Zitto Kabwe: Adui, Rafiki, Kipenzi

Zitto Kabwe: Adui, Rafiki, Kipenzi

Dada yangu Juliana, pole!, unamatatizo bila ya wewe kujijua!.

Pasco wa jf sio Chadema, hajawahi kuwa na hatawahi kuwa!.

Hayo niliyokueleza sio matusi ni ugonjwa na seriously ukiumwa magonjwa ya ndani, ukifika kwa daktari ni lazima umvulie!, hivyo hayo matatizo yako ya kisaikolojia ambayo wewe hujajijua, unapokuja humu kila uchao kutuvulia hiyo ..yako, wasiokujali wanakuacha tuu eundelee!, sisi tunaokujali ndio tunaokushauri, acha kutuvulia ,,na kutukalia ...!.
Mimi ni mwana saikolojia, hivyo nikisoma 'the motive behind' baadhi ya mabandiko yako, ni 'attention seeking!'. haitakusaidia huko ulipo, utaishia kutumika tuu kama pe.. na kuwa disposed off!.

Athari kubwa kwa tatizo lako sio siasa, sio chama bali ni familia!, please it from me!, kwa mwanamke, 'deep rooted neurosis' isipotibiwa, inaweza hata kusababisha 'frigidity!" na wengi wenye tatizo hili wanaweza wasijijue na kwa sababu haliwatesi wao!.

Pasco wa jf sio mwanachama wa chama chochote, hategeme cheo chochochote kutoka kwa yeyote, amekuwa hivyo toka uchaguzi wa 1995 alipokuja na "Mada Moto!" na baadae "Kiti Moto". Uchaguzi wa 2000 nikaja na "Ulingo wa Siasa!", uchaguzi wa 2005 nilikuwa UDSM na uchaguzi wa 2010 nilikuwa nahudumu kwa wazungu fulani!. Uchaguzi huu wa 2015 niko tena free, narudi tena ulingoni, CCM nitakuja, Chadema nikwenda, CUF nitapita na NCCR nitakanyaga, heshima yangu itabaki pale pale!, tena thank God huwa sithubutu kuwataja hawa wanasiasa wavua ch... wanaosubiri kupanda kisiasa kwa kupitia migongo ya watu, vinginevyo ungeniona!, ungenikimbia!.

Kiukweli Juliana nakupenda mno kwa ndati ndio maana nakuambia haya!, tibu tatizo lako!.
Ulipotimuliwa Chadema, sikumbuka kama kuna yeyoye aliyekulilia humu kama mimi!, naomba nikukumbushe tuu
[h=3]Wito: CHADEMA Watendeeni Haki Wanachama Wenu Ili ...[/h]
Pasco

Kaka kwa mtu anayejitambua na kujithamini atalichukua hili na kulifanyia kazi lakini kwa mtu anayejikweza hajui maana ya kujishusha mbele za watu na kutaka kuonekana kwa watu hakika huyo hajitambui na mtu kama huyo ni aheri kumwelekeza mbuzi kunywa maji kuliko kiumbe mzito kama huyo.
 
Dada yangu Juliana, pole!, unamatatizo bila ya wewe kujijua!.

Pasco wa jf sio Chadema, hajawahi kuwa na hatawahi kuwa!.

Hayo niliyokueleza sio matusi ni ugonjwa na seriously ukiumwa magonjwa ya ndani, ukifika kwa daktari ni lazima umvulie!, hivyo hayo matatizo yako ya kisaikolojia ambayo wewe hujajijua, unapokuja humu kila uchao kutuvulia hiyo ..yako, wasiokujali wanakuacha tuu eundelee!, sisi tunaokujali ndio tunaokushauri, acha kutuvulia ,,na kutukalia ...!.
Mimi ni mwana saikolojia, hivyo nikisoma 'the motive behind' baadhi ya mabandiko yako, ni 'attention seeking!'. haitakusaidia huko ulipo, utaishia kutumika tuu kama pe.. na kuwa disposed off!.

Athari kubwa kwa tatizo lako sio siasa, sio chama bali ni familia!, please it from me!, kwa mwanamke, 'deep rooted neurosis' isipotibiwa, inaweza hata kusababisha 'frigidity!" na wengi wenye tatizo hili wanaweza wasijijue na kwa sababu haliwatesi wao!.

Pasco wa jf sio mwanachama wa chama chochote, hategeme cheo chochochote kutoka kwa yeyote, amekuwa hivyo toka uchaguzi wa 1995 alipokuja na "Mada Moto!" na baadae "Kiti Moto". Uchaguzi wa 2000 nikaja na "Ulingo wa Siasa!", uchaguzi wa 2005 nilikuwa UDSM na uchaguzi wa 2010 nilikuwa nahudumu kwa wazungu fulani!. Uchaguzi huu wa 2015 niko tena free, narudi tena ulingoni, CCM nitakuja, Chadema nikwenda, CUF nitapita na NCCR nitakanyaga, heshima yangu itabaki pale pale!, tena thank God huwa sithubutu kuwataja hawa wanasiasa wavua ch... wanaosubiri kupanda kisiasa kwa kupitia migongo ya watu, vinginevyo ungeniona!, ungenikimbia!.

Kiukweli Juliana nakupenda mno kwa ndati ndio maana nakuambia haya!, tibu tatizo lako!.
Ulipotimuliwa Chadema, sikumbuka kama kuna yeyoye aliyekulilia humu kama mimi!, naomba nikukumbushe tuu
Wito: CHADEMA Watendeeni Haki Wanachama Wenu Ili ...


Pasco
jinsi alivyo empty headed,hata hapa hatokuelewa!
 
......
Ulipotimuliwa Chadema, sikumbuka kama kuna yeyoye aliyekulilia humu kama mimi!, naomba nikukumbushe tuu
Wito: CHADEMA Watendeeni Haki Wanachama Wenu Ili ...


Pasco

Aaah....

Hata hivyo Pasco wa JF nakushukuru sana kwa msaada wa ushauri wa kitabibu wa kisaikolojia unaoutoa kwa Juliana. Juliana ni mwaafrika tena mtanzania mwenzetu. Hivyo, hatuna budi kumsaidia afya yake inapozorota...lakini akishapona tumdhibiti asilete madhara kwenye mikakati yetu ya kuboresha maisha ya watanzania na waafrika kwa ujumla.
 
Aaah...! Kumbe Pascal Mayalla ndiye Pasco wa JF...!! Umeeleza kuwa ulimlilia Juliana alipotimuliwa wewe kama Pasco. Nimeenda kwenye uzi ule uliotoa link hapo juu sikuona hata tone la bandiko la Pasco wa JF akimlilia Juliana. Nakumbuka uliwahi kukanusha kwa kusema kuwa Pasco wa JF ni tofauti na Pasco Mayalla, baada ya wana JF kusema ID hizi mbili ni za mtu mmoja. Jitahidi kutunza kumbukumbu unapotoa maelezo yanayopindisha ukweli.

Hata hivyo Pasco wa JF nakushukuru sana kwa msaada wa ushauri wa kitabibu wa kisaikolojia unaoutoa kwa Juliana. Juliana ni mwaafrika tena mtanzania mwenzetu. Hivyo, hatuna budi kumsaidia afya yake inapozorota...lakini akishapona tumdhibiti asilete madhara kwenye mikakati yetu ya kuboresha maisha ya watanzania na waafrika kwa ujumla.

Kwa Sheria zetu Za humu ndani ..mtu Ana hiari ya kuwa verified member au hoax ......usipoteze muda kujua nani ni nani humu JF ....ni Kama kutaka kuingia chumbani kwa baba yako na mama yako ...usiku !!!!!
Sheria zetu ziko wazi .....hazina tofauti na Za Intelligence ....." Ni kosa la jinai kumtangaza mtumishi au wakala ...." ....humu ndani watu wanafanya kazi kubwa kuliko hata Hiyo ya TISS ...na wao wenyewe huvuta Mpunga wa kukusanyia taarifa na kuja Huku ..,wakapata nondo Za uhakika ......so leave PASCO ..alone usitake kumjua ,.hadi Siku akiamua yeye mwenyewe kuja open ....unafanya kosa ..Sana lamkukemewa
 
SIJAONA KATIKA COMMENTS ZAKO ZOOOTE kwenye thread hii ambayo imejadili contents..,zote zinataja jina July na kumshambulia, hakuna iliyojibu ama kushambulia hoja.

Lakini hili pia linanirudisha kule kule kwenye andiko langu lililopita kuwa Vijana wa Chadema mna uwezo mdogo sana wa kufikiri...mdogo mno.

Sitaki kusema kuwa wewe ni Nguin ..KILAZA ...hapana ...,ila napata mashaka Kama kila aliyejibu unamuoa hajakujibu ...count me off kwa sababu pengine Mimi sikuona content yeyote yenye MANTIKI Kama nilivoelezea awali .....Zaidi ya kuhisiwa kuwa pengine ...uko so depressed ..,na ukiacha Ndugu yetu Mwigulu ambaye kidogo amekuwa na moyo wa kibinadamu ....wengine hawajataka kuwaamini ...na kuwafanya mpate inferiority complex syndrome ....na kawaida ya Hali Hii ....ni kutafuta namna yeyote ya kupata attention kwa watu....

Nakumbuka kibwagizo cha wimbo wa ...DDC MLIMANI PARK ORCHESTRA ....( literally to tell you kuwa wengine Huku sio watoto wenzako ....)
Kisa Hiki kilimkuta Almarhum Muhidin Gurumo ...Baada ya Kurubuniwa na Kujiunga na band ya Ochestra Safari Sound " wana ndekulle " ...kwa ahadi ya Gari ..,nyumba na mengine ..Baada ya muda akagundua kuwa ahadi zilikua uwongo na akawa anajipitisha kwa bwana wa zamani ...ili arudiwe ..

Kwenye wimbo huu Cosmas Chidule akaimba...

" sio wewe peke yako wako wenzio waliondoka ...
Na bado tunapanda nao ,
UDA NA DALA DALA ...

ULISEMA MWENYEWE UMEPATA BWANA MWENYE PESA EHEEEEE....
ATAKUJENGEA NYUMBA.....
ATAKUNUNULIA GARI EEEE..
SASA UNALIA......
 
Kuna kashfa inaenda na kujirudia kuwa Bwana Zitto Zuberi Kabwe (Mwanasiasa msafi kuliko wanasiasa wote kuwahi kutokea Tanzania) ni moja ya watu walionufaika na mgao wa fedha za escrow, japo sijawahi msikia akitamka kwa ulimi wake kuwa hajapokea, ameishia kusema watu wachunguze, nitaendelea kuamini katika misingi ya mtu ni huru mpaka pale itakapothibitika kua ana makosa.

Lakini kaka yangu huyu amekuwa ni mtaalamu mzuri wa matumizi ya "fallacy" kwa waliosoma falsafa wataelewa. Zinapozuka kashfa dhidi yake, huwa anatumia A kujibu swali B.

Tundu Lissu alipomkashifu kwa kupokea pesa toka kwa Mkono na mpaka sasa ana miliki magari mawili ya Mkono, Bwana Zitto aliishia kuhamishia kashfa kwa Mh. Mbowe, na kusema haongei na kifaranga yaani Lissu, hii kwenye falsafa inaitwa appeal to mockery ab absurdo lakini pia mbinu nyengine mheshimiwa hutumia ni Argumentum ad misericordiam au kwa lughanyepesi appeal to pity (inatafsiriwa kama kuweza kushinda mjadala kwa kuvuta hisia na huruma ya walio wengi) Ilipozuka kashfa kuwa bwana Zitto Kabwe kuna ufisadi anafanya kupitia kampuni ya Gombe advisors, Bwana Zitto alijibu ameumizwa sana kwa kuwa yupo busy anamuuguza mama ( Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema Peponi aamin) ilipoibuka tena bungeni kashfa ya kupokea hela za escrow alisema tumuache mama apumzike kwa amani.

Lakini kwa kuwa vifaranga vimekuwa, na hana anayemuuguza, tunaomba sasa atujibu kwa ufasaha kwa kuwa maelezo yake ya awali yalijaa na uuguzi, kuhusu mikataba wa leka Dutigite kwa upande mmoja na NSSF na TANAPA kwa upande mwengine

Kampuni ya Leka Dutigite ina wana hisa 16, 15 kati yao ni wasanii wa kizazi kipya wenye hisa asilimia 5 kila mmoja hivyo kuwa idadi ya asilimia 75 na asilimia 25 zilizobakia zinamilikiwa na Gombe advisors. Swali huyu Gombe ni nani?

Ukienda kuangalia makabrasha ya Brela Gombe advisors inamilikiwa na watu wawili, mtu mmoja mwenye jina la kikenya mwenye asilimia 25 na Bwana Zitto kabwe ambae kwenye fomu amejijaza kama mchumi badala ya kiongozi wa Umma

Kwa hiyo kumbe NSSF na TANAPA mashirika ya Umma ambayo yanakaguliwa yasifanye ufisadi na Bwana Zitto kabwe kwa mkono wa kulia, ukija mkono wa kushoto unakuta Bwana Zitto kabwe ndo mwanahisa mkuu kwenye mikataba ya kibiashara baina ya NSSF, TANAPA na leka dutigite, japo yeye anadai hakuna mgongano wa kimaslahi.

Katika tenda moja, NSSF iliilipa Leka Dutigite shilingi milioni 120, milioni 90 kati ya hizo zilitolewa siku moja baada ya kuwekwa, siku moja kabla ya uchaguzi wa kamati ya hesabu za mashirika ya umma PAC uliomfanya Bwana Zitto kuwa mwenyekiti wa kamati na kumng'oa mzee Cheyo aliyekuwa anafanya kazi kwa weledi mkubwa. Coincidence?

Na ni bahati nzuri kuwa hizo pesa zilienda kutolewa na Habib Mchange, (bank statement inaeleza hivyo) aliyefukuzwa Chadema kwa kosa la kuwa kibaraka wa Zitto na kupanga mapinduzi ndani ya Chama, leo ndio katibu mkuu wa LekaDutigite kampuni ambayo Zitto anasema hana maslahi humo, kwa nini aweke watu wake?

Sasa hapa kuna maswali yanajitokeza

1. Je NSSF na TANAPA ni mashirika ya Umma au hapana? Na je Zitto ni kiongozi wa Umma au Hapana?

2. Je Zitto anayakagua haya mashirika au hapana?

3. Je katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 sura ya 6 sehemu ya 2 Na sheria ya utumishi wa Umma inamruhusu kiongozi kama yeye kuingia mkataba na mashirika ya Umma ukiachila mbali mashirika yanayoripoti chini yake?

4. Kama Gombe advisors si kampuni ya faida, kwa nini ijimilikishe hisa asilimia 25% Za Leka Dutigite? Je si ingekuwa sahihi ingebaki kuwa mshauri tu na wasanii wakagawana asilimia 100 ya kampuni ili wanapogawana faida wagawane kwa uwiano sawa kutokana na mgawanyo wa hisa zao.

5. Kwanini aweke watu wake wa karibu kuwa ndio viongozi wa Leka Dutigite kama yeye ni mdhamini tu na mshauri wa wanamuziki?

Mimi naamini hakuna ujanja ujanja unaodumu kwa muda mrefu nchi hii kabla haujagundulika, Chama Chake kimeshamjua, ipo siku hao anaowatumia kwenye ujanja ujanja wake watamgeuke na ukweli utawekwa hadharani. lakini hadi hapo yatakoapotokea hayo, bado nasubiri siku nione Zitto Kabwe akiikosoa NSSF na TANAPA kwa kuwa mpaka sasa kila akiongea mifano mema hutolea mashirika haya mawili. Mimi ndio yule yule niliyemtabiria kufukuzwa kwenye chama siku aliyochaguliwa kuwa kiongozi wa chama
 
.... ,.hadi Siku akiamua yeye mwenyewe kuja open ....unafanya kosa ..Sana lamkukemewa
Point taken at high order seriousness !. Realy I mean it, please, edit my text in 'your post with quote' by removing a paragraph with kind of name calling as I have done in my original post.
 
Huyu ni mtu ambaye CCM wanatamani awe na nafasi ya juu ya uongozi katika chama kikuu cha upinzani
images

Kuvuliwa vyeo kwa Zitto Zuberi Kabwe na Dr Kitila Mkumbo kutakuwa na visingio vingi, ukweli ni kwamba
"NDANI YA CHADEMA AKILI NDOGO INATAWALA AKILI KUBWA" It is natural kwamba akili ndogo ikitawala akili kubwa,
1) Yatatumika mabavu na nguvu nyingi kuizuia akili kubwa kupanda juu,
2) Zitatafutwa sababu nyingi na visingizio uchwara kuhalalisha kuizima akili kubwa tofauti na vigezo vya hoja kwakuwa akili ndogo haiwezi kuizidi akili kubwa kwa hoja,
3) Hutumika vitisho vingi kuzuia akili kubwa kuchukua hadhi yake
4) Akili ndogo ni rafiki wa akili ndogo mwenzake, hivyo akili ndogo huzungukwa na akili ndogo kwakuwa ushauri wa akili kubwa akili ndogo hushindwa kutumia ama kushindwa kuonesha umiliki mbele za watu. Kwenye chadema wenye akili wote wako nje ya uzio wa chemichemi ya mawazo.

Pale bungeni watu wanaoweza kufundisha na waliokuwa wakifundisha hata unaibu waziri kivuli hawapati kwakuwa wanatumia akili zaidi badala ya nguvu.

Lakini walioishia kidato cha kwanza, pili, tatu na zero ndio think tanks na ndio majembe ya chadema kwakuwa wanatumia mabavu na manguvu zaidi kuliko akili sawasawa na matakwa mahitaji ya akili ndogo inayoongoza akili kubwa.

Vijana wahitimu wa vyuo wanaopenda siasa waliandikiwa barua kuwazuia kuhutubia mkutano wowote wa hadhara sawasawa na matakwa ya akili ndogo inapotawala akili kubwa. Zito, Kitila, Christowaja, Matiko, Opulukwa, Baregu, Leticia, Selasini, Arfi, Akunay, Naste wengi wao MA holders kwa chadema ni rejects. Ukiwa mwanafamilia au ukoo au kazi au wito maalum wa viongozi ndio utakwepo kwenye list.

I know Zitto tangu tukiwa chuoni, he is a brilliant and consistent politician, namjua Dr Kitila tangu chuoni, he is resourceful. Hivi kosa walilofanya ni kubwa kuliko mchango wao waliofanya kwenye kuwajenga watanzania kuwaamini vijana kwenye siasa? Je kosa lao ni kubwa kuliko mchango wao unavyohitajika? Vijana tuko kazini na wakati huohuo tuko mafunzoni.

Sio adhabu nzuri ya kuwafukuza ama kuwaondoa kwenye fursa ya kujifunza zaidi.
Haya ndio madhara ya AKILI NDOGO KUTAWALA AKILI KUBWA, HOFU NDIO HUTAWALA


Ni sawa na kocha wa Yanga kung'ang'ania apewe jukumu la kupanga timu ya Simba kupambana na Yanga, au kocha wa Barcelona kupanga timu ya Real Madrid kwa ajili ya El Clasico.
 
Njia ya Muongo fupi tunamsubiri apande majukwaani na ACT-MWANDIGA yake aanzishe mashambulizi, atapata majibu yanayomstahili kabisa..
 
Mimi naamini hakuna ujanja ujanja unaodumu kwa muda mrefu nchi hii kabla haujagundulika,
ni kweli kabisa njia ya mwongo kama alivyo mnafiki huwa ni fupi - ni suala la muda tu. yetu subira!!
 
Niliwahi kuona thread hapa inayoeleza kuwa Kinana katika safari zake za kukiua chama chake huko mikoani alifika katika kata mojawapo wananchi bila aibu wakamtaka akanushe/au athibitishe kuwa ni lini ataacha biashara ya kuua tembo wetu kwa maslahi binafsi. Nasikia aliukimbia mkutano huo bila kujibu. Naona ZZK anajaribu kujijengea mazingira kwa wananchi ambapo siku moja watamuuliza maswali ambayo itamuwea vigumu kujibu.
 
Tunamsubiri Zitto kwa hamu apande jukwaani na ACT yake lakini awe tayari amejiandaa kisaikolojia kuleta majibu ya tuhuma zake zote za ufisadi anaohubiri kuwa anaupinga na hata fedha walizochukua na mwenzake Filikunjombe kwenye uchunguzi wa sakata la Tegeta Escrow
 
siku za zitto mbona zinahesabika ngoja aende ACT aanze kupanda majukwaaani ndo ataona
 
Zitto Kabwe ni adui yao, akina nani hao? Ni rafiki yao, hao wenye uswahiba naye wapoje? Ni kipenzi chao, wasifu wa hao wanaompenda ni upi? Andiko hili linachambua kila kipengele katika muktadha mpana.

ADUI

Kunguni ni mdudu anayechukiwa sana na binadamu. Hawezi kuwa na jema hata kidogo. Huo wema wa kunguni umeanza lini? Ni mchokozi, msumbufu, mharibu starehe ya usingizi. Sisi tuliopitia maisha ya kulala na kunguni tunaelewa. Ambao hawajapitia, heri yao!

Wasifu huo ndiyo ukaibuka msemo wa "damu ya kunguni", anayesemwa au kujisema kuwa na damu ya kunguni maana yake anachukiwa na watu. Hana jema, kila atakalofanya, litageuzwa kwa uzuri wake kisha kupewa sifa mbaya. Lengo kuu ni kwamba aonekane mbaya kila siku.

Unamsifiaje mtu mwenye damu ya kunguni mbele za watu? Kama hutachekwa, basi na wewe utachukiwa. Utawekwa kapu moja na mwenye damu ya kunguni. Almasi ya mwenye damu damu ya kunguni ni chupa, dhahabu ni shaba.
Pamoja na kazi kubwa aliyofanya, akiongoza kamati yake ya Hesabu za Serikali (PAC) kusoma, kuchambua na kutafsiri makabrasha ya ripoti ya CAG (Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali) kuhusiana na skendo ya Tegeta Escrow, na kutoa mapendekezo.

Pamoja na kuukataa usingizi, kuamua kukesha akilinda ripoti ya PAC ili kuhakikisha haichakachuliwi kwa namna yoyote ile. Pamoja na ushujaa wa kuchambua madudu katika Akaunti ya Tegeta Escrow na kuwaumbua (naming and shaming) wahusika, bado damu ya kunguni ilidhihirika kuwamo ndani ya Zitto.

Kosa lake lilikuwa kuunga mkono muundo wa pendekezo (formulation), lililotolewa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge. Lililohusu namna ya kuishauri serikali (mamlaka ya uteuzi), kuchukua hatua za kumwajibisha Katibu Mkuu aliyesimamishwa, Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi.

Kabla ya Chenge, kila pendekezo liligonga mwamba, Spika Anne Makinda, alitaka lugha laini zaidi katika kuishauri serikali. Chenge alipotoa formulation yake, ikaungwa mkono haraka sana. Spika akaona ina nafuu kubwa. Zitto na Halima Mdee waliiunga mkono, wabunge wengi wa CCM wakashangilia.

Zitto akashauri, mapendekezo yaliyobaki ambayo yaliwagonga nyundo moja kwa moja, Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Fredrick Werema, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, yaandikwe kama Chenge alivyoshauri.

Spika Makinda akaona "mambo si ndiyo hayo", akakubali, wabunge wa CCM wakagonga meza kwa fujo. Spika akawauliza wabunge, sauti ya wengi ikasikika "ndiyoooo". Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, akashtuka, akasema hapana, "mnatuburuza."

Msimamo wa Mbowe ukaibua zogo bungeni. Wabunge wa upinzani, hususan wale wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wakamuonaZitto msaliti. Inakuwaje anakubali pendekezo la Chenge?

Zitto alishakuwa na sifa ya usaliti. Kwamba anakisaliti chama chake (Chadema) na upinzani kwa jumla. Kitendo kile cha kuunga mkono pendekezo la Chenge, akatafsirika kama "mja asili asiyesahau asili yake", alionekana amerudia zake za usaliti.

Chenge pia ni walewale wa damu ya kunguni, kwa hiyo hana jema. Pendekezo litolewe na Chenge? Haikuingia akilini kabisa kwa wapinzani! Kosa kubwa ni kwamba wapinzani badala ya kutathmini na kuona ubora au ubaya wa pendekezo la Chenge, wao wakamwangalia mtoa pendekezo, Chenge!

Laiti ‘msumari' wa Zitto kwa kugandamizia pendekezo la Chenge, ungepita, leo hii Waziri Mkuu na Masele nao wangekuwa tumbo joto. Haikuwa hivyo, wapinzani walimuona Zitto anasaliti kwa sababu hawaamini katika "baniani mbaya kiatu chake dawa", kwao Chenge ni baniani ambaye kiatu chake hakiwezi kuwa dawa, asilani, abadan!

Baada ya hapo, mitandao ya kijamii ikaingia kazini, Zitto alishambuliwa kwelikweli. Wachache waliojua ubora wa pendekezo la Chenge, walitetea kuwa Zitto alikuwa mjanja sana, mwenye akili akili za kimkakati kuunga mkono pendekezo la Chenge. Wengi hawakumwelewa, walimshambulia, walimponda.

Kama alichokisema Zitto, kingetamkwa na Tundu Lissu, hali isingekuwa mbaya kwa kiasi kile. Tatizo la Zitto ana damu ya kunguni. Alivyokuwa anatenda kazi yake kwa umahiri mkubwa, wasiomwamini walikuwa wanamfuatilia kwa umakini, wakiamini lipo eneo atateleza wamseme.

Zitto ni sawa na mchezaji mzuri asiyependwa. Kama ilivyowahi kutokea kwa Ryan Giggs, Manchester United au hata hapa Tanzania Haruna Niyonzima, Yanga, na wengineo, wakishika mpira, wanacheza vizuri sana, wanafanya mambo mengi makubwa yanayostahili pongezi lakini hawashangiliwi, ila kosa moja litasababisha azomewe kila upande. Kisa hawampendi, amewaudhi! Siku hizi Niyonzima hazomewi.

Wakati wa kuelekea kusomwa kwa ripoti ya PAC kuhusiana na Tegeta Escrow, pamoja na kuwepo kwa watu kumuunga mkono Zitto na kumtia moyo kwamba asiogope, wapo nyuma yake, wapo waliotamka bila kificho: "Zitto ni msaliti, muda utakapofika atapindisha ukweli ili kuwaokoa wachotaji wa fedha za Tegeta Escrow."

Kwao, Zitto na waliochota fedha za Escrow ni walewale. Kwa maana hiyo walitoa angalizo huku wakimfuatilia kwa makini mithili ya macho ya mashabiki kwa mchezaji mzuri wasiyempenda anapokuwa anachanja mbuga na kupiga chenga za maudhi uwanjani, wakisubiri akosee wamzoemee. Alipounga mkono tu pendekezo la Chenge, wakazomea, wakasema "si tulisema!"

Hata baadaye, ipo hoja iliibuka kwamba katika Tegeta Escrow, Zitto alitumiwa na makundi ya CCM kwa ajili ya mnyukano wa mbio za Urais 2015. Wapo waliosema ‘alishikishwa' kiasi kikubwa cha fedha na mzee Reginald Mengi ili kumwadabisha Muhongo kwa sababu wana bifu la vitalu vya gesi.

Hayo ni matokeo ya kuwa na damu ya kunguni, ufanya jema litageuzwa kuwa baya na ukitenda baya ndiyo kabisa. Katika mazingira kama hayo, wengi hujikuta wanayumba. Japo anajitahidi kubaki kwenye mstari, mara nyingi Zitto ameshayumbishwa na mashambulizi mpaka kujikuta anajibishana na wanaomchokonoa, au kutamka yasiyopendeza.

Zitto ni adui wa CCM, kwa maana ni mbunge mnoko. Kazi yake imeshaivua nguo serikali ya CCM mara kadhaa. Ni kiherehere, kwa sababu anafuatilia sana. Na akishafuatilia hana siri, haraka sana yataonekana mitandaoni, Twitter, Facebook na kadhalika kabla ya kufika bungeni.

Unoko wa Zitto unaosababisha asipendwe na CCM pamoja na serikali; Palipo na wizi au kashfa yoyote ile, lazima kivuli chake kitaonekana na atasema kuhusu skendo husika. Hali hiyo imesababisha aingie kwenye misukosuko mingi. Muwinda huwindwa!

Mwaka juzi, katika Bunge la Bajeti, kuelekea bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, Bodi ya Tanesco ilimsimamisha kazi, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu, William Mhando. Baada ya uamuzi huo, ikaibuka kashfa kuwa bodi ilifanya makosa ya kukiuka sheria ya manunuzi katika kununua mafuta ghafi.

Ikabainika kuwa pamoja na makosa ambayo Mhando anatajwa kuwa nayo, yapo maelezo kuwa tofauti yake na bodi, ilisababishwa na yeye kupinga ukiukwaji wa makusudi wa sheria ya manunuzi. Kwamba mshindi wa zabuni ananyimwa halafu anapewa aliyeshindwa.

Zabuni imetangazwa, makampuni kadhaa yamejitokeza kuwania tenda. Kila moja inatangaza ofa yake, baadaye baada ya kupima vigezo kampuni moja ikashinda. Ajabu iliyopewa tenda ikawa kampuni tofauti na ile iliyoshindaa. Hiyo ni kashfa, na kulikuwa na sura ya wazi kwamba rushwa ilichukua nafasi.

Zitto akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) wakati huo, akamwandikia barua Spika Makinda, kuomba kamati yake iruhusiwe na bunge kuhoji pande zote mbili, Mhando na bodi ya Tanesco.

Haraka sana picha likageuka; Ikaelezwa kuwa Zitto alihongwa na makampuni ya mafuta kwa ajili ya kumtetea Mhando. Hali ilikuwa mbaya sana mpaka akaita mkutano na waandishi wa habari kujitetea lakini haikusaidia. Ilisababisha mpaka baadhi ya wabunge kuomba uongozi wa POAC uondolewe.

Spika Makinda alipoiagiza Kamati ya Ngwilizi (Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi) kufanya uchunguzi, ikabainika Maswi na Muhongo, walisema uongo kwa lengo la kushawishi bajeti yao ipite na kuwadhibiti waliokuwa wakiipinga kwa kupitia kashfa ya ununuzi wa mauta ghafi.

Kipindi hicho, Zitto alitoka kwenye mstari, alimtumia SMS Maswi akamwambia: "Maswi sijawahi kugombana na wewe kwa kuwa nakuheshimu sana. Tuhuma ambazo wewe na waziri wako mnazitoa dhidi yangu ni uongo, uzushi na za kupikwa.

"Mwambie waziri wako na wewe binafsi, sijawahi kushindwa vita ya kulinda credibility yangu, sipendi ujinga hata kidogo, mimi nina uhuru wa kusema ninachokiamini, sina bei, tupambane tu tuone nani ataumia."

Maswi na Muhongo walionywa na bunge wakati huo, ila baada ya matokeo ya sasa katika skendo ya Tegeta Escrow, tayari Maswi ameshasimamishwa kazi, Muhongo anaendelea kuvutiwa ‘uradi kwa tasbihi'. Swali nani ameumia? Majibu yapo wazi.

Siri moja, ukiwa mtu halisi hutafeli hata mara moja. Vita ya Maswi na Muhongo upande mmoja na Zitto upande wa pili, inanipa majibu kuwa mkweli ameendelea kuwa imara pamoja na misukosuko yote. Mzushi, pigo moja tu, leo yupo chali. Kwa hapa Zitto ni halisi zaidi.

Zitto akaichachafya serikali ya CCM; Alimtaja Waziri wa Fedha wakati huo, Mustafa Mkullo kwamba ni fisadi, kisha akalinyooshea kidole Baraza la Mawaziri kwamba lilihongwa ili kulifuta Shirika Hodhi la Rasilimali za Mashrika ya Umma (CHC) kwa sababu za kifisadi.

Mawaziri wakawa wakali, wakamtaka Zitto athibitishe, yeye aliwasilisha uthibitisho wake na kuanzia hapo ikawa kimya. Mawaziri walinywea! Haihitaji kutumia darubini kujua kuwa Zitto ni adui wa Baraza la Mawaziri kwa sababu alisema lilihongwa. Mawaziri hawawezi kumpenda. Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri ni Rais, kwa maana hiyo JK hawezi kumfurahia.

Mkullo alisema Zitto anatumika na kwamba anahongwa. Zitto akatoa uwanja huru, kila mmoja aruhusu kuchunguzwa ikibainika yeye (Zitto) amewahi kuhongwa, atajiuzulu uenyekiti wa POAC, ubunge na ataacha siasa.

Akamtaka Mkullo kutangaza kuwa tayari kuuacha uwaziri endapo itathibitika amehusika na ufisadi akiwa Waziri wa Fedha. Mkullo alinywea lakini ripoti ya CAG ya mwaka 2012, ilimng'oa Mkullo pamoja na mawaziri wengine saba.

Kabla ya kung'oka, mawaziri walikuwa wabishi, Zitto akaanzisha mchakato wa kukusanya saini 70 ili zihalalishe hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu. Mambo kabla hayajawa mabaya sana, Mkuu wa Nchi aliwaondosha mawaziri wote waliokumbwa na kashfa. Je, huyo si adui wa serikali ya CCM?

Ni Zitto aliyetimuliwa bungeni mwaka 2007 kwa sababu ya kupeleka bungeni hoja ya Buzwagi, akimtaja aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, kusaini mkataba kimagumashi, kinyume hata na agizo la Rais, aliyetaka isisainiwe mikataba mipya ya madini mpaka kwanza ile ya awali ipitiwe upya.

Zitto akaonekana mbeya, kizabizabina, aliyekusudia kuivua nguo serikali na kumharibia ulaji Karamagi, akasimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge. Hii ni kuthibitisha kuwa Zitto ni adui wa CCM na ubunge wake umekuwa mwiba kwa maovu ndani ya Serikali ya CCM.

Mwaka 2008, baada ya hotuba ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, alipotangaza kujiuzulu, Zitto aliomba muongozo kwamba kwa mujibu wa Katiba, Waziri Mkuu anapojiuzulu na Baraza la Mawaziri linavunjika, kwa maana hiyo mawaziri wote hawana kazi. Mawaziri walimzomea, walimuona mnoko, anayechonga sana. Walipinga! Hawakujua wanapinga Katiba.

Ni Zitto ambaye alishawekewa sumu kwenye maziwa, akaokolewa na simu ya marehemu Amina Chifupa, aliyemwambia asiendelee kunywa, ni sumu. Akatibiwa Hospitali ya Rufaa, Bugando, Mwanza. Ni Zitto aliyenusurika kifo kwa ajali kadhaa, ikiwemo zilizotajwa kusukwa!

Ni adui wa wapinzani, maana anaonekana ni msaliti, anayetumiwa na CCM kudhoofsha upinzani nchini. Zilishatolewa ripoti kadhaa (japo hazikuwahi kuthibitishwa), zikionesha namna Zitto alivyo na ukaribu na Usalama wa Taifa pamoja na Serikali.

Taarifa kwamba Zitto ni msaliti wa upinzani, zilianza tangu mwaka 2008. Maneno hayo yameendelea kuchukua nafasi mpaka leo. Sura hiyo imemfanya Zitto kuonekana kibaraka, mamluki wa CCM. Wasambazaji wa maneno haya walifaulu, ila hawakuweza kummaliza.

Hiyo ndiyo sababu ya Zitto anapokuwa kwenye wakati muhimu zaidi kushughulikia mambo nyeti kwa taifa, badala ya kuungwa mkono kwa asilimia 100, wapinzani wanakuwa wanamtolea macho, wakivizia akosee wamzomee!
Uthubutu wake wa kutaka vyama vyote vya siasa vinavyopata ruzuku serikalini vikaguliwe na kusisitiza kwamba havijakaguliwa, uliongeza kasi ya kuonekana msaliti wa upinzani na kwa chama chake (Chadema). Akawa adui mkubwa wa wapinzani. CCM nayo ikazidi kumuona mnoko, adui, ukaguzi-ukaguzi nini?

RAFIKI

Zitto ni rafiki wanamageuzi, wanaoamini
katika fikra huru za kisiasa. Wanaopenda siasa za mawazo huria pasipo kubanwa na vyama. Hii ndiyo sababu wale wanaoonekana vimbelembele, kuongeaongea, kuzozazoza bila kukistahi chama chao cha CCM, kama Deo Filikunjombe, Kangi Lugora na wengineo, ni marafiki hasa wa Zitto.

Anne Kilango Malecela (CCM), aliwahi kuniambia kuwa anampenda na kumwamini sana Zitto kwa sababu ni mwanasiasa mwelewa asiye na katikati. Kilango: "Kama Zitto anaona kitu hakipo sawa, atasimamia hivyo mpaka mwisho."
January Makamba aliwahi kumzungumzia Zitto: "Ni mwanasiasa ambaye sitapata shida kufanya naye kazi kwa sababu anapenda ushirikiano. Anapokuwa na hoja yake, huzungumza na wabunge wa vyama vyote bila kubagua, ndiyo maana mara nyingi hoja zake huungwa mkono na wengi."

Kwa wanamageuzi, Zitto amekuwa kielelezo cha uswahiba naye kutokana na kumbukumbu ya alichokifanya katika skendo ya Buzwagi, saini za kumng'oa Waziri Mkuu, Tegeta Escrow na kadhalika.

Ni hao ambao wamekuwa wakijiuliza, kama Zitto ni mamluki, mbona ni yeye ambaye amekuwa mstari wa mbele kuanzisha hoja nzito za kuitikisa Serikali? Hata katika Tegeta Escrow, naye alitajwa kupokea mgawo, swali: Ni mtu gani anayeweza kula rushwa halafu akamuumbua aliyempa?

KIPENZI

Zitto ni kipenzi cha wasanii hasa wanamuziki wa kizazi kipya. Ndiye mwanasiasa ambaye jina lake linasikika kwenye nyimbo nyingi, kuliko mwingine yeyote. Vilevile watoto wa shule na vijana vyuoni, wanampenda na kumchukulia kama kioo cha maisha yao yajayo, kwa wale wanaoota kuwa wanasiasa.

Mpango wake wa kupigania haki za wasanii na kufanikisha kuzifanya kazi za sanaa kuwa biashara rasmi inayotambulika serikalini, iliongeza chachu kwa wasanii kumpenda, ingawa hata kabla, alikuwa kipenzi chao.

Haiba yake, ndiyo sababu ya wanamuziki Bwana Misosi, Ben Pol, Jay More, Roma, Kala Jeremiah na wengine wengi kumuimba katika nyimbo zao.

Mradi aliouanzisha wa Kigoma All Stars "Leka Dutigite", kusaidia wanamuziki wa Mkoa wa Kigoma kujiunda pamoja kama kampuni na wote kuunganishwa kwenye Shirika la Hifadhi ya Jamii la NSSF, hivyo kuwezesha kupata bima ya afya, ni pointi nyingine iliyofanya wasanii wampende zaidi.

Ukiwa bungeni, utajionea jinsi watoto wanavyompenda Zitto. Wanapokwenda bungeni kwa ajili ya ziara ya kujifunza (study tour), wanapomuona Zitto huchanganyikiwa. Humkumbilia, kumkumbatia na kupiga naye picha. Wanampenda! Ni kipenzi chao!

By Luqman Maloto
Ama kweli uandishi ni kazi ya watu... Hii habari isingeweza andikwa na mtu asokuwa na kipaji na utaalam wa uandishi na sijui kilitokea nini hata watu wasione umuhimu wa yale mafiga matatu - Ubarikiwe!
 
siku za zitto mbona zinahesabika ngoja aende ACT aanze kupanda majukwaaani ndo ataona
Sijawaeleweni mimi, bado mnamtaka Zitto au hampendi kuona akienda ACT? Binafsi nisichoweza kuamini ni kile kinachosemwa kwamba ZITTO siyo mchafu, hili nakataa, haya mengine ya kupanda majukwaani siwezi kumhukumu.
 
Sijawaeleweni mimi, bado mnamtaka Zitto au hampendi kuona akienda ACT? Binafsi nisichoweza kuamini ni kile kinachosemwa kwamba ZITTO siyo mchafu, hili nakataa, haya mengine ya kupanda majukwaani siwezi kumhukumu.

Mkuu Kama umekiri zitto ni mchafu well done mkuu
 
Davesto kuwa na ubinaadamu. Hakuna msiba ulio na mwisho. tumuacheni mama apumzike jamani.
 
Last edited by a moderator:
Habari ya mjini mpini wa Escrow umewaingia CCM pabaya wakakaa nchale...wakinuka nchale....wakisimama nchale ,scandal ya ufisadi inafanana na GOLDENBERG iliyoing'oa serikali ya KANU ya Kenya twende kazi ....moja wa ma actor ni Harbinder Singth Seth yule yule international mwenye mafunzo makali ya kuiangusha serikali bila kuigusa
 
Back
Top Bottom