Zitto: Kikwete ni Rais wa ajabu.

Zitto: Kikwete ni Rais wa ajabu.

leo hii mpo mtandaoni na kutoa maoni sababu ya kikwete .. kikwete ni mvumilivu sana atakuja kukumbukwa atakapoondoka .. kuna nchi nyingine mitandao kama jamii forums wangeshaifunga kitambo...
kama ilivyo facebook kwa baadhi ya nchi

bravo zito! hakika weye ni mwanasiasa uliyekomaa
Uhuru wa kutoa maoni sio Hisani ya rais, ni haki ya kikatiba na ipo kwenye katiba.
swala la kutukana sio maoni hayo, ni kosa la kisheria.

Msichanganye mambo kama walevi wa gongo.
 
Marais wa nchi kubwa wanakuja sawaaa.....kufanyaje? kwa maslahi ya nani?...........loading answers
 
zitto kigeugeu alisema atawazuia wabunge wa chadema kusifia serikali ya ccm......au huyu sio zitto yule aliyesema hivyo!!!!? Tafakari!

Harafu eti anamsifu rais kwa ujio wa rais wa china na wa marekani? Kuna faida gan ya ujio wao? Ukolon mamboleo hautoisha Afrika na tutaendelea kunyonywa tu,wenzetu Latin America,Asia na baadhi ya nch za kusin mwa jangwa la Sahara washaanza kuwakataa hawa Mabepari,hawana impacts za kukufanya wewe uendelee bali kurud nyuma lkn sis tumebaki kusifia,kuchekelea,kupongezana bila kuangalia madhara yake. Tutafakari hata nje ya box pia!
 
ukisoma kwa makini sana hutamwelewa zito.Ni kwamba ametumia lugha fulani kwa akili kumponda kikwete.Alafu kaeleza kuwa ni kweli ni dhaifu.Kwa kiongozi kuwa dhaifu ni moja kwa moja inchi itayumba.Kutoa maoni kwa wananchi bila kuingiliwa hili kidogo nakubali alafu nakataa.moja ya masharti ya wafadhili wetu kama marekani[millenium funds]ni utawala bora,kupiga vita corruption,haki za binadamu n.k.Sasa huyu mr Vasco da Gama.alilijua hilo ndio maana watu waliokuwa wanatoa maoni yao walikuwa wanashughulikiwa kwa siri mfano Ulimboka,kibanda,mwagosi na wengine.Na pia kuna ushaidi wa text mgs watu utumiwa ambazo hazionyeshi zimetoka wapi.Ni system ya usiri ambayo ilikuwa inawatisha watoa maoni,lakini kwa kuangalia ni yupi tumshughulikie.kuna watu wengine wanaogopa kuwashughulikia.kwa hiyo bwana zito kwa hili swala sitakubaliana na wewe kwa 100%.Na kuhusu kuwaleta viongozi hili sio heshima.Hivi tumewaalika waje au wao walipanga kuja?.alafu kama sisi tumewaalika kuja hapa hizo gharama za mapokezi ni nani anatoa?na ni kiasi gani?.Kama ni sisi tutagaharimia hayo mapokezi.Watanzania wanataka kujua ni kiasi gani kimetumika ili tuweze kuona jinsi gani feed back ya huo ujio na au hasara.Na kama hizo pesa tungeweza kuzipeleka kwenye madawati,shule,walimu wapewe posho nzuri ingekuwa ni vizuri zaidi.MUNGU IBARIKI TANZANIA NA ILI TUPATE VIONGOZI SMART KUONGOZA NCHI HII.
 
Ben saa nane tena.....!!!

kukuthibitishia Zito amekuacha mbali ni pale unapotoa maoni kwenye nyayo zake na kusema baada ya yeye kusema

common man ur better than this

....and what do you mean? Hapo Red ulitaka kusema nini? Andika kwa kiswahili tu kama hujui kiingereza.
 
Huyu zzk ni kama vile ana kichwa cha mende,maana anaweza leo akaja na mambo ya kumtuhumu JAKAYA, Kesho akaja na mambo ya kukanusha alichokisema.Ila contradiction zote hizo huwa anazifanya bila ya yeye kujua kuwa nini anachokifanya.Huyu huyu zzk kichwa chake tayari kimefuta kumbukumbu ya maovu ya sirikali ya huyu baba mkwe wake inayoyafanya kwa wananchi?.Kwa uelewa wa bwana ZZK yeye anajua vurugu ni mpaka zifikie kiwango gani ndo aite kuwa hayo ni MACHAFUKO?,Mtwara,Mbeya,Mwanza,Arusha,Iringa Zanzibar na Geita machafuko yote yaliyotokea sehemu hizo yeye anaona hiyo ndo Amani?.Issue hapa cyo kwamba JAKAYA ni mvumilivu ila sisi wananchi ndo ni WAVUM
ILIVU.

Mkuu hilo la kuwa JK nin baba mkwe wa ZZK lina ukweli? Maanake haya maneno nimekuwa nikiyasikia sana mjini,heb niweke sawa hapo.
 
-Kwenye Sera za Mambo ya Nje hatuangalii matukio ya kutembelewa.Sera yetu ya Mambo ya Nje ambayo tenets zake ni za tangu enzi za Mwl.Nyerere zinatakiwa kufanyiwa overhaul.

Leo hii unashindwa kumtofautisha Rais na Waziri wa Mambo ya Nje.

Ikiwa unawezesha Marais 2 wa Mataifa makubwa ambayo yana ambitions za kuchota raslimali(Ambition za kibeberu) huku mikataba ikiwa ya Siri na huthubutu kuweka wazi ili watanzania wajue kama tumenufaika ama la,does it make you a vibrant leader? Huo ni udhaifu

Hatuwezi kujivunia kutembelewa na Mabeberu ikiwa hatujui na wala hatushirikishwi katika mikataba iliyosainiwa.Hapo wananchi tutakua tumemsaidia Chifu Mangungo.

2:Economic Diplomacy:Hadi sasa sera zetu za mambo ya nje zimeshindwa kwenda kasi na trend ya Dunia.Kenya wamelichukulua hili kwa umakini.Wizara imeshindwa ku-intergrate wizara ya Fedha na uchumi,viwanda na Biashara,Kilimo,Mali asili na Utalii na wizara ya Uwezeshaji.Tumekomalia uzururaji wa Rais kama nguzo kuu ya sera za Mambo ya nje.Tunatekeleza Sera ya Kuomba na Kushukuru

Membe ni msomi mzuri kwenye International Relations na ana uwezo lakini Rais hawezi kukwepa lawama za kuingilia Foreign Affairs.

Katika mamia ya Ziara za Rais nje ya nchi isije kuonekana kuwa ndiyo utekelezaji wa Sera za Mambo ya nje.Hapana!

Kukiwa na Sera imara kila jambo linaenda vizuri badala ya kutegemea kipaji cha kutembea cha Rais.Sera ni institutional Mechanism.Taasisi imara na sio watu imara wa kukata mbuga halafu wanarejea na matunda mwitu yenye sumu na kuiangamiza familia pole pole kwa miaka mingi ijayo.

Ni nini sera yetu kwa Afrika?Nini sera yetu specific kwa EU?Ni nini sera yetu kwa Middle East?Ni nini Sera Yetu kwa SADC.Ni ipi sera yetu kwa Latin America?Ni utashi na kipaji cha Rais kuweza kuweka pozi la Picha na wakuu wa nchi hizo tu?Uimara wa Rais hapa Siuoni zaidi ya kipaji chake tu cha kutembea na kuimarisha Album

Actually Rais asingekua na njia nyingine ya kuficha udhaifu wake zaidi ya kutoa uhuru wa maoni ambao ni constitutional Right.Siyo Hisani.

Positive criticisim
 
Tena Chadema wanapaswa kumshukuru Kikwete na Mzee Makamba kwa kuwapandisha chat ya siasa.
 
Positive criticism
 
Zitto naye afahamu collective responsibility!waliosema rais ni dhaifu ni watu wa chama chake sasa na yeye anapokuja kuongea kinyume na wenzie tumueleweje?kwa nini anapenda kujionyesha kuwa tofauti na wenzie hadharani?pamoja na yote,yeye kama mbunge wa upinzani anataka kutuambia kuwa yote haya yanayoendelea ktk awamu ya nne ni rais safi kabisa na wala si dhaifu?kweli kabisaa Zitto anaamini hivyo?kweli kabisa ujio wa hao marais yeye anaona ni jambo la kujivunia?Zitto kama umechoshwa na vita kaa kando askari wenzio waendelee.
 
Busara mtu huzaliwa nazo wala busara haziuzwi dukani. Maoni yake yanaashiria busara zako bwana Zzk.
 
Zitto kafilisika kihoja!
Rais mzuri duniani anapimwa kwa mambo makubwa 3
1.Kuimarisha uchumi-JK kashindwa
2.Commander-in-Chief-Majeshi yetu yanapigana vita isiyo na faida yyt huko Congo na yalienda Comorro
3.Usalama wa nchi-vurugu za Mtwara

MB wa Jamhuri ya TZ anaposifia kaa sababu tu JK kawa mstahimilivu au kwasababu tu kamleta Obama sio tu anajichanganya bali pia apuuzwe

1. 1985 Nchi ilifikia hatua haikuweza hata kulipia Mafuta iliyoagiza mara baada ya Meli kutia Nanga, Juhudi za Mzee Mwinyi, Mzee Warioba na Cleopa Msuya zilinusuru aibu baada ya kupata msaada wa Mugabe.
2. 1967-1980 Tulishiriki kwenye vita nyingi za kusini mwa Africa
3. Uhuru wa wananchi kutoa maoni ilikuwa ni ubeberu na ukibaraka kutoka Mataifa ya magharibi
4.Foleni kununua sukari na unga ilikuwa kali kuliko kugombea daladala ya mbagala au gongo la mboto
 
Hii ni kali pia.Bora tusubirie uzinduzi wa serikali yetu ya tanganyika chini ya chadema 2015.
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), amesema Rais Jakaya Kikwete ni mtu wa ajabu na kueleza kuwa kama si uvumilivu wake nchi ingekuwa katika machafuko makubwa.

Zitto ametoa kauli hiyo juzi, wakati akizungumza katika Kipindi cha Makutano kinachorushwa na Redio Magic FM ya jijini, Dar es Salaam ambapo alitakiwa kuelezea kipindi cha uongozi wa rais huyo ambaye amebakiza miaka miwili madarakani.

Akijibu swali hilo, Zitto alisema kiongozi huyo wa nchi anapaswa kuheshimiwa kutokana na uamuzi wake wa kuruhusu uhuru wa maoni tofauti na ilivyo kwa viongozi wengi duniani.

Mbunge huyo alisema, huchukia watu wanaposema, Rais Kikwete ni dhaifu na kuwataka kutotumia vibaya uhuru wa kutoa maoni.

“Naomba nisieleweke vibaya, lakini ukweli ni kwamba, Rais Kikwete ameacha kiasi kikubwa uhuru wa watu kutoa maoni. Sasa rais anaweza kutukanwa lakini yeye hachukii. Ni vema wananchi wakaacha kutumia vibaya uhuru huo.

“Kikwete ni mkuu wa nchi aliyejaribu kwa kiasi kikubwa kuwafanya watu kuwa huru. Kama rais angekuwa ni mtu mwenye hasira, ni wazi kwamba nchi ingekuwa katika machafuko makubwa,” alibainisha Zitto.

Pia alimwagia sifa, Rais Kikwete kwa kuimarisha uhusiano wa kimataifa na kuwezesha katika kipindi kifupi viongozi wawili wa mataifa makubwa kuja nchini.

“Rais ame balance (ameweka uwiano sawa) wa uhusiano wa kimataifa. Tunashuhudia ndani ya miezi mitatu marais wawili wanakuja nchini yani Rais wa China, Xi Jinping ambaye alikuja mapema mwaka huu na Rais wa Marekani, Barack Obama anayetarajia kuja nchini, Julai Mosi mwaka huu,” alisema mbunge huyo.

Mbali na sifa hizo, alimtahadharisha rais kuwa anapaswa kuwa makini na watu aliowaita wafaidhina ambao wanateka watu maarufu wakiwamo waandishi wa habari.

Alisema watu hao wanaweza kufuta sifa za uongozi wa Rais Kikwete kutokana na tabia iliyoanza kujengeka nchini hususan ya utekaji, kung’oa kucha na kutoa macho kama alivyofanyiwa Mhariri Mtendaji wa New Habari, Absolom Kibanda.

“Matukio yanayoendelea nchini yanaweza kumwondolea sifa rais. Sasa tunashuhudia waandishi wanaanza kuuawa na wengine kuzuriwa ni vema akakemea vitendo hivyo visiendelee kuwepo ndani ya jamii yetu,” alisema.

Zitto alimtaka rais kuhakikisha vurugu za kidini ambazo zimeanza kuchipukia nchini zinakomeshwa kwa nguvu zote ili Watanzania waendelee kuishi kwa kupendana kama ilivyokuwa miaka iliyopita.

“Kuhusu suala la udini na vitendo vya rushwa, namuomba Rais Kikwete awe mkali kwa kuvidhibiti. Iwapo vitadhibitiwa mapema ni wazi atamaliza uongozi wake na heshima kubwa,” alisisitiza Zitto.

Habari: JAMBO LEO.
 
Hili halipingiki . Utulivu na Ustaarabu wa JK.. Umesaidia sana kulinda Amani ya nchi yetu , la sivyo angefanya Reaction za Hapo kwa Hapo , hii inchi isngekua na Amani tuliyonayo kwa Sasa. Kwa hilo 2 , kila m2 anastahili kumsifu JK kwa Ustaarabu , uvumilivu na Adamu katika kufanya Maamuzi Makubwa . La sivyo ingewacost Wengi sana .. ! (Wekeni Uchama Mbali kwa haya Aliyosema Zitto) .

Watu wanamsakama Jk kwa sabab nchi imemshinda! We unadhani kwa hali hii atamfunga nani amuache nan? Atamuua nani na amuache nan? JK kachafuka kotekote nenda hata huko kijijin kabisa kila mtu anajuta kwa nin alimchagua. Watu mpaka wanawaza bora kijit angepewa Salim A.Salim mambo yangeenda vyema!
 
Ni ngumu sana kuhukumu kutokana na habari iliyokuwa narrated na Jambo Leo...
 
-Kwenye Sera za Mambo ya Nje hatuangalii matukio ya kutembelewa.Sera yetu ya Mambo ya Nje ambayo tenets zake ni za tangu enzi za Mwl.Nyerere zinatakiwa kufanyiwa overhaul.

Leo hii unashindwa kumtofautisha Rais na Waziri wa Mambo ya Nje.

Ikiwa unawezesha Marais 2 wa Mataifa makubwa ambayo yana ambitions za kuchota raslimali(Ambition za kibeberu) huku mikataba ikiwa ya Siri na huthubutu kuweka wazi ili watanzania wajue kama tumenufaika ama la,does it make you a vibrant leader? Huo ni udhaifu

Hatuwezi kujivunia kutembelewa na Mabeberu ikiwa hatujui na wala hatushirikishwi katika mikataba iliyosainiwa.Hapo wananchi tutakua tumemsaidia Chifu Mangungo.

2:Economic Diplomacy:Hadi sasa sera zetu za mambo ya nje zimeshindwa kwenda kasi na trend ya Dunia.Kenya wamelichukulua hili kwa umakini.Wizara imeshindwa ku-intergrate wizara ya Fedha na uchumi,viwanda na Biashara,Kilimo,Mali asili na Utalii na wizara ya Uwezeshaji.Tumekomalia uzururaji wa Rais kama nguzo kuu ya sera za Mambo ya nje.Tunatekeleza Sera ya Kuomba na Kushukuru

Membe ni msomi mzuri kwenye International Relations na ana uwezo lakini Rais hawezi kukwepa lawama za kuingilia Foreign Affairs.

Katika mamia ya Ziara za Rais nje ya nchi isije kuonekana kuwa ndiyo utekelezaji wa Sera za Mambo ya nje.Hapana!

Kukiwa na Sera imara kila jambo linaenda vizuri badala ya kutegemea kipaji cha kutembea cha Rais.Sera ni institutional Mechanism.Taasisi imara na sio watu imara wa kukata mbuga halafu wanarejea na matunda mwitu yenye sumu na kuiangamiza familia pole pole kwa miaka mingi ijayo.

Ni nini sera yetu kwa Afrika?Nini sera yetu specific kwa EU?Ni nini sera yetu kwa Middle East?Ni nini Sera Yetu kwa SADC.Ni ipi sera yetu kwa Latin America?Ni utashi na kipaji cha Rais kuweza kuweka pozi la Picha na wakuu wa nchi hizo tu?Uimara wa Rais hapa Siuoni zaidi ya kipaji chake tu cha kutembea na kuimarisha Album

Actually Rais asingekua na njia nyingine ya kuficha udhaifu wake zaidi ya kutoa uhuru wa maoni ambao ni constitutional Right.Siyo Hisani.

Duh Dogo kwa siasa za fitna na kuviziana.Hizi ulizoweka hapa ni msumari wa moto kwa Zitto.hongera kwa misimamo thabiti though!
 
Zitto mwenyewe haeleweki mara atishie kuuuaa hadi panya!
 
Kuwa na viongozi wa namna hii ni janga kwa taifa, hawaoni mbele, hawaangalii maendeleo ya Taifa, wao ni umimi tu.

Mh. JK amefanikiwa katika sekta gani?1
1. Uchumi- Ameshindwa kabisa, uchumi wa Tanzania unazidi kuyumba na kuporomoka kila kukicha
2. Elimu- Tumeshuhudia matokeo mabaya kupita yote katika historia ya matokeo kutoka NECTA, amejenga shule za kata ila nadhani bora hata primary schools za miaka ya 80
3.Rushwa- Nchi imekuwa na hali mbaya na harufu ya rushwa katika sekta zote inanuka sehemu zote Tanzania
4. Udini na Ukabila- Kipindi cha mh.JK tumeshuhudia mporomoko wa juu sana katika historia ya Tanzania kwa upande wa dini...hii haijawahi kutokea

Uhuru wa kutoa maoni na vyombo vya habari, tumeshuhudia mauaji mengi yenye utata mkubwa sana, hasa wa wanahabari.

Nashindwa kuelewa bwana Kabwe alimaanisha nini hapa. Mheshimiwa Kikwete ameliangusha Taifa kwa kiasi kikubwa sana, hastahili hata alama 20 kati ya 100.
 
hahahahahahaha
acha nicheke.

hivi uhuru wetu wa maoni ni hisani ya rais?
yani zitto anataka kutwambia kuwa angekuwa yeye ni rais leo hii tusingepata fursa ya kumkosoa?

Ina maana zitto angekuwa kwenye kiti cha jk ange funga na kuuwa wengi maana angechukia sana?

Yani zitto anataka hata haki yetu tuipigie magoti? uhuru wa kutoa maoni ni haki yetu hata angekuwa nani. Ina maana kipindi cha mkapa watu hawakutoa maoni?

HETI HUWA NA CHUKIA MTU AKIMUITA RAIS DHAIFU. hivi zitto ni kweli jk hana udhaifu kwenye utendaji? mbona utaki kumwambia ukweli unampanba?

zitto wewe si ndio ulipiga marufuku wabunge kuisifia serikali ya ccm? au sio wewe?

zitto ni kweli maendeleo yanapimwa kwa kutembelewa na wageni wengi?

Inaelekea ukiwa rais siku ukiitwa dhaifu huyo mtu kesho yake lazima aage dunia.

zitto ni kweli hakuna sababu ya jk kuitwa dahifu? hivi ni kweli haya matatizo yote uliyo yasema hakuna linalotokana na udhaifu wake kataika utendaji?

hii tabia ya ukigeugeu si nzuri kabisa nadhani hata yeye ana kushangaa kabisa.
 
Back
Top Bottom