Mbala-mwezi
Member
- Sep 27, 2009
- 22
- 3
Wakati mjadala wa mgawo wa umeme ukizidi kushika kasi, na jana kijana Zitto kuamua kuvunja ukimwa kwa kutoa mapendekezo ya aina mbili; kushinikiza IPTL iwashe mitambo wakati mazungumzo yanaendelea..na kutaifisha mitambo ya Dowans....hotuba ambayo bado imetanda kwenye mijadala Tz kuanzia ndani ya JF, magazetini na sasa mitaani...mwenyewe leo ameelekea ujerumani kimasoma ambako anachukua PhD katika masuala ya sayansi ya uchumi.
Najua Ujerumani hakuna mgawo...tunapojadili hotuba yake eneo muhimu zaidi liwe kutoa mapendekezo au kupitisha mapendekezo na hatua za kuchukua kuhakikisha mapendekezo mazuri yanatekelezwa na serikali badala ya kubishana huyu hivi, huyu vile huku mgawo ukiendelea kutikisa nchi.