Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Status
Not open for further replies.
Nikusahihishe kidogo. Mnyika na Halima hawakuwepo kabisa Dodoma siku ya tukio au walikuwepo lakini hawakuja kwenye kikao na kisha Bungei. Mimi nilikuwepo kwenye kikao na kusema wazi mawazo yangu kuwa sioni kama ku walk out ni mkakati mzuri. Kwa kuwa sikuunga mkono maamuzi hayo niliamua kutokwenda kabisa Bungeni. Nimeshalisemea hilo na kulitolea maelezo hapa JF. Sikutaka kuwa mnafiki na kujificha katika pazia la wengine. Sasa kama ni uamuzi wa makos umeshatokea, muhimu ni kusahihisha makosa na kwenda mbele. Nawaomba radhi wale wote niliowaudhi kwa msimamo niliochukua na hivyo mkaumia. Mimi niliona ndio msimamo sahihi (kutokwenda Bungeni kabisa na kama kwenda kuto walk out). Wengi mmeona haukuwa msimamo sahihi. Nimesikia. Tupige mstari na tuendelee na kazi nyingine.


Hapo hapo Mkuu Zitto Kabwe... kwa nini ulilopoka TBC? naita kuropoka kwa sababu ni wambea na VIHEREHERE hutaka kila wafanyalo kwa siri lijulikane kwa wote na kusifiwa na wabaya wa upande mwingine au kiswahili fasaha inaitwa KUJIPENDEKEZA........Ungenyamaza kama hao unaowaita Mnyika ungepungukiwa nini? Mbona Mnyika hajaenda TBC kusema kwa nn hakuwepo Bungeni au HiyoDodoma yenyewe?..Tubu mtu wangu na useme tena huko huko TBC1 ili tuone kweli wewe mwana mageuzi
 
Nionyeshe wapi nimesema kuna mvurugano ndani ya chama. Sijasema hivyo. Hiyo ni tafsiri yako na una haki ya kuweka tafsiri ya jambo lolote. Siwezi kukuingilia uhuru wako wa kutafsiri.


Sasa unaposema gazeti linalomilikiwa na watu wa karibu wa mwenyekiti linakuhujumu kwa makusudi kwa habari za uongo unakusudia tutafsiri vipi?


Siasa za maji taka kama ulivyoziita zitafanywa bila ya kuwepo mvurugiko?

Huo ndo ujumbe uliopokelewa leo hapa JF. Kataa wee lakini hiyo dhana haikuwemo vichwani mwetu mpaka ulipokuja wewe na maelezo yako marefu.
 
Hapo hapo Mkuu Zitto Kabwe... kwa nini ulilopoka TBC? naita kuropoka kwa sababu ni wambea na VIHEREHERE hutaka kila wafanyalo kwa siri lijulikane kwa wote na kusifiwa na wabaya wa upande mwingine au kiswahili fasaha inaitwa KUJIPENDEKEZA........Ungenyamaza kama hao unaowaita Mnyika ungepungukiwa nini? Mbona Mnyika hajaenda TBC kusema kwa nn hakuwepo Bungeni au HiyoDodoma yenyewe?..Tubu mtu wangu na useme tena huko huko TBC1 ili tuone kweli wewe mwana mageuzi

Amekili Mkuu kwamba suala hili limewauzi wengi anaomba msamaha..... Binafsi kwa hili nimemsamehe but i will be expecting more from him next time
 
Sasa unaposema gazeti linalomilikiwa na watu wa karibu wa mwenyekiti linakuhujumu kwa makusudi kwa habari za uongo unakusudia tutafsiri vipi?


Siasa za maji taka kama ulivyoziita zitafanywa bila ya kuwepo mvurugiko?

Huo ndo ujumbe uliopokelewa leo hapa JF. Kataa wee lakini hiyo dhana haikuwemo vichwani mwetu mpaka ulipokuja wewe na maelezo yako marefu.

Zitto kashatuambia hatabiriki, kwa hiyo kutegemea consistency kutoka kwake ni an exercise in futility.

Mara atakwambia Komu ana gazeti linalomuandika vibaya, mara hakuna mgogoro. Huyu inaonekana anaweza hata kukutafsiria what "is" is.
 
MwanaHalisi linamilikiwa na watu wawili wenye hisa sawa. Hakuna mwenye hisa nyingi kumzidi mwenzie kati ya Komu na Kubenea. Vile vile Komu na Kubenea wameoa nyumba moja. Kwenye MwanaHalisi Komu na Kubenea ndio wamiliki pekee. Kama wewe unajua wamiliki wengine tuambie.

Hapo naona kama unatupa taarifa ambazo hatukuhitaji kuzijua, isitoshe, kwa kusema hivyo unataka kutupa ujumbe gani? Na kwanini?

Kweli kama ni kijambo kimepata mjambaji..........
 
Zitto kashatuambia hatabiriki, kwa hiyo kutegemea consistency kutoka kwake ni an exercise in futility.

Mara atakwambia Komu ana gazeti linalomuandika vibaya, mara hakuna mgogoro. Huyu inaonekana anaweza hata kukutafsiria what "is" is.

Na kutotabirika ni sifa njema eee!

Chadema nzima haitabiri lakini tusimlaumu sana kwa hilo. Leo Slaa anasema hatumtambui rais, siku ya pili Mbowe anauliza dhana ya kutomtambua rais imetoka wapi

Leo mtu analilia ubunge kwa nguvu zote mpaka kuwaaibisha viongozi wengine wa chama, baada ya siku 7 za ubunge anasema kaboreka.

Mwengine anajisifu kwenye post ya juu kuwa kazi ya uteuzi wa viti vya wanawake alitunukiwa yeye, baada ya post 20 anasema demokrasia ilitumika.
 
mkuu kama unakiri kwamba unahujumiwa na gazeti linalomilikiwa na mwenyekiti wako.... je huoni hapa kuna tatizo? na yawezekana unalijua au unalifumbia macho tatizo hilo..... kwanini msimalize tatizo.... hii ni sawa na kula chakula na kurudisha sahani kwa mpishi bila kuosha.., mpishi atakupakulia chakula tena bila kuosha sahani..... tumbo likiuma daktari atakwambia kamuulize mpishi wa chakula...... kama hamtatui matatizo kwa kufuata taratibu zilizowekwa mtarudi tena kwenye majimbo ya uchaguzi kuomba kura ......
 
Wanaodai kufunga mjadala juu ya Zitto kabla ya kupatikana ufumbuzi wa tatizo hilo ni wababe tu kama wababe wengine wote, tofauti hawa kwasasa hawana dola vinginevyo wangelipenda kuziba kila mtu mdomo. Sasa nirejee kwenye mada; suala la Zitto limegusa hisia za watu wengi kwasababu tangu kwa chati yake ipande katika medani ya siasa hapa nchini, mwenendo wake umekuwa ni wakutilia shaka. Ingawaje hivi sasa anadai kuwa amekuwa akiendesha mambo yake kwa mujibu wa katiba ya chadema, lakini lazima tukubaliane katiba yeyote ile utoe muundo wa uongozi wa taasisi husika; muundo huo pamoja na mambo mengine ubainisha ni nani kielelezo cha uongozi katika taasisi hiyo; huyo kiongozi kielelezo ndiyo huwa msemaji mkuu wa taasisi husika; kiongozi mwingine yeyote katika taasisi hiyo hawezi kuonekana akipingana hadharani na kiongozi huyo kielelezo kwa masuala yanayohusu taasisi husika, kama ambavyo Zitto amekuwa akifanya
 
Mwaka 2010 - 2011 nimeamua kujikita kwenye Rural Growth, Gas and Petroleum sub-sectors and Leadership Ethics. Rural growth kwa ajili ya kusukuma nguvu katika cutting poverty levels vijijini. Bado ukuaji wa uchumi wa Taifa letu haufiki chini na hivyo hauendani kabisa na kupungua kwa umasikini. Ajenda hii imesahaulika sana sana. Baada ya kupata sheria mpya ya madini (bado ina mapungufu kidogo), napeleka nguvu kwenye kuhakikisha kuwa Gesi Asilia na Mafuta yanafaidisha nchi yetu. Lengo ni kusukuma kuwe na Sheria mpya ya Gesi na Mafuta ili kuepuka yaliyotukuta kwenye sekta ya Madini. Nina muswada wa sheria nilioandika ili kubadili sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Serikali kukataa kuuchapisha. Ninadhamiria kuhakikisha kuwa muswada ninaurudisha Bungeni. Lengo ni kutenganisha Biashara na siasa kwa kuanzisha blind trusts. Pia lengo ni kufanya sheria ya maadili iwe effective na wananchi wawe na uhuru zaidi wa kukagua mali za viongozi wao.

Mabo mengine ni masuala ya chama mfano suala la Katiba mpya nk.

Sawa kabisa . Ujaliwe afya na nguvu yakutimiza mjukumu hayo vizuri. Will wana jf tuanaotka kusaidiana na wataka mabdiliko tukiomba official contact zako?

Otherwise kutoa challenge na mchango wa ziada.
Miimi nina ushauri. Jimboni/Mkoani kwako sijui kama kuna maktaba. kama ipo najua itakuwa haina reources za kutosha. Angalia uwezekano wa Maktaba ya Mkoa iunganishwe na Interntet. Makataba ya Mkoa ipate mtaaalamu wa IT atakayewasaidia kupat info mbali mbli. Dunia ya sasa ni ya digital. In short Tafuta jinsi ya kuomba makataba zote tanzania ziwe zina vituo vya Computer center.

  • walimu wa shule mbali kupata taarifa current za mambo ambayo hawana vitabu.
  • madaktari ,wauguzi wahandisi wa mkoa kujifunza mambo mapya.
  • Wafanyakazi wengine wa serikali
  • Wanafunzi
maktaba za mikoa zinaweza kuwa na projector na amabzo zitatumika kuonyesa kuazima shule kuonyesha baadhi practical mabazo mpaka leo wanajifunza kwa notes.
Inasikitisha kuona hata Shule za mijini wanshindwa kuona hata practical zinazoweza kupatikana youtube for free

Idea ni kuona maktaba zote tanzania zinazokufa zinakuwa na Department inyoitwa Regional Computer Center
 
Ungesema hiyo habari imeandikwa na Ansbert Ngurumo kupitia Mwanahalisi,kuliwa na umuhimu gani wa kusema mwandishi ni Press secretary wa Mbowe.

Unaendelea na siasa zako za maji taka kumtaja Antony Komu ni mmiliki wa Mwanahalisi na kuwaacha wamiliki wengine wenye hisa nyingi kama Kubenea kwasababu sio wachaga.
Hii si mara ya kwanza kuihusisha Chadema na ukabila ni wazi unataka wakufukuze ili ukaseme Wachaga wamekufuza.Cha kushangaza mpaka sasa hivi haujui Watanzania wengi wameshaelewa Chadema hakuna ukabila na hakuna atakaye kufukuza.

Ukikuwa utaacha.
 
Kaka Zitto usione hapa JF watu wanakuhukumu kwa sana, WE LOVE YOU MEN, tuna wivu na wewe maana tunakupenda kama kijana mwenzetu, wewe ni muumini wa dini fulani, MUNGU wetu ana wivu sana na sisi maana anatupenda kuliko, KILA AKUPENDAE huwa na wivu na kila siku ujue asiekuwa na wivu na wewe basi hakupendi, MUNGU huchukizwa sana kuona wanae tunaenda opposite na njia njema, WanaJF Tuna imani na wewe tunachukizwa sana kuona ndugu yetu, kijana mwenzetu unaenda kinyume na tunayojua unayakalia kidete(I mean mapinduzi ya kweli), tuna Wivu kuona usema ovyo ovyo TBC1, ukitaka kumuua nyani FUMBA macho ndugu yangu, usipate kumuhurumia, WEWE Unamhurumia Kikwete asipate aibu, Kaka Usitufanye imani yetu ipotee kwako, WE LOVE YOU MEN....Make us continue loving you mzee...
 
Zitto na wewe bana. Wewe ipotezee tu hii JF au kama huwezi ingia na ID mpya tofauti (kama haunayo tayari) maana sasa unawapa fodder ya kukufanya wewe mada kila kukicha.

Haunufaiki na chochote hapa katika haya majibizano na watu wanaotumia vivuli vyao kama utambulisho. Hujui nani ni nani. Kuna wengine wamekaa mkao wa kula wakisubiri utie neno nao waliteke nyara, waspin wapendavyo, halafu mwishowe unaonekana kama wewe ndiye hujui hata ukifanyacho.

Mimi ningekuwa wewe na u public figure wako, walahi tena ningeipotezea JF.
 
Zitto na wewe bana. Wewe ipotezee tu hii JF au kama huwezi ingia na ID mpya tofauti (kama haunayo tayari) maana sasa unawapa fodder ya kukufanya wewe mada kila kukicha.

Haunufaiki na chochote hapa katika haya majibizano na watu wanaotumia vivuli vyao kama utambulisho. Hujui nani ni nani. Kuna wengine wamekaa mkao wa kula wakisubiri utie neno nao waliteke nyara, waspin wapendavyo, halafu mwishowe unaonekana kama wewe ndiye hujui hata ukifanyacho.

Mimi ningekuwa wewe na u public figure wako, walahi tena ningeipotezea JF.
I beg to differ brother, In todays world... hii pia ni mojawapo ya medium ya wanasiasa kuweza kuwa karibu na wananchi wao.. The point sio kuacha kuja hapa, lakini point ni kuwa very careful with what you write
 
Majuzi Mods walimuomba Zitto ajibu tuhuma humu ndani; kwa kiasi fulani "alieleweka" pale tu ilipothibitika kwamba alikuwa na mchango mkubwa kwa chama chake CDM wakati wa uchaguzi! Lakini sasa it is obvious kuna nyufa ndani ya CDM! Ule mpango wa kutokwenda Bungeni siku waliposusia hotuba ya JK(ingawa anadai alifanya hivyo kwa kuwa hakukubaliana na maamuzi ya CDM) bado nadhani kisiasa ilikuwa ni pigo kwa CDM! Na athari zake ndiyo hizi tunaziona....MPASUKO! Kunakosekana umoja ndani ya CDM....!!
Siamini kama ZK anaweza kujiunda CCM an NCCR kwa kuwa atakuwa amejivunjia heshima yake kwa kiwango kikubwa na atakuwa amedhoofisha nguvu ya upinzani (which is a negative thing kwake)! Je, tatizo ni nini? Tatizo ni ubinafsi na mgogoro mkubwa kati ya ZK na FM!! Hawa jamaa ni vijana wadogo na wana bifu kubwa sana na ilidhihirika pale ZK alipotaka kuwania uenyekiti wa CDM taifa!! Kwa mantiki hii maamuzi yoyote yale, maelekezo yoyote yale from FM kwa ujumla hayakubaliki kwa ZK!!
Wakipatanishwa hawa wawili badi CDM itakaa sawa, ila lazima FM akubali mabadiliko na afahamu kwamba ZK ni zaidi yake kisiasa.....

CDM hibomolewi na ZK, inabomolewa na FM na uongozi wa juu! ZK yeye hakubaliani na uongozi ki-msingi? Does he has a point? We need to becritical, tusimlaumu sana! Namfahamu ZK, japo kuwa ni opportunist pia ni critical thinker na hakubali kuyumbishwa anapoona ana haki.
Nawasilisha!
 
I beg to differ brother, In todays world... hii pia ni mojawapo ya medium ya wanasiasa kuweza kuwa karibu na wananchi wao.. The point sio kuacha kuja hapa, lakini point ni kuwa very careful with what you write

Kuwa karibu na wananchi wanaojificha utambulisho wao? Hell to the no bruh....sasa humu unaweza ukakuta Mbowe yumo, Slaa yumo, Mabere Marando yumo....na huenda wanampaka matope Zitto kwa kutumia majina bandia wakati yeye yupo kwa jina la kweli. I don't think it's fair...but that's just me.
 
Zitto umesomeka, kwa muungwana mtu akiomba radhi ni vyema akasamehewa, But we are watching you!. Nakutakia afya njema katika majukumu yako ya ubunge. Nimependa agenda yako ya maadili ya viongozi lakin kumbukeni nguvu zetu nyingi zielekezwe kwenye katiba kwasababu kama tutapata katiba mpya basi hata haya mengine yatakuwa yametatuliwa.
 
................

Haunufaiki na chochote hapa katika haya majibizano na watu wanaotumia vivuli vyao kama utambulisho. Hujui nani ni nani. Kuna wengine wamekaa mkao wa kula wakisubiri utie neno nao waliteke nyara, waspin wapendavyo, halafu mwishowe unaonekana kama wewe ndiye hujui hata ukifanyacho.

Mimi ningekuwa wewe na u public figure wako, walahi tena ningeipotezea JF.

Hahahahahah Umesema kweli kabisa Inawezekna kwa mjadala wa leo wengine wako wanatafuta Heading ya gazeti
 
Kuwa karibu na wananchi wanaojificha utambulisho wao? Hell to the no bruh....sasa humu unaweza ukakuta Mbowe yumo, Slaa yumo, Mabere Marando yumo....na huenda wanampaka matope Zitto kwa kutumia majina bandia wakati yeye yupo kwa jina la kweli. I don't think it's fair...but that's just me.

Hakuna tatizo kama atakuja hapa yeye kama zitto na kuongelea yanayomuhusu unafikili hapa akija na kuanza kuwabana mafisadi, au mikataba mibovu, au jinsi tunavyohitaji katiba mpya? nani atapindisha ukweli??? haya mambo personal anaweza akajibu shortly tu kwamba sio kweli na ukweli ni ABC
 
Ndugu wana JF,
Kumekuwa na mada nyingi sna humu ndani ambazo zinajaribu kuonyesha kuwa mimi ni mkosaji na kunipaka matope sana. Nimejdiliwa mno katika jf na hata kuzushiwa mambo mengi sana. Kuna wanaonisema kwa dhati y moyo wao kwamba nimekosea hapa na pale na kuna wanaoona huu ndio wakati wa kumwangusha Zitto na hivyo kuendeleza propaganda za kila namna.

Hii makala imetoka katika gazeti la Mwanahalisi la wiki iliyopita. Imeandikwa na Ansbert Ngurumo, Mhariri wa Tanzania Daima na Press Secretary wa Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA. MwanaHalisi linamilikiwa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa CHADEMA ndugu Antony Komu. MwanaHalisi limekuwa mstari wa mbele kunipaka matope na kutoa propaganda chafu dhidi yangu na sijui ni kwa faida ya nani.

Nadhani mmenijadili vya kutosha. Itoshe kusema nimesikia. Yale ambayo ni makosa nitajirekebisha maana mimi ni binaadamu. Yale ambayo ni uzushi, uwongo na propaganda nitayadharau.

Jambo moja nilisema na nimeshalisema huko nyuma ni kwamba, nimekuwa mwanachama wa CHADEMA toka nikiwa nina umri wa miaka 16 na sasa nina miaka 35, sijawahi kuwa mwanachama wa chama kingine chochote cha siasa. Sitegemei kuwa mwanachama wa chama kingine chochote cha siasa tofauti na CHADEMA. Sijawahi hata siku moja kusaliti chama changu na wala sitajaribu kufanya hivyo. Nina utii kwa Katiba ya chama changu na kwa chama kama Taasisi (Asasi). Pamoja na kutofautiana kimawazo na viongozi wenzangu (wote hatuwezi kufikiri sawasawa) sijawahi kukiuka maamuzi halali ya vikao vya chama kwa mujibu wa Katiba.

CHADEMA ni taasisi inayokua na hivyo changamoto zinaongezeka kila siku. Ni jukumu letu kuhakikisha kuwa tunazikabili changamoto hizi bila kuathiri kazi iliyombele yetu ya kujenga Tanzania yenye demokrasia ya kweli na yenye watu wenye fursa ya kuendeleza maisha yao.

Siasa za kupakana matope. Siasa za kumalizana. Siasa za maji taka, hazitasaidia nchi yetu wala chama chetu. Ifikapo mwaka 2015, wanachama wataamua nani atabeba bendera ya chama kwa njia za kidemokrasia. Hakuna sababu ya kuanza kumalizana sasa. Tukajenge chama wilayani na vijijini ili ifikapo uchaguzi ujao tuwe na mawakala kila kituo, walinde kura zetu na tuweze kushika Dola na kuongoza.

Watanzania mtusaidie katika jukumu hili. Jumamosi njema

Ni vizuri ulivyoweka msimamo wako Hadharani hivyo kuondoa maneno maneno ya watu ( marafiki wa CDM na MAADUI wa CDM na wananchi wa kawaida wenye mapenzi mema na nchi yao)

Lakini kwa upande wangu umeibua hisia za kuwepo mgogoro mkubwa ndani ya CDM maana umetubainishia kuwa Ansbert Ngurumo ni Press Secretary wa Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA na pia MwanaHalisi linamilikiwa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa CHADEMA ndugu Antony Komu katika POST yako umeonyesha kuwa gazeti la MWANAHALISI lipo mstari wa mbele ktk kukuchafua, nanukuu"MwanaHalisi limekuwa mstari wa mbele kunipaka matope na kutoa propaganda chafu dhidi yangu na sijui ni kwa faida ya nani". Hivyo kwa mtazamo wako na maelezo yako yanabainisha kuwa CHADEMA mnatafunana wenyewe kwa wenyewe kama SENENE swali kichawani mwangu mnatafunana kwa maslahi ya CHAMA au BINAFSI au ya Adui CCM?

Lakini ni vyema ufahamu na tufahamu kuwa Ansbert Ngurumo ana haki ya kuwa na mawazo yake na msimamo wake tofauti na wa mwenyekiti, pia ana haki ya kutoa msimamo wake. Cha kujiuliza je msimamo alioutoa katika makala yake alilazimishwa na wenyekiti au una mlengo wa kumjenga mwenyekiti na kumualibia ZITTO?

Je makala za kumchafua ZITTO katika gazeti la Mwanahalisi(kama anavyolalamika ndugu yetu ZITTO) je ni maelekezo ya mmiliki wake Antony Komu au ni maoni na misimamo ya waandishi wa Makala hizo?

Ni vyema Mpiganaji Mwenzetu ZITTO akawa makini ktk suala hili maana kitendo chake cha kutoingia BUNGENI kimewaumiza wanaharakati na wapiganaji wengi, Lakini maoni na ufafanuzi alioutoa TBC 1 huo umewaudhi na kuwa kwaza na kuwavunja imani wanaharakati, wapiganaji, wana CDM na WATANZANIA wengi wapenda mapadiliko. ZITTO kwa kiukweli umetuumiza na kutukwaza mimi ni mmoja wa watu ambao tunakuamini na kuona wewe ni kiongozi shupavu na mkweli kwa CHAMA na NCHI yako. Lakini kwa maoni na utetezi wako TBC1 hapana je ungekaa kimya nini kingetokea, wajua kutoingia kwako Bungeni ilikuwa ni habari tosha kwa wanahabari je kabla ya kutoa utetezi wako na maoni yako ulipima kwanza? Je una kumbukumbu nzuri na TBC1 ilichokuwa inakifanya wakati wa kampeni kuidhoofisha CHADEMA? Je Kituo hicho cha TV yaani TBC1 uliona ndio kituo sahihi kwa wewe kutolea ufafanuzi au utetezi wako? Pia kusema kuwa kikao mlichokaa wabunge na kupiga kura ili kukubaliana kama mtoke bungeni au la wakati Rais anahutubia mliotaka msitoke mlishindwa hivyo waliotaka mtoke walishinda je wewe kutokufuata makubaliano ya kikao si ndio kukiuka DEMOKRASIA unayoihubiri siku zote? si kukisaliti CHAMA chako maana ni CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO? kweli unadhamini MAENDELEO unayosema yameletwa na KIKWETE jimboni kwako na Kuikana DEMOKRASIA ktk chama chako? Pia kusema ni kweli umefanya kosa kwa kushiriki ktk kutoka ktk Bunge kama mlivyo kubaliana na una subiri ADHABU ya CHAMA, (ZITTO kiongozi wangu na mpiganaji wangu kweli ulikuwa serious) Huoni kuwa una watega viongozi wenzako kwa kufanya kosa makusudi halafu unasubiri wenzako wakuadhibu ili baadae ulalamike/uwashutumu kuwa wanakuadhibu kwa sababu hauko kundi lao (yaani wewe ni mpinzani wa mwenyekiti)?

Ninamaswali mengi juu yako Kiongozi/kamanda ambayo nahitaji majibu, lakini ustaharabu wako wa kukiri kosa na kutuelezea kwa kifupi nini kinachoendelea au anachohisi unatendewa kwangu naona hupo sahihi na bado upo nasi ktk mapambano.

USHAURI WANGU KWAKO, MBOWE NA CHADEMA
CHADEMA Kilianzisha mapambano ktk kipindi kigumu cha 1995 lakini hakuna aliyegungua kuwa chama hicho ni NURU na MKOMBOZI kwa watanzania HADI MWL. NYERER alipotubainishia kuwa amesoma sera za vyama vyote na amekubali kuwa sera za CHADEMA ni sera za CHAMA mbadala, watu bado walikuwa wazito kuelewa lakini mapambano mliyoyaendesha toka 2000 hadi 2010 yamebainisha ukweli. Katika kuijenga CHADEMA hakuna asiyeuona mchango wa MBOWE, SLAA, ZITTO,MTEI, BOB MAKANI, BAREGU, Late CHACHA WANGWE, ARFI, KOMU,REGIA MTEMA, KAFULILA(nahodha aliyejitosa baharini),NDESA,MDEE na wengi wengi toka waanzilishi hadi waliojiunga wakati wa kampeni kama kaka SHIBUDA, kila mmoja anamchango wake ktk ujenzi wa CHAMA.
Ni wazi kuwa chama ni kundi la watu waliokubaliana kiitikadi na kisera kugombea ili kuchukua madaraka ya kuongoza nchi. na si kundi la watu wenye mawazo sawa,akili sawa na waliokubaliana kiitikadi na kisera kugombea ili kutwaa madaraka ya kuongoza nchi kwakuwa mnatofautiana mawazo na akili hivyo ni wazi mnaweza kutofautiana ktk utekelezaji wa sera, au kuongoza chama husika, hivyo kutofautiana ni lazima pia kutofautiana kunaweza kupelekea chama kwenye migogoro (Disputes) na ni wazi kuwa migogoro ikitumiwa vyema uimarisha CHAMA hiyo ni positive effect ya Disputes hivyo si vyema kiunyesha Watanzania mna migogoro badala ya kuitatua ndani ya chama ili iweze kuimarisha chama, nje ya chama kuna watu wakila aina wenye mapenzi na wasio na mapenzi kwa chama. JAMANI ACHENI KUCHEZA NA MEDIA KATIKA MASUALA SENSITIVE KWA CHAMA wanachama wamewapa uongozi hivy onyesheni uwezo wenu wa uongozi kwa kutatua migogoro ya ndani ya chama bila kuinadi ktk media.

Kuhusu nani agombee urais 2015 chama kama kawaida kipige utafiti wa kisayansi ili kumpata mgombea na si viongozi muanze kujijenga kwa kuchafuana ili muonekane mnafaa mbinu hizo ni za CCM acheni kuturudisha turikokimbia. PIA UCHAGUZI mkuu wa CHADEMA uonyeshe Demokrasia ya kweli na si kuombana kutoa majina mjenge mazoea ya ndani ya chama ya kukubali kushindwa au kushinda ili yakitokea hukunje ya chama ktk chaguzi za nchi tuwe kweli mfani wa DEMOKRASI kwa kukubali kushinda na kushindwa kama chaguzi ni za kidemokrasia na si mbinu ya CCM ya kupita bila kupingwa hapo dhana ya cham cha DEMOKRASIA itapoteza maana

ZITTO na viongozi wenzako kumbukeni kujikwaa si kuanguka(sio mimi wahenga ndivyo wasemavyo) jipangeni kuendeleza mapambano. JAMANI MUDA HUU NI VITA YA KUDAI KATIBA MPYA, TUME HURU YA UCHAGUZI, MGOMBEA BINAFSI na MAZINGIRA SAWA YA UENDESHAJI SIASA NCHINI, MGAWANYO SAWA WA RASILIMALI ZA NCHI, KUONDOA UMASIKINI ULIO TAMALAKI NCHINI na KUTOKOMEZA UFISADI.
NYINYI CHADEMA NDIO WAPIGANAJI MLIO MSTARI WA MBELE KUSITASITA NI KUTUSALITI( WAYAHUDI USEMA NI HERI MMOJA AFE KWA AJILI YA WENGI) ZITTO NA VIONGOZI WENZAKO Huu SIO wakati wa kuchagua silaha, eti silaha hii sio nzuri na hii ni nzuri suala lililopo ni kuwa kama silaha inauwezo wa kummaliza ADUI itumike hata kama ni KOMBEO

nawasilisha
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom