Mbala-mwezi
Member
- Sep 27, 2009
- 22
- 3
Wakati mjadala wa mgawo wa umeme ukizidi kushika kasi, na jana kijana Zitto kuamua kuvunja ukimwa kwa kutoa mapendekezo ya aina mbili; kushinikiza IPTL iwashe mitambo wakati mazungumzo yanaendelea..na kutaifisha mitambo ya Dowans....hotuba ambayo bado imetanda kwenye mijadala Tz kuanzia ndani ya JF, magazetini na sasa mitaani...mwenyewe leo ameelekea ujerumani kimasoma ambako anachukua PhD katika masuala ya sayansi ya uchumi..najua ujerumani hakuna mgawo...tunapojadili hotuba yake eneo muhimu zaidi liwe kutoa mapendekezo au kupitisha mapendekezo na hatua za kuchukua kuhakikisha mapendekezo mazuri yanatekelezwa na serikali badala ya kubishana huyu hivi, huyu vile huku mgawo ukiendelea kutikisa nchi.
Karibuni ataitwa mheshimiwa dokta Zitto Zuberi wa Kabwe.Phd itasaidia vipi constituents waliompa ubunge? Naona Zitto priorities zake muhimu ni kutafuta umaarufu bungeni na kujiendeleza binafsi tu
koba upo kaka ? ulijichimbia wapi lakini ?Germany Elimu bure na ukimaliza waambie wananchi wako umesoma bure kwa ajiri ya watu wenye vision walioona umuhimu wa kusaidia binadamu wote ili kufikia malengo yao na kujikomboa na sio bunge mnalopeana mikopo ya mamilioni kununua magari ya kifahari huku vijana wakinyimwa pesa za kula vyuoni na kuwafukuza eti wamegoma...magari mliyopeana mikopo na mafuta ya bure na bila aibu mkajiongezea madereva bungeni yanatosha kuwasha umeme nchi nzima!
koba upo kaka ? ulijichimbia wapi lakini ?
Kitila
Kwa wanaotaka kusoma Phd (free) Zurich
I hope ni free of tuition fee tu, mtu awe na stipend, hali kadhalika nauli. Return ticket hadi huko si chini ya dola 1000, kama upo Zurich sema kabisa na kadirio la gharama za kuishi kwa mwezi.
wanasihasa wa bongo washaona kuwa na PhD ni ujiko
watu kiwanja wanazo na wala huwezi kujua kama wanazo.
Ujinga au upumbavu?? chagua mwenyewe?Huyu Zitto lini kapata bachelor's?