Zitto mbabe wa Bungeni, hakususia hotuba ya Rais

Zitto mbabe wa Bungeni, hakususia hotuba ya Rais

Membe ni mojawapo wa makomredi wanaochukia rushwa nchi.alishiriki kwa kiasi kikubwa kulifanya fisadi likatwe na ccm,na akasababisha pia fisadi lisiende ikulu..asante Bernard Camilius Membe,gesi yetu imebaki salama

Mkuu hapa ni kujichanganya huyu Membe alipata wapi uwezo wakuhakikisha wenzie wanakatwa nayeye asijihakikishie kubaki,lakini pia kwenye ufisadi wa hela za Ghadafi na yule balozi wao kama vile alitajwatajwa.
 
Sasa me kuna kitu siwaelewi hawa wanamsifia zitto kwa kutotoka bungeni, kwakuwa wabunge waliotoka ni wale wanaounda ukawa, sasa zitto angetoka km nani? Na kama angetoka hawa wanaomsifia wangekuja na mada ingine ambayo ingesema "zitto ajipendekeza ukawa" alikuwa hana option zaidi ya kubaki ndani, ukawa walitoka either wakaenda sehemu kujadili mambo yao kwakuwa ni team moja, sasa zitto angetoka angeenda wapi???? Lodge akasubili mkutano uishe au angeenda bar. Ikumbukwe kuwa CCM inapenda watu wa kuambiwa lia, nawao wanalia, wakisema chutama badi naww uchutame rasivyo utakuwa useless kwao
Mkuu kitufe cha like sikioni lakini usijali kula tano
 
Vyama vyenye wabunge wa upinzani ni CHADEMA, NCCR, CUF na ACT na hivyo vyama 3 na muunganiko wa UKAWA isipokuwa ACT nashangaa wanaomsifia Zitto hivi angetoka angekwenda kuungana na nani? Ndani ya Bunge hili Zitto ni sawa na Mtoto yatima.

Huyo Mbatia alojifanya msemaji wa Lowasa kapata wabunge wangapi??? Acheni unafki... Zito anajitambua.
 
Mhe Zitto Kabwe Hongera kwa kuwaonyesha Watanzania tofauti kati ya ACT Wazalendo na UKAWA kuanzia tarehe 5/11/15 siku ambayo mgombea Urais wa ACT alikwenda Diamond Jubilee Hall na kuonyesha ukomavu na uzalendo tofauti na UKAWA na jana wewe mwenyewe ulipoamua kubaki ndani ya Bunge kuungana na wabunge wa CCM kusikiliza hotuba ya Mhe Rais. Hukufanya vile kupingana na UKAWA la hasha! Ulifanya vile kuonyesha kuwa ACT Wazalendo ni mpinzani mshiriki na siyo mpinzani mkosefu! Aidha kuacha wenzako wanatoka na ukabaki peke yako ni kitendo cha ukomavu na ujasiri. "Better him from within than Him from without" (Shakespeare) Wengi tunakupongeza! Membe.

sifa za kijinga.
 
hili la mzee kuwa kamanda halioni ila analiona la Zito kusfiwa na ccm......

Sio Kamanda tu... Aliachiwa chama afanye afanyavyo ili aingie Ikulu. Kwa kutumia mbinu zote zilizopo duniani safi na chafu ilimradi aingie Ikulu. Kwa kutumia yeyote duniani bila kujali ni gaidi au binadamu wa kawaida afu leo mnasemaje??? Mmepoteza uhalili wa kusema chochote chenye mashiko...
 
ACT wazalendo hatuna siasa za kushikiwa akili, tunauhakika na kila tufanyalo
 
Zito ni ndumila kuwili pia kigeugeu hata chama cha kinaitwa ACT wanafiki si wazalendo tena. Njaa amewafanya wajitoe fahamu mfano prefeselii kitila sasa kawa prefeselii wa mitandao kazi kuwafurahisha ccm.

Njaa kuzidi ya CHADEMA ya kumkabidhi Lowasa Chama na kumtukana Dr. Slaa??? Acha unafki basi Mungu anakuona mpaka ndani ya moyo wako.
 
Kuna watu wanaongozwa na akili ya mpiga pesa za michango yao, kama wamerogwa hawawezi hata kuhoji imetumikaje.
 
Nakumbuka wakati zzk anaingia bungeni mara ya kwanza aliibua kashfa ya mgodi sikumbuki kashfa gani, na bwana 6 kipindi hicho ni spika akamtoa nje na kumfumgia asiingie bungeni kwa kipindi flani, wakati zito anatoka hao hao ccm walikuwa wakimzomea, leo hao hao ccm wanamsifia, kweli kuishi tz ni kuona mengi nakataa ule msemo unaosema kuishi kwingi ni kuona mengi, kuishi tz ni kuona mengi
 
Zitto mlimfukuza, mkamtukana, mkamlaumu sana tena waziwazi leo hii mmeanza tena kwani mmesahau Kuwa hayupo tena CDM? Hamna mamlaka nae tena au nako mnataka kumvua uanachama?

Poleni sana.......unaacha mke then unaanza kumfuatilia😜😜😜😜😜😜😜😜😜😜😜😜
 
Hatma ya Zitto kisiasa inaelekea Omega, ile dhana kuwa anatumika na CCM inazidi kujidhihirisha!
 
Last edited by a moderator:
Msome Zitto.
Anasema hata yeye hamtambui Dr.Shein kuwa rais wa Zanzibar na ndio maana wakati Shein anaingia bungeni,hata yeye hakusimama kumpa heshima.
Anasema,alipoingia Dr.Magufuli,rais halali,yeye alisimama na hakuwa na haja ya kutoka nje ya bunge kwa kuwa rais halali anakuja kulihutubia bunge.
Kama Muislam mwenzangu na msomi kabisa,Zitto aliona najisi ikingia bungeni na akakubali kuheshimu kikao kilichonajisiwa hata kama kulikuwa na vingine halali!
Hapa Zitto hana la kujitetea ameshiriki kikao na watu wenye najisi na hivyo kumnajisi na yeye.
Zitto amepata najisi ya u-ccm na hawezi takasika tena.
 
Back
Top Bottom