Zitto kugombea urais 2015?

Status
Not open for further replies.
Mh Zito ikiwekwa clip ya jana ya TBC utaumbuka. Mimi mwenyewe nilidhani "photoshop"
 
Zitto akitajwa tu hapa JF kila mmoja anachomoka kutoka kwenye pango lake, angalau apate moja, wawili kutoka kwake ama asikie wengine wanasema je kumhusu. Hii ni kuonyesha kuwa kijana Zitto ni figure ya kitaifa.

Na amekuwa akitumiwa kama nanga kwa wale walio marafiki zake, na kama upanga kwa wale walio adui zake.

Lakini Zitto namwaminia kwa kusoma katikati ya mistari kwa kila issue inayoinuliwa ama kwa nia ya kumjenga au kumbomoa.

Amefanikiwa kuwa kijana mwanadiplomasia wa kitanzania mwenye uwezo sii tu wakuyakwepa majungu nchini kwake bali mwenye uwezo wa kujenga mahusiano ya kitaifa na kimataifa. Ref. Mazungumzo yake na raisi wa Ujerumani. Mtakumbuka kuwa rais mtarajiwa Dr W. Slaa aliombwa na chama kuwania urais wakati tayari alishachukua form ya kuwania ubunge. Hii inaonyesha kwamba Slaa hakimbilii ikulu bali anatumwa na watu.

Ni dhahiri kwamba Zitto angeweza kuombwa ili atumwe yeye ikulu na anao uwezo huo kwani raia tumeuona uwezo wake wa kusimamia masuala ya kitaifa bungeni. Kizuizi pekee kwa zitto katika urais kwa sasa ni umri. Hivyo Zitto ana kila sababu ya kuwa rais wa Tanzania baada ya Slaa. Na hilo kijana atazidi kulingarisha katika bunge lijalo kwa hoja zake makini za uzalendo na utetezi wa rasilimali za nchi. Kwa sasa nguvu zote zimeelekezwa kwa Slaa katika nafasi ya urais ila imebidi tuwe na mjadala huu kwa sababu ya dhamira ya upotoshaji habari uliyofanywa na TBC1 kumhusu Zitto.

Dr SLAA KUTINGA MAGOGONI.
INAWEZEKANA!!
 
Maneno mazuri. Kama Zitto anajitambua kuwa ni target ya watu wanaosubiri mkono udondoke iwe kwa mazuri au mabaya inabidi awe mwangalifu anapotamka ajaribu kuchuja maneno. Wengi wanamwangalia kosa kidogo tu litakuzwa. Ni sawa na kudondoka kwa rais jangwani, wangapi siku hiyo walidondoka pale jangwani lakini aliyeonekana ni mmoja tu. Wakati anajiuliza hayo vile vile ajaribu kujiuliza kwa nini TBC ika select tukio hilo likawa News na si mengine.
 
Na mimi ngoja nikusaidie. Chance ya Zitto kugombea 2015 si kuwa ni ndogo tu ila haipo kabisa kwa vile katiba haimruhusu he will be 39 by that time. Kwa hiyo bado narudia tena conclusion yako ni butu kwa vile ime base kwenye wrong hypotheses.
Jaribu kuelewa katika context.
Mimi ninachoongelea hapa ni Zitto kusema ana mpango wa kugombea 2015 wakati chama cha chake kiko kwenye kampeni za kumuuza mgombea urais wao kwa wananchi.Swala la kwamba 2015 hatakuwa na sifa za kugombea,huko ni kujaribu kutoka nje ya hoja yangu.
 

Inabomoa na hata wananchi waliokuwa wanaelezwa hawakumshangilia. Sometimes watu huwa wanainuliwa na vyama vyao lakini wakifika bungeni wanaona kuwa wamefika kule kwa juhudi binafsi. Nahisi huyu bwana asipopata support kubwa ya chama chake anaweza kudondoshwa. Na ikumbukwe kuwa Kikwete ameruka jimbo lake ili aje kulikomboa mwishoni kabisa
 

Zitto kishaona kwamba Slaa hawezi kuukwaa Rais mwaka huu wala hiyo 2015 kwa namna zozote zile. Ametathmini kwa makini sana. Always mtu makini sana huwa hapendwi popote Duniani.
 
.

kuna mgogoro chadema, haiwezekani katikati ya kampeni za kumnadi Dr Slaa naye Zitto anajipigia kampeni ya Urais mwaka 2015 badala ya kumpigia kampeni Slaa. Kwa mfano, Slaa anashinda( utani tu) na kisha akawa na vipindi viwili 2010- 2020 kwa mujibu wa katiba.Haijawahi kutokea hapa nchini chama kinamnadi mgombea wake wa urais na mwingine ndani ya chama hicho hicho hatokei katika uzinduzi wa kampeni za chama chake (chadema) pale Jangwani na kuibukia kwao kigoma kutangaza Urais. Wenye akili watajiuliza kulikoni chadema? Je, wanastahili kuingia IKulu na mwendo huo.
 

Huyu dogo kwa ujumla wake hafai kabisa. Acha atapetape tu.
 


Ngabu, Nilichukizwa sana na distractions zako kwa hoja iliyopo mbeleni, kwa kusahihisha makosa ya kiuandishi ya Mh. Zitto badala ya kumlima maswali yahusianayo na mjadala kwa ku-capitalize kwenye fursa hii aliyopata kuweza kuingia JF...

Lakini baada ya kusoma hiyo ya Kibs na tahariri yako juu yake imebidi nicheke tu... :becky: So funny!!
 
Zitto kishaona kwamba Slaa hawezi kuukwaa Rais mwaka huu wala hiyo 2015 kwa namna zozote zile. Ametathmini kwa makini sana. Always mtu makini sana huwa hapendwi popote Duniani.

...there are so many contradictions in your statement, kama ingelikuwa ni kinyesi, basi ni kile chenye harufu ya embe!!!
 

Mh. Zitto, nakuunga mkono kwa maneno hayo. Huu ni wakati wa kusaidia mabadiliko yatokee na si kuyayumbisha. Pia nakusihi nawe uangalie maneno yako kwenye hizi kampeni, yasije kuwa kikwazo huko mbeleni.

Btw, unafikiri TBC wamefanya hivyo makusudi ili kuleta uchonganishi baina ya Wanachadema?!
 

watanzania bwana sasa na wewe umeona huo mwenendo huo ni ishu siyo, zitto sawa kaongea hivyo, lakini kwamtazamo wangu hicho si kizuizi cha chadema kuingia ikulu, kwa madai ni mwenendo mbaya, upi mwenendo ulio mzuri kwa wale ambao tayari wako ikulu,
nachelea kusema zitto kachemka na kupungukiwa na hekima, hata kama yeye anaona huo ni mtazamo wake kuona slaa hawezi kuingia ikulu, ni wazi kuw anaye sasa ni mbabaishaji, kwani mtu aliyeshiba hekima na busara hawezi kuutangaza undani wa nyumba yake hadharani basi ni awe wazi kuvaa sare za ccm kweupe ili atambulike na jamii, kama walivyofanya cuf kuuza uzaliwa wao wa kwanza kwa ccm kwa kigezo cha maridhiano
 

Wapenda mabadiriko tumwombe mungu sana hali ya sasa sio nzuri. habari niliyoipata kutoka kikao cha jana lumumba ni kuwa mmnyika asipite na nguvu kubwa zitaelekezwa huko lakini kwa Zitto ana baraka kubwa sana na kama chadema watamtimua basi atateuliwa na raisi kuwa mbunge. sasa nakuja huku na kuikuta hii tena ya kuwa Raisi basi inabidi niwe hoi mtu aliye niambia nilidhani ananitania.
 

Sasa kwa nini hukuingia na kuanza kumlima hayo maswali kama uliona mimi sikufanya hivyo?
 

Zitto,

Hujajibu swali, ulisema chochote kuhusu urais 2015? Walichosema wananchi ni nini na ulichosema wewe ni nini?

Majibu yako yanaonyesha unataka kuwa obscurantist na kubadilisha topic.

JF haijulikani kwa "ceasefire" na staha za kuogopana. JF inajulikana kwa kushikana mashati katika kutafuta ukweli. Ukituambia habari za ceasefire na staha tunaona umeshikwa pabaya na unatafuta pa kutokea.
 
Hao wananchi wa kijiji cha Kidahwe walisema nini na wewe ukasema nini? Tuhabarishe tafadhali...

Niliuliza hivyo kwenye post #84

Zitto,
Hujajibu swali, ulisema chochote kuhusu urais 2015? Walichosema wananchi ni nini na ulichosema wewe ni nini?

Kumbe na wewe umeliona hilo na kuuliza kile kile nilichouliza mimi....huyu jamaa analeta usanii hapa
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…