni mambo mkiwa open minded badala ya kufikiria kupinga tu ....
 
Ni Upumbavu Sana Kuhisi Kuwa Zitto Ni Mchumia Tumbo Na Msaliti,wakati Huohuo Mnawakubali Na Kuwalilia Juu Ya Watu Kama Lowassa,kingunge Na Sumaye...
 
Wamesahau fisadi naye alikuwa kamanda hahaha ipo siku watanyokaaa na wataelewa hufanyi siasa za mbowe mtoto wa mjini
 
Back
Top Bottom