Zitto mbabe wa Bungeni, hakususia hotuba ya Rais

Zitto mbabe wa Bungeni, hakususia hotuba ya Rais

Membe ni Nani katika siasa za Tanzania,JK alihitaidi ambebe lkn hakubebeka,asubiri huruma ya Magufuli tu
JPM hawezi kumbeba,jamaa anajipendekeza tu.Huyo ndo alikuwa dalali wa JK kutwa kuzunguka Ulaya na Marekani,na kusahau maendeleo ya nchi.Trilioni 2 kwa ziara za Rais,huyo jamaa alitakiwa saizi awe lock up
 
Mhe Zitto Kabwe Hongera kwa kuwaonyesha Watanzania tofauti kati ya ACT Wazalendo na UKAWA kuanzia tarehe 5/11/15 siku ambayo mgombea Urais wa ACT alikwenda Diamond Jubilee Hall na kuonyesha ukomavu na uzalendo tofauti na UKAWA na jana wewe mwenyewe ulipoamua kubaki ndani ya Bunge kuungana na wabunge wa CCM kusikiliza hotuba ya Mhe Rais. Hukufanya vile kupingana na UKAWA la hasha! Ulifanya vile kuonyesha kuwa ACT Wazalendo ni mpinzani mshiriki na siyo mpinzani mkosefu! Aidha kuacha wenzako wanatoka na ukabaki peke yako ni kitendo cha ukomavu na ujasiri. "Better him from within than Him from without" (Shakespeare) Wengi tunakupongeza! Membe.
Huna aibu kumpaka Mafuta ya chupa mwenzio? Sema pole kwa kusifiwa na mtu aliyeifilisi nchi yetu tanzania, hafai, umesikia Rais wetu alivyosema juu ya ofisi yake? huyo akikusifia huwezi kuwa rafiki wa Magufli.
 
Membe ni mojawapo wa makomredi wanaochukia rushwa nchi.alishiriki kwa kiasi kikubwa kulifanya fisadi likatwe na ccm,na akasababisha pia fisadi lisiende ikulu..asante Bernard Camilius Membe,gesi yetu imebaki salama

Wizara iliyotajwa kufisadi mabilion ya fedha kwa safari za kipuuzi nje ya nchi ni wizara ta mambo ya nje iliyokuwa chini ya Membe.
 
Hata Lyatonga alikuwa anasifiwa sana na akina LUKUVI, ila sidhani kama sasa anakumbukwa tena!

Kuitumikia CCM inahaitaji uwe na akili ya uwendawazimu!
 
Leo hii zitto anapongezwa na wanaccm kwa kitendo kimoja tu cha kubaki bungeni jana..........zitto huyu huyu anayeitwa mpinzani wa kweli sikuwahi kusikia akipongezwa wala kusifiwa na mwana ccm wakati wa swala la buzwagi,richmond, kagoda wala escrow.Cha ajabu sifa zake hazina mwendelezo unaotoka nyuma kukumbushia alichokifanya bungeni ila unaanzia jana na kuendelea.......ni zitto huyu huyu aliyehofia mpaka chakula cha hotelini wakati wa uwasilishwaji wa ripoti ya PAC mpaka kulazimika kumwita ndugu yake aje kumpikia chakula dodoma......leo ni shujaa wa ccm.......Jamani tusiwafanye watanzania wajinga kiasi hiki,..........Hizi siyo sifa ni kejeli kwa ndugu yangu zitto.
 
Sasa me kuna kitu siwaelewi hawa wanamsifia zitto kwa kutotoka bungeni, kwakuwa wabunge waliotoka ni wale wanaounda ukawa, sasa zitto angetoka km nani? Na kama angetoka hawa wanaomsifia wangekuja na mada ingine ambayo ingesema "zitto ajipendekeza ukawa" alikuwa hana option zaidi ya kubaki ndani, ukawa walitoka either wakaenda sehemu kujadili mambo yao kwakuwa ni team moja, sasa zitto angetoka angeenda wapi???? Lodge akasubili mkutano uishe au angeenda bar. Ikumbukwe kuwa CCM inapenda watu wa kuambiwa lia, nawao wanalia, wakisema chutama badi naww uchutame rasivyo utakuwa useless kwao
 
Ni kijana Mahiri na anajua siasa ya nyakati na wakati muafaka, sasa jiulize hao walio toka bungeni kwanza alifata nini mle ndani? Au je hawato ingia tena Bungeni? Ni ujinga tu wanao fanya
 
Ajabu ya mambo ya siasa yalivyo jana alikuwa mpinzani leo hii a napongezwa kwa kubakia bungeni huyo ndio Zito wa ACT wazalendo
 
Interest ndicho alichokiangalia....nipe nikupe ndio siasa za dunia

Watanzania now wameshikwa na upepo wa Magufuli
hawazungumzi why UKAWA walitoka nje
wanazungumza Magufuli alisema nini na nini kimetokea after..

UKAWA wanaweza jikuta wako sidelined na 'hot issues'...na upepo wa siasa...
 
Back
Top Bottom