logician mkuu
JF-Expert Member
- Jun 2, 2014
- 792
- 221
Bado sana , CHADEMA mpaka waache uaharakati ndipo kitakua.
Niliooona Hii makala yenye kichwa cha habari cha Kingereza ...na kuandikwa na mmoja wa wasomi wetu wa Sasa mwenye masters ...basi nikajuwa ni makala ya Lugha ya Kingereza ...kumbe ni Kama makala Za ijumaa au bongo movie Zenye vichwa Vya habari Vya Kingereza makala Za Kiswahili ...
Kama ulidhamiria kufikisha UJUMBE Kiswahili ...basi kichwa cha habari weka Kiswahili ....
Juliana Shonza kwanza hakuna Chuo Kikuu cha Mlimani. Pili,kiingereza hakikupendi hivyo achana nacho. Tatu,hongera kwa kujua kutumia computer na mitandao kwa ujumla. Nne,CHADEMA na Zitto hawakuhusu. Tano,maDC wameshateuliwa. Sita,msalimie shemeji.
Juliana Shonza,
Kuna wakati nilimuona Zitto kuwa ni kijana mwenye aakili na mwenye mvuto kisiasa na nikajuwa yupo kwa ajili ya wananchi. Lakini baada ya sakata la Barrick na alipoanza kuelekezewa misaada jimboni kwake na Barrick na baada ya muda wa kuingizwa kwenye kamati ya madini na Kikwete akaanza kutembelea vogue, nikawa nna doubt nilivyomfikiria awali.
Juzi kuhusu suala la escrow na aliposhindwa kutetea hoja zake bungeni na mpaka alipoulizwa kuhusu na yeye kupokea fedha kutoka kwa Seth akajidai kujiliza bungeni na kusingizia kifo cha mama'ke, isitoshe, ile kukubali kila kilicho azimiwa awali na kamati yake kubadilishwa na nafasi yake kuchukuliwa bungeni na Anna Kilango, nikapata uhakika kabisa kuwa kijana ni bogus tena hafai kabisa na hana zaidi ya maslahi yake binafsi.
Juliana Shonza,
Kuna wakati nilimuona Zitto kuwa ni kijana mwenye aakili na mwenye mvuto kisiasa na nikajuwa yupo kwa ajili ya wananchi. Lakini baada ya sakata la Barrick na alipoanza kuelekezewa misaada jimboni kwake na Barrick na baada ya muda wa kuingizwa kwenye kamati ya madini na Kikwete akaanza kutembelea vogue, nikawa nna doubt nilivyomfikiria awali.
Juzi kuhusu suala la escrow na aliposhindwa kutetea hoja zake bungeni na mpaka alipoulizwa kuhusu na yeye kupokea fedha kutoka kwa Seth akajidai kujiliza bungeni na kusingizia kifo cha mama'ke, isitoshe, ile kukubali kila kilicho azimiwa awali na kamati yake kubadilishwa na nafasi yake kuchukuliwa bungeni na Anna Kilango, nikapata uhakika kabisa kuwa kijana ni bogus tena hafai kabisa na hana zaidi ya maslahi yake binafsi.
RED: Ni ngumu kupata wafuasi makini wenye hekima, busara; wanoheshimu utu, wasio na viburi, na mengine kama haya kama your inner most goal imejwengwa kwenye msingi huu. Nakuhakikishia, ni sahihi Zitto kuwa na wafuasi kama Juliana, Arfu,Mtella na wengineo kama hawa....... lakini HOFU yangu ni kuwa hatujaiimarisha wala kuiandaa ipasavyo CDM kuwaongoza watanzania, bado katika chama chetu tunalo tatizo la Uongozi..,I HAVE A FEAR OF BEING RULED BY A LESSER"
.......
I didn't find him,he finds me!!!!!!what kind of english is that?!!!!mama umeolewa tulia na mmeo,kama hawezi kupiga kazi pole.Zitto alishawahi kusema mkome kumuhusisha kwenye mambo yenu.
Lengo ya hiyo statement ni kueleza kuwa ZZK alimtokea, hata akiwa akiwa nje ya nchi, huwa anamuwaza Juliana na kumpigia trancall!, kitu ambacho hakueleza ni baada ya kurejea na kukaa pamoja, walimaliziaje!, hicho kilichomaliziwa ndicho kinachokumbushiwa na nficho kinach hitajika!.Mwisho, jifunze kiingereza. I didn't find him, he finds me hii inadhihirisha kuwa bado unahitaji kujifunza si kiingereza tu, na mengine mengi...
Juliana waliokuja sio wote ni vijana wa Chadema, sisi wengine sio Chadema, ila kiukweli, una matatizo ya 'deep rooted neurosis' bila wewe kujitua!. Usipoitibu, utapata 'frigidity!".Ni kama nilivyofikiri awali, fikra zangu hazikunidanganya kuwa baada ya kuyaandika haya watakuja vijana wa chadema walioamka na mning'inio kuanza kutukana na kutaja habari ya ndoa yangu na kila kashfa...
Kwa bahati mbaya, nililitegemea hilo tangu mwanzo kabisa hivyo halinikatishi tamaa hata kidogo...nitaendelea kuwaangushia vitu vizito vyenye ncha kali..
Dah! Picha tamu hili. Juliana Shonza njoo huku. Naona mmeanza kuinukiana - wewe wasema hakunaga kama yeye wenzio wasema ni bogus na mchumia tumbo. Niko pembeni hapa naangalia trela kabla ya picha lenyewe.
Soma hapa uniambie kama hoja hazijajibiwa.Mbona hakuna anayejibu hoja kwa hoja.Zaidi ya kumshambulia mtoa mada.Au mada haijaeleweka?
Kwanza si kweli kuwa nguvu ya Zitto ndio iliyojenga chama. Si kweli hata kidogo. Zitto amejengwa na chama na kufanywa maarufu na chama, kisha kiburi cha sifa kimemwingia.
Pili, inadhihirisha dhana ya usaliti. Zitto akiwa ndani ya CHADEMA, alipaswa kuainisha changamoto za chama na kujaribu kuzitatua katika timu iliyopo, na si kudhani kuwa AKILI YAKE ndio itajenga chama. Hii imedhihirika sasa. Baada ya yeye na vibaraka wenzake kama Juliana Shonza kuondoka CHADEMA, chama kimekuwa imara zaidi. Chama kimekuwa hakina migogoro kabisa. Chama kimejengeka zaidi na watu wana imani zaidi na chama.
Tatu, kama kweli uongozi wa Zitto ndicho kilichokuwa kinahitajika kukuza chama, Zitto ana nafasi katika chama chake kipya cha ACT-Tanzania. Zitto atoke CHADEMA, tuone kama ACT-Tanzania itakua kama anavyoota.
Nne, wewe kama mwana CCM ambaye una hakika kuwa Zitto ni hazina, kwa nini haushauri viongozi wa chama chako wamchukue Zitto na kumfanya kiongozi ndani ya CCM ili mumkomboe Mtanzania kwa kubadili fikra za kifisadi na za ulevi wa madaraka zilizo CCM na zenye madhara makubwa kwetu sisi kwa kuwa ndio wanaogawa rasilimali za Taifa?
Tano, unathibitisha kuwa kazi ya Zitto ndani ya CHADEMA ilikuwa kutengeneza makundi ya kumjenga yeye mwenyewe. "I have a fear of being ruled by a lesser" hii ni kauli isiyokilenga chama, ni ya kibinafsi. Ni mtu anayetafuta yeye madaraka, tena asiye na subira. Bora chama kivurugike kwa sababu ni yeye tu anayedhani anaweza. Kauli hii inadhihirisha kuwa mtu huyu anajitafuta mwenyewe.
Sita, kama ulidhani umeandika uzi huu kumjenga Zitto, hakika unazidi kumchafua.
Mwisho, jifunze kiingereza. I didn't find him, he finds me hii inadhihirisha kuwa bado unahitaji kujifunza si kiingereza tu, na mengine mengi...