Zitto: Kikwete ni Rais wa ajabu.

Zitto: Kikwete ni Rais wa ajabu.

Akili ndogo haiwezi kutawala akili kubwa mdimu mzee wa kupgia debe I.O.C Ana uwezo upi BEN SAANANE Ambaye anadai ana maadu 11 tsa wanasiasa na 2 waandshi wa habari na atawashughuliki (i.e kung'oa kucha na meno) na atahakksha wanahama nchi huo ndio uwezo...ma brother ur wrong huwa nakuabali some v ur post bt apo upo wrong kaka...mdmu hana jpya
 
Akili ndogo haiwezi kutawala akili kubwa mdimu mzee wa kupgia debe I.O.C Ana uwezo upi BEN SAANANE Ambaye anadai ana maadu 11 tsa wanasiasa na 2 waandshi wa habari na atawashughulikia yeye mwenyewe (i.e kung'oa kucha na meno cz kushughulikia mtu ni kumtendea mabaya bila mipaka) na atahakksha wanahama nchi huo ndio uwezo...ma brother ur wrong huwa nakuabali some v ur post bt apo upo wrong kaka...mdmu hana jpya
 
Akijibu swali hilo, Zitto alisema kiongozi huyo wa nchi anapaswa kuheshimiwa kutokana na uamuzi wake wa kuruhusu uhuru wa maoni tofauti na ilivyo kwa viongozi wengi duniani.

Mbunge huyo alisema, huchukia watu wanaposema, Rais Kikwete ni dhaifu na kuwataka kutotumia vibaya uhuru wa kutoa maoni.

hakuukuta huo uhuru wa kutoa maoni katika katiba tena yenye viraka kibao?
 
Zitto Kabwe: Marufuku wabunge wa CHADEMA kuisifia serikali ya CCM!

https://www.jamiiforums.com/newreply.php?do=newreply&p=6355633


Mhe. Zitto amesema wabunge wa CHADEMA wamekuwa wavumilivu sana dhidi ya serikali kutokana na baadhi ya mambo ambayo serikali inayafanya chini ya kiwango. Amesema haya wakati akihoji kiasi kikubwa cha bilioni za fedha ambazo zilitengwa kwa ajili ya kulipa madeni na hazikutumika kulipa madeni. Zitto anahoji zilikwenda wapi. Na katika kuhoji hilo, ametoa amri kwa wabunge wote wa CHADEMA kutovumilia mambo ya hovyo hovyo yanayofanywa na serikali.


Pamoja ya kwamba natambua kuwa Mhe. Zitto ni naibu katibu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, sikutarajia asimame na kuagiza kwamba nawapa amri kwamba mfanye hivi au vile. Nilidhani angetumia lugha ambayo ni laini kidogo kwa kusema sisi kambi ya upinzani kuanzia sasa hatutavumilia hizi porojo za serikali. Badala ya kuwaambia wenzake kwamba natoa amri kwa wabunge wa CHADEMA kuhoji chochote chenye mashaka.


Pamoja na kuridhishwa na utendaji kazi wa Zitto, napenda kushauri kwamba apunguze ukali wa maneno dhidi ya wenzake hasa anapokuwa kwenye public places ikiwemo bungeni.


Naomba kutoa hoja.

Hivi Juliana Shonza ameolewa jamani? Kanona siku hizi si mchezo........
 
Ngumu kumesa kwa kweli ben saanane anamsfia membe....zito-jk...cdm take kea

Acha upotoshaji nimesifia Taaluma yake katika kutoa matamko lakini ameshindwa kuitumia taaluma yake kufanya overhaul ya foreign Policy.Rais kujiingiza na kuwa kama waziri wa mambo ya nje ni jambo la Ovyo na Membe alistahili kujiuzulu.Sipendi majukumu yangu yaingiliwe,sijui hilo Membe analionaje ikiwa katika taaluma ya Diplomasia suala la itifaki linapewa kipaumbele.?

JK alikua waziri wa Mambo ya Nje kwa Miaka 10.Wakati Rais wake anahubiri UTANDAWAZI JK yeye alishindwa kuanda mechanism ya economic diplomacy.Baada ya USSR kusambaratika miaka ya 1990,Miaka michache iliyofuata JK alikua waziri wa Mambo ya Nje.

Nchi kadhaa zilibadili mwelekeo wa Sera za mambo ya Nje lakini sisi bado tuliganda tu.Tunaishia kusifia kutembelewa na viongozi mabeberu.I can imagine jinsi akina Chifu Mangungo wa Msovero walivyokua wakisifiwa na waliowazunguka kwamba mmepata wageni weupe "Wazungu" .Pongezi ambazo hawakujua zitakua maombolezo baada ya kugundua kuwa wanauzwa
 
Hahaaa mzee wa sumu yaani wewe chuki zako kwa zitto bado hazijakuisha tu?
Mungu amuweke mbali na bahasha yako ile unabebeaga sumu maana tuliokuwa tumetumiwa na Mungu kumuokoa hatupo tena huko.

Actually Huna cha kuchangia katika topic zaidi ya kulitaja jina langu tu.Obsession....!

Anyways,I miss you Benazir!
 
Zitto anapomwagia misifa ya kijinga Mzee wake.uhuru wa kutoa maoni si hisani ya Kikwete hiyo ni haki ya kikataba.
 
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), amesema Rais Jakaya Kikwete ni mtu wa ajabu na kueleza kuwa kama si uvumilivu wake nchi ingekuwa katika machafuko makubwa.

Zitto ametoa kauli hiyo juzi, wakati akizungumza katika Kipindi cha Makutano kinachorushwa na Redio Magic FM ya jijini, Dar es Salaam ambapo alitakiwa kuelezea kipindi cha uongozi wa rais huyo ambaye amebakiza miaka miwili madarakani.

Akijibu swali hilo, Zitto alisema kiongozi huyo wa nchi anapaswa kuheshimiwa kutokana na uamuzi wake wa kuruhusu uhuru wa maoni tofauti na ilivyo kwa viongozi wengi duniani.

Mbunge huyo alisema, huchukia watu wanaposema, Rais Kikwete ni dhaifu na kuwataka kutotumia vibaya uhuru wa kutoa maoni.

“Naomba nisieleweke vibaya, lakini ukweli ni kwamba, Rais Kikwete ameacha kiasi kikubwa uhuru wa watu kutoa maoni. Sasa rais anaweza kutukanwa lakini yeye hachukii. Ni vema wananchi wakaacha kutumia vibaya uhuru huo.

“Kikwete ni mkuu wa nchi aliyejaribu kwa kiasi kikubwa kuwafanya watu kuwa huru. Kama rais angekuwa ni mtu mwenye hasira, ni wazi kwamba nchi ingekuwa katika machafuko makubwa,” alibainisha Zitto.

Pia alimwagia sifa, Rais Kikwete kwa kuimarisha uhusiano wa kimataifa na kuwezesha katika kipindi kifupi viongozi wawili wa mataifa makubwa kuja nchini.

“Rais ame balance (ameweka uwiano sawa) wa uhusiano wa kimataifa. Tunashuhudia ndani ya miezi mitatu marais wawili wanakuja nchini yani Rais wa China, Xi Jinping ambaye alikuja mapema mwaka huu na Rais wa Marekani, Barack Obama anayetarajia kuja nchini, Julai Mosi mwaka huu,” alisema mbunge huyo.

Mbali na sifa hizo, alimtahadharisha rais kuwa anapaswa kuwa makini na watu aliowaita wafaidhina ambao wanateka watu maarufu wakiwamo waandishi wa habari.

Alisema watu hao wanaweza kufuta sifa za uongozi wa Rais Kikwete kutokana na tabia iliyoanza kujengeka nchini hususan ya utekaji, kung’oa kucha na kutoa macho kama alivyofanyiwa Mhariri Mtendaji wa New Habari, Absolom Kibanda.

“Matukio yanayoendelea nchini yanaweza kumwondolea sifa rais. Sasa tunashuhudia waandishi wanaanza kuuawa na wengine kuzuriwa ni vema akakemea vitendo hivyo visiendelee kuwepo ndani ya jamii yetu,” alisema.

Zitto alimtaka rais kuhakikisha vurugu za kidini ambazo zimeanza kuchipukia nchini zinakomeshwa kwa nguvu zote ili Watanzania waendelee kuishi kwa kupendana kama ilivyokuwa miaka iliyopita.

“Kuhusu suala la udini na vitendo vya rushwa, namuomba Rais Kikwete awe mkali kwa kuvidhibiti. Iwapo vitadhibitiwa mapema ni wazi atamaliza uongozi wake na heshima kubwa,” alisisitiza Zitto.

Habari: JAMBO LEO.

Hili halipingiki . Utulivu na Ustaarabu wa JK.. Umesaidia sana kulinda Amani ya nchi yetu , la sivyo angefanya Reaction za Hapo kwa Hapo , hii inchi isngekua na Amani tuliyonayo kwa Sasa. Kwa hilo 2 , kila m2 anastahili kumsifu JK kwa Ustaarabu , uvumilivu na Adamu katika kufanya Maamuzi Makubwa . La sivyo ingewacost Wengi sana .. ! (Wekeni Uchama Mbali kwa haya Aliyosema Zitto) .
 
Hekima za Kikwete zitaanza kuthaminiwa akitoka madarakani.

Huyu Zzk huwa simuelewag!!

leo hii mpo mtandaoni na kutoa maoni sababu ya kikwete .. kikwete ni mvumilivu sana atakuja kukumbukwa atakapoondoka .. kuna nchi nyingine mitandao kama jamii forums wangeshaifunga kitambo...
kama ilivyo facebook kwa baadhi ya nchi

bravo zito! hakika weye ni mwanasiasa uliyekomaa

Mwanahalisi ilifungiwa awamu zilizopita si ya kikwete.. Ally Singano Zona na Daudi Mwangosi waliuawa awamu ambazo uvumilivu haukuwepo!. Kikwete angekuwa madarakani hao wasingeuawa. Hata Dr. Ulimboka, Kibanda na Mwakyembe wasingedhurika kama JK angekuwa madarakani kwa sababu ni mvumilivu mno!
 
Wapinzani kazi yao kupinga.., sasa kama hawa wapinzani wakitumia muda wao mwingi kusifia inabidi tuwaite
"Cheer Leaders", Sometimes nikimwangalia huyu kijana all I can say ni kwamba... "Ni mtu wa Ajabu Sana"
 
Hili halipingiki . Utulivu na Ustaarabu wa JK.. Umesaidia sana kulinda Amani ya nchi yetu , la sivyo angefanya Reaction za Hapo kwa Hapo , hii inchi isngekua na Amani tuliyonayo kwa Sasa. Kwa hilo 2 , kila m2 anastahili kumsifu JK kwa Ustaarabu , uvumilivu na Adamu katika kufanya Maamuzi Makubwa . La sivyo ingewacost Wengi sana .. ! (Wekeni Uchama Mbali kwa haya Aliyosema Zitto) .

Ni mvumilivu sana!.. Shehe ILUNGA katangaza hukumu ya kifo kwa viongozi wa kanisa tangu agosti mwaka jana amevumiliwa mpaka februari 2013 (alipotoroka/toroshwa kwenda Mombasa), baada ya makanisa kuchomwa moto na viongozi wa kikristo kuanza kuuawa.
 
