Zitto, Makamba na mwakilishi wa TANESCO ndani ya mdahalo wa Star Tv

Hii midahalo ndo inatupumbaza huku wananchi tukiendelea kupigika kwa maisha haya yanayoshabihiana na ya jehanamu

Kama ni lazima kuwa na hii midahalo basi iwahusishe wataalamu wa sekta husika ili waje na suluhisho la mgao wa giza.

Lakini kuendelea na midahalo ya wanasiasa hakuna tutakachofaidika, tutaendelea na mgao wa giza na kuwatafutia umaarufu wa bei chee hawa wanasiasa.
 
Hivi mnyika amekosa hadhi kiasi cha kutaka kusaidiwa na JF member ashiriki wapi au ashiriki mijadala ipi?

Acheni ushabiki bana
 
tatizo lenu mnatoa hoja hapa kwa kutumia "masaburi" kufikiria. Mhe. Zitto Kabwe ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayosimamia Hesabu za Masahirika ya Umma. Tanesco ni shirika la Umma, ambalo Mhe. Zitto na Kamati yake wanapitia Hesabu zake. Acheni chuki binafsi.

Mbona povu linakutoka hivyo? Kila kitu mnakimbilia kusingizia chuki, chuki, chuki!

Mdahalo hauhusishi mashirika ya umma. Mdahalo hautahusu tanesco. Mdahalo utahusu nishati. Na unapozungumzia nishati ya umeme nchini unazungumzia mashirika ya umma na makampuni binafsi ambao kwa pamoja ndio wanawezesha upatikanaji wa umeme.

Mapenzi binafsi yasikufanye ukashindwa kutambua mambo madogo kama hili.
 
@Painstruth,
With due respect naomba nitofautiane na wewe. Kama umesoma vizuri michango ya hawa wanaJF utagundua one key question kwamba ni 'vigezo gani vilitumika' kumualika ZITTO na sio Mnyika (waziri kivuli wa wizara ya Nishati). Madai kwamba Mnyika ni mweupe (nadhani ulimaanisha ni mbumbumbu) in comparasion to Zitto yanaweza kuwa na walakini. Ni mweupe kwa vipi? Kuna evidence gani zinazothibitisha haya madai ya weupe wa Mnyika? Ni lini na ni wapi Mnyika amehojiwa kuhusu energy na ikagundulika kuwa ni mweupe? Michango ya Mnyika kuhusu Energy ipo, wasiliana na ofisi za bunge wakupe Hansard.

Kwenye red: uko sahihi kwamba nani kamualika Zitto, na kwa nini Zitto (shadow Finance Minister) na sio Mnyika (Shadow Energy Minister)? Star Tv au waandaji wa huu mdahalo walifikiaje uamuzi wa kuwa na Zitto na sio Mnyika? Kwa bahati nzuri Bongo ni tambarare sana na comments tunazotoa hapa zinatokana na mambo tunayoona mtaani.

Mkuu kuna watu hapa jamvini hataki kuona ama kusikia zito anaguswa hata kama ni kwa jambo jema.

Kwamba leo mnyika hafai na hana maana kabisa kwakuwa tu zito katajwa. Huu ni uhuni wa fikra. Hawa wote ni viongozi wetu lazima tuwaheshimu na kuwajadili kwa usawa bila kuonyesha dharau kwa yeyote.
 
Hivi huu mdahalo kumbe ni leo ee, haya ngoja tusubiri masaa kadhaa yaliyosalia.
 
Hivi mbona Zitto huzungumziwa vibaya na baadhi ya watu hapa JF hata kama atakuwa kaalikwa..Wenye kuandaa mdahalo wamemtaka Zitto na sio Mnyika, kosa liko wapi. halafu inaonyesha mdahalo huu hauna maana kwa sababu kenda Zitto lakini angeenda Mnyika ungekuwa wa maana..Hizi chuki zenu zinatokana wapi.. Ushikaji wa Zitto na Makamba unahusu nini? all my friends are CCM or CUF, tunaweza kuzungumzia tofauti zetu bila kushikana mashati.. mbona mnataka kujenga chuki ambazo hazina msingi wowote isipokuwa UBAGUZI...Na mkiendelea hivi itakuwa haina tofauti na Ubaguzi wa kidini, kabila, jinsi na sasa hivi Uchama..Hatutakiwi kwenda huko!

Na huyu Mnyika yuko wapi siku hizi? Toka achaguliwe mbunge kaingia mitini hana haja na JF tena...Na mtanisamehe sana maanake nasikia toka Mnyika ameukwaa Ubunge basi ndio mheshimiwa sana kuliko hata alowakuta!..
 
Ni mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Masharika ya Umma, ikiwamo TANESCO
 
Nadhani hakuna tatizo kwa uwepo wa zitto, hata yeye ni mwenyekiti wa kamati ya bunge inayohusika na mashirika ya umma na Tanesco ni shiirka la umma pia. Kama ngeleja angehudhuria hapa Mnyika ingekuwa nafasi yake.
 
Lisemwalo lipo kama halipo laja. Kimsingi sioni ubaya wa mh. Zitto kwenda kwenye mdahalo badala ya Mnyika.

Suala ambalo wapenda maendeleo tunatakiwa kujiuliza na kuliangalia kwa makini ni kwa nini baadhi ya wapenda maendelea wamekuwa ni wafuasi wa falsafa za CDM lakini wamekuwa wakimshutumu Zitto kila kukicha!?.Huyu bwana kuna tetesi zinavuja ndani ya Chama kutokana na mitazamo yake binafsi ambayo inamalengo ya kujiimarisha yeye kisiasa zaidi kuliko kukiimarisha chama.

Ila ninachofurahi ni kuwa wapende maendeleo wamekuwa wakiandika wazi wazi kwenye mitandao ya kijamii kama onyo .Hii inamanufaa hasa kama tetesi hizo ni za ukweli,pia hata kama si za ukweli anayo nafasi ya kuwa prove wrong wanaomshutumu coz inawezekana ni chuki binafsi.
 
Hivi mbona Zitto huzungumziwa vibaya na baadhi ya watu hapa JF hata kama atakuwa kaalikwa..Wenye kuandaa mdahalo wamemtaka Zitto na sio Mnyika, kosa liko wapi. halafu inaonyesha mdahalo huu hauna maana kwa sababu kenda Zitto lakini angeenda Mnyika ungekuwa wa maana..Hizi chuki zenu zinatokana wapi.. Ushikaji wa Zitto na Makamba unahusu nini? all my friends are CCM or CUF, tunaweza kuzungumzia tofauti zetu bila kushikana mashati.. mbona mnataka kujenga chuki ambazo hazina msingi wowote isipokuwa UBAGUZI...Na mkiendelea hivi itakuwa haina tofauti na Ubaguzi wa kidini, kabila, jinsi na sasa hivi Uchama..Hatutakiwi kwenda huko!

Na huyu Mnyika yuko wapi siku hizi? Toka achaguliwe mbunge kaingia mitini hana haja na JF tena...Na mtanisamehe sana maanake nasikia toka Mnyika ameukwaa Ubunge basi ndio mheshimiwa sana kuliko hata alowakuta!..
Ukweli mchungu huu! Hayuko active kama tulivyodhani kuwa akíingia bungeni tungepata fursa ya kuona mengi kutoka kwake.hafanyi vibaya bungeni lakini sio kivile tulivyotegemea.mfano tumekubwa na giza la kihistoria lakini hatujaona akimtoa jasho Ngereja kivilee!

Humu JF ndo kabisaa amesusa, sidhani kama umuhimu wa JF umepungua kwake kiasi hicho.napenda utulivu wa Mnyika lakini awe active na kusikika,yapo mengi tu hasa wizara yake na jimbo lake.

Zitto yupo active sana, pamoja na jukwaa hili kumsemea vibaya lakini hakosekani humu inapobidi ni kitu kinachomsaidia kujua mitizamo halisi ya watu juu yake.

Inabidi Mnyika awe makini sifa zisimharibu, aendelee kuwa kijana wa watu na kujichanganya pia kutoa mawazo yake wazi mfano JF.
 
Kwani lazima iwe CCM vs CDM? What about watanzania wakijadiliana kama watanzania?
 
Wakuu hivi punde Star Tv wametangaza kuwa Jumapili ya tar 16.10.2011 kutakuwa na Mdahalo kuhusu Nishati na Tanzania tuitakayo. Mdahalo utaongozwa na Rosemary Mwakitwange kuanzia saa 3.00 mpaka saa 5.00 Usiku.

Washiriki ni Zitto Kabwe (Mb), William Mhando (CEO-Tanesco), January Makamba (M/kiti-Kamati ya Bunge nishati na Madini) na Eliakim Maswi (Jairo wa sasa i.e Kaimu Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini)

Huyo elikimu siyo yule mwingereza?
Eliakimu mallya?
 
Hello - stop the bikering and wait for the discussion to begin.

It's not who take part that matters but what is raised in the debate and what is covered by the participants.Does it answer the questions raised by the majority of Tanzanians ?

Remember this not a school debate or an eloqusion contest.
 
Wakuu hivi punde Star Tv wametangaza kuwa Jumapili ya tar 16.10.2011 kutakuwa na Mdahalo kuhusu Nishati na Tanzania tuitakayo. Mdahalo utaongozwa na Rosemary Mwakitwange kuanzia saa 3.00 mpaka saa 5.00 Usiku.

Washiriki ni Zitto Kabwe (Mb), William Mhando (CEO-Tanesco), January Makamba (M/kiti-Kamati ya Bunge nishati na Madini) na Eliakim Maswi (Jairo wa sasa i.e Kaimu Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini)

LIVE TEXTS TO FOLLOW:

Uwii wameningeleja hata huku zenji!
Yatayojiri yatandikwe jamvini jamani!
 
mdahalo ndo unaanza....Zitto na Makamba wako ndani, mwakilishi wa Tanesco bado
 
Back
Top Bottom