Zitto kugombea urais 2015?

Zitto kugombea urais 2015?

Status
Not open for further replies.
Naitamani sana hiyo siku atakayochukua form na wazee wa chadema wasimuwekee nongwa. Zitto hakika anamvuto na pia mkimcheki anaonesha nia ya dhati, yapaswa wote tumuunge mkono, na hiyo itakuwa ni nusura ya chadema.otherwise mkijichanganya akagombea out of CDM basi chadema itabaki kuwa kama NCCR ilivyo kwa sasa.

Zitto please tunakuombea uchukue form. kura yangu itakuwa ya kwanza

Acha ushabiki wa kijinga hapa!
 
Bado nina imani naye japo anatakiwa kukumbuka kuwa Anapaswa kuwa moto au baridi sio viguvugu namna hii
 
Wakuu! Kuna tetesi ZITTO ameanza kujipanga [network and financial] ndani na nje ya CDM, kugombea uraisi 2015.
LICHA YA ADUI HATARI ITAKAYOIUA CCM KWA HARAKA ZAIDI NDANI KWA NDANI HIVI KARIBUNI, CHAMA HIKI KIKO MBIONI KUJITWISHA MIZIGO MIPYA KUMBEBA LOWASA NA HASA KUFANYA MAUAJI YA SAUTI PINZANI KISIRI KUSAFISHA NJIA

Kama uliwahi kufikiria kwamba CHADEMA ndicho adui mkubwa itakayoiua CCM basi kumbe kweli huelewi kabisa siasa za taifa hili zilivyo lakini hivi sasa kundi dogo ndani ya CCM linaloshikilia uhai wa chama hiki kiko mbioni 'KUSAFISHA NJIA KWA NAMNA YOYOTE ILE mmoja wao kushaka dola 2015.

Kwa wadadisi wa mambo, adui mkubwa zaidi na wa kutisha ajabu tayari yuko chumbani kwao CCM na hivi karibuni italipuka kuliko KINU CHA NYUKLIA CHA JAPAN na kutuma mionzi itakayoifuta kabisa CCM bukia chama cha upinzani namba 4 baada ya NCCR-Mageuzi hapa nchini.

Kwa kugusia tu kwa uchache; adui namba moja na hatasri mno hadi hivi, kwa haki kabisa kwa misingi ya kichama walichojiwekea, ni kwamba kule Wa-Tanzania Visiwani wanakiona CCM kama Chama kilichowasaliti kushika dola baada ya Mhe Benjamin Mkapa.

Hakika jambo hili la USALITI WA CCM KWA WATANZANIA VISIWANI ni tishio kubwa hivi sasa ambapo majina zaidi kutoka Bara yaendelea kutajwa KUMRITHI Mhe Kikwete ambaye naye kwanza hata hatima yake bado haiko wazi kwa umma wa Tanzania.Kwa jinsi mambo yalivyo nchini itakavyolipua Naona baada ya CCM kuwatapeli Wa-Tanzania Visiwani nafasi ya kugombea Urais, katika ule mpango wao maalum wa SIASA ZA KUKABIDHIANA UONGOZI WA NCHI KWA ZAMU KWA WATOTO WA WAKUBWA tu Bara na Visiwani.

Kitendo cha kikundi fulani kujipenyezea fedha haramu kupitia kwa akina Rostam Aziz na Edward Lowasa katika dakika za majeruhi kushawishi maamuzi kumtosa Mhe Salim Ahmed Salim (ambaye alipendwa sana bara na kuaminiwa mno na CCM-Mwalimu Nyerere) kule Dodoma, ndipo jini dume lenye vichwa viwili lilipozaliwa na kuleta salamu za maangamizi kwa hiki chama kilichowahi kupata umaarufu wa miaka mingi sana na kuaminiwa wa wengi nchini.

Miongoni mwa hizo salamu ni pamoja na (1) Wana-Mtandao badala ya Wana-CCM (ambao nao walikujakugawanyika mbele ya safari na kuwa (i) Wanamtandao Walaji (MAFISADI WA HIVI LEO) na Wanamtandao Waliwa ambao nao mahasibu yao mazito na yanayo nuka mno tutakuja kuyaelezea siku nyingine humu, (2) Wana-CCM Bara ambao lao ni kuwatumia baadhi ya Wana-CCM maswahiba kutoka Visiwani wakiwachezesha kama mchezo wa CHESS au DRAFT KISIASA ili kuzuia Wa-Tanzania wa kawaida Bara na Visiwani kuwa na maamuzi yoyote juu ya nani awaongoze isipokua tu maamuzi yote yatatoka siku zote kwa hii CCM Bara tu kwa sura zima ya Jamhuri yetu ya Muungano Tanzania.

Sasa kwa ujio wa CHADEMA na kuendelea kupendwa sana kwa chama hiki na azma yake ya KURUDISHA UONGOZI WA NCHI MIKONONI MWA WANANCHI WENYEWE kote Bara na Visiwani, na haya madai Moto Moto ya sisi Vijana kutaka Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi kote ndani ya taifa letu tayari zimekua ni mwiba mchungu katika ngozi ya kikundi hiki cha WAJANJA WACHACHE Wana-CCM Bara ambao mpaka hivi sasa, kwa mujibu wa habari nyeti za ndani sana chumbani mwao, kila ramani ya kisiasa wanalolichora linagoma kabisa, fedha walizokwisha wekeza kwenye juhudi hizi zote Bara na Visiwani zakumbwa na hatari za wazi mno na migawanyiko kuongezeka kila kukicha kati yao.

Hata nako ndani ya kikundi hicho cha hao Wajanja wachache Wana-CCM kumeibuka nako Migawanyiko mikali ya KI-KANDA kwa namna ambayo hata juhudi gani zifanyike hakuwezekani kupatanishwa kitu hata wakafanya kazi kwa pamoja.

Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani ya CCM katika ujumla wake, hali si shwari hata kidogo mle!! Wapo hata wale ambao, kwa ufinyu tu wa mawazo, wamefikia mahala wamependekeza MAJINA 15 ya baadhi ya watu mashuhuri na tishio kwa maslahi yao KUUAUA. Lini wauawe na kwa MTINDO GANI usioweza kuleta tafrani kwa kile wanachokiita 'Tishio la Nguvu ya Umma' kutokuweza kuwakumba.

Japo tatizo letu Wa-Tanzania tuliowengi ni mpaka tushikishwe jambo kiganjani ndio tuamini na wakati mwingine kugutuka kukiwa kumechelewa sana, miongoni mwa HAYO MAVUNO YA MIKONO YA KI-SHETANI tayari wameorodheshwa baadhi ya vinara wa kupinga madhambi ya CCM kwa njia mbali mbali nchini.

Kati ya watu wanaolengwa wamo (i) baadha ya viongozi tishio kwa kinyang'anyiro cha kiti cha urais 2015 waliomo ndani na nje ya hicho kikundi cha Rostam Aziz na Edward Lowasa. Pia, (ii) wapo baddhi ya viongozi wa serikali za wanafunzi nchini, (iii) baadha ya Wana-JF ambao wametajwa kama 'wakorofi na waharibifu', (iii) baadhi ya viongozi wa dini katika kanda fulani ambao wameelezewa kuwa na 'vinywa pana' na kuonekana kukisaidia CDM, (iv) wafanyabiashara wanaohofiwa kukifadhili CHADEMA hivi sasa na (v) na baadhi Wanataaluma wanaoonekana kujitolea kukisaidia CDM ki-mikakati ambayo hadi sasa yaelezewa KUKIDHOOFISHA MNO hiki chama tawala.

Sasa chama hiki chaonekana kubuni (1) mkakati mpya wa UONZOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA kukabidhiwa kwa zamu ile ile ila safari hii ni NDANI KWA NDANI TANZANIA BARA na vile vile ni (2) kwa KUZINGATIA AMA URAFIKI, UJIRANI AU UDINI kufanya hivyo.

Hata hivyo nako mambo si yenyewe baada ya wale wafadhali wa Uarabuni (Libya, Misri na Iran) nazo kukumbwa na matatizo kibao, yale yanayoendelea na yale ambayo yatalipukia kwao miezi michache ijayo; kikundi hiki ndani ya CCM kimechanganyikiwa kupindukia kwani kwani ufadhili wao hauna uhakika tena huku wananchi tukiendelea kulishikilia bando DOWANS na mianya mingine itakayotumika kuchota kodi zetu kuyatekelezea haya yote.

Dawa ya yote haya wanayopangwa kutekelezwa kwa mikono ya giza ni (1) kuhakikisha kwamba kila mmoja wetu anageuka kuwa mlinzi wa mwenzie dhidi ya juhudi hizi hatari, (2) kusimama kidete kwa KUSISITIZA Katiba Mpya ya Wananchi na Tume Huru ya Uchaguzi kupitishwa Bungeni mwezi ujao, (3) kuendelea kuhakikisha kwamba UTEUZI WA JOHN MIMOSE CHEYO kushika tena ile kamati kule bungeni haiwi tena kichochoro tena cha Mafisadi kujichotea fedha kununulia kura na kutekelezea mambo machafu huku Cheyo akijifanya hajaona kitu kwenye vitabu vyetu!!
 
Ni uwezo tu....kama nikweli hizo tetesi sioni tatizo...................
 
ZITO ni kijana msomi, ana uwezo wa kujenga hoja.

Sasa tatizo ni mambo na habari za kukinzana kuhusu migongano ndani ya CHADEMA. Hata wanachama na wananchi wana mashaka.

Inabidi ZITO ajijenge na ajenge imani kwa Wanachama na Wananchi.

Aachane na mambo ya Dowans, NSSF na mambo mengine yanayomchafua. Inatakiwa aweke msimamo wazi na ausimamie.

Huo ni ushauri wangu tu, kadri mtakavyoona inafaa Wananchi...
 
Its hot (vikao vimeanza) Watu wa karibu yake wanadai ana cheza kete na BAVICHA, pesa NSSF (kiwira) na mashirika mengine, wadau wake wanasema CHADEMA ama NCCR isue ni kwamba kaanza harakati, wanajigamba atakisambaratisha CDM. My take 100% atachemka, mpeni kchwa aone!
 
zitto amekuwa akifanya mambo mengi sana kujiuwa kisiasa.na ikiwa ataendelea hadi kufika 2015 nyota yake itakuwa imezimika, besides simwoni kama mtu haswa wa kugombea urais wa nchi apitie chadema ama ccm. bado sana. unafahamu ni mwepesi sana kununulika na kusaliti wenzie yule?
 
Kwa mara ya kwanza naona umetoa ushauri "Mzuri" kwa chadema.

Kaka mie uzalendo mbele chama chochote kikitoa point yenye mlengo mzuri kitaifa mie huwa nipo pamoja naye.ukileta negative atitude usitegemee kuwa nitakuunga mkono never. Unajua kwa siasa ya bongo chadema ikiendelea kumuweka mbele mbowe na slaa chama kitakufa wala sio muda mrefu, ndio maana nasupport Zitto achiwe mzigo.Zitto sijawahi kumuona kwenye movement za kuhamasisha vurugu kuonesha kuwa yupo kizalendo zaidi. Na ukichek Zitto ndiye aliyeipaisha chadema hilo liko wazi.
 
Kaka mie uzalendo mbele chama chochote kikitoa point yenye mlengo mzuri kitaifa mie huwa nipo pamoja naye.ukileta negative atitude usitegemee kuwa nitakuunga mkono never. Unajua kwa siasa ya bongo chadema ikiendelea kumuweka mbele mbowe na slaa chama kitakufa wala sio muda mrefu, ndio maana nasupport Zitto achiwe mzigo.Zitto sijawahi kumuona kwenye movement za kuhamasisha vurugu kuonesha kuwa yupo kizalendo zaidi. Na ukichek Zitto ndiye aliyeipaisha chadema hilo liko wazi.
Ana haki ya kugombea,hata hivyo hatujajua kwa tiketi ya chama gani,je issue ya umri nayo? ni miaka mingapi kabla hujaruhusiwa kugombea urais?Kama Zitto atakuwa amequalify then atakutana na kina Slaa na Mbowe depending on how watazichangisha karata zao za kisiasa kwa miaka hii kabla ya uchaguzi ujao.

Kuna wengine pia kina Lissu nk....Swali langu kama ulikuwa makini,lile neno mzuri nililiweka kwenye quotation marks,hopefully unaelewa implications zake,utafsiri ni juu yako,however nilikuwa nikimaanisha kwamba ni kivipi utaweza kutoa ushauri mzuri kwa chadema since ni wazi kuwa hukipendi kabisa chama hicho?
Napita tu neways...
 
Kama katiba itakuwa hii ya sasa mtajisumbua kujadili vitu ambavyo havipo. Sina hakika kama takuwa amefikisha miaka 40 iliyopo kwenye katiba labda 2020
 
Kaka mie uzalendo mbele chama chochote kikitoa point yenye mlengo mzuri kitaifa mie huwa nipo pamoja naye.ukileta negative atitude usitegemee kuwa nitakuunga mkono never. Unajua kwa siasa ya bongo chadema ikiendelea kumuweka mbele mbowe na slaa chama kitakufa wala sio muda mrefu, ndio maana nasupport Zitto achiwe mzigo.Zitto sijawahi kumuona kwenye movement za kuhamasisha vurugu kuonesha kuwa yupo kizalendo zaidi. Na ukichek Zitto ndiye aliyeipaisha chadema hilo liko wazi.
Ndio maana nimesema mtu kama wewe unanishangaza sana. Slaa na Mbowe wamefanya kazi kubwa kuifikisha CDM hapo ilipo. Sasa wewe unataka tutupe lulu yetu na kutuzugha kuwa unaweka uzalendo mbele. Mweeh!
 
As it stands today, it will be very unfortunate for CDM to place Zitto as their presedential candidate in 2015. It would have lost the GOLDEN CHANCE to lead the Tanzanians. He is a chameleon, always giving contradictory remarks and most of the time his change of position is accompanied by unfound arguments which unknowingly to Zitto send message to those who are knowledgable of the matter that he is lying. Yes, He has the potentials but he has not yet proven to be that worthy for the moment (the president of the Tanzania!! Hell NO!!). He needs to work out his undisclosed ties for us to trust him again (as before 2007). If I were to advise CDM, I would say, this is the critical issue which if not taken with the required weight NOW before 2015, a major conflict could errupt within the CDM when those who use him would want to see him dissecting the party (by forcing to become the presidential candidate for CDM even though there are others who are trustworthy than he is) leaving CCM win a landslide victory in the presidential elections due to anger that will have been created then within the party (between CDM members who support Zitto for the reasons they know themselves; knowingly or not knowingly what he is up to. And those who are patriotic and know what is going on. The scenario will be just like the one which we still witness that disrupted CCM in October 2010 elections after the names of those whom the members rejected were returned as candidates for various posts. I DO NOT RULE OUT THE POSSIBILITY THAT EVEN WITHIN THE CDM MEMBERS THERE ARE TRAITORS.
 
Wakuu! Kuna tetesi ZITTO ameanza kujipanga [network and financial] ndani na nje ya CDM, kugombea uraisi 2015.

Labda kama katiba itabadilishwa vinginevyo kufikia 2015 Zitto atakuwa hajiafikia miaka 40 na katiba ya sasa inataka mgombea asiwe chini ya 40.
 
Labda kama katiba itabadilishwa vinginevyo kufikia 2015 Zitto atakuwa hajiafikia miaka 40 na katiba ya sasa inataka mgombea asiwe chini ya 40.

Hivi walioweka kipengele cha miaka 40 kama kigezo cha mtu kufaa kuwa Rais wa Tanzania,walikuwa na lengo gani?Kwa mfano mtu ana miaka 35 na ana sifa zote za kuwa Rais wa Tanzania lakini kwavile hajafikisha miaka 40 basi hafai,na mtu asiye na sifa lakini kwavile ameshafikisha miaka 40,basi anafaa.Anayejua anifafanulie hii logic manake binafsi naona ni kama lengo fulani hivi la kuwanyima vijana hii nafasi.
 
Kama katiba itakuwa hii ya sasa mtajisumbua kujadili vitu ambavyo havipo. Sina hakika kama takuwa amefikisha miaka 40 iliyopo kwenye katiba labda 2020

Hata kama Katiba itaruhusu watoto wa miaka 12 kugombea urais, Zitto ana swali moja kubwa la kujibu kabla watu serious hawajamuunga mkono: ukigeugeu alikokuonesha mwaka juzi wa kukubali kutumwa na fisadi ROSTAM kupiga kampeni ya mitambo ya DOWANS kwa malipo duni ya VX Landcruiser second hand na flat Upanga! Akiingia Ikulu si atauza hata Tausi wa Ikulu kwa ROSTAM?
 
Hata kama Katiba itaruhusu watoto wa miaka 12 kugombea urais, Zitto ana swali moja kubwa la kujibu kabla watu serious hawajamuunga mkono: ukigeugeu alikokuonesha mwaka juzi wa kukubali kutumwa na fisadi ROSTAM kupiga kampeni ya mitambo ya DOWANS kwa malipo duni ya VX Landcruiser second hand na flat Upanga! Akiingia Ikulu si atauza hata Tausi wa Ikulu kwa ROSTAM?



ha ha ha mkuu unaua!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom