Zitto anaongea nini?
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), amesema Rais Jakaya Kikwete ni mtu wa ajabu na kueleza kuwa kama si uvumilivu wake nchi ingekuwa katika machafuko makubwa.
Zitto ametoa kauli hiyo juzi, wakati akizungumza katika Kipindi cha Makutano kinachorushwa na Redio Magic FM ya jijini, Dar es Salaam ambapo alitakiwa kuelezea kipindi cha uongozi wa rais huyo ambaye amebakiza miaka miwili madarakani.
Akijibu swali hilo, Zitto alisema kiongozi huyo wa nchi anapaswa kuheshimiwa kutokana na uamuzi wake wa kuruhusu uhuru wa maoni tofauti na ilivyo kwa viongozi wengi duniani.
Mbunge huyo alisema, huchukia watu wanaposema, Rais Kikwete ni dhaifu na kuwataka kutotumia vibaya uhuru wa kutoa maoni.
"Naomba nisieleweke vibaya, lakini ukweli ni kwamba, Rais Kikwete ameacha kiasi kikubwa uhuru wa watu kutoa maoni. Sasa rais anaweza kutukanwa lakini yeye hachukii. Ni vema wananchi wakaacha kutumia vibaya uhuru huo.
"Kikwete ni mkuu wa nchi aliyejaribu kwa kiasi kikubwa kuwafanya watu kuwa huru. Kama rais angekuwa ni mtu mwenye hasira, ni wazi kwamba nchi ingekuwa katika machafuko makubwa," alibainisha Zitto.
Pia alimwagia sifa, Rais Kikwete kwa kuimarisha uhusiano wa kimataifa na kuwezesha katika kipindi kifupi viongozi wawili wa mataifa makubwa kuja nchini.
"Rais ame balance (ameweka uwiano sawa) wa uhusiano wa kimataifa. Tunashuhudia ndani ya miezi mitatu marais wawili wanakuja nchini yani Rais wa China, Xi Jinping ambaye alikuja mapema mwaka huu na Rais wa Marekani, Barack Obama anayetarajia kuja nchini, Julai Mosi mwaka huu," alisema mbunge huyo.
Mbali na sifa hizo, alimtahadharisha rais kuwa anapaswa kuwa makini na watu aliowaita wafaidhina ambao wanateka watu maarufu wakiwamo waandishi wa habari.
Alisema watu hao wanaweza kufuta sifa za uongozi wa Rais Kikwete kutokana na tabia iliyoanza kujengeka nchini hususan ya utekaji, kung'oa kucha na kutoa macho kama alivyofanyiwa Mhariri Mtendaji wa New Habari, Absolom Kibanda.
"Matukio yanayoendelea nchini yanaweza kumwondolea sifa rais. Sasa tunashuhudia waandishi wanaanza kuuawa na wengine kuzuriwa ni vema akakemea vitendo hivyo visiendelee kuwepo ndani ya jamii yetu," alisema.
Zitto alimtaka rais kuhakikisha vurugu za kidini ambazo zimeanza kuchipukia nchini zinakomeshwa kwa nguvu zote ili Watanzania waendelee kuishi kwa kupendana kama ilivyokuwa miaka iliyopita.
"Kuhusu suala la udini na vitendo vya rushwa, namuomba Rais Kikwete awe mkali kwa kuvidhibiti. Iwapo vitadhibitiwa mapema ni wazi atamaliza uongozi wake na heshima kubwa," alisisitiza Zitto.
Habari: JAMBO LEO.
Asante Ben, umewakilisha sehemu kubwa ya mawazo/mchango niliotaka kuutoa. Zitto bana! amefanya uchambuzi kama mojawapo ya magamba!-Kwenye Sera za Mambo ya Nje hatuangalii matukio ya kutembelewa.Sera yetu ya Mambo ya Nje ambayo tenets zake ni za tangu enzi za Mwl.Nyerere zinatakiwa kufanyiwa overhaul.Leo hii unashindwa kumtofautisha Rais na Waziri wa Mambo ya Nje.Ikiwa unawezesha Marais 2 wa Mataifa makubwa ambayo yana ambitions za kuchota raslimali(Ambition za kibeberu) huku mikataba ikiwa ya Siri na huthubutu kuweka wazi ili watanzania wajue kama tumenufaika ama la,does it make you a vibrant leader? Huo ni udhaifuHatuwezi kujivunia kutembelewa na Mabeberu ikiwa hatujui na wala hatushirikishwi katika mikataba iliyosainiwa.Hapo wananchi tutakua tumemsaidia Chifu Mangungo.2:Economic Diplomacy:Hadi sasa sera zetu za mambo ya nje zimeshindwa kwenda kasi na trend ya Dunia.Kenya wamelichukulua hili kwa umakini.Wizara imeshindwa ku-intergrate wizara ya Fedha na uchumi,viwanda na Biashara,Kilimo,Mali asili na Utalii na wizara ya Uwezeshaji.Tumekomalia uzururaji wa Rais kama nguzo kuu ya sera za Mambo ya nje.Tunatekeleza Sera ya Kuomba na KushukuruMembe ni msomi mzuri kwenye International Relations na ana uwezo lakini Rais hawezi kukwepa lawama za kuingilia Foreign Affairs.Katika mamia ya Ziara za Rais nje ya nchi isije kuonekana kuwa ndiyo utekelezaji wa Sera za Mambo ya nje.Hapana!Kukiwa na Sera imara kila jambo linaenda vizuri badala ya kutegemea kipaji cha kutembea cha Rais.Sera ni institutional Mechanism.Taasisi imara na sio watu imara wa kukata mbuga halafu wanarejea na matunda mwitu yenye sumu na kuiangamiza familia pole pole kwa miaka mingi ijayo.Ni nini sera yetu kwa Afrika?Nini sera yetu specific kwa EU?Ni nini sera yetu kwa Middle East?Ni nini Sera Yetu kwa SADC.Ni ipi sera yetu kwa Latin America?Ni utashi na kipaji cha Rais kuweza kuweka pozi la Picha na wakuu wa nchi hizo tu?Uimara wa Rais hapa Siuoni zaidi ya kipaji chake tu cha kutembea na kuimarisha AlbumActually Rais asingekua na njia nyingine ya kuficha udhaifu wake zaidi ya kutoa uhuru wa maoni ambao ni constitutional Right.Siyo Hisani.
Ngoja Raia wakosee na kumpa mzee Laigwanani EL, Mtaona moto wake...Ukikohoa tuu ndani/lupango/unaozea segerea. Anakulaga mori na maamuzi yake ndio kama alivyosema magumu,haangalii madhara yatokanayo/what's next. Yangu macho.MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), amesema Rais Jakaya Kikwete ni mtu wa ajabu na kueleza kuwa kama si uvumilivu wake nchi ingekuwa katika machafuko makubwa.
Zitto ametoa kauli hiyo juzi, wakati akizungumza katika Kipindi cha Makutano kinachorushwa na Redio Magic FM ya jijini, Dar es Salaam ambapo alitakiwa kuelezea kipindi cha uongozi wa rais huyo ambaye amebakiza miaka miwili madarakani.
Akijibu swali hilo, Zitto alisema kiongozi huyo wa nchi anapaswa kuheshimiwa kutokana na uamuzi wake wa kuruhusu uhuru wa maoni tofauti na ilivyo kwa viongozi wengi duniani.
Mbunge huyo alisema, huchukia watu wanaposema, Rais Kikwete ni dhaifu na kuwataka kutotumia vibaya uhuru wa kutoa maoni.
Naomba nisieleweke vibaya, lakini ukweli ni kwamba, Rais Kikwete ameacha kiasi kikubwa uhuru wa watu kutoa maoni. Sasa rais anaweza kutukanwa lakini yeye hachukii. Ni vema wananchi wakaacha kutumia vibaya uhuru huo.
Kikwete ni mkuu wa nchi aliyejaribu kwa kiasi kikubwa kuwafanya watu kuwa huru. Kama rais angekuwa ni mtu mwenye hasira, ni wazi kwamba nchi ingekuwa katika machafuko makubwa, alibainisha Zitto.
Pia alimwagia sifa, Rais Kikwete kwa kuimarisha uhusiano wa kimataifa na kuwezesha katika kipindi kifupi viongozi wawili wa mataifa makubwa kuja nchini.
Rais ame balance (ameweka uwiano sawa) wa uhusiano wa kimataifa. Tunashuhudia ndani ya miezi mitatu marais wawili wanakuja nchini yani Rais wa China, Xi Jinping ambaye alikuja mapema mwaka huu na Rais wa Marekani, Barack Obama anayetarajia kuja nchini, Julai Mosi mwaka huu, alisema mbunge huyo.
Mbali na sifa hizo, alimtahadharisha rais kuwa anapaswa kuwa makini na watu aliowaita wafaidhina ambao wanateka watu maarufu wakiwamo waandishi wa habari.
Alisema watu hao wanaweza kufuta sifa za uongozi wa Rais Kikwete kutokana na tabia iliyoanza kujengeka nchini hususan ya utekaji, kungoa kucha na kutoa macho kama alivyofanyiwa Mhariri Mtendaji wa New Habari, Absolom Kibanda.
Matukio yanayoendelea nchini yanaweza kumwondolea sifa rais. Sasa tunashuhudia waandishi wanaanza kuuawa na wengine kuzuriwa ni vema akakemea vitendo hivyo visiendelee kuwepo ndani ya jamii yetu, alisema.
Zitto alimtaka rais kuhakikisha vurugu za kidini ambazo zimeanza kuchipukia nchini zinakomeshwa kwa nguvu zote ili Watanzania waendelee kuishi kwa kupendana kama ilivyokuwa miaka iliyopita.
Kuhusu suala la udini na vitendo vya rushwa, namuomba Rais Kikwete awe mkali kwa kuvidhibiti. Iwapo vitadhibitiwa mapema ni wazi atamaliza uongozi wake na heshima kubwa, alisisitiza Zitto.
Habari: JAMBO LEO.
leo hii mpo mtandaoni na kutoa maoni sababu ya kikwete .. kikwete ni mvumilivu sana atakuja kukumbukwa atakapoondoka .. kuna nchi nyingine mitandao kama jamii forums wangeshaifunga kitambo...
kama ilivyo facebook kwa baadhi ya nchi
bravo zito! hakika weye ni mwanasiasa uliyekomaa
-Kwenye Sera za Mambo ya Nje hatuangalii matukio ya kutembelewa.Sera yetu ya Mambo ya Nje ambayo tenets zake ni za tangu enzi za Mwl.Nyerere zinatakiwa kufanyiwa overhaul.
Leo hii unashindwa kumtofautisha Rais na Waziri wa Mambo ya Nje.
Ikiwa unawezesha Marais 2 wa Mataifa makubwa ambayo yana ambitions za kuchota raslimali(Ambition za kibeberu) huku mikataba ikiwa ya Siri na huthubutu kuweka wazi ili watanzania wajue kama tumenufaika ama la,does it make you a vibrant leader? Huo ni udhaifu
Hatuwezi kujivunia kutembelewa na Mabeberu ikiwa hatujui na wala hatushirikishwi katika mikataba iliyosainiwa.Hapo wananchi tutakua tumemsaidia Chifu Mangungo.
2:Economic Diplomacy:Hadi sasa sera zetu za mambo ya nje zimeshindwa kwenda kasi na trend ya Dunia.Kenya wamelichukulua hili kwa umakini.Wizara imeshindwa ku-intergrate wizara ya Fedha na uchumi,viwanda na Biashara,Kilimo,Mali asili na Utalii na wizara ya Uwezeshaji.Tumekomalia uzururaji wa Rais kama nguzo kuu ya sera za Mambo ya nje.Tunatekeleza Sera ya Kuomba na Kushukuru
Membe ni msomi mzuri kwenye International Relations na ana uwezo lakini Rais hawezi kukwepa lawama za kuingilia Foreign Affairs.
Katika mamia ya Ziara za Rais nje ya nchi isije kuonekana kuwa ndiyo utekelezaji wa Sera za Mambo ya nje.Hapana!
Kukiwa na Sera imara kila jambo linaenda vizuri badala ya kutegemea kipaji cha kutembea cha Rais.Sera ni institutional Mechanism.Taasisi imara na sio watu imara wa kukata mbuga halafu wanarejea na matunda mwitu yenye sumu na kuiangamiza familia pole pole kwa miaka mingi ijayo.
Ni nini sera yetu kwa Afrika?Nini sera yetu specific kwa EU?Ni nini sera yetu kwa Middle East?Ni nini Sera Yetu kwa SADC.Ni ipi sera yetu kwa Latin America?Ni utashi na kipaji cha Rais kuweza kuweka pozi la Picha na wakuu wa nchi hizo tu?Uimara wa Rais hapa Siuoni zaidi ya kipaji chake tu cha kutembea na kuimarisha Album
Actually Rais asingekua na njia nyingine ya kuficha udhaifu wake zaidi ya kutoa uhuru wa maoni ambao ni constitutional Right.Siyo Hisani.
Kwa mara ya kwanza labda naweza kusema naungana na Bw.Zito Kabwe kwa kiasi kikubwa, pamoja na mambo mengine yote Bw.Kikwete anapaswa sana kusifiwa kwa hilo, watu wengi wanachoshindwa kuelewa ni kwamba Raisi wa Tanzania ana nguvu sana, Raisi Kikwete anaweza kuamua sasa hivi kusiwe na Chama cha Upinzani ikawa hivyo, anaweza kuamua Bw.Tundu Lisu awekwe jela maisha na ikawa hivyo, kwa kosa tu la kuhoji muungano, au Bw.Msigwa kumuita Bw.Kinana jangili.
Bw. Slaa amesema mara nyingi sana Majukwaani kwamba Raisi ni Fisadi yeye pamoja na Familia yake, amemdhalilisha sana Raisi Kikwete, lakini ameachwa aseme anavyotaka, watu wengi wanachosahau ni kwamba Raisi Kikwete anaweza kuamua sasa hivi tu CHADEMA ifutwe na hakuna kitu mtafanya mtaishia kulalamika humu basi, anaweza kuamua tu kumshughulikia Bw.Slaa na msimsikie tena na hakuna kitu mtafanya!
Watu wengi wanasahau CHADEMA wanakuwa na kesi wanakwenda Mahakamani na mara nyingine wanashinda kama kesi za Ubunge, kitu ambacho kwa nguvu na ushawishi alionao Raisi wa Tanzania angeweza kuingilia Mahakama na kuzuia, lkn hakufanya hivyo, Bw. Slaa amesema mara nyingi kwamba Nchi haitawalika wakati kuna Raisi wa nchi hilo peke yake lingetosha hata kumpa kesi ya Uhaini lkn ameachwa!
CHADEMA wameanzisha Ukanda kinyume na Katiba ya TZ jambo ambalo wangeweza hata kushitakiwa kwa uhaini wakati wa Mlm Nyerere lkn wameachwa!
Wanaandamana wanavyotaka, kitu ambacho wakati wa mlm Nyerere wasingeweza kufanya wameachwa, kwanza katika hali ya kawaida kama Raisi angeamua kutokana na nguvu aliyokuwa nayo hata hao Wabunge kama akina Bw.Nasari au Lema wasingeshinda Uchaguzi, lkn bado Raisi Kikwete akawaambia watu waacheni tu washinde!
Hivyo pamoja na mapungufu yake naweza kusema Raisi Kikwete ni moja kati ya Maraisi ambao ni wavulimivu sana na labda hajui au hataki kutumia madaraka yake MAKUBWA sana ambayo Katiba inampa kuwashughulikia wanaombeza na kumdharau hata kumuita dhaifu, hilo peke yake nchi nyingine hata TZ yetu ni Uhaini lkn akina Bw.Mnyika bado wanatembea huru, tena siku nyingine wanaalikwa Ikulu na wnashikana mikono, hilo linawezekana Tanzania tu!

Hivi aliyesema kwanzia leo ni marufuku CHADEMA kuisifia selekali si ndo huyu huyu au?
Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums