TANMO
JF-Expert Member
- Apr 12, 2008
- 12,046
- 12,542
Hii makala imetoka katika gazeti la Mwanahalisi la wiki iliyopita. Imeandikwa na Ansbert Ngurumo, Mhariri wa Tanzania Daima na Press Secretary wa Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA. MwanaHalisi linamilikiwa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa CHADEMA ndugu Antony Komu. MwanaHalisi limekuwa mstari wa mbele kunipaka matope na kutoa propaganda chafu dhidi yangu na sijui ni kwa faida ya nani.
Kwa mantiki hii unanilazimisha kuamini kuwa una mgogoro Binafsi na mmoja wa uliowataja hapo juu. Kwa faida ya nani huo mgogoro? mimi sijui....
Sijafanya kikao chochote na Lowasa. Kulikuwa na kikao cha Lowasa na Mbowe ambacho mimi nilishiriki kama Naibu wa Mbowe Bungeni. Hata hivyo sijafanya kikao kingine chochote.
Makala hii imeandikwa kwa lengo baya na ndio maana mwandishi kaficha jina lake. Kama ana guts aweke jina lake wazi na aje na ushahidi wa haya aliyoyaandika.
Inawezekana, swali langu kwako: kwa nini kila kukicha unaandikwa wewe tu? isitoshe sioni tatizo la mwandishi kuficha jina, kwa uzoefu wangu hii si mara ya kwanza kuona makala imeandikwa na mwandishi maalumu, labda tuseme analinda usalama wake.. Hivyo hapo penye nyekundu sidhani kama kuna ulazima wa huyo mwandishi kufanya hivyo.
Sijawahi kusema mahala popote kuwa ndani ya CHADEMA kuna udini. Ninaomba clip ya TBC iwekwe hapa jamvini na mtu anionyeshe wapi nimesem kuwa ndai ya CHADEMA kuna udinni. Tafadhali usinywe sumu unazopewa.
Hapo umenena. Kama kuna mwenye hiyo clip waungwana itasaidia kwa wale ambao hatujabahatika kuona kauli ya Mheshimiwa sana Zitto kuwa CHADEMA kuna udini..
Labda kwa kuongezea tu, Ndugu yangu Zitto jitahidi kuepuka kuwapatia watu nafasi ya kukuhukumu kwa maneno yako mwenyewe. Au kama huwezi kuvumilia basi tafuta mtu awe mshauri wako wa kisiasa ambaye atakuwa anakupa mwongozo wa nini useme na nini usiseme au ukiseme kwa kutumia maneno yapi, Siasa nayo ni sanaa wandugu. na neno likishatoka basi halirudi.
Silence can be misinterpreted but never misquoted, Even a stubborn fool is thought to be wise if he keeps silent.