Zitto kugombea urais 2015?

Zitto kugombea urais 2015?

Status
Not open for further replies.
kwa kweli huyu kijana nimemfuatilia kwa muda mrefu na kugundua ni miongoni mwa viongozi wa chache ambao wana nia ya dhati ya kuwakombania wananchi wa nchi hii ya Tanzania

pia ni kijana mwenye maono na uwezo wa kujenga hoja, ni mtu mwenye kujiamini na kuwa tayari kuusimamia na kuutetea msimamo wake

ni mtu asiendeshwa na emotion kama viongozi wengine, ni kiongozi pekee karibu vyama vyote vya siasa na wasiokuwa na vyama wanamuheshimu na kumpenda

kwa kweli zitto anafaa kuwa mgombea wa chadema 2015

Kijumla anafaa sana LAKINI TATIZO LAKE PEKEE NI DINI YAKE. Je Chadema watalikubali hilo safari hii maana yake alipogombea Uenyekiti walimtoa kwa sababu za mavirigiza.
 
2015 zito atakua na miaka 39 kikatiba bado atakua hajatimiza viogezo vya kugombea uraisi
Zitto bado ni kijana asiyekua na msimamo kwani amediriki mara nyingi kwenda kinyume na maamuzi ya chama (CDM)
Zitto anaganga njaa na ndo sabab huwafuata fuata viongozi wa ccm na kuwasifia ili wampende hivyo hafai kwa sababu ni ndumi la kuwili.
hafai kua raisi wa tz kwa kpndi hiki labda 2025 akishakua mzima mwenye uwezo mzuri wa kufikiri kama the redeemer Dr Slaa.
 
CCM mnampigia chapuo Zitto kwa sababu mnajua hana msimamo, kama kamati ya madini ilimuyumbisha ataweza uraisi. Usijali atagombea ila kupitia NCCR MAGEUZI maana ndo mpango wake.
 
Ninachoweza kusema tu ni kuwa zito ananafasi kubwa ya kufika mbali sana kisiasa japo kuna watu wamekata tamaa au hawampendi kwa jinsi anavyofanya baadhi ya mambo yake ya kisiasa.
 
Tunataka katiba mpya kwanza; hao wanaowaza kugombea sasa kabla hatujaona mchango wao katika kupata katiba mpya wanatamaa na masilahi binafsi.

HUU NI WAKATI WA KUTAFUTA KATIBA MPYA ZAIDI YA HAPO NI KUPOTEZA MUDA.
 
Kwani itasaidia nini akigombea?ama sifa tu maana CCM LAZIMA WASHINDE PIGA UA HUO NDO UKWELI
 
Kijumla anafaa sana LAKINI TATIZO LAKE PEKEE NI DINI YAKE. Je Chadema watalikubali hilo safari hii maana yake alipogombea Uenyekiti walimtoa kwa sababu za mavirigiza.

Utakuwa lini na akili timamu wewe sheikh?
 
Hivi hizo habari zimetoka TBC1 tu? Je Zito mwenyewe kasemaje kazikubali?
 
Kuna taarifa (toka TBC1) kuwa leo Zitto katoa tamko rasmi kuwa ana mpango wa kugombea urais wa Tanzania mwaka 2015 na akawaomba wananchi wampe kura nyingi ili apate hadhi ya kuweza kugombea urais wa nchi hii.

Kila la heri mkuu Zitto, walau una nia! Je, katiba itabadilishwa?

LAKINI

... kwa hiyo ya kina Membe na Chikawe ya kweli??
 
Utakuwa lini na akili timamu wewe sheikh?

Kwani uongo? Hebu tuambie ni kitu gani kilichomfanya baraza la wazee wa Chadema kumuengua jina lake wakati wa uchaguzi mkuu wa chadema katika nafasi ya mwenyekiti Taifa
?
 
Kwani uongo? Hebu tuambie ni kitu gani kilichomfanya baraza la wazee wa Chadema kumuengua jina lake wakati wa uchaguzi mkuu wa chadema katika nafasi ya mwenyekiti Taifa
?

Unapenda kutoa majibu mepesi kwenye maswali magumu! Jaribu kutumia akili kidogo
 
Kwa kweli nampenda sana Zitto kwani siku zote yu makini na kauli zake na ana msimamo sana kwa yale anayoyakubali na sio mnafiki.

hata Chadema walipomgomea rais ndani ya bunge yeye alibaki na kusema hakutumwa na wapiga kura wake kutomtambua rais. Aliipongeza wazi wazi Serikali ya CCM kwa kujenga barabara nyingi za lami katika jimbo lake kuliko jimbo lolote kule kigoma na mengine mengi.

Mimi naona kuna dalili za kila aina kuona jina la Zitto linafifia na kufa kabisa hususan ndani a Chadema sababu kubwa na chanzo chake Pale alipotaka kuingilia himaya ya MBOWE kwa kuamua kugombea nafasi ya Uenyekiti Taifa wa Chadema na kuleta upinzani mkali sana na upepo ulibainisha wazi angeshinda nafasi hiyo toka kaskazini.

Pili nasukumwa kusema labda Dini yake inaweza kuwa kikwazo cha Chadema kumpendekeza kuwa rais.

naamini kama atapelekwa kwa wananchi yeye na Dr Slaa basi Slaa ataachwa vibaya sana kama alivyookolewa MBOWE katika Uenyekiti.

Na Chadema wanalijua hilo na jamii nzima amelielewa na kama hamumtaki basi mtoeni uanachama aende chama kingine kama hayajatokea yale ya kafulila.
 
Ur Bogus and Mentally retarded...karne hii unaendeleza ujinga wa mambo ya Ujima?
 
Duh,kweli harakati za ukombozi ni kaazi kweli kweli.Sijui mfumo wetu umetujaza woga kiasi gani.loh.
Tufike mahala tuweke vigezo vya Kiongozi tumtakaye.Hebu tujadili vigezo tuache kujadili watu
This is a democratic setting and everybody has a right to express his views and positions. What is needed therefore is credible, free and fair election, which respects the wishes and choices of Tanzanians
 
Nipo naangalia Taarifa ya habari, nimemuona Zitto Kabwe akihutubia kwenye kampeni za kuomba ubunge huko jimboni kwake kigoma. Katika mkutano huo Kabwe anawaeleza wananchi kuwa mwaka 2015 hataenda tena jimboni hapo, lakini si kugombea ubunge tena bali ni URAISI. Hivi ni nini mantiki ya hii kauli kwa kiongozi mwandamizi wa chama.

Je ni kauli ambayo inaleta taswira gani, Je inajenga au inabomoa?

mwaka 2000 Dr Ghalib Bilal alitangaza kugombea Urais wa Zanzibar wakati akijua fika kua ni utamaduni wa chama chake kumwachia mgombea aliye madarakani atimize miaka 10(by the Karume alikua ametumikia miaka 5 tu akiwania ngwe nyingine ya miaka 5), mwaka 2010 John Shibuda(akiwa ccm) alitangaza pia nia ya kugombe urais kupitia CCM wkt JK hajamaliza muda wake!!! kuna ubaya gani kwa zitto kugombea Urais kupitia chama ambacho hakishika hata dola??? ktk demokrasia hakuna ntu mwenye hati miliki ya wadhifa wowote
 
Mwacheni Zito, yeye ni mwana siasa ana haki kikatiba kugombea chochote kile kinachogombewa kwa kufuata katiba ya nchi. Kama kasema atakwenda kugombea Uraisi ni sawa. Anajua; labda wamekubaliana, au ana njia zake anazojua. Inawezekana kesi za Mtikila zikafanikiwa na tukawa na mgombea huru.

Demokrasia wacheni ichukue mkondo wake. Ama CDM hakuna primary ameshapitishwa na hivyo anaanza kupiga debe. Na anauhakika katiba itapitisha tutaanza na mgombea mwenye miaka 35 kiti cha Uraisi. Mimi bado natafakari.
 
Unapenda kutoa majibu mepesi kwenye maswali magumu! Jaribu kutumia akili kidogo

ReV Fr
Kuwa muwazi na mkweli , usilete mas'khara penye ukweli. Naomba jibu la suala langu na kama hujui basi sema sijui nitakusaidia.
 
Ur Bogus and Mentally retarded...karne hii unaendeleza ujinga wa mambo ya Ujima?

Matusi na lugha za kabehi za nini father? lete hoja kupingana na hoja zangu kama unazo?

Unajidhalilisha hivyo mzee mwenzngu, kama huna hoja ni bora kukaa kimya utajitunzia hishma yako.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom