petrinamwana
JF-Expert Member
- Dec 9, 2011
- 900
- 345
Ukawa mmechemka haha mlikuwa mnatafuta iwe kick watu wawapongeze sasa mtandaoni wanamuongelea zitto na magufuri hahaha kalata mmezichanga vibaya
Jiandaeni kisaikolojia 2020 mana wafuasi wengi wa UKAWA Kimbilio lao litakuwa ACT mana kwa sasa ndo chama pekee cha Upinzani kilicho makini na chenye viongozi wenye busara na vichwa vilivyotulia ambao wako kwa ajili ya maslah ya wananchi na sio yao binafsi kama UKAWA,
Lakini kama Zitto angeamua kutoka nje angekaa wapi? Maana mi namini UKAWA walipotoka nje kuna mahali walienda kukusanyika na kuongea mambo yao. Je, Zitto angekaa wapi na angeongea na nani na nini? Nampongeza sana kwa hilo.
Lakini ssem wakae wakijua kuwa Zitto kubaki ndani sio kwamba aliwaunga wao mkono. Jengo la bunge na bunge lenyewe sio mali ya ssem. Zitto alibaki ndani kama mbunge na sio mwanachama wa ssem. Alibaki ndani kutimiza wajibu wake kisheria, pia alibaki ili ajifunze na kuona kasoro ziko wapi ili apate mahali pa kuanzia katika kutekeleza mipango yake ya upinzani kisiasa. Asante Zitto kwa kujitambua na naamini hutakuwa kama mzee Cheyo au Lyatonga. Pia najua hutakuwa tayari kucheza ngoma usiyoijua
Tukumbuke kuwa kipindi cha sakata la escrow account, Zitto akiwa Mwenyekiti wa PAC tayari alishakuwa msaliti, mnafiki, CCM n.k. Lakini mbona hakufanya kazi kwa maslahi ya CCM? Uzuri wa Zitto hafanyi jambo ambalo haoni kama litaleta tija kwa wananchi, kwa hilo muiteni majina yote mabaya mnayojua lakini tunaomkubali tutaendelea kumuona kama mwanasiasa makini mwenye kujali maslahi ya nchi na wananchi.
Zitto na Jakaya ni smart politicians kwa hapa Tanzania. Fuatilia utaniambia.
Kama ulimsikiliza Kitila Mkumbo ni kwamba alichofanya Zitto ni msimamo wa chama chao cha ACT. Wao kama ukawa hawawatambui viongozi wa zamani wa znz ambao wamengangania madarakani. Lakini waliazimia viongozi hao wakiingia bungeni wasisimame ila wakae tu na si kutoka nje. Naona alichofanya Zitto ndicho kitendo sahihi na cha kiungwana kwa kuwa wao act wanamtambua rais na walitaka Zitto awe bungeni kusikiliza hotuba ya rais ya ufunguzi wa bunge.
Leo lowassa naye kamanda
Ukiona mpinzani anakusifia rudi nyuma jitafakari! ! Kwanini mtu unayepingana naye akusifie?
Je umemshinda?
Je amekushinda?
Je ametambua udhaifu wako na anakulia timing? Yaan kwanini akusifie? ??????????
Na mtu akimsifia fisadi anafaa kuwa rais tufanyaje?