Urais hautafutwi by hook and crook kama utashi wa mtu binafsi kwa sababu tu yeye kama yeye anataka kuwa rais. Rais ni kiongozi wa jamii na jamii ndio inayoona ni nani anayefaa kuwa rais na siyo personality.Zitto is a quality young leader ila nadhani he is rushing na hiyo ndoto yake ya urais ya 2015
Hizo ni hisia zako lkn kamwe sitoziamini, ninavyoona mimi Zitto Kabwe ni mpigani shupavu. Na kuwa mbunge wa chama cha upinzani hakumaanishi usiwe na uhusiano wa karibu na wabunge au viongozi wa chama tawala.
Jamani vyama vingi visiwe sababu ya kuwaacha marafiki zetu au kutokukaribisha marafiki wapya. Imekuwa muda mrefu akishutumiwa mhe Zitto kuwa ni kibaraka wa chama tawala especially alipotaka kugombania nafasi ya uwenyekiti wa CHADEMA na hii ilikuwa ni haki yake kikatiba. Kwa hiyo kwangu mimi hizi zote ni njama za kumuondoa Zitto katika duru ya kisiasa. Na ndugu zangu siasa sio ugomvi siasa ni hoja.
Kwa hiyo Zitto kuwa na ukaribu na viongozi wa chama tawala sio kosa sisi hatupigani vita na CCM tunapambana nao kisiasa so hakuna sababu ya mwanachadema au kiongozi wa chadema kutokuwa na mawasiliano na viongozi wa CCM.
Jamani hapa kuna kitu nyuma yake na ikiwa huu ndio itakuwa mwenendo wetu hatutofika popote na tutake tusitake Zitto kama mzito ametoa msaada mkubwa sio tu ktk chama bali kwa taifa kwa ujumla na asiyejua ni mchango Zitto kautoa ktk chama na taifa kwa ujumla basi ni mbumbumbu.
mimi sioni kama unatakiwa kutukana ndo ueleweke,kumbuka humu ndani watu wamesoma na ni watafiti wazuri sana,so be polite and wise,usikurupuke,sasa naomba ukae ulete facts ili tukujibu kwa facts,usilete taarabu
kwanza naomba nikuulize na ujibu critically,hivi wakati Zitto akihutubia na kusema 2015 yeye ndo ataipeperusha bendera ulimsikia mwenyewe ama uliipata kama SHOP TALKS? kama ulimsikia naomba utwambie alifata taratibu ZIPI na za CHAMA kipi
Pili,unasema siasa si ugomvi ndo maana Zitto anawasiliana na CCM kwa hyo tusimlaumu,mbona juzi kati Mbowe alikutana na JK wakatokea kwenye gazeti wamekumbatiana,kwanini hapa wanaCDM hawamsemi Mbowe?
Tatu,kukifanyia chama kazi haialalishi mtu atende kinyume na chama,kuna taratibu kwa viongozi na kwa wanachama,kwanini ukiuke taratibu za chama alafu ukisemwa unajitetea eti umekifanyia kazi nyingi chama kwahiyo wasikuseme?unaona sawa?
Kati ya vitu ambavyo CHADEMA wame-prove kuwa wapo makini ni namna ambavyo wameweza kum-handle Zitto, chama ndiyo kilimfikisha hapo alipo, umaarufu wake ulianza pale alipotolewa bungeni lakini CDM ikaamua kumbeba na kuunganisha watu ili ichukulie kitendo cha kufukuzwa bungeni na matokeoa ya ushujaa wake, na msimamo dhidi ya maslahi ya taifa, kweli watu wakjitokeza kwa wingi baada ili kuitikia wito wa chama.
Alipoona makutano ya watu kiasi kile akajua hii ni shauri ya yeye kama yeye kama Zitto na si chama, imani ikajengeka ndani yake kuwa yeye ni zaidi ya chama, akaanza kufuata utashi na hisia zake, kama treni iliyoacha reli...waandishi waliokuwa wanamsifia wakaona mwelekeo wake hatari, Kibanda akaandika kuonya, Ngurumo akaandika, Happiness Katabazi akaandika, wengi wakaandika, sikio la kufa halisikii dawa, magazeti makini yakaachana naye, akaenda kuibukia kwenye magazeti ya udaku, akayashambulia magazetu yetu kuwa, magazeti ya udaku ndiyo yenye nguvu na yasomwayo na watu wengi duniani, hakufafanua watu wa aina gani. Muda si mrefu urafiki na magazet hayo ukaisha baada ya kuandika skendo zake za ngono na wasichana kadhaa wanaodhani kuwa majina yao ni makubwa hapa nchini, kumbe yanafahamika tu na wala hayana ukubwa wowote.
Turudi kwenye mada...akazua hali ambayo ilitafsiriwa kama kizaazaa ndani ya CDM, nadhani alifanya makusudi ili afukuzwe aondoke "kishujaa"(kama alivyopokewa jangwani) kwasababu kuna watu ndani ya CCM walimdanganya kuwa akifukuzwa na hata akiipoteza nafasi ya ubunge, atapewa wa kuteuliwa na rais, pia kupewa unaibu waziri, na ili kumhakikishia hilo akajengewa ukaribu na idara za usalama na watu mashuhuri walio pretend kwenda kwake kupata ushauri na msaada wa mambo kadhaa, akazidi kuwa jeuri, lakini maskini kijana huyu hakujua kuwa watanzania walishamuona kimeo muda mrefu uliopita kiasi cha viongozi wa CDM kuwekwa katika msukosuko na wananachama wao kuwa kwa nini wanamlea, lakini uongozi ulionyesha ukomavu kwa kuendelea kuwa naye na kumkumbusha maadili ya chama na siasa kwa ujumla.
Kabla ya kampeni mwaka za mwaka jana, alitishia kutogombea, lakinibaadaye akapima akapima akaona namna maisha yatakavyokuwa magumu nje ya siasa, kwani hakuna kazi itakayomlipa kama siasa, ukichukulia kwa muda huo alishaamua kushiriki siasa kwa maslahi binafsi, hivyo akabatilisha msimamo wake na kuamua kutetea kiti chake, kampeni zilipowadia, akijua kuwa chama chake kimesimamisha mgombea wa nafasi ya urais, lakini akaonyesha kuibeza hatua hiyo kwa kusema kuwa, tunakwenda kuchagua wabunge na madiwani kwani rais tayari tunae tumuache amalize muda wake, lakini uongozi wa CDM uliendelea kumvumilia, Kitendo hicho cha uongozi wa CDM kuendelea kumvumilia kimebomoa sana Image ya Zitto kwa jamii,na kuifanya CDM ionekana kama chama imara kinachoweza kuishi pamoja hata inapotokea wakatofautiana mawazo kati yao.....kwa hili CDM nawapa sifa sana. Zitto amechuja lakini hilo halitambui tena kwasababu sasa hivi anaishi kwa kutegemea taarifa za wapambe. Ameaminishwa kuwa kila ampingae ni walewale wanaotumiwa dhidi yake.
Sasa hivi ni naibu Kiongozi wa kambi ya Upinzani bungeni anaongoza watu wasio mkubali watu ambao walipiga kura ya kumkataa, maamuzi ambayo hayakuwahi batilishwa popote pale, lakini kwasababu ya upenzi wake kwa madaraka bila kujari anaongoza kwa mazingira gani as long as anapata chake, katika hili Zitto hataki kutumia akili yake kama mwanasiasa kijana na msomi kama anavyotaka kutambulika, ameamua kung'ang'ania madaraka hayo bila suluhu ya aina yoyote, hataki kupisha nafasi hiyo kwa mtu mwingine anekubalika.
Zitto ambaye nahisi kila aonapo wakina Mnyika, Lema Lissu na wengineo wakitoa hoja zinazotikisa bunge huwa hajisikii vizuri kwa kuumia moyo, akitamani hali hiyo ya bunge kutetemeshwa kwa hoja ingesababishwa na yeye. alijaribu kutengeneza 'msukule/Zombi' wake pale bunge (Kafulila), lakini sijui ulipoishia, japo kuna yule bint, simkumbuki jina lake ila nadhani ni wa viti maalum CDM, lakini wote wapo off-color.
Huyo ndiye Zitto kabwe, ambaye sasa anataka atambulike kama rais mtarajiwa, kwani ameshatangaza dhamira yake ya kugombea urais mwaka 20015, Zitto ambaye watu wakimkubusha wajibu yeye anadhani ni watu wanaomuonea husda kwa 'mafanikio' yake kisiasa, Zitto anayeamini moyoni na kichwani mwake kuwa yeye ni zaidi ya chama, lakini mdomoni anahubiri kuwa hakuna aliye zaidi ya chama.
Nimeandika si kwa mtiririko rasmi wa uandishi na utoaji habari, bali kwa mtindo wa kugusia gusia tu ili kukumbusha, kwa lengo la kuendelea kufikiri na kutafakari kwa pamoja.
Kati ya vitu ambavyo CHADEMA wame-prove kuwa wapo makini ni namna ambavyo wameweza kum-handle Zitto, chama ndiyo .......
Alipoona makutano ya watu kiasi kile akajua hii ni shauri ya yeye kama yeye kama Zitto na si chama, imani ikajengeka ndani yake kuwa yeye ni zaidi ya chama, akaanza kufuata utashi na hisia zake, ..........................
tatizo la hili jukwaa wote sisi tunajidai ni watu wa kukosoa. Ukiuliza ebu great thinker chagua wizara , shiraka au jimbo moja unaloweza kuwa kiongozi. Taja mikakati mipango na maamuzi gani utafanya. Only few can answer this question
Most of us are just reactive waiting Ziitto to do this or kikwete to do this or Slaa to that.
Please let stop this trend.
Musembi Ungekuwa wewe ndo zitto ungefanya nini?
Kwanza nimezitaja hizo sifa ili aelewe aliyetowa "analysis" za hao "viongozi" watatu ni mtu mwenye upeo wa kuchambuwa.
