Zitto Arejea Ujerumani kwa PhD

Yep, kweli kabisa ukiwa na PhD kwenye maswala ya kuwachamba vibibi vya kitasha nivigumu sana watu wakajuwa, maana ofisi yako ni maliwatoni most of the time.

ona huyu naye anavyokurupuka...Kuosha vibibi unasomea mwezi na wanakupa kazi.
nazungumzia wanasiasa haohao
hivi wewe unajua kama Goldon Brown ana PhD?au Condoleeza Rice,tena aliipata akiwa na miaka 26?
 
Put record straight jamani,

Mh. Zitto hafanyi PhD. He is doing his Masters. Jamani watu mkileta mada hapa ni vyema kufanya research. Sasa angalia thread nzima wamemuamini mleta mada, wakati na yeye hana uhakika na anachokiandika. Next time please do your research siyo kuja hapa kutoa info ambazo wewe mwenyewe huna uhakika nazo. NA HAPA NAANDIKA KWA CONFIDENCE MAANA NAJUA KABISA MKUBWA ANAFANYA MASTERS na Siyo PHD.

Otherwise, jamani, tujifunze kitu kimoja. Kutokubaliana siyo uadui. Kama hukubaliani na Mh. Zitto nadhani ni kwa mtizamo wa hoja, na si vyema kuanza kudemonize each other. Thats politics. Tushindanishe hoja. emotions zetu zisitufanye tuone wale wasiokubaliana na mawazo yetu kama wasaliti. Hapana siyo vyema. After all we cant be the same and our way of thinking is and must be different. Personally sikubaliani na mtizamo wa Zitto katika hili la DOWANS lakini sina budi kuuheshimu mtizamo wake. Maana atleast yeye kauweka wazi..ni tofauti na sisi tuanoandikia kwenye keyboard ya computer bila kuongea mbele ya umma. We should stand up and be counted.

Otherwise na mimi ningependa Serikali inunue mitambo hii moja kwa moja toka kiwandani. Kama inaweza kuagiza mashangingi mia saba kutoka Japan..kwanini ishindwe kuagiza genereta mbili toka GE or Siemens? Something fishy is in the pipeline.

Otherwise kwa Mh. Zitto, kila lakheri katika masomo yako. Elimu ni lulu. It neither has limits nor an end. Ongeza ujuzi urudi tulijenge taifa.

Masanja,

Mkuu
Hiyo kazi ya kuagiza magari ya serikali ina watu wa kati aisee.....for sure (Nafahamu) Manji ni mmoja wao..........
 
ona huyu naye anavyokurupuka...Kuosha vibibi unasomea mwezi na wanakupa kazi.
nazungumzia wanasiasa haohao
hivi wewe unajua kama Goldon Brown ana PhD?au Condoleeza Rice,tena aliipata akiwa na miaka 26?

Ndugu, nilikuwa nachekesha tu na vilevile kuonyesha kwamba kazi anayofanya mtu mwenye PhD na somo alilochukulia PhD ni viashiria tosha vya yeye kujulikana ana PhD.
 
Naomba nisahihishe kidogo. Sijaanza PHD bado. Ninaandika proposal ya PHD na nimepewa mpaka mwezi Mei mwakani kuwa nimemaliza na proposal kupitishwa na msimamizi wangu katika chuo cha WHU-OttoBeisheim School of Management. Ninajiandaa na shahada ya uzamivu katika uchumi rasilimali - Resources economics na nikifanikiwa, inshaallah, nitaanza rasmi kusoma ili kupata Doctorate of Economic Sciences.
Wakati huu ambao ninaandika proposal nimejienroll Bucerius Law School kwa masomo ya sheria za Biashara, shahada ya uzamili - ninaandika kuhusu mfumo wa kodi katika sekta ya madini (fiscal stability clauses in the mining sector. Unnecessary evil?).

Hivyo, naomba ieleweke kuwa bado sijaanza masomo ya PHD kama MBALAMWEZI alivyoandika hapa. Sijui Mbalamwezi katoa wapi habari hizi maana angeniuliza kwanza.......................
 
Hapa tumekuelewa mkuu na umeonesha umakini wako katika kufanya mambo yako vinginevyo tungesikia tu kuwa unaitwa Dr, kilalakheri..
 
Germany Elimu bure na ukimaliza waambie wananchi wako umesoma bure kwa ajiri ya watu wenye vision walioona umuhimu wa kusaidia binadamu wote ili kufikia malengo yao na kujikomboa na sio bunge mnalopeana mikopo ya mamilioni kununua magari ya kifahari huku vijana wakinyimwa pesa za kula vyuoni na kuwafukuza eti wamegoma...magari mliyopeana mikopo na mafuta ya bure na bila aibu mkajiongezea madereva bungeni yanatosha kuwasha umeme nchi nzima!

heee kumbe elimu bure ??
 
Naomba nisahihishe kidogo. Sijaanza PHD bado. Ninaandika proposal ya PHD na nimepewa mpaka mwezi Mei mwakani kuwa nimemaliza na proposal kupitishwa na msimamizi wangu katika chuo cha WHU-OttoBeisheim School of Management. Ninajiandaa na shahada ya uzamivu katika uchumi rasilimali - Resources economics na nikifanikiwa, inshaallah, nitaanza rasmi kusoma ili kupata Doctorate of Economic Sciences.
Wakati huu ambao ninaandika proposal nimejienroll Bucerius Law School kwa masomo ya sheria za Biashara, shahada ya uzamili - ninaandika kuhusu mfumo wa kodi katika sekta ya madini (fiscal stability clauses in the mining sector. Unnecessary evil?).

Hivyo, naomba ieleweke kuwa bado sijaanza masomo ya PHD kama MBALAMWEZI alivyoandika hapa. Sijui Mbalamwezi katoa wapi habari hizi maana angeniuliza kwanza.......................

kwa hiyo bado upo Bongo haujaondoka?naona hili sakata la umeme linashika hatamu sasa
 
hongera zitto kabwe ..inaonyesha unasotea phd....na sio kama za wale wenzetu za urusi[political science] au za kununua ...na inafurahisha pale mtu mwenye phd akiongea unaweza kukubali bila kuambiwa...tofauti na wanaojiiita madr lakini wanaongea utumbo...

au wale wanaopewa degree za bure ..na kukimbilia haraka haraka kujiita dr...wanasahau kuna watu kama mwalimu anazo 30...honoraria....au hata malecela na salim...lakini hawatambii...,mwenzetu anakadegree kamoja ka kudandia mazungumzo ..tayari dr........wakati mazungumzo ya zanzibar yanamshinda!!
 
Naomba nisahihishe kidogo. Sijaanza PHD bado. Ninaandika proposal ya PHD na nimepewa mpaka mwezi Mei mwakani kuwa nimemaliza na proposal kupitishwa na msimamizi wangu katika chuo cha WHU-OttoBeisheim School of Management. Ninajiandaa na shahada ya uzamivu katika uchumi rasilimali - Resources economics na nikifanikiwa, inshaallah, nitaanza rasmi kusoma ili kupata Doctorate of Economic Sciences.
Wakati huu ambao ninaandika proposal nimejienroll Bucerius Law School kwa masomo ya sheria za Biashara, shahada ya uzamili - ninaandika kuhusu mfumo wa kodi katika sekta ya madini (fiscal stability clauses in the mining sector. Unnecessary evil?).

Hivyo, naomba ieleweke kuwa bado sijaanza masomo ya PHD kama MBALAMWEZI alivyoandika hapa. Sijui Mbalamwezi katoa wapi habari hizi maana angeniuliza kwanza.......................

Hongera kwa uamuzi ulioufikia wa kufanya Phd-na kila la heri. Utakapomaliza masomo yako utufahamishe ili tukupongeze pia.
 
wanasihasa wa bongo washaona kuwa na PhD ni ujiko
watu kiwanja wanazo na wala huwezi kujua kama wanazo.
what kind of nonsense is this? are you implying watu wasisome? kwani kiwanja wakiwa nazo na wasiseme who cares? acheni wivu wa kijinga, kama vp na nyie kasomeni.
 
what kind of nonsense is this? are you implying watu wasisome? kwani kiwanja wakiwa nazo na wasiseme who cares? acheni wivu wa kijinga, kama vp na nyie kasomeni.

Naomba kuuliza tatizo la Zitto hapa ni lipi? hadi kushambuliwa namna hii.
1.Tatizo ni kuwa nawazo la kujiendeleza kielimu?
2.Tatizo ni kusimamia mawazo yake na anavyoona kulingana na uelewa wake juu ya umeme na dowans??
3.ama tatizo ni lile lile la alipojaribu kuwania uenyekiti??
 
Dark City kwa uelewa wangu wa haraka huna hoja ya maana. Zitto ametoa mawazo yake, je ya kwako ni yapi tuyachambue? Au unaona donge mwenzio anaenda kusoma PhD. Argue ukiwa na pointi sio kubwabwaja bila mwelekeo.
 
what kind of nonsense is this? are you implying watu wasisome? kwani kiwanja wakiwa nazo na wasiseme who cares? acheni wivu wa kijinga, kama vp na nyie kasomeni.

@carmel sometimes hutakiwi kupoteza mda wako kujadili coments za mtu kama huyo....wametumwa wengine alafu wamesahau JF is the home for great thinkers....Pole carmel!
 
Huyu jamaa kweli nae ana msimamo wa kueleweka, na ina maana sasa siasa basi au?

Ni nini hasa anachohitaji zaidi au ndio ku-please umma ya kuwa Zitto has a Phd. He has already established himself as a young innovative politician why throw that away now.

You got the basics of the economy, Your a politician now not an ecnomists. Offer thoughts to ecnomists and argue with them. Let them advise you with the basics of economy make your mind if you intend to remain in politics.

Unajua this is why africans suffer Phd, Phd, Phd so what they get it wrong all the time this economists. If he wanted to become a better politician I think Law would have been the skill he needed to become a better speaker and politicians rather than a Phd on something he already has a concept of hit.

Learn to be a better politician than concentrate on pleasing the public with unnecesary credentials. Use examples of useless scholars we have in the government who are not performing. If anything its because they are in the wrong employment.
 
Phd itasaidia vipi constituents waliompa ubunge? Naona Zitto priorities zake muhimu ni kutafuta umaarufu bungeni na kujiendeleza binafsi tu

Sasa wewe ulitaka afanyeje?, Ni nani asiyetaka maendeleo binafsi?, ni mungu tu, maana hata kuupata huo ubunge ni maendeleo binafsi. Tuache ubabaishaji, personal development ni first priority for any rational human being. But that development should not come at the cost/suffering of other human beings like mafisadi wengi wanavyoifanya Tanzania. Kwani maendeleo ya nchi yatachochewa na maendeleo binafsi halali ya wananchi wake. OVER!
 
Karibuni ataitwa mheshimiwa dokta Zitto Zuberi wa Kabwe.
Ila awe mwangalifu asije na u dr wa wakina Kamara na wenzie! Lazima atuthibishie pasipo shaka Kwamba kasotea kabla hatujabadilisha jina lake na kulitanguliza na dokta.
Kweli bwana it is tempting kupata PhD kwa mlango mbovu. Kinacho nishangaza ni namna atakavyotumikia mabwana wawili. Nimesoma Ujerumany, PhD ni full time na kama uchanguzi ni mwakani sijui ataprogess namna gani.....labda kama atajitambulisha kwa undani zaidi
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom