Zitto Kabwe alikuwa na nguvu gani isiyo ya kawaida?

Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
18,783
66,962
Leo nimelikumbuka bunge la spika Sitta la mwaka 2005-2010.

Lilikuwa ni bunge la aina yake. Matukio mengi sana yalitokea katika bunge lile mpaka likagharimu nafasi ya hayati Sita kama Spika wa Bunge.

Ila leo, nimekumbuka zaidi matukio ya Zitto Kabwe.

Tukio la kwanza ni kuhusu ajali ya hayati Salome Mbatia. Chini ya kapeti inasadikika ajali ile ilipangwa iondoe uhai wa Zitto lakini jamaa alishtuka.

Tukio la pili, ni lile la kunyooshewa kidole bungeni na Mh. Mudhihiri Mudhihiri pale ambapo Zitto alituhumiwa kusema uongo bungeni.

Wiki chache baadae, Mh. Mudhihiri alipata ajali na ule mkono aliomnyooshea Zitto ukakatika mpaka leo ni mlemavu.

Zitto ana nguvu gani ya ziada?
 
Kila jambo hutokea kwa sababu zake, na wakati wake,

Zitto anaheshimika kwenye uimara wake akiwa kwenye Kambi ya upinzani

Ajali ya Mudhihir ichukuliwe kama ajali zingine tu, tusikuze mambo.
 
Back
Top Bottom