Kuhusu hizo sifa (ni baadhi tu), hunijuwi sikujuwi, ukipenda zikubali ukipenda usizikubali.
Kuhusu kuziongelea kiingereza, napenda uelewe kuwa mimi nimeanza masomo yangu ya awali wakati bado tu Tanganyika na wakati huo, kiswahili kilikuwa ni somo moja tu la "swahili", masomo yote yalikuwa ya kiingereza, utaniwia, mtaniwia radhi ikiwa nnatumia maneno ya kiingereza kujielezea. Msamiati wa kiswahili cha kisasa hunipiga chenga na kuna kauafadhali fulani nitumiapo kiingereza kwa baadhi ya maneno. Hujitahid sana kuandika kiswahili kila niwezapo.
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Mimi maono yangu ni kwamba katika CDM ni ZITTO peke yake ambaye anaweza kutusogeza toka point A to B nchini Tanzania. Wengine wote wanafaa kuwa wasaidizi wake. Sisemi kwamba hawafai, lakini katika Presidential level, Zitto is the right choice. Slaa ni mtendaji, let him be PM na Mbowe labda VP. Huu ni ukweli ambao hata Stevie Wonder anaweza kuuona.
Napita.
tatizo la hili jukwaa wote sisi tunajidai ni watu wa kukosoa. Ukiuliza ebu great thinker chagua wizara , shiraka au jimbo moja unaloweza kuwa kiongozi. Taja mikakati mipango na maamuzi gani utafanya. Only few can answer this question
Most of us are just reactive waiting Ziitto to do this or kikwete to do this or Slaa to that.
Please let stop this trend.
Musembi Ungekuwa wewe ndo zitto ungefanya nini?
Musembi,
Usiwe mpumbavu kwa kushabikia upuuzi, werevu walio wengi wanajua ushujaa wa huyu kijana wa kigoma, na si kweli kuwa CDM imemvumilia kwa ajili ya ukomavu wa kisiasa usitudanganye we know mchezo mchafu wa viongozi wenu wanapoona mtu anae jiweza anatishiia umaarufu.
Unapotaja watu waliofulia ktk chadema na bado wamekumbatiwa na chama huwezi Mzito Kabwela ndugu, ukamuucha mwenyekiti Freeman Mbowe................. mbowe alipata umaarufu ktk bunge from 2000-2005 akautumia kugombea urais na watu mlimsifia, lakini leo dogo janja katangaza nia mnamponda kwa sababu mmelishwa sumu.
Chadema wamemkaba Zitto muda mrefu..... Tazama Mnyika alivyotengenezewa njia akiwa mgongoni kwa Zitto, kutoka kaimu naibu katibu mkuu mpaka kapora tonge la Zitto la kambi ya upinzani bungeni.............
Huyu jamaa yuko juuu hata kama CDM imeona alivyo na mlengo wa kulia coz wao ni Conservatives
mimi sioni kama unatakiwa kutukana ndo ueleweke,kumbuka humu ndani watu wamesoma na ni watafiti wazuri sana,so be polite and wise,usikurupuke,sasa naomba ukae ulete facts ili tukujibu kwa facts,usilete taarabu
kwanza naomba nikuulize na ujibu critically,hivi wakati Zitto akihutubia na kusema 2015 yeye ndo ataipeperusha bendera ulimsikia mwenyewe ama uliipata kama SHOP TALKS? kama ulimsikia naomba utwambie alifata taratibu ZIPI na za CHAMA kipi
Pili,unasema siasa si ugomvi ndo maana Zitto anawasiliana na CCM kwa hyo tusimlaumu,mbona juzi kati Mbowe alikutana na JK wakatokea kwenye gazeti wamekumbatiana,kwanini hapa wanaCDM hawamsemi Mbowe?
Tatu,kukifanyia chama kazi haialalishi mtu atende kinyume na chama,kuna taratibu kwa viongozi na kwa wanachama,kwanini ukiuke taratibu za chama alafu ukisemwa unajitetea eti umekifanyia kazi nyingi chama kwahiyo wasikuseme?unaona sawa?
Tusimshambulie msembi hayo ni mawazo yake,pia naomba nimuunge mkono msembi,hebu niulize wapenda mageuzi ktk tanzania hii inayomilikiwa na watu wachache,yuko wapi zitto kama yule wakati ni kiongozi UDSM?yukowapi zitto kama yule kabla hajafukuzwa bungeni?yuko wapi zitto kabla hajateuliwa kuwa mwenyekiti kamati ya hesabu za mashirika ya umma?jibu siyo zitto yule tuliyemzoea kabadilika hata ufunguzi wa matawi ya chama chake UDOM,ST JOHNS,MIPANGO,na kwingineko hatujamwona akijihusisha kitu ambacho kwa miaka ya nyuma ni lazima yeye ndo angekuwa mstari wa mbele,ni ukweli usiofichika mh zitto anahitaji kurudi kundini kabla ya huo uamzi wake huo na sisi kama vijana tuko tayari kumpokea kwa gharama yoyote maana hiki ndo chama pekee chenye kutufikisha safari tuliyoianzisha.TOGETHER WE CAN.dalali