Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Status
Not open for further replies.
Zitto sio tegemeo la CDM hata kauli zake na vitendo vyake sioni kama vina athari kwa CDM mimi naona nimpuuzi anaye stahili kupuuzwa tu
 
Zito wa mwanzo sio wa sasa......nawaeleza iq ya zito ni kubwa kuliko mnavyofikiria na msidhani hajui anachofanya na impact yake ......he is the only target now by ccm party to get through chadema...........we know how to deal with him!
 
Kutokana na kichefuchefu (haswa baada ya kusema anamtambua JK ni amiri jeshi mkuu na alama ya bunge na hivyo si vizuri kutoka bungeni na kwa kiburi kabisa kusema anasubiria hatma yake chamani kutokana na uamuzi wake huo) ambacho mh. Zitto Kabwe ameendelea kuleta ndani ya CHADEMA wana JF wenzangu nilikuwa ninatoa mapendekezo kuwa huyu jamaa ni wa kuogopwa kama ukoma, na ni kidudu hatari kuliko KIRUSI CHA UKIMWI kwa wana upinzani, wapigania haki na kwa wananchi wa Tanzania waliodhulumiwa haki zao kwa muda mrefu na chama tawala cha CCM. Kwangu mimi namwona ni msaliti mkubwa wa Watanzania na upinzani. Hivyo ni nilikuwa napendekeza aondolewe CHADEMA haraka kwani amepandikizwa na CCM. Nakishauri CHADEMA kimvue uanachama ili kunusuru upinzani wa ukweli ambao umebaki peke yake CHADEMA. Je wana JF wenzangu mnaonaje? Je aendelee kubaki CHADEMA au aondolewe. Ushauri utakaopatikana hapa ukiambatana na sababu za msingi, naomba CHADEMA waufanyie kazi.

kwanza kabisa sahihisha kauli yako (highlighted) maana kwa uelewa ulikuwa unataka wana chadema ndani ya JF wachukue mapendekezo yako, Hapa JF kuna watu wa nyama mbalimbali na wengine hawana vyama kabisa kazi yao nikuchambua issues bila kuwa bias.
Pili kwa mtazamo wangu Zitto haogopi , ni msema ukweli na kila jambo aliangalia critically bila kujari limetoka kwa mwenyekiti au katibu. kwa kutumia uhuru wake wa mawazo wanachadema wasiokubali kupishana mawazo na kila mtu kuwa huru kutoa maoni yake bila uoga wanamwona hafai. Zitto ni asset kwenye chadema na mkubali kutofautiana mawazo kwa nia njema ya kujikosoa na kendeleza chama, zama za yes sir na kupigia makofi kila tu zinadumaza akili
 
Tusiendelee kumjadili Zito atajiona maarufu sana, vyovyote iwavyo...........kama amepewa hela na CCM na zinampa kiburi hiyo ni juu yake lakini ajue tu kwamba hela si kila kitu, na asijaribu kufikiri ataweza kukiuwa chama-CDM yeye ndiye atakufa kisiasa, akiondoka Mungu anawanyanyua wengine zaidi yake. Mungu wetu yu hai!

Zito wa mwanzo sio wa sasa......nawaeleza iq ya zito ni kubwa kuliko mnavyofikiria na msidhani hajui anachofanya na impact yake ......he is the only target now by ccm party to get through chadema...........we know how to deal with him!
 
jamani hapa cha ajabu nn? kutofautiana na kuonyesha wazi msimamo wako na so kuburuzwa tuuu unaondoa kuonekana mnafiki!!! ni chama gani chenye democrasia hii, hakuna... fanya hivyo CCM uone, muulizeni 6, ni majeruhi wa haya kutofautiana na misimamo kandamizi ya cc, wee wach bana!! Hii CDM ni D ya kweli
CCM kweli hawafai, hata akina Kafulila, Mwera na leo mwentekiti wa BAWACHA waliwafukuza! Unaupungufu wa kumbukumbu kichani.
 
Mhe. Zitto Zuberi Kabwe,

Pole kwa majukumu ya kila siku ya kuwakomboa watanzania. Binafsi nakufagilia sana kutokana na uelewa wako na ushaarabu Mungu aliokujaalia. Najua wapo wanaokubeza kutokana namisimamo yako lakini wewe umekuwa kiongozi wangu bora maana siku zote umekuwa ukijenga hoja na huwa hukurupuki. Naomba ufafanuzi wa kutounga mkono kitendo kilichofanywa na wabunge wa chama chako maana wewe binafsi hukiafiki. Kisheria Bunge la Tanzania linakamika panapokuwa na Rais "Bunge pamoja na Rais" yaani Rais ni sehemu ya buge kama alivyosema mama makinda jana pale bungeni. Nadhani kwa nyie kuendelea kuingia bungeni inamaana mnamkubali Rais ila kuna shinikizo linafanya muonyeshe kuwa mnamkataa au pengine ni kuganga njaa. Maana mkiquit hamtapata posho na mishahara.

Kwakua nakuamini nategemea utanijibu ipasavyo kwa hekima na ufasaha zaidi ama mnaingia bungeni kuganga njaa au laa...................

nafikiri umekurupuka na haujui unataka nini kama mtu makini nadhani ungalipaswa kutambua wanachokipinga chadema ni mchakato mzima uliopelekea jk kutangazwa kuwa rais na wala sivyo unavyofikiri wewe na kuhusu swala la kugaanga njaa wale wa ndio mzee na naunga hoja kwa asilimia mia moja 100% linawafaa zaidi kwa wapiganaji wa chadema halina nafasi hilo be informed muzee!
 
huyu ndiye aliunga mkono mitambo ya dowans (richmond) inunuliwe/ ni fisadi huyu Zitto jamani
 
Hata ccm wana nafuu,hawatoki nje ya vikao vya chama na kuanza kuropoka hovyo kwenye vyombo vya habari.
Jamaa ni destructive kwenye chama.Kuna haja gani ya kuzungumzia kile kilichotokea nyuma ya pazia.Kwa sasa hivi chadema wamuache tu, atajimaliza mwenyewe tu kama CUF walivyojimaliza.
nani kakuambia kuwa CUF imekufa? we shall see. Natamani mmfukuze huyo zitto ili mjiweke wazi nyinyi ni watu wa aina gani
Kwa taarifa yenu umaarufu wa chadema upo sehemu chache tu kama kilimanjaro (except Mwanga and same) na mbeya tu sehemu nyingine zilizobaki ni umaarufu wa mhusika mwenyewe ndo maana hata mlipomfukuza kafulila na jimbo mlilifukuza pia.
 
Ndugu Wana JF,

Kuna uwezekano mkubwa baadhi ya wabunge wa chadema wenye muelekeo wa kuitambua serikari ya JK na kutaka kushirikiana na CCM na huenda wakatajwa kuwa kwenye Baraza la mawaziri la JK, Lengo likiwa kuleta msuguano na mitafaruku ndani ya chama chetu cha chadema.

Kwani misimamo mingi ya bwana ZITTO KABWE imekuwa ikiwapa talking point wapinzani wakubwa wa chadema hususani CCM, na nadhani JK anaweza kuwateuwa baadhi ya wabunge wa chadema hususani ZITTO KABWE kama wachambuzi wengi wa masuala ya kisiasa wanavyo speculate, Je ikiwa baadhi ya wabunge wa chadema watateuliwa chadema wamejipanga vipi kukabiliana na suala hilo lenye nia ya kutaka kuongeza msuguano na kukidhohofisha chama? watakubali uteuzi au watawazuia wabunge hao kushiriki kwenye serikari ya ccm, na je uamuzi wowote wa chama utakuwa na repucation gani kisiasa?

Ni mtazamo wangu huru, wadau tujadili hili.
 
Zito mzigo kwa CDM. Bora amwagwe.Bora chama kiende bila Zito.
 
zitto ni mzigo yeye anafanya mambo as if alipokuwa spika wa bunge la UDSM..no way aende tu ...hafai hata kidogo kuwa CHADEMA na kumuacha ni hatari auende akajiunge na TLP au CCM
 
Zito mzigo kwa CDM. Bora amwagwe.Bora chama kiende bila Zito.

Je hakuna repucation zozote kama chama kikimwaga ZITTO, kwani kumekuwa na propaganda za udini CHADEMA na hizo propaganda zinatumiwa makusudi na CCM ili kumweka ZITTO kama icon ndani ya chadema hivyo basi kama Chadema kita mwaga ZITTO , CCM hawawezi take advantage kukimaliza chama chetu kisiasa?
 
Ngoja yatokee kisha tutajadili! We are yet to get to the river, how do we cross the bridge?
 
Ndugu Wana JF,

Kuna uwezekano mkubwa baadhi ya wabunge wa chadema wenye muelekeo wa kuitambua serikari ya JK na kutaka kushirikiana na CCM na huenda wakatajwa kuwa kwenye Baraza la mawaziri la JK, Lengo likiwa kuleta msuguano na mitafaruku ndani ya chama chetu cha chadema.

Kwani misimamo mingi ya bwana ZITTO KABWE imekuwa ikiwapa talking point wapinzani wakubwa wa chadema hususani CCM, na nadhani JK anaweza kuwateuwa baadhi ya wabunge wa chadema hususani ZITTO KABWE kama wachambuzi wengi wa masuala ya kisiasa wanavyo speculate, Je ikiwa baadhi ya wabunge wa chadema watateuliwa chadema wamejipanga vipi kukabiliana na suala hilo lenye nia ya kutaka kuongeza msuguano na kukidhohofisha chama? watakubali uteuzi au watawazuia wabunge hao kushiriki kwenye serikari ya ccm, na je uamuzi wowote wa chama utakuwa na repucation gani kisiasa?

Ni mtazamo wangu huru, wadau tujadili hili.

Wabunge wote wa Tanzania wameteuliwa na vyama vyao na endapo watapoteza uanachama wa chama kilichomfikisha Bungeni atakuwa amepoteza Ubunge. Chama kinachounda Serikali ya Muungano ni CCM na hakuna makubaliano kati ya CCM na Vyama vingine kushirikisha wabunge wao katika Serikali, hivyo siyo rahisi mbunge yeyote wa chama cha upinzani kushirikiswa kwenye serikali bila ridhaa ya chama chake.
 
Hiyo itakuwa njia ya kuidhohofisha chadema. Wakiteuliwa wakatae wasipokubali maamuzi ya chama wafukuzwe. Chadema ziyo ya mtu moja
 
Wabunge wote wa Tanzania wameteuliwa na vyama vyao na endapo watapoteza uanachama wa chama kilichomfikisha Bungeni atakuwa amepoteza Ubunge. Chama kinachounda Serikali ya Muungano ni CCM na hakuna makubaliano kati ya CCM na Vyama vingine kushirikisha wabunge wao katika Serikali, hivyo siyo rahisi mbunge yeyote wa chama cha upinzani kushirikiswa kwenye serikali bila ridhaa ya chama chake.

JK aliposema atashirikisha wapinzani kwenye serikari yake alikuwa ana maanisha CUF au? Je akifanya uteuzi wa kichokozi kwa kumteuwa ZITTO ambae amekuwa PRO-JK kwa sababu zinazoeleweka itakuwaje?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom