Zitto Kabwe: Adui, Rafiki, Kipenzi

Zitto Kabwe: Adui, Rafiki, Kipenzi

kwa asilimia kubwa ya vijana kujiunga n chadema kivutio alikua ni Zzk hapo hamna ubishi zzk alikua na nguvu ndani ya chama kuanzia ngazi za chini tofauti na m/kiti hiii inafahamika na ndio chanzo cha zzk kutazamwa ka anaenda kuchukua kiti cha chama basi akaundiwa zengwe baada ya vikao vya vifaranga fyatu kutumiwa na chairperson na jamaa wakaanza kupiga kelele mara zzk anataka kukagua hesabu za chama bila kutupa tarifa mara anatumiwa na ccm wenye akili zetu tulijua hiyo ni team ya kampen iliyokuj kwa tyming juu ya m/kiti mtarajiwa na ni hapohapo baada ya zzk kusimamishwa uanachama ndio kukafanyika uchaguzi wa kiti taifa na mbowe alipita ka anaokota ila kaa utafakari kama zzk angkuwapo apambane na mbowe lazima kamasi zingewatoka na ndio maana watu wanaamini kama cdm imekaa kiukanda na hii inatokana na mwasisi wa cdm kumwita zzk na kumzuia asigombee uenyekiti kwa madai bado mda wake. Hivi inaingia akilini kama demokrasia ipo ndani ya cdm chama changu wasimwache zzk asimame na wapiga kura wamwadhibu kwa kura? Ok ngoja nikubaliane na wahenga kua mti mwema ndio unapigwa mawe tumeona matunda yako ndani na nje ya cdm kaka zzk! Pole na misukosuko ya maisha ya kisisasa na ya kifamilia pia pole kwa kuondokewa na mama yetu bi Shida na nitumie nafasi hii kukupa moyo kwamba tupo pamoja na wewe ndani na nje ya cdm una pipo wengi wanaokuaminia

All the best in 2015
 
zitto ni kama Enzi za mrema wengi tuliingia mkenge .kiongozi wa upinzani lazima ujipambanue pasipo shaka kuwa wewe hauna bei lakini kwa tuhuma izi nani atakuhamini kwa mfano mdogo amechukua ela za iptl kupitia kwa mdogo wake utamwanimi vipi mtu wa ivyo zitto lazima akitaka haaminike asiwe kama popo mara mnyama mara ndege sisi wakristo yesu anasema lazima uchague moja kuwa baridi au moto sio vuguvugu maana waliovuguvu anasema nitawa tapika.zitto ni vuguvugu.hakuna mpinzani wa haina yake ndo maana yeye na ccm wanawekeana po.
Aamniniwe na nani wakati nyinyi mlishaaminishwa kwamba yye ni msaliti tatizo akiwaambia mlete uthtibitisho wa usaliti wake mnabaki kimya name mane no yenu ya mitaani yasio na maana zitto ni mwanasiasa makini anaejua nni anacho kifanya nasio hao viongozi wenu wa maandamano na matusi usifikiri wanachadema wote wana akili kama cdm wa arusha
 
.

Nilikuwa nafuatilia thread ii lakini nilipo fika kwako, nikaona nitoe hojakidogo kisha niemndelee tena mwishoni baada ya kupia yote na kutoa hoja ya jumla. ZITO AGOMBEE 2015 na sio 2025.
Nakubaliana na wewe. Kuelekea 2015 anatakiwa aanze kugombea 2015.
 
Habari za weekend wana bodi,

natumai mu wazima ninyi nyooote kwa ujumla,bila kupoteza muda naomba nianze kuchambua kila kipengele hapojuu ktk mUktadha mpana.!!!!!!KAMA NI MVIVU WA KUSOMA IPOTEZEE MAPEMAAAAAAA!!!!!!!
ZITTO NI ADUI;

Inafahamika kuwa kunguni ni mdudu mdogosana anaechukiwa sana binadamu'hawezi kuwa na jema hata kidogo'huo wema wa kunguni umeanza lini?nimchokozi,msumbufu,muharibu starehe za watu.Sisi tuliopitia maisha ya kulala n kunguni tunamwelewa,ambao hawajapitia heri yao.wasifu huo ndio ukaibua neno "Damu ya kunguni"
Anaesemwa au kujisema kuwa na damu ya kunguni maana yake anachukiwa na watu,hana jema,kila analofanya litageuzwa kwa uzuri wake nakupewa sifa mbaya.Lengo kuu ni kwamba aonekane mbaya kila sik.

Pamoja na kazi kubwa alioifanya yakuiongoza kamati yake ya PAC kusoma,kuchambua na kutafsiri makabrasha ya ripoti ya CAG kuhusiana na skendo ya Tegeta Escrow nakutoa mapendekezo.Pamoja na kuukataa usingizi nakuamua kukesha akiinda ripoti ya PAC ili kuhakiksha haichakachuliwi kwanamna yoyote.Pamoja na ushujaa wa kuchambua madudu ktk account ya Tegeta Escrow nakuwaumbua wahusika bado damu ya kunguni ilidhihirika kuwa ndani ya ZITTO.

Kosalake lilikuwani kuunga mkono muundo wa pendekezo lililotolewa na Andrew Chenge lililohusu namna ya kuishauri serikali kuchukua hatua ya kumwajibishakatibu mkuu aliesimamishwa wizara ya nishati na Madini Bwana Eliakim Maswi.
Kabla ya Chenge kila pendekezo liligonga Mwamba,spika Makinda alitaka Lugha laini zaidi ktk kuishauri serikali.Chenge alipotoa Furmulation yake ikaungwa mkono kwaharaka sana, spika akaona inanafuu kubwa.
ZITTO AKAIUNGA MKONO,wabunge wengi wakashangilia.ZITTO akashauri mapendekezo yaliobaki ambayo yaliwagonga nyundo moja kwa moja Waziri mkuu Mizengo Pinda,aliyekuwa Mwansheira Mkuu Fredrick Werema na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Prf Sospeter Muhongo,yaandikwe kama chenge alivyoshauri.Spika Makinda akaona mambo si ndo hayo!akakubali,wabunge wa ccm wakagonga meza kwa furaha,Spika akawauliza wabunge na saui ya wengi ikajibu "Ndiooo!"Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Mh Freeman Mbowe akashtuka akasema "hapana mnatuburuza",msemo wa Mbowe ukaibua zogo bungeni.
wabunge wa upinzani haswa wale wanaounda UKAWA wakamuona Zitto msaliti.Inakuwaje anakubali pendekezo la chenge?Zitto alishakuwa na sifa ya usaliti kwamba anakisaliti chama chake[chadema}na upinzani kwa ujumla.
kitendo kile chakuunga mkono pendekezo la Chenge akatafsirika kama Mja asili aliyesahau asili yake.Alionekana kuwa amerudia zake za usaliti.

Kosa kubwa ni kwamba badala ya wapinza kutathmini na kuona ubaya au ubora wa pendekezo la chenge wao wakaangalia mtoa pendekezo "Chenge".
LAITI MSUMARI Wa ZITTO kwakugandamiza pendekezo la chenge ungepite,leo waziri mkuu na masele wangekuwa tumbo joto.
Wapinzani walimuona Zitto anasaliti kwasababu hawaamini katika Baniani mbaya kiatu chake dawa'kwao Ziito ni baniani mbaya ambae kiatu chake hakiwezi kuwa dawa asilani abadani.
Baada ya hapo mitandao ya kijamii ikaingia kazini,Zitto alishambuliwa kwelkweli,wachache waliojua ubora wa pendekezo la Zitto walitetea kuwa Zitto alikuwa mjanja sana,mwenye akili,akili za kimikakati kuunga mkono pendekezo la chenge.wenyewe hawakumwele walishambulia,walimponda.
Nidhahiri alichokokisema Zitto kingesemwa na TL hali isingekuwa mbaya kiasi kile.Tatizo la zitto nikwa na damu ya kunguni.

alipokuwa antenda kazi yake kwa umahiri mkubwa,walikuwa wakimfuatilia kwa umakin mkubwa wakiamini lipo eneo atateleza tu ili wamseme.
Zitto ni sawa na mchezaji mzuri asiependwa na watu kama ilivyowahi kutokea kwa mchezaji wa MAN u,Ryan Giggs au kwa hapa Tz ni kwa Niyonzima wa YANGA, wakishka mpira wanacheza vizuri sana,wanafanya mambo mengi mazuri yanayostahili pongezi,lakini hawashangiliwi lakin kosa moja litasababisha wazomewe kila upande kisa hawampendi amewaudhi.

WakTI wa kuelekea kusomwa kwa ripoti ya pac KUHUSIANA NA tEGETA eSCROW,pamoja na kuwepo kwa watu waliomuunga mkono ZITTO na kumtia moyo asiogope wapo nyuuma yake,wapo waliotamka bila kificho'Zitto ni msaliti" muda utakapofika atapindisha ukweliili kuwaokoa waliochota pesa za Escrow.
kwao Zitto na waliochota pesa za Escrow niwalewale.Kwahiyo walitoa angalizo huku wakimfuatilia kwa umakinimithili ya mashabiki kwa mchezaji mzuri wasiempenda anapokuwa anachanja mbuga na kupiga chenga za maudhi wakisubiri akosee ili wamzomee.Alipounga mkono tu pendekezo la chenge wakamzomea huku wakisema"Tulisema'

hata baadae iliibuka hoja kuwa ktk Tegeta Escrow Zitto alitumiwa na makundi ya CCM kwaajili ya mnyukano wa mbio za uraisi 2015.
Wapo waliosema kwamba alishikishwa kiasi kikubwa cha fedha na Mengi ili kumwadabisha Muhongo kwasababu wana BIFU la vitalu vya gesi.Hayo ni matokeo ya kuwa na damu ya kunguni,ukifanya jema linageuzwa kuwa baya na ukifanya baya nio kabisaa!ktk mazingira kama hayo wengi hujikuta wanayumba,japo Zitto anajitahidi kubaki kwenye mstari but mara nyingine ameshayumbishwa na mashambulizi mpaka anajikuta anajibishana na wanaomchokonoa au kutamka yasiopendeza.

Zitto ni adui wa ccm kwamaana ni mbunge mnoko,kazi yake imeshaivua nguo serikali ya ccm mara nyingi,nikihereher kwasababu huwa anafutatilia san na akishafuatilia huwa hana siri,haraka sana utayaona ktk mitandao ya kijamii fb,twitter nk kabla yakufika bungeni.unoko wa Zitto unasababishwa asipendwe na serika ya ccm kwasababu palipo na kashfa au wizi wowowte lazima kivuli chske kionekane na atasema tu kuhusu skendo husika.hali hiyo imesababisha aingie kwenye misukosuko miiingii"muwinda huwindwa".

Mwaka 2012 ktk bunge la bajeti kuelekea bajeti ya wizara ya nishati na madini bodi ya Tanesco ilimsimamisha kazi aliekuwa mkurugenzi mkuu WILLIU MHANDO,baada ya uamuzi huo ikaibuka kashfa kuwa bodi ilifanya makosa ya kukiuka sheria ya manunuziktk kununua mafuta ghali,ikabainika kuwa pamoja na makoa ambayo mhando alibainika kuwa nayo,yapo maelezo kuwa tofauti yake na bod ilisababishwa na yeye kupinga ukiukwaji wa makusudi wa sheria ya manunuzi kwamba mshindi wa zabuni ananyimwa na kupewa alieshindwa.Hiyo ni kashfa na kulikuwa na sura ya wazi kuwa RUSHWA ilitumika.

Zitto akiwa nimwenyekiti wa kamati ya hesabu za mashirika ya umma{POAC}wakati huo, akamwandikia barua spika Makina akimwomba kamati yake iruhusiwe na bunge ichunguze pande zote mbili yaani mhando na bodi ya Tanesco haraka san.
picha likageuka haraka sana ikaelezwa kuwa Zitto alihongwa na makampuni ya mafuta ili amtetee mhando,hali ilikuwa mbaya sana mpaka akaitisha mkutano na waandishi wa habari ili kujitetea lakin haikusaidia chochote,ikasababisha mpaka baadhi ya wabunge kuomba u0ngozi wa POAC uondolewa.

Spika Makinda alipoagiza kamati ya Ngwilizi ifanye uchunguzi ikabainika kuwa MASWI NA MUHONGO walisema uongo kwa lengo la kushawishi bajeti yao ipite na kuwadhibiti waliokuwa wakiipinga kwakupitia kashfa ya ununuzi wa mafuta ghali.
Kipindi hicho ZITTO alitoka kwenye mstari,alimtumia sms Maswi nakumwambia"Maswi sijawahi kugombana nawewe kwasababu nakuheshim sana,tuhuma ambazo wewe na waziri wako mnazitoa dhidi yangu ni uongo,uzushi na zakupikwa.Mwambie waziri wako nawewe,binfsi sijawahi kushindwa vita yakulinda credibility yabngu,sipendi ujinga hata kidogo"!!mimi nina uhuru wakusema ninachokiamini,sina bei,tupambane tu tuone nani ataumia""Maswi na Muhongo walionywa na bunge wakati huo,ila baada ya matokeo ya sasa ya skendo ya Tegeta Escrow tayari MUHONGO NA MASWI wapo nje ya wizara.Majibu yapo wazi!!

Siri moja,ukiwa mtu halisi kamwe huwezi feli hata siku moja,vita ya Maswi na Muhongo upande mmoja na Zitto upande wapili inanipa majibu kuwa mkweli ameendelea kuwa imara pamoja na misukosuko yoote.Wazushi pigo moja tu chaalii!!kwa hapa Zitto ni halisi zaidi.

ZITTO akaichachafya serika li ya CCM,,alimtaja waziri wa fedha wakati huo Mustapha Mkulo kwamba ni fisadi,kisha akalinyooshea kidole baraza la mawaziri kuwa lilihongwa ili kulifuta shirika hodhi la la rasilimali za mashirika ya umma{CHC]KWASABABU ZA KIFISADI.
Mawaziri wakaa wakali wakamtaka Zitto athibitishe,yeye aliwasilisha uthibitisho wake na kuanzia hapo ikawa kiiimyaaa!!Mawaziri walinywea.

haihitaji kujua kwamba ZITTO ni ADUI wa baraza la mawaziri kwasababu alisema baraza lilihongwa hivyo mawaziri hawawezi kumpenda.mwenyekiti wa baraza la mawaziri ni raisi,kwamaana hiyo JK hawezi kumfurahia .
Mkulo alisema Zitto anatumiwa na anahongwa,ZITTO akatoa uwanja huru,kila mmoja aruhusu kuchunguzwa na ikibainika yeye atabainika amehongwa basi atajiuzuru uenyekiti POAC,ubunge na ataacha SIASA.
Akatamka kuwaMkulo kutangaza kuwa tayari kuuacha uwaziri endapo itabainika amehusika na ufisadi akiwa waziri wa fedha,mkulo alinywea lakini ripoti ya CAG ya mwaka2012 pamoja na mawaziri wengine saba.

kabla ya kung'oka mawaziri wengine walikuwa wabishi.ZITTOalianzisha mchakato wa kukusanya saini 70 za wabunge ili zihalalishe hoja yakutokuwa na imani na waziri mkuu.
mambo kabla hayajakuwa mabaya sana mkuu wa nchi aliwaondoa mawaziri woote waliokumbwa na kashfa ile.J huyo si adui wa serikali ya CCM?

NI ZTTO aliyetimuliwa bungeni mwaka 2007 kwasababu yakupeleka bungeni hoja ya BUZWAGI akimtaja aliyekuwa waziri wa Nishati na Madini Nazir Karamagi kusaini mkataba kimagumashi kinyume hata na agizo la raisi aliyetaka isisainiwe mikataba mipya ya madini mpaka ile ya awali ipitiwe upya.
ZITTO akaoneka mbeya,kizabizabina alietaka kuivua nguo serikali na kumharibia ulaji Karamagi akasimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge.
Hii inadhirisha kuwa ZITTO ni ADUI wa CCM,na ubunge wake umekuwa mwiba kwa maovu ndani ya serikali ya CCM.
Mwaka 2008 baada ya hotuba ya aliyekuwa waziri mkuu EL alipotangaza kujiuzuru ZITTO aliomba muongozo kwamba kwa mujibu wa katiba,waziri mkuu anapojiuzuru na baraza la mawaziri linavunjika,kwamaana hiyo mawaziri woote hawana kazi.
Mawziri walimzomea,walimuona mnoko,aliechonga sana.

Ni ZITTO alishawekewa sumu kwenye maziwa,akaokolewa na simu ya maehemu AMINA CHIFUPA akimwambia asiendelee kunywa ni sumu.Akatibiwa hospitali ya rufaa BUGANDO.
Ni ZITTO ndie alienusurika kifo ktk ajali kadhaazilizotajwa kusukwa.

ni adui wa wapinzani maana anaonekana ni msaliti anaetumiwa na CCM kudhoofisha upinzani nchini.Zilishtolewa ripoti kadhaa[japo hazikuthubitishwa]zikionyesha namna ZITTO alivyo na ukaribu na usalama wa Taifa pamoja na serikal.

Taarifa kwamba zitto ni msaliti wa wapinzani zilianza rasmi tangu mwaka 2008,maneno hayo yameendelea kuchukua nafasi mpaka leo,sura hiyo imemfanya ZIITO aonekane kibaraka na mamluki wa CCM.
Wasambazaji wa maneno hayo walifaulu lakini walishindwa na bado wanashindwa kummaliza.

Hayo ndio majaribu au Mitihani anayoipata ZITTO anapokuwa kwenye wakati muhimu wa kushughulikia mambo nyeti kwa yenye maslahi kwa taifaBadala kuungwa mkono kwa asilimia 100,wapinzani wanakuwa wanamtolea macho huku wakisubiri akosee wamzomee.Uthubutu wa kutaka vyama vyote vya siasa vinavyopata ruzuku toka serikalini vikaguliwe na kusisitiza kwamba havijakaguliwa,uliongeza kasi ya kuonekana msaliti wa upinzani na kwa chama chake[CHADEMA].Akiwa adui wa upinzani CCM nao ikazidi kumuona mnoko,UKAGUZIUKAGUZI WANINI?

RAFIKI;

ZITTO ni rafiki wa wanamageuzi wanaoamini ktk fikra huru za kisiasa.Wanaopenda siasa za mawazo huria pasipo kubanwa na vyama.hii ndio sababu wale wanaoonekana vimbelembele,wanoongeaongea,kuzoazoa bila kukistahi chama cha CCM kam DEO FILIKUNJOMBE,KANGI LUGORA na wengineo ndio marafiki hsawaa wa Zitto.
ANNE KILANGO MALECELA[CCM],niliwahi kumsikia kuwa anampenda na kumwamini sana ZITTO KABWE kwasababu ni mwanasias mwelewa asiye na katikati.Kilango"ZITTO akiona kitu hakipo sawa atasimama kidete mpaka mwish.

Kwa wanamageuzi,ZITTO amekuwa kielelezo cha uswahiba nao kutokana kumbukumbu ya alichokifanya BUZWAGI,SAINI YA KUMG'OA WAZIRI MKUU,TEGETA ESCROW N.K.Ni hao tu ambao wamekuwa wakijuliza kuwa ZITTO NI mamluki au ?Mbona ni yeye ambae amekuwa mstari wa mbele ktk kuibua hoja nzito za kuitikisa serikali?Hata ktk Tegeta Escrow nae amekuwa akitajwa kupokea mgao.SWALI,Nimtu gani anaeweza kula rushwa halafu akamuumbua aliempa?

KIPENZI;
ZITTO ni kipenzi cha wananchi wenye hali za kawaida na wasanii wa muziki wa bongo fleva,ni mwanasias ambae jina lake linasikika ktk nyimbo nyingi kuliko mwingine yeyote!vilevile watoto na vijana vyuoni wanampenda na kumchukulia kioo cha maisha yao yajayo kwa wale wenye ndoto za kuwa wanasiasa.
Mpango wake wa kupigania haki za wasanii kufanikisha kuzifanya kazi za sanaa kuewa biashara rasmi inayotambulika serikalini iliongeza chachu ya wasanii kumpenda ingawa hata kabla alkuwa kipenzi chao.

ZITTO KABWE ni mwanasiasa anaeongoza kwa kuwa na followers wengi ktk mtanda wa TWETTER nchin kuliko mtu yeyote baada ya raisi JK KUJITOA. NI HAYO TU KWA LEO.
 
Umecopy na kupaste
 
Haya ya Ngeleja ymenifanya niikumbuke post hii kweli Zitto Kabwe adui je kama adui, adui wa akina nani? Kama rafiki, je rafiki wa akina nani?
 
Ni Kijana wa Makamo mwenye jina kubwa katika medani za siasa nchini Tanzania, ni Kiongozi mwenye misimamo thabiti na ya kipekee, mwenye maamuzi makini yenye kushirikisha akili ipasavyo, ni msomi na mtaalamu wa uchumi, ni mtu ambaye hakati tamaa lakini pia ni mmoja katika watu ambao hawana hofu na hawaogopi..,hizo ni baadhi ya sifa zinazoambatana na Jina Ruyangwa Zubeir.

Binafsi nilikutana nae nikiwa nimemaliza kidato cha sita na naelekea kujiunga na Chuo Kikuu cha Mlimani - Dar es salaam. I didn't find him, he finds me.,kuanzia hapo akawa ni Kaka, Mshauri na Mwalimu wa siasa kwangu, tukashirikiana na kusaidiana katika kila lililohusu siasa na yaliyohusu maisha yetu nje ya siasa.

Siku moja alisafiri kuelekea Malaysia, akiwa huko akanipigia simu, akinieleza kuwa amepatwa na HOFU. Nikataka kuhoji juu ya hofu yake, akaniambia atazungumza na mimi akisharudi, kwa maneno yake alisema "Si vyema nikaielezea HOFU yangu kwa njia ya simu, tutazungumza" Nilimuelewa lakini nikabaki na sintofahamu na shauku ya kutaka kujua nini kilimfika Kaka yangu huyo kipenzi.

Aliporejea nchini, akafanya kama alivyoahidi, akaniita kuzungumza, ilikuwa ni Nyumbani kwa Kaka yake Zitto maeneo ya ADA estate Kinondoni, ndipo alipoizungumza hofu yake ambayo imekuwa ikimsumbua katika moyo na nafsi yake. Akanieleza "ndugu yangu, nimetumia nguvu kubwa ya kila namna katika kuijenga CHADEMA, nguvu na maarifa niliyowekeza ndani ya CHADEMA yanalenga kuboresha maisha ya watanzania na maisha yangu, lengo langu likiwa kuleta ukombozi wa kweli kwa watanzania, kuifanya CHADEMA kuwa mbadala wa CCM na kuipa nguvu CDM ili kuhakikisha inaikomboa Jamii iliyozama katika dimbwi la umasikini ya watanzania.."

Alipofika hapo, akaniangalia usoni na akatambua kuwa bado nilikuwa katika sintofahamu ya yale anayoyasema, akaendelea "Tumefanikiwa kuwafanya watanzania waiamini Chadema, lakini HOFU yangu ni kuwa hatujaiimarisha wala kuiandaa ipasavyo CDM kuwaongoza watanzania, bado katika chama chetu tunalo tatizo la Uongozi..,I HAVE A FEAR OF BEING RULED BY A LESSER"

Alipomaliza maongezi yake nikawa nimemuelewa nadhani kuliko mtu mwingine yeyote kwa wakati huo, na nikawa tayari kuungana nae katika kuondoa HOFU yake, hofu iliyojaa ndani ya kifua chake ya kuongozwa na watu dhaifu wasio na uwezo ndani ya Chama, wasio na maono, wasio na nia njema na waliokosa sifa kuu ya kiongozi bora ya UADILIFU. Zitto akanishauri nami nikaupokea ushauri huo kuwa "we should give the party A NEW BRAND..ili kiimarike zaidi na kiweze kuwakomboa watanzania.

Kwa bahati mbaya sana, na labda ni kwa sababu ya uchu wa madaraka, wenzetu hawakutuelewa, wakadhani na kufikiri kama alivyofikiri FARAO wakati MUSA alipomwambia, niacheni wana wa Israel wawe nyuma yangu, nitawaongoza katika nchi ya maziwa na asali.,Viongozi wa CHADEMA wakasema kama alivyosema FARAO, kuwa ninyi ni WASALITI, FARAO alimwambia MUSA nilikutwaa, nikakulea kama mwanangu na leo unataka kunisaliti..MUSA mwenye hekima aliyofundishwa na MUNGU mwenyewe, akawa hodari wa maneno na matendo akasema "SIFANYI haya kwa ajili ya nafsi yangu, bali kwa maslahi mapana ya Taifa hili" akawaambia maneno hayo wana wa Israeli pia kuwa " Njooni na mimi nitawaongoza njia, tokeni MISRI nitawaonyesha Nchi ya Maziwa na Asali:" nao wana wa Israeli hawakumsikiliza.

Ndio ni Zitto aliyeibua kashfa kubwa ndani ya Serikali na kuitingisha Serikali kwa kipindi chote alichokuwa bungeni, kwa HOJA zenye mashiko, ameibua kashfa za Buzwagi, Escrow na nyinginezo Kubwa ambazo zilitishia kuangusha utawala, hata mafanikio ya Upinzani katika chaguzi za hivi karibuni kwenye Serikali za mitaa unatokana na kazi hiyo ya Zitto bungeni, lakini bado WANA WA ISRAEL wanamuona ni MSALITI kwa sababu FARAO kawaambia kuwa huyo ni MSALITI.

CHAMA CHA SIASA hakiwezi kuendeshwa kwa matukio, ni siasa zilizopitwa na wakati kutengeneza matukio ili kukipa chama KICK, mara CCM wameingiza Kontena la kura feki, mara mashine za BVR zimechakachuliwa, mara DR Slaa anategewa sumu auawe, Mara CCM imeingiza mamluki wake ndani ya CDM na hivyo tutafukuza wasaliti wote, Mara mabomu kwenye mikutano yao, na kila kituko, CHAMA CHA SIASA HAKIFANIKIWI kwa kufanya siasa za vituko na matukio, muda wa kuomba sympathy kwa watanzania umeisha, CHADEMA kina umri wa miaka zaidi ya 20, KINGEWEZA KUWA TAYARI KIMEIMARIKA KAMA KINGEKUWA NA UONGOZI MAKINI NA IMARA, lakini bado kimebaki kuwa chama cha kiharakati ambacho watanzania bado wanahoji na wanakosa uhakika kuwa kinaweza kuwa chama cha siasa na kuweza kuwaongoza.

Zitto aliyaona haya miaka takribani 8 iliyopita, na akataka mabadiliko bahati mbaya akili ya ZITTO ilikuwa mbinguni na ALISHINDWA kui-connect ama kuwasiliama na WAFUASI na VIONGOZI waliopo ardhini na wengine ndani ya udongo ambao hawaoni chochote isipokuwa GIZA TOTORO, hakuna tofauti kwao baina ya mchana na usiku.

ZITTO atabaki kuwa MSALITI na CHADEMA itabaki kuwa ya WANAHARAKATI...
 
Hahaha Juliana bwana

ukaamua kumsaidia Zitto kuondoa hofu iliyokuwa kifuani mwake??? hahahahaha

Unanikumbusha mwalimu aliposema mambo ya kuwa na koiongozi anayekwenda kumuambia mke wake mambo ya serikali
 
Matukio ya CHADEMA tumeyazoea , wao waendelee tu wakichoka watatulia.
 
Back
Top Bottom