Hili halipingiki . Utulivu na Ustaarabu wa JK.. Umesaidia sana kulinda Amani ya nchi yetu , la sivyo angefanya Reaction za Hapo kwa Hapo , hii inchi isngekua na Amani tuliyonayo kwa Sasa. Kwa hilo 2 , kila m2 anastahili kumsifu JK kwa Ustaarabu , uvumilivu na Adamu katika kufanya Maamuzi Makubwa . La sivyo ingewacost Wengi sana .. ! (Wekeni Uchama Mbali kwa haya Aliyosema Zitto) .

Katika mshikamano wenu wa kumsifia mzee wenu huyo mkumbuke kuwa kukaa kimya juu ya wizi wa EPA,MEREMETA,IPTL n.k ni Silent Compliment kwa wezi hao na wezi/mafisadi watarajiwa(Potential Thugs).

Eti hii nayo ni political Tolerance?Labda kama Kamusi/dictionary zimekua updated na kutoa maana ya ziada kwenye neno uvumilivu wa Kisiasa/political tolerance.Otherwise kwa kuwa wanaotoa hoja hizi wana sababu binafsi kuliko mwongozo wa taaluma zao.Umaarufu wa shahada zao utakua umeshuka kwa kiwango kikubwa.Taifa na kizazi kijacho hakitendewi haki kwa sababu ya tamaa na unafiki wetu
 
Hivi Juliana Shonza ameolewa jamani? Kanona siku hizi si mchezo........[/QUOTE]

Subiri miezi sita ijayo atakuwa na dogodogo.. Mtela kafanya mambo.
 
"Naomba nisieleweke vibaya, lakini ukweli ni kwamba, Rais Kikwete ameacha kiasi kikubwa uhuru wa watu kutoa maoni. Sasa rais anaweza kutukanwa lakini yeye hachukii. Ni vema wananchi wakaacha kutumia vibaya uhuru huo.

Kumwambia serikali yake inahusika na EPA ni matusi? Kumwambia serikali yake imewaua Ally Zona na Mwangosi ni matusi?... Kumwambia Serikali yake imenyamazia kwa muda mrefu uchomaji wa makanisa na mashambulizi dhidi ya mapadre na maaskofu ni matusi?
 
...Pia alimwagia sifa, Rais Kikwete kwa kuimarisha uhusiano wa kimataifa na kuwezesha katika kipindi kifupi viongozi wawili wa mataifa makubwa kuja nchini.

"Rais ame balance (ameweka uwiano sawa) wa uhusiano wa kimataifa. Tunashuhudia ndani ya miezi mitatu marais wawili wanakuja nchini yani Rais wa China, Xi Jinping ambaye alikuja mapema mwaka huu na Rais wa Marekani, Barack Obama anayetarajia kuja nchini, Julai Mosi mwaka huu," alisema mbunge huyo.

Huyu ndiye anataka urais wa nchi yetu? Hafai. HAO mabepari, kupe na wanyonyaji ni watu wa kushangiliwa? Akina Isike, Mkwawa na wafuasi wao wangewashangilia walowezi hivi sasa tungekuwa huru?.. Zitto Zyapunga.
 
Mwanahalisi ilifungiwa awamu zilizopita si ya kikwete.. Ally Singano Zona na Daudi Mwangosi waliuawa awamu ambazo uvumilivu haukuwepo!. Kikwete angekuwa madarakani hao wasingeuawa. Hata Dr. Ulimboka, Kibanda na Mwakyembe wasingedhurika kama JK angekuwa madarakani kwa sababu ni mvumilivu mno!

Hujui kwamba kufungiwa kwa gazeti la MWANAHALISI ilikuwa ni sherehe kwa huyo Baba Chachage Zitto alafu leo hii anajifanya kupotosha umma eti uhuru wa maoni wa kikatiba ni hisani za Rais kama sio umburura wa kisiasa na kujipendekeza huku.

Shame upon him.
 
Last edited by a moderator:
Hekima za Kikwete zitaanza kuthaminiwa akitoka madarakani.

Na udhaifu wake unatugharimu 'tangu yuko madarakani', na utaendelea kutugharimu mpaka kizazi cha tatu na cha nne!
 
Back
Top Bottom