Ndugu zangu wana JF,
Toka asubuhi nimekuwa nikisoma maoni yenu kuhusiana na habari iliyorushwa na TBC1 kuhusiana na mimi kugombea Urais mwaka 2015. Kwanza, sio jambo zuri sana kudakia mambo bila kuwa na hbri za kutosha na kuhukumu watu. Watu makini husikia au kusoma mambo, kuyatafakari na kisha kuyatolea maoni. Pili, ni vema ifahamike kuwa mazingira niliyokuwa ninahutubia ni mazingira ya namna gani na kwamba
kauli ya Urais ni kauli kutoka kwa wananchi wa kijiji cha Kidahwe na wala sio kauli yangu. Ni kauli na maono ya watu wa Kigoma na nadhani sio dhambi hata kidogo. Mimi ni mwanasiasa na ninafahamu kanuni za mchezo huu. Kamwe siwezi katika kipindi hiki kuanza kutoa kauli za kuondoa attention kutoka kwa mgombea Urais wa chama changu. Mimi siwezi kuzuia TBC kutoa habari wanayotaka kutoa na wala siwalaumu TBC kwa kutoa habari hiyo kwani ni jambo lililotokea na umma una haki ya kuhabarishwa. Mimi nipo jimboni kwangu ninafanya kampeni za kuomba kura za HESHIMA. Pia ninamwombea kura Katibu Mkuu wangu Dr. Slaa ili awe Rais. Kila tukio la kampeni zangu ninaweka katika blogu yangu na pia katika facebook
Zitto na Demokrasia. Ninaomba wenye kuhitaji kufuatilia matukio ya Kigoma wafuatilie huko.
Ndugu zangu, busara ya kawaida inasema hiki ni kipindi cha kufanyakazi za kutafuta mabadiliko katika nchi yetu. Sio kipindi cha kushutumiana na kuzushiana mambo. Tuwe na staha. Hatutaleta change katika nchi yetu kwa kusemana na kusengenyana. Hatutaleta mabadiliko kwa kutegeana makosa. Angalau kwa kipindi hiki basi tuelekeze nguvu zetu katika kusaka kura za kuleta mabadiliko. Tunahitaji Madiwani, Wabunge na Rais.
Ninasononeshwa sana na muda unaopotea kusema Zitto hivi ama vile. Najua kuna Zitto haters humu. Basi fanyeni ceasefire ili tupite katika mchakato huu wa kusaidia mabadiliko katika nchi yetu. Mie nipo Kigoma nasaka kura za chama changu. Nanyi kokote mlipo chakarikeni. Kuna muda wa kutosha mwingi wa kutoa maoni kuhusu Urais wa Zitto mpaka ifike 2015. Wenye ya kusema watasema mengi na nitawasikiliza. This is Slaa time, not my time........... lets focus!