VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Katika hali ya kustaajabisha, maafisa na wafanyakazi wa kawaida wa Kampuni ya Umeme Tanzania (TANESCO) walirukaruka kwa furaha baada ya kusikia na kujua uhamisho wa aliyekuwa Waziri wa Nishati Januari Makamba. Maafisa na watumishi hao wa Makao Makuu ya TANESCO walionesha furaha yao ya wazi kwakuwa walikuwa 'hawamtaki' Waziri Januari Makamba.
Wana-TANESCO wanashukuru na kumkaribisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Daktari Doto Biteko na kujiapiza kufanya naye kazi vyema. Hatahivyo, watumishi hao wamedai kuwa wanaendelea na maombi na mfungo wao ili Mungu amuongoze Rais Samia kumuondoa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Maharage Chande.
Makamba na Chande ambao ni marafiki wa karibu wa muda mrefu walikuwa hawakubaliki na wafanyakazi wa TANESCO kwa kile kinachosemwa kuwa wana kiburi, dharau na waligusa na kuondoa haki mbalimbali za wafanyakazi zikiwamo kufutwa kwa safari za kikazi. Nyaraka za ki-TANESCO zinaonesha kuwa kuna safari nyingi-hata zile zenye umuhimu ambazo zimefutwa na Chande kwa maelekezo ya Makamba.
Maombi ya wana-TANESCO yatafanikiwa?
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam